Nilivyonusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali miaka 15 iliyopita. Tanzania kufariki ni dakika 0 tu!

Nilivyonusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali miaka 15 iliyopita. Tanzania kufariki ni dakika 0 tu!

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Ni miaka 15 sasa imepita tangu ninusurike kuuawa na walimwengu. Nilikuwa nikiishi Tabora, na jioni moja, nilikuwa natembea mjini Tabora. Wakati natembea, nikajihisi kubanwa haja ndogo, nikawa nakatiza mtaa wa Salimini. Kwa wale wenyeji wa Tabora, mnafahamu ule mtaa ulivyo wa Kiswahili. Nikawaomba niingie kwenye nyumba moja mtaani hapo ili niombe sehemu ya kujisaidia haja ndogo (chooni).

Nje ya nyumba ile alikuwa amesimama kijana mwenye umri wa miaka 18 au 19, nilimuomba na akanielekeza nipite kwenye korido niende mpaka uwani. Wakati napita kwenye korido, nilikutana na mwanamke na mwanaume wakiwa wanazungumza. Niliwasalimia, na mimi nikaendelea na safari yangu kuelekea uwani. Nilipofika uwani, kabla ya kuingia chooni, nikawa ninakunja suruali yangu mpaka ukaribu na magotini (kawaida yetu Waislamu huwa tunafanya hivi ili utakapokuwa unajisaidia haja ndogo, zile cheche za mikojo zisirukie nguo). Ghafla nilisikia sauti ya mwanamke ikitokea nyuma ikiita "mwiziiiiii, mwiziiiiii."

Ile kugeuka, namuona yule mwanamke niliemuona kwenye korido anakuja mbio huku akakamata kuni. Akaanza kunipiga na ule ukuni sehemu za mabegani huku mimi nikihangaika kupangua kile kipigo na kujitetea kuwa mimi sio mwizi. Yule mwanamke alipoona ananipiga na ukuni na mimi sianguki, akabeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto ili animwagie usoni. Dah, lahaula! Akatokea yule mwanaume aliyekuwa nae akamuambia "achaaaaa!" Kujinusuru, nilibidi nirukie kwenye korido nitokee mlango wa mbele ili nikimbie (hapa nilifanya kosa kubwa). Nilianza kukimbia barabarani huku yule mwanamke akiendelea kuita "mwiziiii, mwiziiiiii."

Watu wakaanza kunikimbiza. Kadiri nilivyokuwa nakimbia, watu walizidi kuongezeka, huku wengine wakiwa wamebeba mapanga. Niliingiwa na fikra za haraka za kuingia kwenye nyumba ya mtu ili ninusuru maisha yangu. Bahati nzuri, nyumba ile niliyoingia ilikuwa ya mjumbe wa serikali ya mtaa. Alichokifanya yule mjumbe (mwanamke wa makamo) aliniambia niingie nijifiche chumbani na yeye akafunga mlango. Lile kundi la watu wenye mapanga walifika kwenye nyumba ile niliyokuwa nimejificha na wakaanza kumlazimisha yule mjumbe anitoe nje huku wakiimba "tunamtaka mwizi weeetúu."

Yule mjumbe alisimama mlangoni na kuwaambia wale watu, "Simtoi nje huyu kijana, ila nitakachofanya, napiga simu polisi waje wamchukue, mtamkuta kituoni." Hii ndiyo ilikuwa salama yangu. Haikupita masaa mawili, walikuja polisi na kunichukua kwenye gari lao. Polisi mmoja alinipiga vibao huku akisema, "Kumbe jamaa mwenyewe mrembo!" (Mimi nina asili ya ushombe shombe kwa mbali).

Nilipofikishwa kituoni, nilijieleza kwa ufasaha na pia nikatoa vitambulisho vyangu ili viwe ni uthibitisho wa kile nilichokizungumza. Bahati nzuri, mfukoni nilikuwa na shilingi laki moja, nikatoa 30,000/- nikawapa wale askari, wakawa wameniachia niende nyumbani usiku ule na kesho yake niende kuripoti. Kesho yake niliripoti polisi, na askari walinikabidhi vitambulisho na kuniambia hakuna kesi. Nikaendelea na majukumu yangu.
 
