Niliwaambia wazazi wasubiri niweke mambo yakae sawa wakanigomea, sasa naona yakitimia

Hauna busara wala hofu ya Mungu, ninaamini hata wazazi wake wanakuona wewe ni mjuaji, mkaidi n.k

Rudi kwa wazazi wako kama wadau walivyokushauri hapo juu, ni dhahiri pande zote mbili zinaona una shida, ni rahisi upande wa mwanamke kufanya mazungumzo na wazazi wako kuliko wewe sababu umeshajitia doa.

Jaribu kuheshimu wazazi kile wanachokwambia, Mungu akusaidie usije ukapata mtoto asiyekusikiliza na asiyejikita ktk imani kama wewe.
 
Kaa kiume wewe usiwape nafasi watu wakuendeshe, utajiingiza kwenye utumwa so fanya hivi
1. Nenda hiyo tarehe na washenga toa posa
2. Kama watakutajia mahari lipa ulicho nacho mfano wakakutajia milion 4 na wewe unayo 1m wape hiyo wakiikataa ondoka nayo na usiwe mbishi wala king'ang'anizi
3. Wakikutoza faini ya kumtia mimba wape wala usibishane nao
4. Wanaweza fanya mambo yao ya send off nk hayakuhusu
5. Ndoa simple ya Bomani na hafla ndogo ya wanafamilia inatosha sio lazima ufanye bonge la harusi
6. Wadhibiti wasivuke mipaka yao hiyo ni familia yako isiingiliwe kwa maushauri nk
7. Mke awe upande wako hataki akaishi na hao wengine anaowasikiliza.
8. Wakwe wakusikilize na wathamini na kuheshimu nia yako ya kuoa kwao wakileta madharau na ujuaji piga chini oa kwingine
9. Usiweke vikao wala mlolongo, wazazi wako na wakwe wafate plan yako hawataki wakae pembeni
Yah, hapo lazima aipange familia yake aende tu hiyo tarehe, kuna makosa alishayafanya na ndo yamezaa yote haya.
 
Jamaa hajalazimishwa bali yeye kalazimisha kuishi na mtoto wa watu mpaka kumpa mimba. Ukute huko watawahi ili ajifungulie ndoani na Binti kaishi na jamaa anaufahamu uchumi wake hivyo katoa ramani nzima kwa ndugu zake,na majigambo ya hapa na pale ile kujitapa wakaona kibopa wamepata. Cha msingi mleta mada aongee na wazazi wake na washenga wao watamuelewa
Hehe... sawa.
 
Tuma mshenga wakazungumze uone kama watabadili msimamo wakikataa tulia watakutafuta
 
Fuata busara za wazee wako boss.

Binti hukuwa umemuoa ila ukajipa umuhimu mpaka unamgomea mzee wake binti ni lini aende kwao.
Hauna discpline kabisa mkuu, 0nadhani ni kwasababu ya kutokuwa na hofu ya MUNGU hivyo hata wazazi unawachukulia poa. Kuna koo huwezi fanya hichi kitu, wazee wanakwambia hatumtambui huyo binti ni wako.
Yaah sure ni dharau.

Kwa wanyabi hua tunaishi nao kigumu bila pande zote kujua. Ila hii ya kua pande zote zinajua na wewe hutaki kwenda kwao kwasababu unazojua wewe ni dharau kwa familia ya mwanamke.

Jitahidi ukutane na wazee wako muliweke sawa, ila chonde usiumize uchumi wako.
 
Ushauri murua kabisa huu.
 
Nilijipanga kwa mwezi wa 3/4 itakapoangukia pasaka kwasababu january hii hela hamna lakini pia ni ngumu hata kumualika mtu akakuelewa.
Ni kweli... Kaa nao uwaeleweshe.. After all yanabaki kuwa maamuzi yako, mtu asikupangie.
 
Ulizingua ulivyomgomea binti kwenda kwao na hutambuliki kitaratibu, hayo mengineyo waachie wazee na mshenga watayaweka sawa ila jiandae mfuko usiwe mtupu.
Swali je huyo binti umemkuta bikra?
Kama jibu ni ndio basi mwamba anatakiwa kabla ya tarehe 15 aende wasikilizane na sio kulipia
Unalipia mtu ili aje akutwishe mizigo ya maisha yake yote??
Mimi ninapingana na hizi hoja za kuwalipia mahari mabinti zetu..
Kwasababu wao wenyewe wamekuwa hawatabiriki yaani hawajali gharama tunazowatolea zaidi wanadhani eti kisa wana kitobo tu wanastahili kulipiwa
Hawajui kama vigezo na masharti vinatakiwa kuzingatiwa..
 
