Niliyoyaona baada ya kuita roho za giza kwa kutumia OUJIA board (don't try this at home)

Niliyoyaona baada ya kuita roho za giza kwa kutumia OUJIA board (don't try this at home)

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Kwa huyo sijamuona ila kwa yule aliyemuita kwa namna alivyoteseka kwa muda wa siku nne akili ina wenge pia kwa shimo alotuonesha ndipo katokea AISEE sio poa.
Jamaa mpaka kaombewa ndio kakaa sawa.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Aliita jini gani hilo? Na hakujiandaa kisaikolojia kimtindo.

Hallelujah!!!
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Kwa huyo sijamuona ila kwa yule aliyemuita kwa namna alivyoteseka kwa muda wa siku nne akili ina wenge pia kwa shimo alotuonesha ndipo katokea AISEE sio poa.
Jamaa mpaka kaombewa ndio kakaa sawa.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Alikutana na chuma 😹😹😹
Kuna binadamu wabishi kila kitu wanataka kujaribu
 
Je wana madhara wakiitwa? Wanapendelea nini sana sana. Vipi kuhusu sifa zao zikoje
Madhara hutokea pale ambapo muhusika atakosea baadhi ya taratibu. Kuhusu kupenda nini inategemea na aina ya jini, zipo aina nyingi na vitu vyao tofauti.

Baadhi ya sifa zao ni hawaonekani kwa macho, wanapenda harufu nzuri ya marashi, wanapenda kukaa chini ya meza au kitanda.
 
😹😹😹 Ulimkuta mzee angekuwa kijana angekuwasha kofi, hiyo Zay ingekuwa Zuchu
Alivosema ali mcomand kwa Sauti ya "Mamlaka za Juu" nikajua kataja kwa Jina la Yesu Tokaaaa, kumbe kuna sauti za mamlaka za juu nyingine Zay Zay Zay ambayo pia ilimuunguza huyo kiumbe.......🀣🀣🀣
 
Habari za wakati huu wana jukwaa

Duniani hatupo peke yetu, vipo viumbe au roho ambazo kwa macho hatuwezi kuziona, zipo katika dimension nyingine, lakini ipo namna tunaweza kuwasiliana au kutengeneza ukaribu nao.

Swala hili halina uhusiano wowote na imani yangu bali ni jambo ambalo niliona katika baadhi ya harakati na tafiti zangu binafsi, kujaribu na kudadisi mambo mapya ni moja ya hulka na tabia yangu.

OUJIA board ni nini?

View attachment 3045441

Ni kipande au ubao ulioundwa kwa mbao na kuandikwa kwa mpangilio wa herufi na namba ambazo hutumika kuita au kufanya mawasiliano na roho za giza. Upande wa kushoto kuna neno YES na upande wa kulia NO, upande wa chini lipo neno linalo someka GOOD BYE.

Ubao huu huambatana na kitufe au kipande kidogo cha mbao ambacho huitwa planchettes, hii hutumika kama pointer, kimbao hicho huwa na umbo la kopa na kishimo kidogo katikati yake.

Matumizi ya vitu hivi viwili yana lengo la kutafuta au kuita roho ambazo zipo karibu yetu katika mazingira tuliyopo kwa wakati huo kwa kuzungusha kipande kidogo juu ya ubao wa OUJiA board.

Baada ya kufuatilia kwa ukaribu mchezo huu na kugundua una uhalisia na kuleta matokeo, ndipo na mimi nikaona ni vyema kujaribu na kujua ni nini hasa hutokea au huonekana.

Nilikuwa na rafiki ambaye anajihusisha na uagizaji wa bidhaa katika soko la Amazon, ndipo nikamuomba tufanye order ya OUJIA board, nilifanikiwa kuipata bidhaa ikiwa katika hali nzuri kama yalivyokuwa matarajio yangu.

Nilikaa nayo kwa muda mrefu pasipo kujaribu kuitumia, sababu ni bado nilikuwa najifunza kwa kutazama videos ili nijue njia sahihi ya kutumia ubao huo. Japo katika video hizo niliona matukio ya kutisha lakini bado niliamini naweza kufanya kwa usahihi bila kupata au kuona madhara yoyote.

Mnamo tarehe 24/ 11/2022, baada ya kurejea nyumbani Mida ya saa tatu usiku, ndipo nikatoa ubao ule na kuutazama kwa dakika kadhaa, nikaona hii ndyo siku sahihi ya kufanya majaribio.

Nikauchukua ubao na kuuweka chini, nikawasha mishumaa mitatu na kuiweka pande tofauti yani mbele, nyuma na pembezoni mwa ubao. Nikatia nia na kufungua zoezi kwa kutamka maneno maalum. Hofu ilinijaa lakini sikusita kwani tayari nilikuwa na kusudi la kujaribu.

