Kuna khudam wa aina nyingi mkuu.
Khudam wa majina ya kijani ndio wana nguvu kuliko majini wowote na ni majini wa koo kuu za kifalme za kijini.
Mkuu kama huyu aswaarul kabiir akitia timu sio kibwengo wala ifrit anabaki hapo,Yani ni ana internal power ya ajabu acha.
Haya bhana ndugu yangu! Ila kuwa nao makini.
Familia yetu ilianza kukumbwa na hiyo mikasa kwa kuwa dada wa baba alitokea kutompenda mama tangu wamefunga ndoa.
Mzee alipofariki mali ziliachwa nyingi. Ukoo ukasema kwa vile ninyi ni wakubwa endelezeni mali za mzee wenu. Aisee! Kumbe Shangazi alichukia kwa sababu hampendi mama. Hapo kisanga kilianzaπππππ
Na kipindi hicho nakaribia kumaliza Chuo kaka zangu walikuwa tayari wameshamaliza.
Kwenye familia yetu peke yangu nimefuata silsila ya mababu zetu kwenye dini: Babu zangu ni sunni madh-heb ya Shafii ila ni ahlu ttwariqa. Na eneo walilokuwa wakiishi tangu karne ya 10 huko inafahimika hivyo!
Binafsi nimefuata mtiririko huo huo! Aisee si unajua watu wa twariqa wana adhkari nyingi sana! Halafu shangazi alituma majini ndani ya nyumba..
Picha linaanza nimelala nimesoma dua kwa ghafla usiku naona kama kuna joto lipo usoni mwangu. Kufungua macho si nikaona kiumbe cheusiii halafu kina macho meupe kinaniangalia kimenisogelea usoni. Halafu ghafla kikarudi nyuma kikapotea.
Kumbe ndugu zangu mchezo walikuwa bado hawajauelewa. Wakahisi nimechanganyikiwa na dini maana muda mwingi nikaanza kuwa nadhikiri. Na ukifika wakati wa kulala nilikuwa silali. Nilikuwa navuta sana nyiradi na kumswalia mtume.
Kwa sababu nisipofanya hivyo nilikuwa silali kwa sababu nilikuwa naona mambo ya ajabu; mara viumbe wembamba sana wamenizunguka wameniweka kati paji lao la uso linaonekana macho tu!
Ilikuwa ukifika chumbani kwangu usiku utanikuta nimekaa kwenye mswala nimejifunika na shuka mwili mzima nimeacha uso tu! Wakajua kama nimedata.
Ila kuna siku usiku walimuona ndani mnyama halafu kwa ghafla alipotea ndipo wakaanza kunielewaππππ