Niliyoyaona baada ya kuita roho za giza kwa kutumia OUJIA board (don't try this at home)

Niliyoyaona baada ya kuita roho za giza kwa kutumia OUJIA board (don't try this at home)

Umekosea kutumia hiyo kitu na sikufundishi. πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

usijaribu Tena siku nyingine kufanya jambo hulijui utaondoka na roho yako. πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Kuogopa ni hali ya kawaida, Lengo lilitimia kwa kuona na kupata uhakika kama inawezekana au La...
Mbona hizo nguvu za giza waweza kuzikuta kila siku maishani kwako. Na zina nguvu.
Tafuta tu watu wasio muamini Mungu, watu waongo, washerati, watu wenye husda, wauaji, wanaotamani nyumba au wake wa watu.
Wako wengi na wana roho mbaya zenye mwili.
Hizo roho zisizo na mwili ni cha mtoto.
Katika yote Alpha na Omega, Mungu wa miungu ni Supreme.
Alikuwepo, Yupo, na yupo milele.
 
Mbona hizo nguvu za giza waweza kuzikuta kila siku maishani kwako. Na zina nguvu.
Tafuta tu watu wasio muamini Mungu, watu waongo, washerati, watu wenye husda, wauaji, wanaotamani nyumba au wake wa watu.
Wako wengi na wana roho mbaya zenye mwili.
Hizo roho zisizo na mwili ni cha mtoto.
Hao ni watu wenye sura za utu na roho za kishetani
 
Kuna aina ya majini wanaitwa Ifrit.

Hawa wana nguvu bhana kuliko jamii nyengine za majini kwa sababu majini yamezidiana uwezo/nguvu.

Hawa wakikuvaa kuwatoa mtiti! Uende kwa mchamungu kweli kweli. Ukienda kwa mbabaishaji wansweza pita nayr naye kimasihara fulani tu mtu akawa kiziwia au kapooza baadhi ya viungo vya mwili.

Kama una makhudam yako yanaweza yakachinjiliwa mbali na Ifriti. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Mbali na hapo kama ukienda kwa waganga wataingia nao mkataba au utapatiwa Pete ya aina fulani ya kuivaa ili umdhibiti. Ukiivua tu unalo!
Kuna khudam wa aina nyingi mkuu.
Khudam wa majina ya kijani ndio wana nguvu kuliko majini wowote na ni majini wa koo kuu za kifalme za kijini.
Mkuu kama huyu aswaarul kabiir akitia timu sio kibwengo wala ifrit anabaki hapo,Yani ni ana internal power ya ajabu acha.
 
You Tube ipo kuanzia season 1 na kuendelea.

Ni show ya muda ila mpaka sasa bado inaendelea. Nilianza kuiangalia 2008 channel ya Sony (DSTV).

Ukitaka kuifaidi kama una smart TV connect kwenye TV and then uiangalie. Ina mpaka masaa mawili (2).
Sawa mkuu sina smart tv ntajaribu kwa simu niichek napenda sana kujifunza vitu vilivyojificha kama hivi ila tu iwe kwa nia njema.
 
Sema hapo walipokuvuta miguu inaonekana wababe sana.!! 😹😹😹
Sasa mimi nataka niwaite niwahoji kuna vitu nataka kujua kutoka kwao
Shauri yako!

Mimi namsaidia ndugu yangu Kosugi kujibu.

Huwa wanatumia mpaka simu (unaweza kudhani ni masihara fulani ila wanatumia). Isipokuwa namba zao hazina mpangilio kama wa kwetu (code zake).

Kuna mwamba alimwambia hivyo hivyo kuwa nataka kukuona! Kaamka usiku ghafla mkojo umembana kufika nje ya mlango wa chumba chake anamuona mtu kasimama kampa mgongo na ana nywele ndefuuu zinaburuzika mpaka chini. Halafu nywele nyeusiii. Jamaa alikimbia!
 
Acha utani kakaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
Kumbe hadi simu wanapiga!?
Aah kudadeki.
 