Ni miaka 15 sasa imepita Toka ninusulike kuuawa na walimwengu, nilikuwa nikiishi tabora jioni moja nilikuwa natembea mjini tabora, wakati natembea nikajihisi kubanwa haja ndogo, nilikuwa nakatiza mtaa wa salimini kwa wale wenyeji wa tabora mnafahamu ule mtaa ulivyo wa kiswahili......nikaona niingie kwenye nyumba moja Mtaani hapo ili niombe sehemu ya kujisaidia haja ndogo ( chooni) ...nje ya nyumba Ile alikuwa amesimama kijana mwenye umri wa miaka 18 au 19 nilimuomba na akawa amenielekeza nipite kwenye korido niende mpaka uwani, wakati napita kwenye korido Ile nilikutana na mwanamke na mwanaume wakiwa wanazungumza, niliwasalimia na Mimi nikaendelea na safari ya kuelekea uwani, nilipofika uwani kabla ya kuingia chooni nikawa ninakunja suruali yangu mpaka ukaribu na magotini ( kawaida yetu waislamu huwa tunafanya hivi ili utakapokuwa unajisaidia haja ndogo zile cheche za mikojo zisirukie nguo) ghafra nilisikia sauti ya mwanamke ikitokea nyuma ikiita mwiziiiiiiiiii, mwiziiiiiiiiiii Ile kugeuka namuona yule mwanamke niliemuona kwenye korido anakuja mbio huku kakamata Kuni ...akaanza kunipigia na ule ukuni sehemu za mabegani huku Mimi nikihangaika kupangua kile kipigo na kujitetea kuwa Mimi sio mwizi, yule mwanamke alipoona ananipiga na ukuni na Mimi sianguki akabeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto ili animwagie usoni, dah lahaula akatokea yule mwanaume aliekuwa nae akamuambia achaaaaaa, kujinusuru ili nibidi nirukie kwenye korido nitokee mlango wa mbele ili nikimbie ( hapa nilifanya kosa kubwa) nilianza kukimbia barabarani huku yule mwanamke akiendelea kuita mwiziiii, mwiziiiiii, watu wakaanza kunikimbiza kadiri nilivyokuwa nakimbia watu wanazidi kuongezeka huku wengine wakiwa wamebeba mapanga.....niliingiwa na fikra za haraka za kuingia kwenye nyumba ya mtu ili ninusuru Maisha yangu....bahati nzuri nyumba Ile niliyoingia ilikuwa ni mjumbe wa serikali ya mtaa alichokifanya yule mjumbe ( mwanamke wa makamo aliniambia niingie nijifiche chumbani na yeye akafunga mlango....lile kundi la watu wenye mapanga walifika kwenye nyumba Ile niliyokuwa nimejificha na wakaanza kumlazimisha yule mjumbe anitoe nje huku wakiimba tunamtaka mwizi weeetúu, yule mjumbe alisimama mlangoni na kuwaambia wale watu simtoi nje huyu kijana ila nitakachofanya napiga simu polisi waje wamchukue mtamkuta kituoni ( hii ndio ilikuwa salama yangu) haikupita masaa mawili walikuja polisi na kunichukua kwenye gari yao . Polisi mmoja alinipiga vibao huku akisema kumbe jamaa mwenyewe mrembo( Mimi Nina asili ya ushombe shombe kwa mbali) nilipofikishwa kituoni nilijieleza kwa ufasaha na pia nikatoa vitambulisho vyangu ili viwe ni uthibitisho wa kile nilichokizungumza na bahati nzuri mfukoni nilikuwa na shilingi laki moja nilitoa 30000/ nikawapa wale askari wakawa wameniachia niende nyumbani usiku ule na kesho yake niende kuripoti , kesho yake niliripoti polisi na askari walinikabidhi vitambulisho na kuniambia hakuna kesi nikaendelee na majukumu yangu.
Hatari sana... But all in all Mungu ni mwema
 
Duwh kufa ni dakika sifuri tu ,mitaa ya salmini ni karibu na chemchem mkuu?
Balaa sana, nilikuja kufanya uchunguzi niligundua yule mama alikuwa ni mgombea wa udiwani mtaa ule kupitia chama Cha cuf akawa amepigwa chini, kwa hiyo kila mtu aliekuwa anapita kwake alikuwa anamuona kama "snitch ".
 