Kwahyo kama hakumkuta bikra amuache?
 
Habarini wana jukwaa.

Mwanzoni mwa mwaka jana (December 2024) wazazi wangu walinishauri tutume wawakilishi waende nyumbani kwa wazazi wa mchumba wangu kwaajili ya utambulisho.

Japokua Binti nilishaanza kuishi naye kwa zaidi ya miezi mitatu, ilihali tulishakaa kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka minne.

Niliwataarifu wazazi kwamba wasubirie kwanza mpaka nitakapoweka mambo sawa ndipo nitawaambia ili tuanze taratibu zote mpaka NDOA.

Binafsi mimi sio mfuasi wa DINI kwahiyo swala la ndoa nilipanga kufunga naye ndoa ya KIMAHAKAMA (Japokua hili sikuwashirikisha wazazi kwasababu ni wafuasi sana wa Dini) na pia sikupanga tarehe, mwezi au mwaka (Nilitegemea akishajifungua ndipo nitaanza kuweka taratibu za tarehe na mwezi wa tukio hilo)

Wazazi walikazania sana hilo swala pasipo kunisikiliza, ikafika mpaka hatua wakasema kama unahofia gharama basi sisi tutagharamia…. Ikabidi niwe mpole.

Wakapanga tarehe, wakapanga watu wa kwenda kisha wakanitaarifu nikatoa baadhi ya fedha kwaajili ya ku sapoti shughuli kisha watu wakaenda.

Walipewa tarehe ya mwisho wa mwaka ndipo wapeleke baadhi ya mahitaji mengine/fedha kiandaliwe chakula kwa pamoja ili ndugu zake na wakwangu waweze kufahamiana.

(KULIKUA NA CHANGAMOTO ZA HAPA NA PALE KUTOKANA NA KUTOKUFIKA KWA TAARIFA KUTOKANA NA CHANGAMOTO YA FAMILIA YAO)

Tulijadiliana na wazazi na mwisho wa mwaka ulishindikana kutokana na ratiba zilizokuwepo kwa upande wa ukoo wangu mwisho wa mwaka.

Juzi kabla ya Christmas aliniambia ameitwa kwao na baba yake kwaajili ya kikao, nikamkatalia akalalamika mpaka kufikia stage ya kulia.

Tarehe 28 walipiga simu kwetu kudai kwamba wanamhitaji binti yao kwaajili ya mazungumzo, wazazi wakanipigia nikawambia hawezi safiri mwenyewe kwasababu pia ni MJAMZITO na kama week mbili zilizopita aliumwa na kulazwa mpaka mimba ikatishia kutosha, akahudumiwa na kushauriwa apate muda wa kutosha wa kupumzika.

Baba yake akataka namba yangu azungumze na mimi nikamwambia binti asimpe, baadae nikawasiliana na wazazi wangu nikaona isiwe shida, jioni yake nilimwambia awasiliane na rafiki yake kisha nitawapeleka… kweli alifanya hivyo na rafiki yake alikubali.

Jioni ilifika nikawapeleka japokua sikuwafikisha nyumbani kwao kabisa, nikawakodishia usafiri mwingine then mimi nikaendelea na safari ya kuelekea migombani. (KILIMANJARO)

(HII SAFARI YA KWENDA KWETU ILIKUA NIMEPENGA KWENDA NAE ILI PIA AKAJUMUIKE NA NDUGU ZANGU)

Mwaka mpya ukafika na safari yangu ya kurudi ilikaribia, nikampigia simu usiku wa tarehe moja kumuuliza kama kesho yake tarehe mbili asubuhi atakua tayari ili nimpitie turudi wote nyumbani akaniambia kuna maongezi wanamalizia then yeye atakuja jioni yake/kesho yake asubuhi tarehe 2 nikaona sio shida kwasababu bado kuna ndugu zangu bado walikuwepo migombani so ingekua rahisi kumpa lift kupunguza changamoto za public transport lakini haikua hivyo kutokana na sababu alizoleta za hapa na pale

Leo asubuhi nimeamka najiandaa na harakati za siku napokea simu nyumbani kwamba upande wa mwanamke wamekaa na wametupa tarehe 15/01 kwamba ndio tarehe ya hilo tukio kwahiyo tunapaswa tutume kiasi cha fedha kwaajili ya maandalizi ya hiyo siku.

