Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Hii sory tamu sana kuisoma huku unaelekea some where uko kwenye bus, mana unakuwa huna time na mtu.
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 21.



Haikuwa safari ya kitoto hata kidogo,tuliingia pale Arusha saa 3 usiku.Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kufika Arusha,japo nimefika mara kadhaa lakini sikuwahi kuwa mwenyeji,mara zote wakati naenda shule Tanga nilikuwa nikipita Arusha.Baada ya kufika Arusha mjini yule jamaa akawa ametuambia inapaswa tupate chakula mahali fulani ili tukimaliza tuondoke kwakuwa tulipokuwa tukienda hakukuwa na chakula wala mtu wa kukipika!.

Tulipomaliza kula tuliondoka zetu kuelekea ambako mimi na Mtatiro tulikuwa hatupajui.Baada ya muda ile gari ikaanza kupiga honi baada ya kufika mbele ya nyumba ambayo ilikuwa na geti;geti lile lilifunguliwa kisha gari ikaingia ndani.Tuliteremka huku tukiendelea kushangaa shangaa ndipo yule jamaa akaja akatuambia tumfuate,tulielekea ndani ambako tulionyeshwa chumba cha kulala ambacho kilikuwa na vitanda 2.

Wakati ule kiukweli hakuna mtu tuliyemkuta pale kwenye ile nyumba zaidi ya yule mtu aliyetufungulia lile geti,sasa kumbe baada ya ile Noah kutuacha pale wao waliondoka na hakuelewa walienda kulala wapi.Asubuhi mida ya saa 2 yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza alikuja kutuchukua na kutuambia inapaswa tuondoke!.Tuliondoka kuelekea Tengeru hatimaye tukafika kwenye nyumba moja ambayo tulimkuta yule bosi wake na Gabi akiwa na jamaa wawili,miongoni mwa wale jamaa tulikuwa nae Mwanza ila yule mmoja sikumfahamu,sasa ilifanya idadi yetu kuwa watu wanne ukimuondoa yule Bosi.Yule bosi alimuita yule jamaa tuliyekuja nae wakaanza kuzungumza kitu ambacho hatukukilewa,sasa baada ya yale mazungumzo jamaa alitoka akawa ameondoka,baada ya muda kuna jamaa mmoja miongoni mwa wale tuliowakuta alikuja akawa ametuuliza mimi na Mtatiro tunavaa viatu namba ngapi kila mmoja.

Baada ya kumueleza size ya namba ya viatu tulizokuwa tunavaa,jamaa aliondoka.Haukupita muda akawa amerudi na viatu aina ya safari boot ambazo kila mtu alipaswa kuchukua size yake!.Sasa ilipofika mida ya jioni yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza alirudi akiwa kwenye gari aina ya Mark 2 nyeupe iliyokuwa na tinted,ile gari iliingia mpaka pale ndani kisha jamaa akawa ametelemka na begi jeusi ambalo lilionekana lilikuwa zito.

Jamaa "Aisee hebu njoeni ndani mara moja"

Baada ya kufika ndani,jamaa hakutaka kupoteza muda,alifungua lile begi ambalo lilikuwa na nguo kadhaa akawa amezitoa na kututaka kila mmoja ajaribu itakayo mtosha.Mimi zilizonitosha ilikiwa ni jeans mbili pamoja na cadet moja iliyokuwa nzito,Mtatiro yeye kwakuwa alikuwa na mwili mkubwa kidogo,alipata nguo ambazo ziliendana na mwili wake vizuri.

Sasa baada ya hapo jamaa alituambia tukae chini kisha akawa ametoa bunduki iliyokuwa kwenye lile begi!.Sikufahamu ile bunduki ilikuwa ni aina gani kwasababu sikuwa mtaalamu wa bunduki kwa wakati huo,ile bunduki ilikuwa ni fupi kisha ikawa imekazwa kwa mapira katikati.Sasa baada ya kuitoa ile bunduki yule jamaa alituambia tumsubiri yule aliyekuwa bosi wa Gabi anakuja.

