Niliyoyaona kwa Mkapa (Lupaso) Stadium leo ambayo kama yasipofanyiwa Kazi basi yanaenda Kujirudia tena Lake Tanganyika 25 July, 2021 ni haya

Kila siku mnalalamika kuwa:
1. Mgalu si mchezaji wa maana;
2. Kagere hapa zei na kocha ingawa bado ni mchezaji jembe.
Leo hii imebadilika! Maajabu haya ya wanasimba
Ndy maana Rage aliwaita MAMBUMBUMBU hakukosea kiongozi wangu
 
Hakumaliza kipindi cha pili
 
Ki Morrison Jana sijui kwanini refa hakukigonga yellow card maana muda wote anamfokea refa
 
Hadija manara tangu aanze kukalia tako moja akili zimemhama kabisa
 
Katika Mambo ninayomchukia Tuisila na Ntibazonkiza ni kwamba wao ni vinara wa kupoteza mipira na bad enough hawakabi kabisa, Tuisila hana msaada kabisa kwenye timu iwapo inashambuliwa mfululizo harafu sio Target man afikapo kwenye final third ya mpinzani the same to Saido yeye ndy kinara wa kupiga pass fyongo kwenye klabu ya Yanga sema mashabiki wengi wa mpira hawafuatilii mpira unavyochezwa wao furaha yao ni kuona goli za faulo anazofunga ndy maana wanamuimba Sana jamaa lkn kiukweli Ana mapungufu makubwa mnooo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Usitutishie hapa na wee, hakna lolote hilo goal lenyewe la ndondokela ndo unajitapa hivyo, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Tukutane kigoma.
 
Darby ya Simba na Yanga kama wewe ni mjuzi wa mpira hupaswi kushangazwaa na haya matokeo ya jana.

Kama mnakumbuka Darby ya Mwaka juzi yanga wakiwa hali dhoofu kaabisa, kipindi cha kwanza simba walitengeneza nafasi wakapata goal 2, kipindi cha pili Yanga wakabadilika wakatengeneza nafasi wakazitumia wakarudisha goal zote 2

Kilichotokea jana Yanga walipata nafasi nyingi kipindi cha kwanza wakaweka kambani simba wakapata nafasi nyingi kipindi cha pili wakashindwa kutumia nafasi.
 
"Mfano Boko alikosa goli ambalo kwa mchezaji ambaye ni makini hakupaswa kukosa"

[emoji115]Mchezaji gani makini hajawai kukosa goli?
 

Safi uchambuzi makini
 
Tulisila jana hakuwa kwenye fomu kama game iliopita simba walikamia kumkaba sana the same na Yakuba, Saido nafikiri tulimsajili kishabiki zaidi lakini hayuko fiti ndiyo maana hana mwendelezo
 
"sajili tatu ambazo Manara kasema basi hapo kwenye ushambuliaji watakuwa wamepaona pia"

Hapo ni kubahatisha tu ktk usajili
Kumpata bora kuliko hao ni gharama kubwa sana

Ndio maana tunavizia ambao wanamaliza mikataba na mara nyingi uwezo wao unakuwa umeshuka
 
"Simba waliaminishwa na viongozi wao kuwa wao ni bora na kama walizifunga Finalist wa kombe la CAF yanga ni nani"
[emoji115]


Kwa mtu anayefatilia mpira hili hutokea
Hata uwe bora ila kuna siku inaitwa "siku mbaya kazini"

Hii kuaminishwa sidhani kama ni Hoja ya msingi.
Yaan nikae nimsikilize mtu aniaminishe[emoji23]
 
Ukiachana na Luis, Kinachoiangusha Simba ni wachezaji wengi wa kigeni hawajui thamani ya Derby. Wanacheza tu ilimradi wapo uwanjani mfano ni uchezaji wa Clatous Chama kwenye Derby zote ni wa kiwango cha chini sana.

Natamani hizi mechi za Deby wawe wanacheza wazawa wengi, kama ilivyo kwa Yanga na unaona jinsi wanavyojitoa kwa timu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…