Niliyoyaona baada ya kuita roho za giza kwa kutumia OUJIA board (don't try this at home)

Ungepiga kiluga au kiswahili au maSharti haya ruhusu
 
😹😹😹 Kwani walikufanyaje mbona husemi??
Halafu sio mbali ni mwaka huu tu mwanzoni.
Yule ndugu yangu alinifundisha kusoma qassam maana si unajua Wapemba kwa kusoma dini!?
Akanifundisha kama nne ambazo unawaita wafuatao;
-Aswaarul kabiir.
-Arruuhaniyyah.
-Maimanah.
-Hamamah.

Mie nilisoma ya arruhaaniyyah hawa huwa ni wa kiroho mara nyingi huja kwa kivuli,mpaka wakuzoee ndio huja kwa sura kabisa.
Kusoma kwake unatakiwa usome usiku katika giza ukiwa umewasha mshumaa wa kijani,mwekundu na njano,uwe na kitezo chenye moto uwe na ubani zuhra,jawi/uvumba na Zafarani.
Urefu wa hiyo azma ni kama karatasi moja,unasoma kwa idadi ya namba tasa.1,5,7 ila ukitaka wake haraka soma mara 71.
Mie nikasoma mara 71 halafu nikapitiwa usingizi.
Wakati wa alfajiri ile adhana inaadhiniwa nilishikwa mguu nikavutwa nikaamka.
Katika meza yangu ya vitabu vya dini niliona kivuli kinasoma vitabu vyangu wallahi kwa sauti.
Nilishtuka AISEE.
Sikuisoma tena.
Sasa kipindi nimeenda Morogoro kufuatilia ishu zangu nikawa nimelala nanenane pale mnadani kwa jamaa zangu.
Usiku nimelala ghafla nilishtuka nikaona wadada weupee wawili.
Mmoja kabla kama sista mavazi meupe mengine Meusi.
Sasa kila nikupige kelele wenzangu hawasikii,yule mweusi alivyotaka kuja nikamzuia kwa ishara ya mkono akasimama yule mweupe mbishi kila nikipunga mkono kumzuia anakuja,akalala kifuani kwangu akabusu mikono yangu,akanipapasa mapaja halafu akanitizamaa akasema kwaheri ila nitarudi tena.
Ghafla niliinuka juu nikarudi tena chini kwa nguvu nikapoteza fahamu.
Tunaamka asubuhi tunakuta maji mekundu usawa wa kizingiti cha mlango yana harufu kali ya marashi kama misk/musk halafu kila niliposhikwa na yule kiumbe PEUPEEE kama gypsum AISEE.
Ilichukua kama siku 5 mpaka ile rangi nyeupe kutoka nilivaa kanzu na gloves wiki nzima.
 
Nilipata hofu sana mkuu, niliamua nimuache auende kwani nilihisi yupo na ananipuliza kwa upepo mkali
Wewe ulichemka sana na bado umechemka, ile roho bado ipo na itakutafuta popote uwapo.

Uzi huu nimekuwekea ulipokosea...

 
Uliwaita majini ya kike na upwiru wako, wamekuja kukuonyesha show unawafukuza 😹😹😹
Dah.!! Nimecheka sana.!!
Ngoja nijaribu hiyo nione mijini ya kiume
 
Kuna makala moja ya kizungu mashuhuda wanaelezea mambo ya ajabu waliyokutana nayo. Mwanamke mmoja alielezea kitu kama hiki aisee.

Alisema walipokuwa mabinti yeye na dada yake walicheza huo mchezo kisiri bila ya wazazi wao kujua ila matokeo yake ni kama walizikaribisha hizo entity kwenye familia yao. Ikawa ni kisanga mtafutano kila ikifika mida ya giza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…