Yule bosi baada ya kurudi na yeye hiyo mida ya saa 2 usiku pia alikuwa na bunduki ambayo niliifahamu ilikuwa SMG.

Bosi "Msiogope bhana haya ni mambo ya kawaida"

Aliendelea "Jamaa yenu mtamkuta Kahama anawasubiri,pale kuna mtu ana hela zangu itapaswa mkazichukue"

Aliendelea "Hii Mashine ningekupatia wewe(Mtatiro)lakini nahitaji kwanza muda"

Aliendelea "Jipe atawapa hiyo nyingine mtaondoka nayo kwenda Kahama halafu hii kuna mtu mtaongozana nae ndiyo atakuwa nayo"

Aliendelea "Sasa naomba simu zenu mziache hapa maana huko hampaswi kwenda na simu"

Basi tulichukua zile simu tukawa tumemkabidhi yule aliyeitwa Bosi.Kumbe muda huo ambao sisi tulikuwa hapo Arusha,Gabi yeye alikuwa Kahama mkoani Shinyanga ambako hatukufahamu alikwenda kufanya shughuli gani!.

Bosi "Nyie mtaondoka kesho kutwa,kaeni hapa mpumzike kwanza"

Baada ya yale mazungumzo,yule Bosi aliondoka na yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza wakawa wametuacha pale kwenye ile nyumba tukiwa pamoja na wale jamaa wawili tuliowakuta.

Kweli!,baada ya siku mbili tuliondoka asubuhi na mapema,ilikuwa mida ya saa 10 usiku ndipo tuliianza safari kuelekea Kahama mkoani Shinyanga,mimi kiukweli sikuelewa kilichokuwa kimetupeleka Arusha ilikuwa ni kitu gani maana hata bunduki zenyewe hatukupewa kwa muda huo bali tuliishia tu kuonyeshwa na kupewa maelekezo,sikuweza kuhoji sana niliamua tu kutulia maana nilikubali mwenyewe kujiingiza kwenye genge la ujambazi!.
Tuliondoka na ile Toyota Mark 2 ambayo tulikuwa mimi na Mtatrio pamoja na yule jamaa tuliyetoka nae Mwanza ambaye alifahamika kwa jina la Jipe,sikujua kama ndilo jina lake halisi lakini hata sisi baada ya kuzoeana tulikuwa tukimuita hivyo!.Dereva aliyekuwa akiendesha ile gari kiukweli alikuwa jamaa fulani wa kawaida sana na mwembamba lakini alikuwa dereva mzuri sana,nakumbuka ile gari ilikuwa ikitembea mpaka unahisi inapaa!.

Baada ya safari ndefu hatimaye tukafika Kahama,sasa tulipofika maeneo ya mgodi wa buzwagi,tuliingia kushoto tukaikamata barabara ya vumbi kuelekea Mwendakulima kwa ndani ndani huko.

Haukupita muda tukawa tumefika kwenye nyumba moja ambayo haikuwa na geti lakini ilikuwa imejitenga mbali na nyumba nyingine,sasa tulipofika hapo ndipo tukakutana na Gabriel ambaye baada ya sisi kuteremka kwenye ile gari alimchukua pembeni yule jamaa wakaanza kuzumngumza!.

Baada ya yale mazungumzo Gabi alituambia tuingie ndani huku yule jamaa akibeba lile begi lililokuwa na silaha kuingia nalo ndani!.Tulipiga stori na Gabi huku yeye akiendelea kutupa moyo kwamba yale mambo yalikuwa ni kawaida tu na hatukupaswa kuwa na hofu!.

Siku iliyofuata ilipofika saa 6 usiku,yule jamaa alituambia mimi na Mtatiro tutaongozana nae kuelekea mahali fulani,sasa alimpatia Mtatiro ile bunduki iliyokuwa imefungwa na mapira kwa nguvu sana na yeye akachukua ile SMG.