Mr. Manson

SIku zote unapo taka kufanya jambo lako hasa nguvu za Giza basi iwe siri yako,

nitakupa kanuni ambazo jamii kubwa za Giza ulimwenguni na hatari hutumia kwa mfano FREEMASONRY, BILDERBERG, CABAL, ILLUMINATI, SKULL AND BONES, na kadhalika...

1. Tafuta kwanza maarifa kuhusu ulimwengu wa Giza

2. unatakiwa kuwa msafi kimwili, usinywe pombe, bangi sigara au kilevi chochote

3. Unatakiwa kujua unaita nini katika ulimwengu huo

4. Ongea lugha yako kwa sababu majini Wana uwezo wa kuongea lugha yeyote duniani

5. Hii ndio muhimu hutakiwi kuwa mwoga kwa sababu ukiwa mwoga wanajua na haitakiwi huna Imani wataondoka na roho yako utakufa tu ukifanya masihara kwa sababu hizo ni falme zenye nguvu Sana Sana Sana
kila la kheri mkuu mengine siruhusiwi kabisa kukuambia kwa sababu wewe sio mwanachama.

Sawa master, sijaribu tena huo mchezo
 
Mwanachama wa chama gani?
Mkuu hii ni Siri yangu binafsi kwa sababu nilichaapa kuwa siwezi kutoa Siri.

tafuta maarifa utafunuliwa na kuishi kwa uhuru katika huu ulimwengu utajifunza mambo mengi Sana.
 
Kuna khudam wa aina nyingi mkuu.
Khudam wa majina ya kijani ndio wana nguvu kuliko majini wowote na ni majini wa koo kuu za kifalme za kijini.
Mkuu kama huyu aswaarul kabiir akitia timu sio kibwengo wala ifrit anabaki hapo,Yani ni ana internal power ya ajabu acha.
Haya bhana ndugu yangu! Ila kuwa nao makini.

Familia yetu ilianza kukumbwa na hiyo mikasa kwa kuwa dada wa baba alitokea kutompenda mama tangu wamefunga ndoa.

Mzee alipofariki mali ziliachwa nyingi. Ukoo ukasema kwa vile ninyi ni wakubwa endelezeni mali za mzee wenu. Aisee! Kumbe Shangazi alichukia kwa sababu hampendi mama. Hapo kisanga kilianzaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Na kipindi hicho nakaribia kumaliza Chuo kaka zangu walikuwa tayari wameshamaliza.

Kwenye familia yetu peke yangu nimefuata silsila ya mababu zetu kwenye dini: Babu zangu ni sunni madh-heb ya Shafii ila ni ahlu ttwariqa. Na eneo walilokuwa wakiishi tangu karne ya 10 huko inafahimika hivyo!

Binafsi nimefuata mtiririko huo huo! Aisee si unajua watu wa twariqa wana adhkari nyingi sana! Halafu shangazi alituma majini ndani ya nyumba..

Picha linaanza nimelala nimesoma dua kwa ghafla usiku naona kama kuna joto lipo usoni mwangu. Kufungua macho si nikaona kiumbe cheusiii halafu kina macho meupe kinaniangalia kimenisogelea usoni. Halafu ghafla kikarudi nyuma kikapotea.

Kumbe ndugu zangu mchezo walikuwa bado hawajauelewa. Wakahisi nimechanganyikiwa na dini maana muda mwingi nikaanza kuwa nadhikiri. Na ukifika wakati wa kulala nilikuwa silali. Nilikuwa navuta sana nyiradi na kumswalia mtume.

Kwa sababu nisipofanya hivyo nilikuwa silali kwa sababu nilikuwa naona mambo ya ajabu; mara viumbe wembamba sana wamenizunguka wameniweka kati paji lao la uso linaonekana macho tu!

Ilikuwa ukifika chumbani kwangu usiku utanikuta nimekaa kwenye mswala nimejifunika na shuka mwili mzima nimeacha uso tu! Wakajua kama nimedata.

Ila kuna siku usiku walimuona ndani mnyama halafu kwa ghafla alipotea ndipo wakaanza kunielewaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom