Niliwaonya Simba kuhusu ulinzi wa CEO Barbara mkapuuza, ameshambuliwa Z'bar

Niliwaonya Simba kuhusu ulinzi wa CEO Barbara mkapuuza, ameshambuliwa Z'bar

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Baada ya kina Francis Mhando wa Efm kumfanyia dhihaka Barbra na kumuita pisi kali chombo ya fundi wakihusisha maneno ya mtandaoni kuhusu mkude kusimamishwa kwamba alimtongoza nilianzisha uzi hapa na kulaumu sana wako walionisapoti wako waliodhihaki kama kawaida maana kwa Ta nzania mwanamke ni chombo cha starehe tena wako hadi wanawake walionicheka hapa jamvini na kuona naongea pumba.

Mwishoni nilimaliza ule uzi kuwaomba Simba wampe ulinzi barbara nikasema kuna siku atashikwa makalio na manyonyo hadharani, haya yametokea huko zanzibar sasa subirini tu siku wachambuzi wa utopolo watamuita kahaba malaya wakiwa hewani ndipo mtaamka sasa.

=======


Bosi Simba adai kushambuliwa Z’bar​


Thursday January 14 2021


bosi simbapic

Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez

Summary

Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez juzi usiku alifanyiwa fujo katika Uwanja wa Amani mjini hapa, muda mfupi baada ya timu hiyo kumaliza kufanya mazoezi uwanjani hapo.
Advertisement

By Mwanahiba Richard
More by this Author

Unguja. Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez juzi usiku alifanyiwa fujo katika Uwanja wa Amani mjini hapa, muda mfupi baada ya timu hiyo kumaliza kufanya mazoezi uwanjani hapo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Barbara alisema alifanyiwa fujo wakati akiswali swala ya Ishah saa mbili usiku katika uwanja huo, baada ya timu kuondoka.

“Wakati naswali walikuja watu wakaanza kunivuta, kunipiga na kuvuta mtandio wangu. Waliniumiza sana,” alisema mtendaji huyo aliyehusisha tukio hilo na mchezo wa fainali kati ya Simba na Yanga uliochezwa jana usiku.

Alisema baada ya tukio hilo aliripoti katika Kituo cha Polisi Ng’ambo alikofunguliwa jalada lenye namba NGB/RB 247/2021, ambapo watuhumiwa kadhaa walikamatwa na kuwekwa ndani usiku huohuo. Gazeti hili lilifika katika kituo hicho ambapo polisi walikiri kupokea malalamiko na kufungulia jalada la shambulio la mwili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadhi Juma Haji alisema hana taarifa juu ya tukio hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
huyo Babra asituchoshe atakua kapigana na pisi nyingine ya Mo ambayo ipo zanzibar
Natabiri kwamba muda siyo mrefu mmojawapo wa wale wachambuzi uchwara walio kwenye payroll ya kuitukana simba atamdhalilisha hewani live lakini kwa kuwa uongozi wa simba wa sasa unakosa watu kama kina Hans pope watanyamaza kimya tu ndiyo maana wajinga wanawashika masharubu.
 
subiri dhihaka zije ataitwa malaya muda si mrefu ,ila nilionya nikaambiwa najipendekeza
kwa jinsi chuki ilivyo kubwa kwa simba haswa kwa wachambuzi uchwara wa utopolo waliojaa maredioni tutasikia makubwa sana na ni mfumo dume tu unaosumbua vichwa vya watu
Mkuu una hasira kinyamaaaa yaaani.

Una cheo gani hapo Simba ??
 
natabiri kwamba muda siyo mrefu mmojawapo wa wale wachambuzi uchwara walio kwenye payroll ya kuitukana simba atamdhalilisha hewani live lakini kwa kuwa uongozi wa simba wa sasa unakosa watu kama kina Hans pope watanyamaza kimya tu ndiyo maana wajinga wanawashika masharubu
Unaongea kishabiki sana. Tz hatuna mambo hayo. Manyau fc hasira za kugongwa jana
 
Unaongea kishabiki sana. Tz hatuna mambo hayo. Manyau fc hasira za kugongwa jana
uzi wa mwaka jana december 30 huo ujinga wa jana umetokea wapi hamjachukua mapinduzi tangu 2007 hongereni wala hakuna mwenye hasira..soma habari tukio limetokea juzi kabla ya mechi kareport polisi na namba ya RB iko hapo inahusianaje na penalts za jana?
 
Wachambuzi hasa wa EFM wamekaa kishubwada sana, wanaweza maliza dakika tatu wanajadili umbea tu wakiongozwa na kile kisada sijui kinaitwa Tunu, siku hizi siwasikilizi tena.
 
mkuu ameuandika huu uzi wake kwa jazba sana. Huyu mkuu itakuwa anacho cheo kikubwa pale Simba SC, au labda tu anamkubali kinyama Madam CEO 😅😅😅 Maana si unaona Madam CEO ni chombo chombo, wa mjini wanaita pisi kali
haya nilytarajia nawakumbusha tu simba waweke ulinzi kwa huyo dada ipo siku atadhalilishwa zaidi ha ya hapo au kubakwa kabisa na kuna watu watashangilia kama wewe
 
Sijaelewa yaani huyo Gonzalez alikuwa anaswali?
haruhusiwi kusali mkuu?waislamu si wanaswali popote walipo kama muda umefika na hawezi kwenda msikitini au? I assume ni muislamu sina hakika kwa hilo
 
haya nilytarajia nawakumbusha tu simba waweke ulinzi kwa huyo dada ipo siku atadhalilishwa zaidi ha ya hapo au kubakwa kabisa na kuna watu watashangilia kama wewe
mkuu mie sishangilii na siungi mkono wala kusapoti udhalilishaji wa Wanawake.
Wanawake ni mama zetu, nawapenda sana wanawake yaani sana.
Na ninakemea vikali vitendo vya kidhalilishaji alivyofanyiwa.
By the way, kesi ipo Polisi, acha mamlaka zifanye kazi yao na wahusika wakibainika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
mkuu mie sishangilii na siungi mkono wala kusapoti udhalilishaji wa Wanawake.
Wanawake ni mama zetu, nawapenda sana wanawake yaani sana.
Na ninakemea vikali vitendo vya kidhalilishaji alivyofanyiwa.
By the way, kesi ipo Polisi, acha mamlaka zifanye kazi yao na wahusika wakibainika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi.
sijaingilia popote nimekumbusha uzi nilioweka tarehe 30 december mwaka jana nilwaambia simba wampe ulinzi huyu dada mambo yamebadilika sana huko maredioni kuna makanjanja yana chuki za waziwazi na simba
na huyu dada ana juhudi sana kuna kitu anataku kuki prove kuna watu hawapendi na ule mfumo dume ulio katika jamii na wengine kama kina kigogo 14 wenye chuki zao na Mo dewji mahasira yao yanamuangukia huyu dada
 
haruhusiwi kusali mkuu?waislamu si wanaswali popote walipo kama muda umefika na hawezi kwenda msikitini au?
Unajua mabint wa kiislam wanaoswali hata kama ana makandokando ni ngumu kumkuta kichwa wazi sasa huyu ceo mara umkute anavuta shisha sasa najaribu kuhusianisha na kusali
 
Back
Top Bottom