Jipe "Mtakuwa manafuata maelekezo yangu kila nitakachokuwa nawaambia!"

Mtatiro "Sawa"
Jipe "Hiyo silaha tayari risasi iko chemba,hivyo kuwa makini!"

Aliendelea "Gabriel atabaki hapa kuweka mambo sawa,sisi tutaondoka na tutawahi kurudi,kule tukifika hakuna kusubiri,tunaenda kufata kilichotupeleka!"

Jipe "Wewe jamaa(mimi)utakuwa kando yetu na utafanya nitakachokuwa nakwambia"

Mimi "Sawa"

Mtatiro alivyokuwa ameishika ile silaha ungemuangalia kwa haraka haraka ungezani uenda alikuwa askari mwenye uzoefu wa miaka mingi,jamaa alikuwaga jasiri sana alikuwa mtu ambaye ulikuwa ukimpatia maelekezo mara ya kwanza basi hurudii tena maana alikuwa na kichwa chepesi!.

Mpaka muda huo ukweli ni kwamba,Mtatiro ndiye aliyenishawishi hadi na mimi kujikuta naingia mkenge!,sikuwa na namna ilipaswa nitafute pesa!.

Zaidi: Sehemu ya 22
Asante sana
 
Millions 50, mnapewa 1.9m mgawane 2 people . Utajuta
 
Umughaka
1.Kwanza hongera wewe ni muandishi mzuri Sana, hebu fikiria kuiendeleza hiyo karama kajipige hata kicourse Cha creative writing uanze kuandika hadithi zako Kaka upige hela zako.
2.Hongera wewe ni mpambanaji na ni mvumilivu Sana nimefuatilia story zako zote mbili hii na ile ya wifi Monica lol😄😄 na una akili pia, shule uzinzi ndio ulikuponza.
3.kwenye hii story yako nimejifunza kuwa kwenye haya maisha usiamini kila unachokiona,au kukisikia hasa linapokuja suala la kipato na utafutaji wa pesa, maana pale watu wanakuona mpiga debe unanawiri kila siku kumbe Kuna behind the scenes 😃,au yule shemeji yako watu wanaona tu biashara ya uvuvi inalipa,kumbe watu wanapulizia mambo motivational speakers wanatumia story zenu kuwapa vijana depression kitaa, mtu anakimbilia kuuza mitumba Ila hela haioni halafu anawaona umughaka na mshikaji wake haooo Gold crest Mara visafari vya hapa na pale Mara Uganda kufunga mzigo kumbe nyuma ya pazia Kuna mengi.
4.Cheti chako cha form four kilikua kizuri tu,haukuwahi kufikiria kujiendeleza? Au ndo ukishashika pesa Tena unaona huwezi kupoteza muda kusoma.
All in all story zako zinafurahisha na kufundisha Sana kila heri kwenye mapambano.Nasikia Huko daslamu Kuna Askari anakagua bodaboda hata akiona imepaki ndani ya geti anagonga anaingia kuikagua na hajawahi kukuta pikipiki Haina kosa😄😄 naye ni mmoja ya wapambanaji
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 7.



Sikutaka kabisa marafiki zangu na watu wanaonifahamu pale stendi wahisi kitu,kiukweli japo nilikuwa mikononi mwa wale askari lakini nilijitahidi sana kuonyesha hali ya kawaida na tena tulipofika kwenye hiace ya kuelekea mjini ni mimi ndiye niliyefanya kazi ya kuwaombea lift nikijifanya niwanangu!

Sasa tulipofika pale mjini kukamata mchomoko wa kuelekea Sirari ilibidi askari mmoja atoe hela amlipie yule mwenzie na mimi kudandia bure,wasingeweza kupanda mchomoko bure kwasababu ilikuwa inachukua watu wachache!.

