Niliweka shada za maua kwenye makaburi matano ya watu wangu wa karibu

Niliweka shada za maua kwenye makaburi matano ya watu wangu wa karibu

Sehemu ya Nne:


Amiri aliingia ndani, begi lake liko mkononi mwangu, mume wangu akamwonyesha sehemu ya kufikia, kilikuwa ni chumba cha kwanza kabisa katika korido, baada ya hapo Amiri akashukuru kisha akaingia humo.

Mimi na mume wangu tukaingia chumbani, na si muda bwana huyo akaingia kwenda kuoga, mimi hapo ndo' nikapata wasaa wa kukagua simu yake.

Nilitazama kwenye 'call logs' na pia kwenye 'messages', kwenye call logs nikakuta rekodi za yeye kuongea na mama yake, kama mara nne hivi, na pia kule kwenye ujumbe vilevile. Moja ya ujumbe ulisema: 'nakuja leo kukuona,' na ujumbe mwingine ukasema: 'nakutumia pesa kabla ya jioni kufika'.

Mbali na hizo, hakukuwa na ujumbe mwingine lakini pia hakukuwa na majibu yoyote kutoka upande wa pili. Hili likanifanya niwaze hivi kweli hamna kilichofutwa hapa? Roho yangu ilikataa.

Lakini, hapa ndo' paliniumiza kichwa zaidi, mama yule na mambo ya kusoma na kuchati huku wapi na wapi? Nakumbuka nilipopata kukaa naye nyumbani kwa miezi na miezi, nilikuwa namsaidia kutazama majina kwenye simu yake na nilikuwa namsaidia kutuma ujumbe au kupigia walengwa wake, leo hii imekuaje? Leo hii wa kutumiwa ujumbe na mwanae?

Hapa kweli nachezewa shere.

Nilitunza namba ile ya mama mkwe kichwani, nikatazama 'gallery' picha kadhaa kisha nikarejesha simu ya mwenye nayo pale alipoiacha, namna ileile alivyoacha, alafu nikatulia tuli kwani alikuwa ametoka bafuni, yaani bwana yule alikuwa anaoga kama mkimbizi, kwahiyo ilinilazimu nisitishe oparesheni yangu kwa muda kungoja muda sahihi kwani sikutaka ahisi chochote.

Lakini sijui kama niliweza. Nilihisi kubanwa na donge kubwa kooni, alafu donge hilo halitulii, linanisuguasugua kwa uchungu nashindwa hata kumeza mate, damu yangu inachemka, kifuani nimejawa na bughudha.

Nilimtazama bwana yule akiwa anajifutafuta maji, nikawa namwona kama kiboko hivi na lile tumbo lake. Nilimtazama nikikamgua na kumkosoa, nikimsema na kumnanga humo kifuani mwangu.

Laiti angesikia hata lepe tu la yale yalokuwa yananisibu asingethubutu kulala na mimi kwa amani. Angeenda kulala chumba kingine tena alale na Amiri kabisa.

Alimaliza shughuli yake, akalala fofofo, hata kula hakula, alisema ameshakula njiani, yuko sawa, basi alipojiweka hapo kitandani, hakuchukua kitambo, akaanza kukoroma kama nguruwe mwenye mafua. Hapo ndo' mimi kuchukua simu yangu na yake kumalizia adhma yangu.

Nilitazama na kuwianisha namba ile ya mama kama kweli ni ya mama, nikabaini ni kweli ndiyo. Hakukuwa na kosa lolote lile. Sasa nikabaki na maswali mwenyewe kichwani, inawezekanaje?

Yani inawezekanaje?

Nilitafuta ujumbe wa miamala ili nione kama kweli alituma pesa na alimtumia nani, nikakuta ametuma laki mbili kwenye namba ileile ya mama yake. Siku hiyo nikalala na mawazo nikijitahidi kutegua kitendawili.

Usingizi ulinikomba nikiwa nayajenga maghorofa kichwani.

Kesho yake bwana huyo hakwenda kazini, alibakia nyumbani akirandaranda na kijana Amiri huku na kule akimwonyesha mazingira lakini pia akimpatia maelekezo ya hapa na pale juu ya kitu cha kufanya kwa mifugo ile.

Amiri alikuwa amevalia nguo zilizochoka; kama kawaida shati na suruali ya kitambaa, nguo hazitamaniki na chini ndala zake ni zilezile, zile alizokuja nazo jana yake.

Kijana huyo alikuwa akimsikiza 'boss' wake kwa umakini na adabu zote, alionekana mnyenyekevu sana, angeitikia kwenye kila alichoambiwa kwa sauti ama kutikisa kichwa. Walipomalizana huko nje walikuja ndani kupata chakula, baada ya kumaliza kula kijana yule aliwahi kuvitoa vyombo vyake akaomba asafishe meza.

Nilimwambia: "usijali, Amiri. Hizi kazi za ndani ni za kwangu, wewe uwanja wako ni kule nje, nisikuchoshe sana."

Jambo hilo likaungwa mkono na mume wangu, naye aliongezea akimtaka Amiri afanye kazi kwa nguvu zote, ikimpendeza basi atamwongezea mshahara wake, mshahara wenyewe anaouongelea ni alfu thelathini, fikiria mtu anaacha familia yake kuja kufanya kazi ya alfu thelathini huku mjini, tena anaambiwa akifanya jitihada ataongezewa alfu ishirini iwe hamsini!

Kweli dunia tambala bovu. Nilimwonea huruma kijana yule, na nilimwonea huruma zaidi alipoanza kazi yake, kazi ile haikuwa nyepesi kabisa haswa kwenda kusaka majani ya ng'ombe na toroli ama kwenda kuwachunga, lakini kijana yule hakuonekana kutia huruma, na wala hakua analalamikia majukumu yake, kila mkitazamana ungemwona anatabasamu na kukusalimu kwa kupunga mkono, ungesema huyu ni mtu, huyu ni binadamu wa mfano, lakini kiuhalisia Amiri hakuwa mtu wa kawaida ...

Amiri alikuwa shetani katika mawindo yake!

Basi hazikupita siku nyingi, kule kazini, meneja, bwana Salum, aliniita ofisini mwake, wito nikipewa na mwalimu ninayefundisha naye darasa moja, mwalimu Beatha.

Mwalimu huyo alinifuata nikiwa nipo darasani, akanipa ujumbe huo pasipo hata kunitazama.

"Meneja anakuita." Alisema kwa sauti ya puani kisha akabinua 'lips' na kuyazungusha macho yake, kitendo ambacho nilikifasiri kama dharau, lakini sikujali nikaondoka zangu kuitikia wito, japo niliona jambo lile bwana meneja alikosea, angenijuza tu kwa simu kama ananihitaji na sio kuwapa maneno hawa makurumbembe ambao najua kabisa walikuwa wanaumizwa nalo, walishatoka kuzungumzia yale ya likizo yangu, sasa kinachofuata kitakuwa ni hiki, nilikuwa naufahamu vema mdomo wa mwalimu yule.

Nilifika ofisini nikaonana na meneja, nikamsikiliza maneno yake yote kisha nikarejea kuendelea na majukumu yangu, nilipofika tu mwalimu Beatha alinidaka na kuniuliza ni nini meneja ameniambia, aliniuliza kana kwamba yanamhusu, na nilipomkatalia kusema jambo alisonya akazungusha tena 'mimacho' yake.

Pale nilibaini swala la 'afya ya akili' ni kubwa mno kuliko tunavyoliwazia. Kuna watu unaweza dhani ni wazima kabisa, kwa muonekano wao, lakini kumbe wana viashiria vya utaahira ndani yao.

Nilimchukulia mwanamke yule kama mgonjwa ili niendelee na mambo yangu vema, hapo mbeleni, kwa kupitia walimu wengine, ndipo nilikuja kubaini ya kwamba Beatha alikuwa na mahusiano na meneja Salum. Hivyo kipindi kile alikuwa ananiona kama tishio kwenye mahusiano yake hayo.

Angejua ...

Basi kama nakumbuka vema, katika wiki hiyohiyo ndo' nilikuja kumshika mume wangu na misheni yake alokuwa anafanya nyuma ya mgongo wangu.

Sijui nilipata wapi wazo lile, lakini siku hiyo nilipofika nyumbani na kuonana mume wangu wazo hilo lilinijia na nikajuta hata kwanini hata halikunijia mapema.

Bwana huyo aliingia ndani kubadili kisha akaenda zake nje kukutana na Amiri, alikuwa ameenda huko kutazama mifugo yake akaacha simu yake ndani.

Nilipojihakikishia kuna usalama, nikaichukua simu hiyo na kupiga namba ile ya 'Mama'. Simu ikaita kidogo na kupokelewa;

halo .... halo.

Mimi nimenyamaza kimya.

Halo ... halo ....

Mimi sijaongea kitu.

Halooo ....

Sauti ile haikuwa ya mama ninayemjua mimi, ilikuwa ni sauti ngeni ya mwanamke nisomfahamu. Nilitafakari kama nishawahi kuisikia popote pale, sikufanikiwa.

Nikiwa nimekaa kimya hivyo, mara mwanamke huyo akaropoka:

"Mume wangu, mbona huongei?"

Hapo ndo' moyo wangu ukalipuka. Mume wangu? Sasa nikawa nimethibitisha yale nilokuwa nayawaza kuwa bwana Mgaya ana jambo lake nyuma yangu.

Nilikata simu kisha nikatulia hapo sebuleni kama vile hamna kilichotokea. Kifua kinanibana kana kwamba kinataka kupasuka. Natamani kutabasamu, natamani kulia, yani sijui kipi ni kipi, lipi ni lipi.

Nikawaza, lakini mbona namba zile ni za mama mkwe kabisa? Sasa imekuaje anapokea mwanamke yule tena akimwita bwana Mgaya mume wake?

