Mpuuze huyo mzee, anadai bila aibu eti Hussein Mwinyi alimshinda Maalim Kihalali kabisa kwa Hussein Mwinyi kupata kura 76% huku Maalim akiambuia 19%
Halafu anaamini eti Maalim hakushinda 2015 kitu kilichowalazimisha CCM kufanya rafu ya kuufuta uchaguzi huo. Anadai hakuna ushahidi, wakati ushahidi ni nyaraka za matokeo za mawakala wa kila chama waliosimamia huo uchaguzi katika kila kituo. Ukijumlisha kura zote za Maalim na Shein, Shein alichapwa waziwazi, Kuona hivyo wakaamua kuufuta uchaguzi!
Huyu mzee anaamini eti kwa kuwa Maalim ni mzee basi eti wapiga kura wanaomjua ni kizazi cha Zamani cha watu wazima wa 1980's na 1990's siyo hiki cha cha leo, Anajitoa akili kwa kukataa ukweli kuwa Maalim ni nguzo ya kisiasa ya Zanzibar siku zote kiasi kwamba si tu kwamba Hussein Mwinyi hawezi kumshinda kwenye sanduku la kura, