mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Miaka ya tisini na mwanzoni nwa miaka ya 2000 kulikuwa na wimbi la vijana kuzamia South Africa,Ulaya au Marekani.
Zilitumika njia zote haramu na halali ikiwemo kuzamia meli mpaka bendi ya Orchestra Vijana Jazz wakatunga wimbo wa Ngapulila.Hemed Maneti na Eddy Sheggy waliimba si mchezo RIP
Mtaani kwetu Chole Road Oyterbay tukiishi na vijana kama akina Tonny na huyu Gentamycin wa jf ,karibu kila nyumba ilikuwa na kijana yuko nje ya nchi.msimchukulie poa Genta,yupo Newsroom kwenye Media House moja kubwa hapa bongo
Kulikuwa na watu wakifanya udalali na michongo ya kupeleka watu nje ,enzi hizo tukiwaita wasanii, kijiwe chao maarufu kilikuwa Shaaban Robert Street ulipojengwa ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere. Na kijiwe kingine kilikuwa Salamanda Cafe kulikuwa na mgahawa unajaza mabaharia ambao meli zao zimetia nanga bandarini,Salamander sasa ndio kuna ofisi za GSM
Mwaka 2001 nikasema liwalo na liwe lazima niondoke nchini, nikamshirikisha mzee akakataa, hapo nina vyeti vangu vya form six na division two ila nilikosa admission ya UDSM kwa kozi ya sheria baada ya kufeli mtihani wa multiculation, wazee wenzangu akina pascal Mayalla wanaukumbuka huu.
Enzi hizo hata kama una division one huwezi kujoin UDSM bila kufanya huu mtihani wa multiculation, na ukiufeli imekula kwako. Ovyo kabisa sijui profesa Luhanga aliwaza nini, kipindi hicho hakuna bodi ya mkopo, ukipata admission ni kama unasomeshwa bure na serikali bila deni
Nilikataa kusoma Tumaini University na vyuo vingine
maana enzi hizo ukitamka neno Chuo Kikuu akili yako inakupeleka UDSM, niliona ndio chuo pekee ninachostahili kusomo, akili ya utoto ilinisumbua.
Nikaona hapa lazima nikasome nje ya nchi,
Mzee akikuwa amenitafutia tempo kwenye ofisi moja huko Posta, ni nikajuana na hawa wasanii, madakali wa kupeleka watu nje.
Hiyo tempo ilikuwa inanilipa sana kwa hiyo michongo yote nilijigharamia, Chuo kikatafutwa, bank statement ikatafutwa ya mchongo, admission letter na form muhimu sana ikiitwa I-20.nikafanya na mitihani ya TOEFL nikapata marks nzuri tu
Nikapewa twisheni ya maswali yanayoulizwa ubalozini.kipindi hicho ubalozi wa USA uko Kinondoni huko ndani ndani karibu na nyumba ya Reginald Mengi
Siku moja kabla ya kwenda ubalozini yule msanii akaniambia tukutane Mwananyamala niende na kiasi cha shilingi 20,000. Sikujua kazi yake ila nikaitikia wito
Kwa mara ya kwanza nikakutanishwa na mganga uso kwa uso eti ana dawa ya kuwapumbaza maofisa wa Ubalozi wa Marekani wasininyime viza. Nikagoma ila msanii akaniambia shauri yako ukikosa viza usinilaumu, unadhani Ulaya watu wanaenda kizembe nikakumbuka gharama nilizotumia kwa shingo upande nikakubali kuoshwa, kesho yake nikaenda ubalozini kuomba viza.
Kama Mungu maswali yote nilikuwa na majibu yake na document zilikuwa zimekamilika nikagongewa viza yangu safiii.
Ikumbukwe hapo mzee hafahamu kitu kuhusu huu mchongo,
Sasa kule USA kulikuwa na rafiki yangu akiishi New York maarufu kama Mudy White mtoto wa Sinza alitangulia kwenda kule mwaka mmoja kabla, tulikuwa tukiwasiliana kwa email na simu, akaniahidi kuwa atanipokea na akanipa address ya nitakapomkuta.
Ikumbukwe sikuwa na school fees ila nilitegemea nikifika kule nibebe box then nipate ada nijisomeshe.
Kufupisha story,siku ya siku nikatua uwanja wa John F Kennedy ambao upo New York, Nikampigia simu jamaa akasema panda MTA au Metro kama wanavyoyaita ni kama mabadsi yetu ya mwendokasi,jamaa akaniambia nipande hayo mpaka Queensbridge nitamkuta,huyo mbiombio nikapanda, nikafika eneo la tukio piga simu weeee kwenye call box simu haipokelewi, giza likaingia nikaambaa ambaa Jamaica Avenue nikalala kwenye kibaraza cha duka
Mfukoni nina dola pungufu ya 50,ambazo kwa USA ni kama huna kitu, tena ukiwa mgeni na huna pa kulala.nimelala sana nje kama homeless.
nikaingia mtaani nikajichanganya kwa kufanya vibarua vya hapa na pale nikazoea mazingira nikawa mwenyeji huku nikiwa homeless kwa miezi kadhaa
Nikapata demu wa kizungu
Nikapata sehemu ya kuishi
nikazaa nae watoto wawili, chuo sikusoma, kuna siku akanitukana ngumi zikapigwa
Mi nilikuwa namnasa makofi tu.
Haikuwa mara ya kwanza kudundana
akapiga simu polisi msobe msobe nikalala selo .
Ikagundulika mimi nina student visa ila sisomi,sijui yule mama alinichongeaje.mara paa nikatunukiwa prohibited Immigrant PI,ofcoz nilikuwa na makandokando mengine
Nilirudi bongo na mapumbu yangu tu na picha nilizopiga nikiwa USA
Namshukuru muddy white alinifundisha kupambana huenda angenipokea ningebweteka
Nilikataa kusoma Tumaini University ila kwa sasa sina degree sina mke,nabangaiza tu mjini na umri umekwenda ila nafurahia maisha