Kuna mahusiano gani hapo? Kwakweli sikuelewa. Nilitamani nimpigie yule mama lakini ningefanyaje na namba enyewe nlonayo ndo' ile anayopokea yule mwanamke nisomjua?

Sikufanya jambo lolote siku hiyo, nikayabeba kifuani mwangu, lakini nisikudanganye usiku ule nilitamani nimkabe bwana yule usingizini nikamuua.

Kila nilipomtazama akiwa anakoroma, nilipatwa na hasira kali, nilimwona kama ndama kitandani, nilimwomba Mungu usiku ule uishe salama, kweli ukapita, kesho yake mapema nikampigia Zai kumwomba aje nyumbani.

Nilihisi napasuka na yale nilobeba kifuani, nilihitaji mtu wa kumshushia angalau nipate kuhema. Kweli Zai akaja na kuniona tu akabaini siko vema. Nilimwambia yale yote yalonisibu akanionea huruma kweli kweli, lakini alichoniuliza kiliniumiza zaidi, na kilikua kweli kabisa.

Aliniuliza, "lakini, Mage, wewe si humpendi yule bwana? Mbona unaumia hivyo?"

Kwa muda nikajihisi mjinga, nini kinaniliza? Yule bwana mwenye tumbo kama kiboko ama kuna kitu kingine?

Lakini ....

Niliwaza.

Lakini yule ni mume wangu, nilisema pekee na nafsi yangu, yule ndo' alonioa na siwezi nikabadili hilo, ndoa yenyewe ni ya kikristo, sasa nifanye nini kumtia adabu?

Hawezi nifanya kanjere kiasi hiko alafu nami nitulie kama mjinga. Nilingoja Zai aondoke ili nipate kusema na nafsi yangu mwenyewe, nipange mikakati yangu ya ushindi, lakini wakati nayangoja hayo mara kikatokea kioja.

Ghafla nilimwona Zai akibadilika na kubadilika mbele ya macho yangu. Mara anazungusha shingo yake, mara anatoa sauti nisizozielewa, mara anapayuka na kukoroma, mara anayabidua macho kama jini, yani alimradi tafarani tafarani!

Kumbe bibie yule alikuwa amepandwa na mashetani. Aisee. Kaa tu kuyasikia haya mambo. Nilichanganyikiwa nisijue cha kufanya. Nilipagawa na kila jambo, kile hakishikiki na wala hiki hakikamatiki.

Ni hapo baadae ndo' nilikuja kukumbuka kuna mtu anaitwa Amiri, basi nikaona nifanye upesi kumwita aje kunisaidia na sakata lile. Lakini nilipopaza tu sauti kuita ikawa ndo' kama nimeyatibua mambo.

Zai alianza kupiga kelele akisema mtoe huyo jini ... mtoe huyo jini ... Mtoe nitammaliza ... Mtoe nitamuua ... Mtoe anakunywa damu ... Mtoe! Mtoe! Mtoe! ... Mtoeee! Kisha akaunguruma kama simba, alooh!

Jasho lilinichuruza kila kona ya mwili. Nilikimbia kule nje nikaangaza kila kona, Amiri hakuwepo. Niliita lakini sikuitikiwa, kote kimya nimeachwa nihanye na majanga yangu mwenyewe.

Sijakaa sawa, nikasikia mtu kule ndani akipondaponda mlango kwanguvu. Upesi nikakimbia kwenda kutazama, hamaki nikamkuta Zai amesimama koridoni, anaupiga mlango wa Amiri kana kwamba anataka kuusaga apate unga.

Anaupiga mlango huo pasi na huruma. Anaupiga akisema nitakuua ... Nitakuuua ... Nitakumaliza .....








***
 
Nimekaa hapa kuangalia uongo upo wapi katika story hii. Unapotunga uzingatie sana vigezo vya utungaji. Yaani usidanganye sana utaniudh. Mugaka anafahamu habari yangu vizuri na moderators. So nakutahadhalisha uwe makini na utulie sana.

Sadist, una fikra za kupambana tu na kukosoa watu, huo ni ugonjwa, tafuta msaada, kwa watu kama sisi tuna thamani tu mda anaoutumia huyu ndugu kuhadithia kitu cha kuvuta hisia wakati tupo on transit/lay over....
 
Sadist, una fikra za kupambana tu na kukosoa watu, huo ni ugonjwa, tafuta msaada, kwa watu kama sisi tuna thamani tu mda anaoutumia huyu ndugu kuhadithia kitu cha kuvuta hisia wakati tupo on transit/lay over....
Yaani unaamini humu ndo utaondolewa stress zako? Maana umekuja nazo.mhusika hajalalamika na ameonesha kujiamini hadi anaahidi kunitag. Wewe kajamba nani unaleta makasiriko. Hii inatokana na nini?kushindwa kwako unataka kuwahamishia wengine lawama. Why cant you just shove it in your as* and run away😂😂😂😂. Mwenye uzi hana neno. Wewe tu unayaleta hapa makalio yako na kuyapigiza pwaaaah.... Huoni kuwa nimekaa hapa. Hujali na huogopi.
 
Back
Top Bottom