Kila nikiangalia nafasi ya hiyo tarehe kwa upande wangu na wazazi wangu inakosekana, lakini pia January ni mwezi mgumu karibia kwa kila mtu.

Nawaza ku abort mission lakini in a good way, nachomokaje kwenye hili wakuu… kwasababu tokea mwanzo nilikua namkataza mwenzangu asiende nikitegemea yote haya lazima yatatokea.

Lakini pia wazazi wangu wamechangia yote haya kwasababu nilishawaonya tokea mwanzo lakini walikataa kunisikiliza.
Mbona hii match unaamua wew na ndugu zako, maana mke wako ni mjamzito,huna haja ya kuwanyenyekea wakwe zako,maana wao ndo wamezingua
 
Tatizo ni kwamba nimeshtukizwa kwa kitu ambacho nilishakiona kitakuja tokea baadae, naona dalili za kutengeneza single mother bila kupenda.
Duu kumbe sheikhe na vitu vya maandalizi ukweni,unaenda toa wewe,je ni kabila gani hilo sheikhe lenye tamaduni hizo ,mahali ukatoe,faini ya kumtia mimba mtoto wao au kuish nae ukapigwe na bado na gharama za mpunga ukazichangie duu?
 
Habarini wana jukwaa.

Mwanzoni mwa mwaka jana (December 2024) wazazi wangu walinishauri tutume wawakilishi waende nyumbani kwa wazazi wa mchumba wangu kwaajili ya utambulisho.

Japokua Binti nilishaanza kuishi naye kwa zaidi ya miezi mitatu, ilihali tulishakaa kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka minne.

Niliwataarifu wazazi kwamba wasubirie kwanza mpaka nitakapoweka mambo sawa ndipo nitawaambia ili tuanze taratibu zote mpaka NDOA.

Binafsi mimi sio mfuasi wa DINI kwahiyo swala la ndoa nilipanga kufunga naye ndoa ya KIMAHAKAMA (Japokua hili sikuwashirikisha wazazi kwasababu ni wafuasi sana wa Dini) na pia sikupanga tarehe, mwezi au mwaka (Nilitegemea akishajifungua ndipo nitaanza kuweka taratibu za tarehe na mwezi wa tukio hilo)

Wazazi walikazania sana hilo swala pasipo kunisikiliza, ikafika mpaka hatua wakasema kama unahofia gharama basi sisi tutagharamia…. Ikabidi niwe mpole.

Wakapanga tarehe, wakapanga watu wa kwenda kisha wakanitaarifu nikatoa baadhi ya fedha kwaajili ya ku sapoti shughuli kisha watu wakaenda.

Walipewa tarehe ya mwisho wa mwaka ndipo wapeleke baadhi ya mahitaji mengine/fedha kiandaliwe chakula kwa pamoja ili ndugu zake na wakwangu waweze kufahamiana.

(KULIKUA NA CHANGAMOTO ZA HAPA NA PALE KUTOKANA NA KUTOKUFIKA KWA TAARIFA KUTOKANA NA CHANGAMOTO YA FAMILIA YAO)

Tulijadiliana na wazazi na mwisho wa mwaka ulishindikana kutokana na ratiba zilizokuwepo kwa upande wa ukoo wangu mwisho wa mwaka.

Juzi kabla ya Christmas aliniambia ameitwa kwao na baba yake kwaajili ya kikao, nikamkatalia akalalamika mpaka kufikia stage ya kulia.

Tarehe 28 walipiga simu kwetu kudai kwamba wanamhitaji binti yao kwaajili ya mazungumzo, wazazi wakanipigia nikawambia hawezi safiri mwenyewe kwasababu pia ni MJAMZITO na kama week mbili zilizopita aliumwa na kulazwa mpaka mimba ikatishia kutosha, akahudumiwa na kushauriwa apate muda wa kutosha wa kupumzika.

Baba yake akataka namba yangu azungumze na mimi nikamwambia binti asimpe, baadae nikawasiliana na wazazi wangu nikaona isiwe shida, jioni yake nilimwambia awasiliane na rafiki yake kisha nitawapeleka… kweli alifanya hivyo na rafiki yake alikubali.