Basi tukaondoka na hatimaye tukafika pale stendi ya mchomoko Sirari,tulipofika pale wanangu walianza kunichangamkia na wengine kuniuliza nilienda wapi,sasa wale askari wakataka kunidhibiti lakini niliwaambia kiaina ya kwamba siwezi kukimbia na wasinidharirishe mbele ya wana,bahati nzuri jamaa walikuwa waelewa na wao wakawa wameniacha najifanya kujizungumzisha mbele ya washikaji kana kwamba sina kosa kumbe moyoni naujua ukweli!.

Baada ya mazungumzo pale stendi na wanangu,nilijikuta kitete chote kimetoweka na kisha nikaandamana na wale mapongo hadi nilipokuwa nimepanga!.Nashukuru Mungu hakuna mtu aliyeshitukia mchezo pale stendi.Basi baada ya kufika hapo nyumbani nilifunua kifuta miguu(zulia)pale mlangoni kisha nikatoa funguo nikafungua mlango!.Sasa ile nyumba sikuwa peke yangu,kulikuwa na wapangaji wengine ambao nao kuna wengine walikuwa kwenye shughuli zao na wengine hasa wanawake walikuwa nyumbani,sasa desturi ikawa ni ileile ya kwamba asifahamu mtu yeyote kwamba wale ni askari,nilipofungua mlango niliwakaribisha kwa sauti ya "Karibuni" ili asitokee mtu yeyote akajua kitu.

Baada ya kufika ndani askari mmoja akaniomba funguo akafunga mlango kisha wakanitaka tuanzie kufanya upekuzi chumbani.Upekuzi haukuchukua muda mrefu kwasababu sikuwa nimejaza mle ndani makorokoro,bali kulikuwa na kitanda pamoja na begi kubwa la nguo na vitu vidogo vya kawaida,sebuleni nako kulikuwa na makochi,TV na redio na picha za ukutani zilizopendezesha sebule.Hakukuwa na vyombo vingi kwasababu nilikuwaga sipiki hapo nyumbani bali nilikuwa nakula kwa mama ntilie,nilikuwa na mabeseni mawili pamoja ndoo mbili tatu nilizotumia kwa ajili ya kuwekea maji ya kuoga na kufulia.

Sasa pesa zangu zote nilikuwaga nazihifadhi kwenye mfuko wa suruali kisha naweka hiyo suruali kwenye begi pamoja na nguo nyingine,wale askari walipekua kila mahali bila kuona kitu chochote.Wakati huo nilikuwa nimebaki na zile fedha haramu kiasi cha shilingi elfu 40,pia nilikuwa nina hela halali kiasi cha shilingi laki moja na elfu themanini.

Askari "Nadhani unajua kilichotuleta hapa ni kitu gani,hebu kuwa mkweli pesa umeweka wapi?,au unataka tutumie nguvu?"

Aliendelea "Mpaka tumefika hapa umekuwa mstaarabu,angalia mambo yasije haribikia hapa"

Baada ya jamaa kuniambia vile na akionekana kumaanisha,nilichukua ile suruali iliyokuwa imetupwa chini kutokana na shaghala baghala ya upekuzi nikatoa zile hela nikamkabidhi jamaa!.

Askari "Haya sasa ndiyo mambo,endelea kutafuta najua bado zipo nyingine!"

Mimi "Hapana afande pesa niliyokuwa nayo ndiyo hiyo"

Askari "Kwanini unatupotezea muda?,siutoe pesa mdogo wangu tuondoke!,au unataka tutumie nguvu?"

