Nilivyonusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali miaka 15 iliyopita. Tanzania kufariki ni dakika 0 tu!

Nilivyonusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali miaka 15 iliyopita. Tanzania kufariki ni dakika 0 tu!

Kwa ufupi ni jamaa aliitwa mwizi na kuponea chupuchupu baada ya kuingia nyumba ya mjumbe na mjumbe kupiga simu polisi kuja kumchukua jamaa, alivyofika kituo cha polisi akatoa rushwa akaachiwa 😎
Unajua wewe ni ndugu yangu? Siku Ile ulinisaidia kunitafsiria kingleza

Leo umenifupishia hii habari, Hakika wewe ni Mtu mwema sana! Mungu akubariki.

Aisee Pole sana kwa huyo jamaa!
 
Balaa sana, nilikuja kufanya uchunguzi niligundua yule mama alikuwa ni mgombea wa udiwani mtaa ule kupitia chama Cha cuf akawa amepigwa chini, kwa hiyo kila mtu aliekuwa anapita kwake alikuwa anamuona kama "snitch ".
Hapo kwenye ugombea umenikumbusha jambo, 2014 kuna kikundi cha chadema kilikosa uongozi wa mtaa mkoani Arusha, sasa kuna wengine walihama kwa aibu ya kukosa uongozi kuna mmama flan hv yeye ht pesa ya kuhama alikosa akabaki mtaani yeye muda wote n kugombana na watu kwa vitu ht vidogo tuu kutokana na hasira za kukosa ulaji 😂
 
Unajua wewe ni ndugu yangu? Siku Ile ulinisaidia kunitafsiria kingleza

Leo umenifupishia hii habari, Hakika wewe ni Mtu mwema sana! Mungu akubariki.

Aisee Pole sana kwa huyo jamaa!
Namba yangu n ile ile na sasa hv imeboreshwa zaidi inapokea M-pesa 😎
Sijasema unitumie pesa, ila nakupa taarifa tuu kuwa namba yangu imeboreshwa zaidi 😎
 
Sikuhitaji kujisaidia hovyo, na kutoka mtaa ule kuelekea vyoo vya kulipia vilipo ilikuwa ni mbali kidogo..
Mwanaume c unaliangusha popote tuu mzee wangu, au ww ndo wale wanajifanya smart kwenye kila kitu?
Ila pia hicho kibegi kimesababisha mana wahuni wengi wanavaa mabegi afu ndani hakuna kitu, kuna mhuni flan mtaani kwenye begi anaweka maboks ili begi lijae
 
Asilimia 90 ya wabongo ni wapumbavu mno linapokuja swala la kushughulikia wanaotajwa kuwa wezi. Unakuta mtu ameitiwa mwizi, mtu haulizi anaokota jiwe anamrushia. Ni upumbavu wa hali ya juu.

Kuna rafiki yangu mmoja aliuawa pamoja na mdogo wake kwa kuitiwa wezi baada ya kugombana na mtu ambaye aliamua kuwaitia wezi. Wameuawa na baadae ikaja kufahamika hawakuwa wezi.

Yupo mwingine nilisoma nae aliitiwa mwizi kwa sababu ya wivu wa mapenzi. Akauawa.

Watu waache tabia ya kujichukulia sheria mkononi. Ukisema hii linakuja pumbavu eti "Wewe hujawahi kuibiwa!"

Ikiwa mtu akidaiwa kumuua mwingine hapa sasa hivi raia watamdhibiti ili afikishwe Polisi. Hili linashindikana vipi kuhusiana na wanaodaiwa kuwa wezi? Lipi kosa kubwa kati ya wizi na mauaji?

Mtu akikutwa anabaka kitoto cha miaka mitatu huwa hauliwi. Anaweza kupigwa kidogo lakini atafikishwa Polisi. Lipi kosa kubwa kati ya kunajisi kitoto na kukuibia wewe hiyo TV yako au godoro?
 
Back
Top Bottom