Uchaguzi 2020 Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha

Uchaguzi 2020 Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha

Ni tabia ya walioshindwa kujenga conspiracy theories; hata Trump ameshindwa uchaguzi wakati akiwa rais, naye anatoa theories kama hizi. Ni jambo la kawaida sana kwa walioshindwa kudai wameibiwa kura. Kama uliyaona kwa nini usipeleke uashahidi mahakamani? Angalu Trump amekuwa anakwenda mahakani ambako anakutana na vigingi, tena wakati mwingine kutoka kwa majaji aliowateua yeye mwenyewe.
 
Kamanda mbona unaturudisha nyuma? Huko tumeshatoka; tulianza na uchaguzi, tukaja na mandamano na sasa hivi habari ya mujini ni watu kukimbia kujificha kwenye balozi za nchi za nje. Nashangaa wewe unaturudisha kwenye upigaji wa kura!
 
Aisee, kwahiyo unataka athibitishe kwa kukuonyesha video ili uamini?! [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] Vijana wa zama hizi mnatisha sana
Ina maana tunapaswa kuamini kila kitu kinachosemwa na mtu? Ukute hata hakuwa msaidizi wa uchaguzi kakaa zake huko kaamua kufungua uzi. Ushahidi ni muhimu kama kweli mnataka wananchi wenye akili zao kuamini na kuwaunga mkono.
 
Mkuu, kuna mashtaka nayaandaa kuhusu huo wizi wa kura unaolalamikiwa. Je uko tayari kusimama kuzimbani kusaidia kutoa ushahidi?
 
Ni tabia ya walioshindwa kujenga conspiracy theories; hata Trump ameshindwa uchaguzi wakati akiwa rais, naye anatoa theories kama hizi. Ni jambo la kawaida sana kwa walioshindwa kudai wameibiwa kura. Kama uliyaona kwa nini usipeleke uashahidi mahakamani? Angalu Trump amekuwa anakwenda mahakani ambako anakutana na vigingi, tena wakati mwingine kutoka kwa majaji aliowateua yeye mwenyewe.

Matokeo ya Urais yanahojiwa mahakamani hapa Tanzania?
 
Ina maana tunapaswa kuamini kila kitu kinachosemwa na mtu? Ukute hata hakuwa msaidizi wa uchaguzi kakaa zake huko kaamua kufungua uzi. Ushahidi ni muhimu kama kweli mnataka wananchi wenye akili zao kuamini na kuwaunga mkono.

Ushahidi ndio kama huu na hata humu mitandaoni kuliwekwa picha za kura za wizi na mambo mengine yaliwekwa wazi. Tungekuwa na taasisi huru huu ushahidi ungewekwa wazi. Sasa hivi ukipeleka ushahidi kwenye mamlaka husika, hao hao wezi ndio wasimamizi wa hizo taasisi! Utaishia kupotezwa tu.
 
Ushahidi ndio kama huu, na hata humu mitandaoni kuliwekwa picha za kura za wizi, na mambo mengine yaliwekwa wazi. Tungekuwa na taasisi huru huu ushahidi ungewekwa wazi. Sasa hivi ukipeleka ushahidi kwenye mamlaka husika, hao hao wezi ndio wasimamizi wa hizo taasisi! Utaishia kupotezwa tu.
Basi msilazimishe watu waamini kila lisemwalo, mtu akihoji anavurumishiwa matusi..si kila ushahidi unaowekwa mtandaoni ni ukweli, mtu yoyote anaweza kuzusha chochote.
 
Hakuna anayekulazimisha kuamini, lakini tulioshuhudia huo uhuni tunaelewa ukweli wa kisemwacho.
Wapo wanaolazimisha yaani ukihoji kidogo unatukanwa, wanataka lolote wasemalo waungwe mkono na tuwaamini. Haipo hivyo
 
Matokeo ya urais yanahojiwa mahakamani hapa Tanzania?
Ndiyo; yanaweza kuhojiwa kabla tume haijamtangaza. Siyo sheria nzuri lakini ndivyo ilivyo. Sheria inakataza kuwa akishatangazwa na tume basi hakuna mahakama inayoweza kuyatengua, ila mahakama bado ina mamlaka ya kutengua matokeo hayo kabla tuume haijayatangaza. Ndiyo maana wasimamizi wa uchaguzi huko majimboni walikuwa wanatangaza matokeo ya rais na ya wabunge, kama mtu hakukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Rais kama yalivyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi, basi anaruhusiwa kuyapinga mara moja mahakamani kabla tume haijayathibitisha. na kwa kawaida kukisha nkuwa na shauri mahakani basi tume haiwezi kuoverule na kutangaza matokeo ya rais. Mwanasheria bingwa Lissu alitakiwa ajue hilo; angeweza kuweka pingamizi wa matokeo ya jimbo moja tu na hivyo kuzuia matokeo yote ya uchaguzi wa rais yasitangazwe na tume hadi shauri hilo liamuriwe na mahakama. Ulalamishi ndio mweingi kwenye jamii yetu hii.
 
Back
Top Bottom