Mimi "Kweli afande pesa yote niliyokuwa nayo ndiyo hiyo"

Jamaa waliendelea kutafuta kila mahali lakini hawakuona kitu,sasa kwakuwa niliwapa zile hela askari mmoja akawa amesema wanipige pingu kwakuwa tayari kidhibiti nilikuwa nacho.Niliwaangukia miguuni nikawasihi wasinipige pingu na sitowasumbua njiani!,yule askari aliyefunga mlango wakati tunaingia ndani kiukweli akawa akinionea huruma sana kama kijana mwenzie na akamwambia mwenzie asifanye hivyo kwakuwa wakati tunakuja sikuwasumbua,sasa yule mwenzie akawa ameendelea kuweka msisitizo kwamba nipigwe pingu!.

Basi baada ya kuwasihi sana huku machozi yakinitoka,wakawa wamekubali na wakanitaka nisije kujaribu kuwakimbia.Sasa wakati tunatoka nikachukua ufunguo nikampelekea dada mmoja aliyekuwa mke wa mpangaji mwenzangu hapo nyumbani,nilimwambia akae na ule ufunguo kuna mahali naenda na nikirudi nitaukuta kwake!.

Tukaondoka na wale askari mpaka stendi tukapanda mchomoko kuelekea Tarime mjini,kwa namna tulivyokuwa tunatembea na wale askari wakiniuliza maswali kadhaa huku nikiendelea kuwajibu nilihakikisha kabisa hakuna mtu anayefahamu jambo lile,mimi sikutaka kabisa kujifanya mjuaji ili kujiepusha na aibu isiyokuwa ya lazima!.

Tulipofika pale Tarime mjini tukitokea Sirari,kuna askari mmoja niliona anaongea na simu na sikufahamu alichokuwa anaongea,sasa baada ya maongezi yale kwenye simu,alimwambia yule askari mwenzake kwamba ahakikishe nakaa chini,basi nilikaa chini huku yule askari mwingine akiondoka kusikojulikana!,wakati nimekaa chini yule askari alikuwa makini sana na mimi na hakutaka kabisa stori na maongezi!.Baada ya dakika 10 niliona difenda imefika lile eneo na kutakiwa kupanda.

Moyo wangu uliuma sana na nilikuwa nawaza napelekwa wapi wakati ilipaswa nirudishwe hadi buhemba nilikokuwa nimetokea!.Sikufahamu hatima ya Gabriel na mkewe iliendelea vipi nilipowaacha!,mimi nilijua huo msalaba tayari ndiyo nishaubeba!.Kilichokuwa kinaniumiza zaidi ni namna wazazi wangu wakija kufahamu ya kwamba mtoto wao nipo polisi au kufungwa gerezani,nilikuwa navuta picha ya Mzee wangu namna atakavyo ongea akisikia nimekamatwa,tena nilijua ndiyo atajihahakishia kabisa kwamba kunitimua pale nyumbani alikuwa sahihi kabisa!.

Basi niliamua kutulia ndani ya difenda na kumuachia Mungu yeye ndiye akawe muamuzi wa lile jambo,kwa hatua niliyokuwa nimefikia sikuwa na msaada wowote zaidi ya kuamini ni Mungu peke yake ndiye anaweza kuniokoa na mkono wa serikali!.

Kuna muda hata kama humjui Mungu na hujawai kukanyaga kabisa kanisani au msikitini,unapofikwa na jambo gumu kiutatuzi ndipo siku hiyo utatamani mahubiri na mihadhara isikike mahali ulipo ili uweze kuamini kuna Mungu na utajaribu kusali sala zote na utatumia lugha zote kumuomba hata kama unayemuomba uliamini hayupo.

Mpaka wakati huo baada ya kujiingiza kwenye upiga debe na vile vistarehe uchwara vya muda mfupi sikuwahi kabisa kukanyaga mlango wa kanisa lakini baada ya kupata hiyo changamoto ya muda mfupi nilikuwa nikimlilia Mungu kimoyo moyo aniokoe na kile kikombe kana kwamba nilikuwa muhudhuriaji mzuri wa ibada!.

