Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Siwezi jiroga kujenga ghorofa kama hata nyumba ya kwanza ya kuishi sina! Kujenga ghorofa hela zinateketea halafu huoni hata hatua uliyopiga
Kama ni kuishi usijenge na Wala usijenge nyumba kubwa sana angalau vyumba vitatu basi na sebule jiko labda na stoo ila uwe na eneo kubwa ni vema ili upande miti ufurahi maana siku ukizeeka na familia ikitawanyike nyumba itakupa upweke sana
 
PCHA YA NYUMBA TUNAOMBA KWA NJE TU
 
Nimenunua 28,000 migongo mipana na Niko site aisee kuwa makini mno na Mungu akuongoze Kuna wakati mafundi wanatupiga
Mimi nimenunua ALAF bati la maxcover Geji 28, mita moja 18320, kwa bati iliokatwa kwa mita 3 roughly ni 55,000 kwa bati moja, kwa nyumba yangu invoice ilikua Mil. 4.5,
 
Nimenunua 28,000 migongo mipana na Niko site aisee kuwa makini mno na Mungu akuongoze Kuna wakati mafundi wanatupiga
Je ni Original?? maana nimeshughudia nyumba nyingi zuri ila bati ndani ya mwaka zimepauka na kuchuja mwishowe test ya nyumba inapotea kabisa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimejenga dar es salaam mkuu
Hongera sana, maisha ni nyumba[emoji4]

Nilianza ujenzi kama utani. Nilikua na pesa ndogo ila mke alinipa moyo na ndio alisimamia kila kitu.

Sasa uchawi bati ndo unanitoa jasho .. anyway, nitamaliza tu mana nimepaua upande kwanza nikahamia.

Mungu atupe nguvu wapambanaji tutimize malengo
 
Unakopa hela benki
 

Samahani Mkuu, huko kwenu ni wapi? Nahitaji kufanya ulinganifu
 
Inawezekana kwa mikoa ambayo hakuna burnt bricks na udongo wa mfinyanzi ni majanga
Mkuu nyumba hizo za bei nafuu zinawezekana kwa mikoa ambayo wanatumia tofali za kuchoma na kujengea udongo baadala ya saruji. Ukienda Mafinga, ujenzi wa aina hiyo ni kawaida kabisa, gharama zinakuwa kubwa kwenye kupaua tu. Vilevile kwa uzoefu wangu ujenzi kwa baadhi ya mikoa, labour charge zipo chini sana, mtu nyumba nzima kuanzia msingi hadi kukamilisha boma ambalo halijaezekwa anakuambia laki 8. Wakati kwa Dodoma nyumba hiyo hiyo utajenga kwa labor chaji ya 3.5M hadi 4.5M. Mikoani huko, labour chaji ya kupaua unaweza kuta laki tatu tu lkni njoo Dodoma utakuta haipungui 1M
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…