Mkuu kama hutojali ,waweza tusaidia karaman tuone..🙏Natamani ningefanya hivyo ila nilishajibu hapo nyuma, kuna watu wakiiona nyumba watagundua ID yangu, kifupi ni nyumba ya vyumba vitatu, kimoja masta, sitting room imeunganika na dinning room, public toilet na jiko, nyumba ina urefu wa mita 9 na upana wa mita 11
Nilianza ujenzi nikiwa 24 nikamaliza nikiwa 27 aisee nilikuwa napenda nyumba kubwa....nikajenga vyumba vya kujiachia....sebule kubwa ....ila kwa sasa natamani nyumba ndogo
Iko na familiaAnzisha familia nyumba hautaiona kubwa tena
Iko na familia
Imetulia, safi.[emoji16][emoji16] ujenzi mtamu askwambie mtu View attachment 2112975
Ukisevu 250K kwa mwezi, kwa miaka 3 ni only 9 Million. Haitoshi hata msingi wa nyumba ya vyumba 3 na makolombwezo mengine. Labda uwe na chanzo kingine cha pesa. Ila kwa laki tano na nusu kwa mwezi, ukitoa matumizi ya mwezi. Hata miaka 9 bado utakuwa unajenga. Mimi naona kujenga kutegemea mshahara pekee ni ngumu sana, labda mshahara uwe mamilioni kwa mweziNdani ya miaka 3 unaweza Jenga hadi kupaua.Hizo pesa nyingi Sana tena unajibana unasevu 250,000 kwa mwezi,hapo una familia .
Hata mimi kwenye ujenzi, hapo kwenye kupata kiwanja na kupaua ndio palikuwa pagumu zaidi, maana huwezi kufanya nusu nusu. Hatua zinazofuata naamini ni nyepesi kuliko zote kwasababu naweza kufanya nusu nusu, labda kwenye Magrili ya madirisha hapo hapo panahitaji kumaliza yote kwa mara mojaMengine yote rahisi,kigumu kwenye ujenzi ni kuweka hela ipatikane Mara 1 ya kununua kiwanja.
Mkuu plumbing phase one mbona imetumia pesa nyingi sana? Imejumuisha mfumo wa majitaka na ujenzi wa Chemba au?Gharama za kupaua zinakua kubwa sababu zinahotajika kwa mara moja, kwa mfano mimi kupaua pekee nimetumia milion 7, hapo ni hela ya fundi bati na mbao. Ila baada ya kupaua, plumbing phase one ime cost 2M, frame za milango mti wa mpili laki tisa, wiring phase one, laki saba, grill 1.5 M, bado mambo yanaendelea
Binafsi naamini finishing kwangu itakuwa rahisi sana kwasababu naweza kufanya kidogo kidogo kwa kila kituNimejiongelea mimi mkuu kama kwako ipo hivyo ni sawa pia .
wakukujua watakufanyaje mbona watanzania tunaishi kama digidigi...Ningeweka picha ila nahofia watu wa karibu kujua ID yangu siunajua anonymity
Huu ndio ukweli, ni kweli finishing ni very expensive kutegemea na finishing ya aina gani mtu unataka, lkn ni ukweli kuwa nyumba ukishaezeka basi umemaliza ujenzi, hatua zilizobaki utajipimia mwenyewe kulingana na msuli wako. Kupaua ndio hatua ngumu kuliko zote kwakuwa inakutaka uifanye kwa mara moja na vifaa vyake ni vya gharama kubwa sanaNdio mkuu...kulaua ndio gharama kubwa kuliko any other stage. Ukimaliza kupaua nyumba imeisha hiyo...tia kashata madirishani mengine unafanya ukiwa humo ndani
And that is the reality. Finishing ni rahisi sana maana unajipimia kulingana na urefu wa kamba yakoFinishing uzuri wake ni mbwembwe utakazo wewe. Unaweza weka choo cha laki nne au choo cha million tatu...urefu wa mfuko wako tuu
Mimi vyumba vitatu kupaua tu na blandaring bati geji 30 migongo mipana imenipiga 12MKupaua ndio stage ngumu kwasababu utahitaji mbao na mabati kwa wakati mmoja nyumba ya kawaida vyumba vitatu ni 4m na kuendelea. Hicho mnachosema finishing ni stages kadhaa ambazo nyingine unaweza kufanya ukiwa ndani ya Boma kwa hela za reja reja.
Yanateketea mahela hapo kwenye kupaua balaaa.Huu ndio ukweli, ni kweli finishing ni very expensive kutegemea na finishing ya aina gani mtu unataka, lkn ni ukweli kuwa nyumba ukishaezeka basi umemaliza ujenzi, hatua zilizobaki utajipimia mwenyewe kulingana na msuli wako. Kupaua ndio hatua ngumu kuliko zote kwakuwa inakutaka uifanye kwa mara moja na vifaa vyake ni vya gharama kubwa sana
Sio inauma mkuu, bali ni ngumu kupata pesa nyingi kwa mkupuo kwa tulio wengi. Shida ndipo inapoanzia na ndio maana kwa tulio wengi sehemu ngumu kuliko zote kwenye ujenzi ni kupaua, the rest is easy hata kama total cost itakuja kuwa kubwaKutoa hela kwa mkupuo kweli inauma. Lakin ya kidogo kidogo ndio inakuaga nyingi mwisho wa siku.
Siwezi jiroga kujenga ghorofa kama hata nyumba ya kwanza ya kuishi sina! Kujenga ghorofa hela zinateketea halafu huoni hata hatua uliyopigaYanateketea mahela hapo kwenye kupaua balaaa.
Sasa olewe wako ulogae ujenge ghorofa hela zinavyo teketea kwenye kumwaga slab unaweza anza kulia. Mifuko ya cement inamezwa na concrete mixer kama lina pepo vile[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tatizo la UJENZI ukiwasikiliza watu, kila pesa utakayokuwa nayo utaambiwa HAITOSHI.Ukisevu 250K kwa mwezi, kwa miaka 3 ni only 9 Million. Haitoshi hata msingi wa nyumba ya vyumba 3 na makolombwezo mengine. Labda uwe na chanzo kingine cha pesa. Ila kwa laki tano na nusu kwa mwezi, ukitoa matumizi ya mwezi. Hata miaka 9 bado utakuwa unajenga. Mimi naona kujenga kutegemea mshahara pekee ni ngumu sana, labda mshahara uwe mamilioni kwa mwezi
Mkuu nilipofanya plumbing nilikua nishanunua tenk na kujenga mnara hivyo ghrama zilihusisha pia vifaa vya tenk kama nilivyosema, ni nyumba ya kwanza, vifaa vingi nilikua sivijui, hivyo yawezekana upigaji pia umehusika katika hilo, si unajua mafundiMkuu plumbing phase one mbona imetumia pesa nyingi sana? Imejumuisha mfumo wa majitaka na ujenzi wa Chemba au?