Baada ya kupakiwa kwenye ile difenda nilipewa amri ya kukaa chini na kusogea mbele kabisa na miguu kuikalisha chini ikiwa imenyooka,ile difenda iliondoka yale maeneo kuelekea Nyamisangura ambako tulipofika pia huko kuna jamaa kama 6 walipakiwa kwenye ile difenda na kufanya jumla yetu wahalifu kuwa 7.Basi baada ya hapo ikaondoka kwa spidi kali huku askari wengine waliokuwa na bunduki wakidandia na kuondoka!.

Sasa tulipofikishwa pale central,baada ya kushuka tulitakiwa kuelekea ndani kwa kukimbia huku mikono tukiambiwa tuweke kichwani!,baada ya kufika ndani askari mmoja wapo wa wale niliokuwa nao akawa ameniambia nifuatane naye.Ndipo akafungua chumba kimoja ambacho baada ya kuingia ndani nikamkuta Gabriel na mkewe akiwa na yule askari niliyewaacha nae pale nyumbani kwake!.

Askari "Ooh umemleta bwana mdogo"

Aliendelea "Unapofika hapa kwetu bwana mdogo hakuna makaochi hivyo unatakiwa ukae chini!".

Basi baada ya hapo nikaona yule askari anatoa ile hela elfu 40 ambayo haikuwa halali anamkabidhi yule askari ambaye ilionekana alikuwa mkuu wa upepelezi!.Kilichonishangaza ni kutokuona ile laki moja na elfu themanini ambayo ilikuwa halali sikuona anakabidhiwa yule afande na ndipo nikagundua wale askari watakuwa waligawana ile hela!.

Basi baada ya mazungumzo ya muda mrefu hapo ndani huku tukiwa tunahojiwa na yule askari kuandika maelezo yetu,alipomaliza akawa amemwambia yule askari tunapaswa kuwekwa rumande!.Kiukweli nilijuta sana moyoni na sitakaa nisahau ile siku.Kabla ya kuingizwa rumande nilimuomba yule afande simu yangu ili niwasiliane na ndugu zangu wawe na taarifa,hakuwa na shida kabisa na alinipatia ile simu na akanitaka niongee nikiwa mle mle ndani ya kile chumba.

Basi baada ya kupewa ile simu,nilimpigia mwanangu mmoja tuliyekuwa tumeshibana sana aliyekuwa mpiga debe mwenzangu pale Sirari!.

Mimi "Nyamori mambo vipi?"

Nyamori "Mzee wa kuzugia mbona sikuoni kijiweni wewe!?"

Sasa kwa pale Sirari jina maarufu nilifahamikaga kama mzee wa kuzugia,hii ilikuja baada ya kila sentensi nitakayoongea nilikuwa naweka neno kuzugia au kuzuga na hii kitu nimekuwa nayo hadi leo hii,nadhani ni mazoea tu!.Sasa jamaa baada ya kupokea simu yeye alianza utani wake bila kufahamu kilichokuwa kinaendelea!.

Mimi "Mwanangu nimepata msala!"

Nyamori "Msala gani tena mzee?"

Mimi "Nipo hapa polisi mwanangu,kama vipi mje kunicheki!"

Nyamori "Haina noma mwanangu ngoja niwashitue wana"

Basi baada ya yale mazungumzo nikawa nimekabidhi ile simu tena kwa yule afande.

Kabla ya kuingizwa lupango,tulitakiwa kukabidhi kila tulichokuwa nacho,mimi mpaka muda huo sikuwa na chochote zaidi ya saa ya mkononi na waleti ambayo haikuwa na kitu zaidi ya makaratasi na tiketi za gari!.Basi kwa mara ya kwanza mwanaume nikaingizwa lokapu ambako baada ya kuingia niliona ni heri ukalazwa chooni wiki nzima lakini si mule ndani!.

Muendelezo > Sehemu ya 8
[emoji433][emoji433][emoji433][emoji433]
 
Back
Top Bottom