Niliyoyaona baada ya kumiliki gari ya Mzungu

Naomba link ya huo uzi mkuu [emoji23]
 
Tatizo ni ku-fit hio engine na gearbox.
1.kuna engine na gerabox mounts lazima ziwekwe
2.drive shaft zikatwe/zibadilishwe ili zikae
3.radiator na hoses zake
4.steering rack(ya Touran ni electric)
Haiwezi kukaa sawa
Kazi iliyofanyika ilikua nzito chief,,baada ya pale ile gari sikuipenda tena maana haikua na vibe ya engine yake original.
 
Dah.... unamjua "Mnyama* ? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji8]
 
Gari za mzungu ziliponishinda tabia ni usalama, stability etc utafikiri ziliwekewa gundi na lami wazungu wametupita vingi mno mno mno gari za wazungu zina mambo mengi ya kisasa mkuu tofauti na mtoyouta[emoji23]
 
Gari za mzungu ziliponishinda tabia ni usalama, stability etc utafikiri ziliwekewa gundi na lami wazungu wametupita vingi mno mno mno gari za wazungu zina mambo mengi ya kisasa mkuu tofauti na mtoyouta[emoji23]
Hiyo au hizo gari zinazosifiwa hazina tofauti na zile za Mjapani. Tatizo ni kuwa huwa tunanunua magari yaliyotumika miaka mingi na maili kurudishwa nyuma. Magari mengi yanayoingia TZ huwa mazee saana lakini utakuta imetembea km 60,000. Mara nyingi huo ni uongo kwa sababu gari iliyotembea km 60,000 bado ni mpya/imara hata ikiwa na miaka 10 au zaidi. Upya/uimara wa gari hutegemea wear and tear ambayo hupimwa na km zilizotembewa.
Kwa hiyo kwenye ununuzi wa gari ukipata gari ya 2017 iliyotembra maili 50,000 ni nzuri zaidi kuliko ya 2020 ilitotembea km 200,000. Ila kwenye technology ya 2020 itakuwa na mambo mengi.
 
Ongea yote mkuu ila gari za mzungu huwezi fananisha na gari za mjapani. Japan katengeneza gari chache zenye hadhi ya kuitwa gari hayo mengine ni usafiri tu mkuu wanayaita makopo yanayotembea [emoji23][emoji23] bahatika kuendesha gari ya mzungu uione tofauti utaleta mrejesho hapa
 
Tingekuuliza kuhusu premio wakati unainunua ungetueleza pengine zaidi ta haya... πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£ Touran ni gari nzuri pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…