Uchaguzi 2020 Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha

Nimekuwa msaidizi katika moja ya kituo cha kupigia kura katika moja ya wilaya mkoani Mara.

Niliyoyaona ki ukweli yanatisha juu wizi wa kura. Kituo nilichosimamia kilikuwa mwambao wa ziwa Victoria, Tundu Antipas Lissu aliongoza kura katika kituo changu kwa kuapata kura 79 na Magufuli kura 31 lakini matokeo yaliyotangazwa Magufuli 37O, Tundu Antipas Lissu kura 6 hii ilitoka na msimamizi msaidizi ngazi ya wilaya kutaka tutoe matokeo yake.

Hapakuwa na uchaguzi ilikuwa ni ujinga tu.
 
Attachments

  • VID-20201103-WA0000.mp4
    919.5 KB
Kuna watu hamjui kusoma nyakati! Anguko la Magufuli kupitia uchaguzi huu liko wazi sana! Mungu amemfunua wazi kabisa uwovu wake, hila na dhuruma! Sasa unataka Afanye nini tena cha ziada?

Ujinga, woga, umaskini (fikra, Mawazo) ndo kitanzi chetu, sasa walio tuongoza ktk mapambano wanaikimbia nchi!

Na ukitaka tusubiri Mungu ashuke kwa style yako bila jitihada za Watanzania kuiponya nchi, tutajikuta level ya Zimbabwe ama mbali zaidi!
Mi naamini mpaka kesho huyu jamaa hata 2015 hakushinda ila meza iligeuzwa kibabe kura zake akapewa mamvi na za mamvi kapewa yeye....

Sent from my itel S31 using JamiiForums mobile app
 
Nimekuwa msaidizi katika moja ya kituo cha kupigia kura katika moja ya wilaya mkoani Mara.

Niliyoyaona ki ukweli yanatisha juu wizi wa kura. Kituo nilichosimamia kilikuwa mwambao wa ziwa Victoria, Tundu Antipas Lissu aliongoza kura katika kituo changu kwa kuapata kura 79 na Magufuli kura 31 lakini matokeo yaliyotangazwa Magufuli 37O, Tundu Antipas Lissu kura 6 hii ilitoka na msimamizi msaidizi ngazi ya wilaya kutaka tutoe matokeo yake.

Hapakuwa na uchaguzi ilikuwa ni ujinga tu.
Ndio maana wasimamizi wa uchaguzi hula viapo vya kutunza siri. Naona hizo ndio siri zenyewe za kutunza.
 
Ni kweli usemacho kuhusu sheria, tuje kwenye uhalisia. Kwa tume na mahakama hizi biased ulitegemea lolote la maana? Kama mawakala wengi walinyimwa fomu za matokeo, ulitegemea kuna lolote la maana lingefanyika?
Kama walikata tamaa kudai haki zao, basi walikubaliana na matokeo; kwa hiyo wasilalamike tena wakati walishakata tamaa wenyewe
 
Nimekuwa msaidizi katika moja ya kituo cha kupigia kura katika moja ya wilaya mkoani Mara.

Niliyoyaona ki ukweli yanatisha juu wizi wa kura. Kituo nilichosimamia kilikuwa mwambao wa ziwa Victoria, Tundu Antipas Lissu aliongoza kura katika kituo changu kwa kuapata kura 79 na Magufuli kura 31 lakini matokeo yaliyotangazwa Magufuli 37O, Tundu Antipas Lissu kura 6 hii ilitoka na msimamizi msaidizi ngazi ya wilaya kutaka tutoe matokeo yake.

Hapakuwa na uchaguzi ilikuwa ni ujinga tu.

Utahukumiwa kwa kukiuka kiapo ulichoapa, mambo mengine jifunze kumeza kama yalivyo.
 
Kama walikata tamaa kudai haki zao, basi walikubaliana na matokeo; kwa hiyo wasilalamike tena wakati walishakata tamaa wenyewe

Unapungukiwa nini wakilalamika? Mifumo yote inamtukuza na kumsujudia rais, kisha utegemee shitaka lako dhidi yake kufanyiwa kazi?
 
Hapa tunataka kuongea mambo ya ukweli; tusitumie muda wetu vibaya kwa kueneza conspiracy theories. Je wewe unafidika na nini hizo conspiracy theories?.
 
Sina chembe ya shaka ya nilichosema, inawezekana uko hapa kutaka kupingana na ukweli. Ni hivi watu wengi hawathubutu kuusema ukweli huu hadharani kwa kuhofia maisha yao, lakini haimaanishi kuwa hawaujui ukweli huu, kuwa rais wetu wa sasa anasujudiwa na kuabudiwa. Labda ww ndio useme unafaidika na nini kwa kujaribu kufunika ukweli.
 
Mpuuze huyo mzee, anadai bila aibu eti Hussein Mwinyi alimshinda Maalim Kihalali kabisa kwa Hussein Mwinyi kupata kura 76% huku Maalim akiambuia 19%

Halafu anaamini eti Maalim hakushinda 2015 kitu kilichowalazimisha CCM kufanya rafu ya kuufuta uchaguzi huo. Anadai hakuna ushahidi, wakati ushahidi ni nyaraka za matokeo za mawakala wa kila chama waliosimamia huo uchaguzi katika kila kituo. Ukijumlisha kura zote za Maalim na Shein, Shein alichapwa waziwazi, Kuona hivyo wakaamua kuufuta uchaguzi!

Huyu mzee anaamini eti kwa kuwa Maalim ni mzee basi eti wapiga kura wanaomjua ni kizazi cha Zamani cha watu wazima wa 1980's na 1990's siyo hiki cha cha leo, Anajitoa akili kwa kukataa ukweli kuwa Maalim ni nguzo ya kisiasa ya Zanzibar siku zote kiasi kwamba si tu kwamba Hussein Mwinyi hawezi kumshinda kwenye sanduku la kura, Bali ni ndoto za mchana kumshinda kwa gepu la 57%!!

Watu wenye akili wakiamua kutetea ujinga wakati wanajua ni ujinga dawa yao ni kuwapuuza tu!
 
Ushahidi gani unaoutaka wewe?
Unao ushahidi?
Tukikutaka utoe ushirikiano upo tayari?
Screenshot_20201105-101734.jpg
Screenshot_20201101-095851.jpg
 
Kuna watu hamjui kusoma nyakati! Anguko la Magufuli kupitia uchaguzi huu liko wazi sana! Mungu amemfunua wazi kabisa uwovu wake, hila na dhuruma! Sasa unataka Afanye nini tena cha ziada?

Ujinga, woga, umaskini (fikra, Mawazo) ndo kitanzi chetu, sasa walio tuongoza ktk mapambano wanaikimbia nchi!

Na ukitaka tusubiri Mungu ashuke kwa style yako bila jitihada za Watanzania kuiponya nchi, tutajikuta level ya Zimbabwe ama mbali zaidi!
Mwambie mdau akupe ushahidi walau kupitia inbox hapa jamvini. Ukitaka muonane itatia shaka, maana utawala huu umeua mnoo.
 
Back
Top Bottom