Nilivyonusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali miaka 15 iliyopita. Tanzania kufariki ni dakika 0 tu!

Halafu bado watu wanaunga mkono ujinga wa mob justice (wananchi "wenye hasira" kujichukulia sheria mkononi).
 
Hiyo ndio serikali ya CCM mkuu .
According to ChatGpt... Serikali iliyojishindwa.👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

Hili ni swali zito na lina mizizi mirefu katika historia, siasa, uchumi, na jamii kwa ujumla. Kuna sababu nyingi zinazoweza kueleza kwa nini, licha ya kuwa madarakani kwa muda mrefu, chama kama CCM hakijafanikiwa kutengeneza maisha bora kwa kila Mtanzania. Baadhi ya sababu kuu ni hizi:


1. Mfumo wa Kisiasa na Uongozi


  • CCM imekuwa madarakani tangu uhuru, lakini utawala wake umepitia vipindi tofauti vya mafanikio na changamoto.
  • Kukosekana kwa upinzani wenye nguvu kwa muda mrefu kumechangia baadhi ya matatizo, kwani ushindani mdogo wa kisiasa unaweza kupunguza uwajibikaji.
  • Rushwa na matumizi mabaya ya madaraka yamekuwa changamoto, yakifanya rasilimali kutumiwa visivyo badala ya kuwanufaisha wananchi wote.

2. Mfumo wa Uchumi


  • Tanzania imepiga hatua katika uchumi, lakini ukuaji huo haujawanufaisha watu wote kwa usawa.
  • Sekta nyingi bado zinategemea uchumi wa kijamaa, kilimo cha kujikimu, na kazi zisizo rasmi, ambazo haziwapi wananchi kipato cha kutosha.
  • Sera za uwekezaji na viwanda zimechelewa kuleta maendeleo ya moja kwa moja kwa wananchi wa kawaida.

3. Miundombinu na Huduma za Jamii


  • Elimu, afya, na miundombinu zimeboreshwa, lakini bado hazijafikia viwango vinavyoweza kusaidia kila mtu kuinuka kiuchumi.
  • Kero kama umeme, maji safi, na barabara bora bado ni changamoto kwa maeneo mengi.

4. Mfumo wa Kijamii na Dhana ya "Tatizo la Mtu Mweusi"


  • Tatizo si mtu mweusi kama rangi, bali ni mifumo ya kijamii, utawala, na historia ya ukoloni iliyoweka mazingira magumu kwa maendeleo ya bara la Afrika kwa ujumla.
  • Nchi nyingi za Afrika zilianza na changamoto kubwa za ukosefu wa rasilimali, elimu, na mifumo ya kiutawala baada ya ukoloni.
  • Kutojitegemea kiuchumi (kwa mfano, utegemezi wa misaada kutoka nje) kumezuia maendeleo ya haraka.
  • Mfumo wa fikra—kama vile kukubali hali duni badala ya kudai mabadiliko—pia unachangia.

Kwa kifupi, tatizo si CCM pekee wala mtu mweusi peke yake, bali ni mfumo mzima wa utawala, uchumi, na kijamii. Lakini kuna matumaini—kwa sababu mabadiliko yanawezekana kupitia elimu, uwajibikaji wa viongozi, na mshikamano wa wananchi kudai maendeleo bora.


Wewe unadhani nini kingeweza kufanyika ili hali ibadilike?
 
Kufumua mfumo mzima wa kiuongozi.......nchi imekuwa ni shamba la bibi
 
Reactions: rr4
Huyo mama ningemtafuta tu aisee

Halafu sijaelewa kidogo hapo kwamba yule wa nje aliyeita "mwizi" ni yule aliyekuonesha choo au?
 
Iliwahi kutokea kule songea, Kuna jamaa alikuwa anasafiri kwenda kuanza kazi ya ualimu maana alikuwa ni ajira mpya, akaingia duka la wakala mmoja kutoa pesa mara paap yule dada akaanza kupiga makelele
"Uwiiiiiiiii' mwiziiiiiiiiii


Watu wakatokea, jamaa akajaribu kukimbia akapigwa bonge la ngwara wakati anataka kujaribu kuinuka Akala ngumi ya USO duuuh sio POA pale pale wakamtupia matairi wakamchoma moto!!

Daaah ilihuzunisha mnooo!!😔😔😔😔😔😔😔😔 Mzazi wake hakuamini mwane ndo basi Tena
 
dah pole sana aise,
kumbe JF ingekua imekosa mdau asie na hatia kwa ukuni,

hadi nimekumbuka ngoma moja sijui ni ya msanii gani yule, inasema,

wanaokwenra jela sio wote wenye hatia🐒
 
Pole mkuu ,huu mtaa upo upande gani mkuu kama watokea Kambarage mkuu
 
Pole mkuu ,huu mtaa upo upande gani mkuu kama watokea Kambarage mkuu
Kama unatokea mtaa wa chemchem unanyoosha na barabara ya lami , mtaanza unaoanza kabla ya kufika barabara inayoelekea kituo Cha Afya ( town clinic) Huo mtaa ndio salimini yenyewe Kuna nyumba nyingi za udongo zimepangana na kwa yule mjumbe wa serikali ya mtaa ni nyuma ya Huo mtaa wa salimini ulizia sehemu inaitwa "kiumeni " zamani kulikuwa na( pool table) napo Kuna nyumba kama mbili tatu za udongo zimepangana. Mtaa unaofuata kwa nyuma yake unaitwa mwanza road. Ndio barabara kuu ya kuelekea malolo hospital.........
 
Chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…