Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Siwezi jiroga kujenga ghorofa kama hata nyumba ya kwanza ya kuishi sina! Kujenga ghorofa hela zinateketea halafu huoni hata hatua uliyopiga
Kama ni kuishi usijenge na Wala usijenge nyumba kubwa sana angalau vyumba vitatu basi na sebule jiko labda na stoo ila uwe na eneo kubwa ni vema ili upande miti ufurahi maana siku ukizeeka na familia ikitawanyike nyumba itakupa upweke sana
 
Binafsi naamini sana kuwa na sehemu yako ya kuishi bila bugudha ya kodi wala maudhi ya wapangaji wengine,
Mambo machacho kuhusu mimi
1. Niko under 30
2. Kipato changu ni kati ya 500k - 550 k kwa mwezi

Baada ya kununua kiwanja، nilianza kununua maatofali kidogo kidogo.
Mambo niliojifunza

1. Anza kujenga na ulicho nacho, kwenye fungu ndio kwenye nyongeza, ukishaweka tofali kama kweli unania ya kugenga kichwa kitapata moto, Mungu atakufungulia

2. Msingi wa nyumba ndio kila kitu, nilipoanza kujenga nilikua na bajeti ndogo, ujenzi ulikuaa wa kimasikini kweli, matokeo yake, sasa nyumba imeisha ila msingi uko chini na kuna vitu ningetamani vingekuepo ila ndo nyumba ishamalizika, hili silijutii kwani ni funzo, hata hapa nilipofika sikutegemea kufika.

3. Hata kama fundi unamuamin, ni muhimu sana kuwepo wakati wa ujenzi, kuna makosa mengi ambayo yanaweza kutokea, kusimamia ujenzi sio kwa kuzuia uizi tu bali hapa usahihi wa nyumba unavyotaka iwe. Nyakati muhimu za kuwepo ni wakati wa kuset msingi wa nyumba, wakati wa kufunga mkanda wa nyumba, ukataji wa madirisha na milango, na kufunga lenta makosa mengi yanatokea hapa

4. Ujenzi hauna gharama kamili, kama ulipiga bajeti ya milioni 30, hakikiaha una milioni tano ya extra. Mengi yanatokea, ikiwemo vitu kupanda bei

5. Kuna muda utakua unajua kua fundi amekula hela ila hakuna jinsi, ikiwa hujui vifaa vya plumbing au umeme, chukua bei ya fundi, nenda madukani kaulizie, ukipata tofauti isio kubwa na ukiwa na uhakika wa kuletewa kitu original ambacho wewe unahofu ya kuuziwa fake , basi mpe tu fundi hela ( kwa wasio na uzoefu)

6. Siku unayomaliza kupaua ndio ujenzi unaanza, kati ya vitu ambayo ni kuhimu katika nyumba na vina gharama kubwa ni kama mfumo wa maji, umeme, milango ya mbao na grill, hivi vitu usivichukulie kirahisi kwenye budget, gharama zake hua ni M M tu.

7. Unapotaka jugenga aim for high, nilikua nimeingia mtego wa kutaka kujenga chumba kimoja na sebure, ila nilipoamua kujenga nyumba ya vyumba vitatu niliona kabisa kama ni kitu ambaacho hakiwezekani ila hatimae imewezekana, lesson-- panga kwa kuangalia wewe unakua au unataka kua nani nani na si sasa hivi una hali gani .
Plan besed on who you want to be not who you are, by this utaepuka regret za kujenga kitu ambacho baadaae hukifurahii sana
PCHA YA NYUMBA TUNAOMBA KWA NJE TU
 
Nimenunua 28,000 migongo mipana na Niko site aisee kuwa makini mno na Mungu akuongoze Kuna wakati mafundi wanatupiga
Mimi nimenunua ALAF bati la maxcover Geji 28, mita moja 18320, kwa bati iliokatwa kwa mita 3 roughly ni 55,000 kwa bati moja, kwa nyumba yangu invoice ilikua Mil. 4.5,
 
Mimi nimenunua ALAF bati la maxcover Geji 28, mita moja 18320, kwa bati iliokatwa kwa mita 3 roughly ni 55,000 kwa bati moja, kwa nyumba yangu invoice ilikua Mil. 4.5,
Mi nimepaua hivo mkuu mahesabu mengine ya mita ngapi na ngapi siyajui kwa kweli ila geji ni 28 bati 80 na bei ni 2240000
IMG_20220211_163924_890.jpg
 
Nimenunua 28,000 migongo mipana na Niko site aisee kuwa makini mno na Mungu akuongoze Kuna wakati mafundi wanatupiga
Je ni Original?? maana nimeshughudia nyumba nyingi zuri ila bati ndani ya mwaka zimepauka na kuchuja mwishowe test ya nyumba inapotea kabisa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimejenga dar es salaam mkuu
Hongera sana, maisha ni nyumba[emoji4]

Nilianza ujenzi kama utani. Nilikua na pesa ndogo ila mke alinipa moyo na ndio alisimamia kila kitu.

Sasa uchawi bati ndo unanitoa jasho .. anyway, nitamaliza tu mana nimepaua upande kwanza nikahamia.

Mungu atupe nguvu wapambanaji tutimize malengo
 
Ukisevu 250K kwa mwezi, kwa miaka 3 ni only 9 Million. Haitoshi hata msingi wa nyumba ya vyumba 3 na makolombwezo mengine. Labda uwe na chanzo kingine cha pesa. Ila kwa laki tano na nusu kwa mwezi, ukitoa matumizi ya mwezi. Hata miaka 9 bado utakuwa unajenga. Mimi naona kujenga kutegemea mshahara pekee ni ngumu sana, labda mshahara uwe mamilioni kwa mwezi
Unakopa hela benki
 
Kila kitu hapo,kwetu fundi anapewa 350,000 kujenga msingi wa mawe..

NYie watu wa Dar hamtakaa mumiliki nyumba maana gharama za ujenzi huko ni kubwa Sana..

Wakati mimi nanunua tofari za kuchoma hadi site kwa 120,, wewe block moja kwa bei ya chini ni 1,000 .

Samahani Mkuu, huko kwenu ni wapi? Nahitaji kufanya ulinganifu
 
Inawezekana kwa mikoa ambayo hakuna burnt bricks na udongo wa mfinyanzi ni majanga
Mkuu nyumba hizo za bei nafuu zinawezekana kwa mikoa ambayo wanatumia tofali za kuchoma na kujengea udongo baadala ya saruji. Ukienda Mafinga, ujenzi wa aina hiyo ni kawaida kabisa, gharama zinakuwa kubwa kwenye kupaua tu. Vilevile kwa uzoefu wangu ujenzi kwa baadhi ya mikoa, labour charge zipo chini sana, mtu nyumba nzima kuanzia msingi hadi kukamilisha boma ambalo halijaezekwa anakuambia laki 8. Wakati kwa Dodoma nyumba hiyo hiyo utajenga kwa labor chaji ya 3.5M hadi 4.5M. Mikoani huko, labour chaji ya kupaua unaweza kuta laki tatu tu lkni njoo Dodoma utakuta haipungui 1M
 
Back
Top Bottom