Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
- Thread starter
- #201
Ndio maana tuna sheria,katiba , kanuni na taratibu zimeweka utaratibu wa namna ya kupambana na uhalifu .Sasa wewe katika kufanya uchunguzi wako huo ulitegemea familia za hao panyaroad wakwambie walikuwa ni wezi? Acha kwanza polisi wafanye kazi yao la sivyo hao vibaka mtawapa nguvu ya kurudi upya maana wanatetewa, huu sio muda muafaka wa kuongea haya.
Ndio maana kuna Mahakama siku zote , ingekuwa Polisi wanaaminika kwa kila Uchunguzi au upelelezi wao kungekuwa hakuna haja ya Mahakama kupima ushahidi na kila siku Polisi wangekuwa wanashinda kesi , ndio maana kuna Mahakama ,ni muhimu sana Ndugu zangu uhalifu ukapambanwa kwa mujibu wa sheria,kama sheria zetu hazifai kupambana na uhalifu tuzibadili ila sio kuzikeuka kwa kumuuwa na kumpiga Risasi Mtuhumiwa.
Hata hao Panya Road wanaofanya uhalifu sheria zipo wakikutwa na hatia wanaadhibiwa sawa na sheria inavyosema kuna kifungo adhabu ya kifo , kifungu cha maisha ,miaka 30 na adhabu zingine . Kwanini wasishtakiwe kwa mujibu wa sheria wajibu wa Polisi ni kufanya upelelezi na uchunguzi kuisaidia Mahakama kufanya maamuzi sio kuuwa watuhumiwa.
Kama tunaona hakuna haja ya kuchunguza na kushtaki Polisi washinikize sheria zibadilishwe ili iwe rahisi wao kufanya wanachokifanya , hakuna mtu anatetea wahalifu ,ninachotaka utaratibu ufuatwe ktk kupambana na uhalifu na kama sheria zetu ni Butu basi tuzibadili na sio Polisi kuchukua hatua ya kuuwa Watuhumiwa bila kuwapeleka mahakamani.