Kunakauli inakatisha tamaa, gharama za kupaua/za bati, zinanitoa damu...ila hapa naona kuwa ukipaua ndio unaanza ujenzi...wtf!!!si bora niache
Kuamua kujenga na kuamua kutokujenga kabisa yote ni maamuzi sahihi, inategemea na kile kinacho kuweka mjini ni nini? I mean nature ya kazi yako, kama unasubiri mshahara, please jenga, kama unafanya biashara and may be hadi watoto na mkeo umewa tune kwenye biashara hadi maisha yao yote hapa duniani then kujenga sio deal kabisa; nitafafanua sababu zote 2.
1. Kwa mtu anaetegemea mshahara ni vizuri uwe na nyumba yako mwenyewe, mambo ya kuajiriwa yana uncertainties nying sana, kuna kufukuzwa kazi, kuna kuacha tu kazi ili utafute kazi nyingine, kuna KUFA na hujaacha urithi kwa wanao na mkeo, kuna kustaafu pia; hapa sasa huna kazi (tuseme Mungu nae hajakuchukua ) unakua busy kutafuta pesa ya chakula na makazi/malazi, may be na watoto wanasoma. Mwanaume unaweza kupata KICHAA, bora utafute pesa ya kula na wanao wapo nyumbani, itakusaidia kuondoka na fedheheha ndogo ndogo hasa za majirani/wapangaji wenzio, au hata ukifa, wanao wanapo mahali pa kivuli. Wanaweza kutukanwa huko mitaani but watarudi nyumbani kwao.
2. Kwa mfanyabiashara wa level ya kati na kubwa, hawa watu kujenga sio deal kiviile, hawa ni watu ambao pesa yao yote inayopitia mikononi mwao ina hesabu, is not ideal kufukia zaidi ya Tsh 50M kwenye ujenzi ilihali hiyo pesa ikizungushwa itazaa pesa zingine zaidi, hawa watu wenyewe ni bora wapange. Kumbuka hawa ni watu ambao hata life style yao iko tofauti na mleta UZI, watoto wanasoma shule za maana, so kiwanja tu kinatakiwa kua sehemu yenye watu wenye status zao, again kwa kua pesa yao yote ina mahesabu then hata nauli za kwenda na kurudi kazini kwao wao wanazihesabu tofauti na mfanyakazi, huyu kukaa mbali sana na sehemu ilipo biashara yake sio poa, angependa kukaa karibu na biashara yake. Ndio Wahindi wanavyo ishi, huwezi kuwasikia wakifiria habari za ujenzi wa nyumba, wameachana na hayo mawazo kabisa. Zamani tulikua tunadhani eti ooh hawa jamaa, huku sio kwao ndio maana hawajengi, but mbona wanafia hapa hapa???