Ni miaka 15 sasa imepita tangu ninusurike kuuawa na walimwengu. Nilikuwa nikiishi Tabora, na jioni moja, nilikuwa natembea mjini Tabora. Wakati natembea, nikajihisi kubanwa haja ndogo, nikawa nakatiza mtaa wa Salimini. Kwa wale wenyeji wa Tabora, mnafahamu ule mtaa ulivyo wa Kiswahili. Nikawaona niingie kwenye nyumba moja mtaani hapo ili niombe sehemu ya kujisaidia haja ndogo (chooni).

Nje ya nyumba ile alikuwa amesimama kijana mwenye umri wa miaka 18 au 19, nilimuomba na akaniielekeza nipite kwenye korido niende mpaka uwani. Wakati napita kwenye korido, nilikutana na mwanamke na mwanaume wakiwa wanazungumza. Niliwasalimia, na mimi nikaendelea na safari yangu kuelekea uwani. Nilipofika uwani, kabla ya kuingia chooni, nikawa ninakunja suruali yangu mpaka ukaribu na magotini (kawaida yetu Waislamu huwa tunafanya hivi ili utakapokuwa unajisaidia haja ndogo, zile cheche za mikojo zisirukie nguo). Ghafla nilisikia sauti ya mwanamke ikitokea nyuma ikiita "mwiziiiiii, mwiziiiiii."

Ile kugeuka, namuona yule mwanamke niliemuona kwenye korido anakuja mbio huku akakamata kuni. Akaanza kunipigia na ule ukuni sehemu za mabegani huku mimi nikihangaika kupangua kile kipigo na kujitetea kuwa mimi sio mwizi. Yule mwanamke alipoona ananipiga na ukuni na mimi sianguki, akabeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto ili animwagie usoni. Dah, lahaula! Akatokea yule mwanaume aliyekuwa nae akamuambia "achaaaaa!" Kujinusuru, nilibidi nirukie kwenye korido nitokee mlango wa mbele ili nikimbie (hapa nilifanya kosa kubwa). Nilianza kukimbia barabarani huku yule mwanamke akiendelea kuita "mwiziiii, mwiziiiiii."

Watu wakaanza kunikimbiza. Kadiri nilivyokuwa nakimbia, watu walizidi kuongezeka, huku wengine wakiwa wamebeba mapanga. Niliingiwa na fikra za haraka za kuingia kwenye nyumba ya mtu ili ninusuru maisha yangu. Bahati nzuri, nyumba ile niliyoingia ilikuwa ya mjumbe wa serikali ya mtaa. Alichokifanya yule mjumbe (mwanamke wa makamo) aliniambia niingie nijifiche chumbani na yeye akafunga mlango. Lile kundi la watu wenye mapanga walifika kwenye nyumba ile niliyokuwa nimejificha na wakaanza kumlazimisha yule mjumbe anitoe nje huku wakiimba "tunamtaka mwizi weeetúu."

Yule mjumbe alisimama mlangoni na kuwaambia wale watu, "Simtoi nje huyu kijana, ila nitakachofanya, napiga simu polisi waje wamchukue, mtamkuta kituoni." Hii ndiyo ilikuwa salama yangu. Haikupita masaa mawili, walikuja polisi na kunichukua kwenye gari lao. Polisi mmoja alinipiga vibao huku akisema, "Kumbe jamaa mwenyewe mrembo!" (Mimi nina asili ya ushombe shombe kwa mbali).

Nilipofikishwa kituoni, nilijieleza kwa ufasaha na pia nikatoa vitambulisho vyangu ili viwe ni uthibitisho wa kile nilichokizungumza. Bahati nzuri, mfukoni nilikuwa na shilingi laki moja, nikatoa 30,000/- nikawapa wale askari, wakawa wameniachia niende nyumbani usiku ule na kesho yake niende kuripoti. Kesho yake niliripoti polisi, na askari walinikabidhi vitambulisho na kuniambia hakuna kesi. Nikaendelea na majukumu yangu.
Dress code, na outlook yako imekuangusha.
 
Back
Top Bottom