Jioni ilifika nikawapeleka japokua sikuwafikisha nyumbani kwao kabisa, nikawakodishia usafiri mwingine then mimi nikaendelea na safari ya kuelekea migombani. (KILIMANJARO)

(HII SAFARI YA KWENDA KWETU ILIKUA NIMEPENGA KWENDA NAE ILI PIA AKAJUMUIKE NA NDUGU ZANGU)

Mwaka mpya ukafika na safari yangu ya kurudi ilikaribia, nikampigia simu usiku wa tarehe moja kumuuliza kama kesho yake tarehe mbili asubuhi atakua tayari ili nimpitie turudi wote nyumbani akaniambia kuna maongezi wanamalizia then yeye atakuja jioni yake/kesho yake asubuhi tarehe 2 nikaona sio shida kwasababu bado kuna ndugu zangu bado walikuwepo migombani so ingekua rahisi kumpa lift kupunguza changamoto za public transport lakini haikua hivyo kutokana na sababu alizoleta za hapa na pale

Leo asubuhi nimeamka najiandaa na harakati za siku napokea simu nyumbani kwamba upande wa mwanamke wamekaa na wametupa tarehe 15/01 kwamba ndio tarehe ya hilo tukio kwahiyo tunapaswa tutume kiasi cha fedha kwaajili ya maandalizi ya hiyo siku.

Kila nikiangalia nafasi ya hiyo tarehe kwa upande wangu na wazazi wangu inakosekana, lakini pia January ni mwezi mgumu karibia kwa kila mtu.

Nawaza ku abort mission lakini in a good way, nachomokaje kwenye hili wakuu… kwasababu tokea mwanzo nilikua namkataza mwenzangu asiende nikitegemea yote haya lazima yatatokea.

Lakini pia wazazi wangu wamechangia yote haya kwasababu nilishawaonya tokea mwanzo lakini walikataa kunisikiliza.
wazazi wako wanaingiloaje kwenye mambo yako?
 
Kataa ndoa, ndoa ni upotevu wa muda.

Angalia kijana usije ukawehuka ukashindwa hata kufika mjini, ukapata ajali kisa mawazo.

Hao watakuoa wewe usipoangalia, kuwa na msimamo kama umeshamtia KIBENDI vimba tu. Wacha waneng'eneke wakichoka mtoto wao atarudi mjini na hiyo sijui sherehe( upotevu wa rasilimali) itakuja baadae maana wewe kwanza bado huna ECONOMIC FREEDOM( wewe ni apeche alolo).

Kaza hao wakwe ukilegea watakuoa wewe.Simamia misimamo yako wewe ndo unaoa na kutoa mahari, kama wewe ndo unaolewa na kutolewa mahari endele kuwaendekeza hao wakwe.

# kataa ndoa,ndoa ni utapeli!!
 
Fuata busara za wazee wako boss.

Binti hukuwa umemuoa ila ukajipa umuhimu mpaka unamgomea mzee wake binti ni lini aende kwao.
Hauna discpline kabisa mkuu, 0nadhani ni kwasababu ya kutokuwa na hofu ya MUNGU hivyo hata wazazi unawachukulia poa. Kuna koo huwezi fanya hichi kitu, wazee wanakwambia hatumtambui huyo binti ni wako.
We nae hakuna kitu kabisa hapo inshu ni hela sio kuwasikiliza wazazi. Upande wa mke wanatama hela wewe unasema jamaa ana kiburi sasa hata akiwa mpole inatakiwa hela
 
Iliwahi kunikuta Mimi pia hii,

Hapo wazazi wake wamekupiga "sanction", yaani "upati utelezi Tena mpaka ukaonekane officially".

Hapo wanamaanisha,
"Harudi Tena kwako ,mpaka ukaonekane ukweni"

Mtego wao Ni kwamba,
"Ukipuuza mpk akajifungua kwao, Mtoto atakaezaliwa sio Mali Yako"

Pia,
"Ukienda kuonekana ashajifungua, watajipatia pesa kutokana na faini ya uchafuzi"

Hivyo wanamtumia Binti yao Kama "bargaining chip" au "ndoano" kukunasa Wewe unaejifanya kupiga piga chenga SUALA LA KURASIMISHA.
 
Back
Top Bottom