Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
- Thread starter
- #181
, Ndio maana kuna Mahakama siku zote , ingekuwa Polisi wanaaminika kwa kila Uchunguzi au upelelezi wao kungekuwa hakuna haja ya Mahakama kupima ushahidi na kila siku Polisi wangekuwa wanashinda kesi , ndio maana kuna Mahakama ,ni muhimu sana Ndugu zangu uhalifu ukapambanwa kwa mujibu wa sheria,kama sheria zetu hazifai kupambana na uhalifu tuzibadili ila sio kuzikeuka kwa kumuuwa na kumpiga Risasi Mtuhumiwa.Zipo sababu zinazopelekea watu kujiingiza kwenye uhalifu mathalani majanga ya Asili e.g. janga la njaa kali/ukame, mtu anaiba ili anusuru maisha yake au ya familia yake. Lakini leo waulizwe hao panya rodi ni nini kinachowasukuma hadi wafanye kama wanavyo fanya??
Najua hawatasema hata kidogo ila ukweli ni kwamba wanatamaa ya maisha ambayo haiwezekani kuyapata, wanavuta bangi,madawa ya kulevya na wanakosa fedha ya kununulia starehe hizo n.k. yaani ni vitu vya kijinga-kijinga. Hawakulelewa vizuri au walikengeuka mawaidha na mafunzo yale waliyofundishwa au maelekezo wanayopata kwa wazazi na kutoka kwa Jamii. Wanadhani ubabe ndio maisha yanaenda.
Wameshupaza shingo. Wao kama wao(Nafsi) binadamu hakuna shida kabisa. Shida iko katika matendo yao. Yaani kile wanachofanya/tenda ndicho hatukubaliani nacho na ndicho kinapigwa vita. Waache au wajiepushe na tabia hii uone kama kuna mtu atawafuata.
Hata hao Panya Road wanaofanya uhalifu sheria zipo wakikutwa na hatia wanaadhibiwa sawa na sheria inavyosema kuna kifungo adhabu ya kifo , kifungu cha maisha ,miaka 30 na adhabu zingine . Kwanini wasishtakiwe kwa mujibu wa sheria wajibu wa Polisi ni kufanya upelelezi na uchunguzi kuisaidia Mahakama kufanya maamuzi sio kuuwa watuhumiwa.
Kama tunaona hakuna haja ya kuchunguza na kushtaki Polisi washinikize sheria zibadilishwe ili iwe rahisi wao kufanya wanachokifanya , hakuna mtu anatetea wahalifu ,ninachotaka utaratibu ufuatwe ktk kupambana na uhalifu na kama sheria zetu ni Butu basi tuzibadili na sio Polisi kuchukua hatua ya kuuwa Watuhumiwa bila kuwapeleka mahakamani.