Nilianza kuzungusha kipande kidogo cha mbao katika herufi na namba zilizoandikwa katika OUJIA board, sikuona wala kusika chochote. Nikajaribu tena kwa mara nyingine huku nikiuliza kwa sauti "Is there any presence of spirits? " Am I alone? "

Nilichagua kutumia Lugha ya kingereza kwa kuhofia labda kiswahili kinaweza sababisha nikaita vigagura au vibwengo vya kiswahili. Wakati bado nazungusha kipande cha mbao (pointer) juu ya ubao, ndipo nikahisi kuna sauti nasikia bila kujua zinatoka wapi.

Nilihisi labda ni woga tu niliokuwa nao, niligeuka nyuma na sikuona kitu, lakini bado nilihisi sauti na upepo kutokea upande wa nyuma. mkono wangu uliokua juu ya ubao ukaanza kusogea bila idhini yangu, hapo nikajua tayari nimepata ugeni.

Nikauliza "what is your name"? Mkono ukasogeza ile pointer mpaka kwenye herufi "J", nikauliza "how old are you" pointer ikajisogeza yenyewe wakati nimeishika mpaka kwenye namba 34.

Nikauliza "do you wish to harm or attack me" pointer ikasogea Mpaka upande ulio andikwa NO. Bado nikawa nahisi upepo au hewa kali inatokea upande wa nyuma nilipokuwa nimekaa, lakini nikigeuka sioni kitu.

Uoga ulinizidi kwani ilikuwa ni usiku sana na nilikuwa pekeyangu, nikaamua nisitishe zoezi na kumalizia mchezo.

Kwa utaratibu wa mchezo huu, baada ya kutosheka na maongezi na Spirit husika, unapaswa kusogeza pointer katika maneno yaliyo andikwa Good bye ili kuruhusu roho hiyo kuondoka na kumaliza game, lakini nilishindwa kufanya hivyo kwani mkono ulikuwa hauwezi kabisa kusogeza kile kibao.

Nikatoa mkono na kuacha ile pointer, ajabu ni kwamba ilianza kuzunguka yenyewe na kurejea kwenye herufi 'J' kisha namba 34. Ubao niliuweka chini kabisa hivyo usidhani kwamba labda ulikuwa kwenye meza na chini kuna sumaku au kitu kingine. Ni kweli kabisa niliona pointer inazunguka yenyewe juu ya ubao pasipo kuguswa na mtu.

Niliogopa sana na nilifanikiwa kutoka nje haraka. Siku ile sijarudi nyumbani kabisa na nikaenda kulala kwa rafiki. Nilipo rejea asubuhi nikachukua ubao ule na nikautupa, ila badae niliurejea na kuuchoma moto kabisa.

Nadhani nilikosea sheria au taratibu za mchezo, pia niligundua sio jambo sahihi kutafuta mawasiliano au ukaribu na roho za giza. Kuanzia siku hiyo mpaka leo, nikilala kwenye chumba changu naota lakini sikumbuki ndoto yoyote, tofauti na sehemu nyingine. Nahisi bado kuna tatzo ndani ya chumba changu, itabidi nihame nijaribu sehemu nyingine.

Hili tukio ni la kweli na nilikutana nalo wala sio hadithi au story ya kutunga, kama yupo atakaye hitaji kujaribu, nipo tayari kumpa maelekezo lakini atambue kwamba ni mchezo hatari sana na sio vyema kuufanya ukiwa pekeyako.

Shukran kwa kusoma andiko hili, karibu share maoni au experience yako kuhusu OUJIA board.

View attachment 3045421


______________________



#BM
Hauitaji ya board kuona spirit au ku interact nazo.. Ukiweza kufungua roho yako utaona mengi sana.. na utakuwa huna hofu
 
Alikutana na chuma 😹😹😹
Kuna binadamu wabishi kila kitu wanataka kujaribu
Alikua anasema alitokeza kutoka chini kuja juu kama kimondo halafu alirudi chini kuja kwenye sakafu huku akimfuata speed pale alipo.
Jamaa alisema alidimua mbio sio za mchezo.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
Na ukimkimbia anakupiga kama zongo unachanganyikiwa maana ni sawa na kumdharau.
 
Alivosema ali mcomand kwa Sauti ya "Mamlaka za Juu" nikajua kataja kwa Jina la Yesu Tokaaaa, kumbe kuna sauti za mamlaka za juu nyingine Zay Zay Zay ambayo pia ilimuunguza huyo kiumbe.......🀣🀣🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sauti za mamlaka zipo nyingi mwenyewe nimeshangaa hii.!!
 
Alikua anasema alitokeza kutoka chini kuja juu kama kimondo halafu alirudi chini kuja kwenye sakafu huku akimfuata speed bale alipo.
Jamaa alisema alidimua mbio sio za mchezo.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
Na ukimkimbia anakupiga kama zongo unachanganyikiwa maana ni sawa na kumdharau.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ufukunyuku wote ulimuisha shenzy zake.!!
Huyo inaonyesha alitaka utajiri akajua atakuja mrembo??
 
Back
Top Bottom