Nilivyonusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali miaka 15 iliyopita. Tanzania kufariki ni dakika 0 tu!

Nilivyonusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali miaka 15 iliyopita. Tanzania kufariki ni dakika 0 tu!

Ni miaka 15 sasa imepita tangu ninusurike kuuawa na walimwengu. Nilikuwa nikiishi Tabora, na jioni moja, nilikuwa natembea mjini Tabora. Wakati natembea, nikajihisi kubanwa haja ndogo, nikawa nakatiza mtaa wa Salimini. Kwa wale wenyeji wa Tabora, mnafahamu ule mtaa ulivyo wa Kiswahili. Nikawaomba niingie kwenye nyumba moja mtaani hapo ili niombe sehemu ya kujisaidia haja ndogo (chooni).

Nje ya nyumba ile alikuwa amesimama kijana mwenye umri wa miaka 18 au 19, nilimuomba na akanielekeza nipite kwenye korido niende mpaka uwani. Wakati napita kwenye korido, nilikutana na mwanamke na mwanaume wakiwa wanazungumza. Niliwasalimia, na mimi nikaendelea na safari yangu kuelekea uwani. Nilipofika uwani, kabla ya kuingia chooni, nikawa ninakunja suruali yangu mpaka ukaribu na magotini (kawaida yetu Waislamu huwa tunafanya hivi ili utakapokuwa unajisaidia haja ndogo, zile cheche za mikojo zisirukie nguo). Ghafla nilisikia sauti ya mwanamke ikitokea nyuma ikiita "mwiziiiiii, mwiziiiiii."

Ile kugeuka, namuona yule mwanamke niliemuona kwenye korido anakuja mbio huku akakamata kuni. Akaanza kunipiga na ule ukuni sehemu za mabegani huku mimi nikihangaika kupangua kile kipigo na kujitetea kuwa mimi sio mwizi. Yule mwanamke alipoona ananipiga na ukuni na mimi sianguki, akabeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto ili animwagie usoni. Dah, lahaula! Akatokea yule mwanaume aliyekuwa nae akamuambia "achaaaaa!" Kujinusuru, nilibidi nirukie kwenye korido nitokee mlango wa mbele ili nikimbie (hapa nilifanya kosa kubwa). Nilianza kukimbia barabarani huku yule mwanamke akiendelea kuita "mwiziiii, mwiziiiiii."

Watu wakaanza kunikimbiza. Kadiri nilivyokuwa nakimbia, watu walizidi kuongezeka, huku wengine wakiwa wamebeba mapanga. Niliingiwa na fikra za haraka za kuingia kwenye nyumba ya mtu ili ninusuru maisha yangu. Bahati nzuri, nyumba ile niliyoingia ilikuwa ya mjumbe wa serikali ya mtaa. Alichokifanya yule mjumbe (mwanamke wa makamo) aliniambia niingie nijifiche chumbani na yeye akafunga mlango. Lile kundi la watu wenye mapanga walifika kwenye nyumba ile niliyokuwa nimejificha na wakaanza kumlazimisha yule mjumbe anitoe nje huku wakiimba "tunamtaka mwizi weeetúu."

Yule mjumbe alisimama mlangoni na kuwaambia wale watu, "Simtoi nje huyu kijana, ila nitakachofanya, napiga simu polisi waje wamchukue, mtamkuta kituoni." Hii ndiyo ilikuwa salama yangu. Haikupita masaa mawili, walikuja polisi na kunichukua kwenye gari lao. Polisi mmoja alinipiga vibao huku akisema, "Kumbe jamaa mwenyewe mrembo!" (Mimi nina asili ya ushombe shombe kwa mbali).

Nilipofikishwa kituoni, nilijieleza kwa ufasaha na pia nikatoa vitambulisho vyangu ili viwe ni uthibitisho wa kile nilichokizungumza. Bahati nzuri, mfukoni nilikuwa na shilingi laki moja, nikatoa 30,000/- nikawapa wale askari, wakawa wameniachia niende nyumbani usiku ule na kesho yake niende kuripoti. Kesho yake niliripoti polisi, na askari walinikabidhi vitambulisho na kuniambia hakuna kesi. Nikaendelea na majukumu yangu.
Pole sana mrembo 😂😂
 
Iliwahi kutokea kule songea, Kuna jamaa alikuwa anasafiri kwenda kuanza kazi ya ualimu maana alikuwa ni ajira mpya, akaingia duka la wakala mmoja kutoa pesa mara paap yule dada akaanza kupiga makelele
"Uwiiiiiiiii' mwiziiiiiiiiii


Watu wakatokea, jamaa akajaribu kukimbia akapigwa bonge la ngwara wakati anataka kujaribu kuinuka Akala ngumi ya USO duuuh sio POA pale pale wakamtupia matairi wakamchoma moto!!

Daaah ilihuzunisha mnooo!![emoji17][emoji17][emoji17][emoji17][emoji17][emoji17][emoji17][emoji17] Mzazi wake hakuamini mwane ndo basi Tena
Wanawake uwa wanakurupuka sana, hapo anawezakua alimfananisha tu
 
Mimi Kuna siku nilikuwa msibani sehemu Fulani hapa Dar es salaam,Sasa nilibanwa na haja ndogo na hiyo sehemu kulikuwa Kuna kajumba kimuonekano ni kama bafu la kuogea Nikawa nawaza niende kumbe Ile ni nyumba ya mtu.Yaani Bahati nzuri kabla ya Mimi kutaka niingie mwenye nyumba akawa ameingia na kutoa kiti kidogo.Siku hiyo siwezi kuisahau maana ningeingia ningeonekana kama naenda kuiba.Nyumba za watu wa dar ni kiboko
 
Mimi Kuna siku nilikuwa msibani sehemu Fulani hapa Dar es salaam,Sasa nilibanwa na haja ndogo na hiyo sehemu kulikuwa Kuna kajumba kimuonekano ni kama bafu la kuogea Nikawa nawaza niende kumbe Ile ni nyumba ya mtu.Yaani Bahati nzuri kabla ya Mimi kutaka niingie mwenye nyumba akawa ameingia na kutoa kiti kidogo.Siku hiyo siwezi kuisahau maana ningeingia ningeonekana kama naenda kuiba.Nyumba za watu wa dar ni kiboko
Na Masikini tulivyo na hasira ulikua unaisha mzee
 
Asilimia 90 ya wabongo ni wapumbavu mno linapokuja swala la kushughulikia wanaotajwa kuwa wezi. Unakuta mtu ameitiwa mwizi, mtu haulizi anaokota jiwe anamrushia. Ni upumbavu wa hali ya juu.

Kuna rafiki yangu mmoja aliuawa pamoja na mdogo wake kwa kuitiwa wezi baada ya kugombana na mtu ambaye aliamua kuwaitia wezi. Wameuawa na baadae ikaja kufahamika hawakuwa wezi.

Yupo mwingine nilisoma nae aliitiwa mwizi kwa sababu ya wivu wa mapenzi. Akauawa.

Watu waache tabia ya kujichukulia sheria mkononi. Ukisema hii linakuja pumbavu eti "Wewe hujawahi kuibiwa!"

Ikiwa mtu akidaiwa kumuua mwingine hapa sasa hivi raia watamdhibiti ili afikishwe Polisi. Hili linashindikana vipi kuhusiana na wanaodaiwa kuwa wezi? Lipi kosa kubwa kati ya wizi na mauaji?

Mtu akikutwa anabaka kitoto cha miaka mitatu huwa hauliwi. Anaweza kupigwa kidogo lakini atafikishwa Polisi. Lipi kosa kubwa kati ya kunajisi kitoto na kukuibia wewe hiyo TV yako au godoro?
Nashkuru Mungu kwenye maisha yangu yote sijawahi kupiga mwizi na sintowahi kamwe.

Siyo kila anaeitiwa mwizi ni mwizi.
 
Mungu ashukuriwe sana kwa kukulinda na kukuokoa...
Kama bado hujaenda kumshukuru yule mama mjumbe na kumpelekea zawadi walau pea ya Kitenge utakuwa umechelewa Ila fanya hivyo. Huyo ndiye Mungu alimpa kibali cha kukuokoa....
 
Back
Top Bottom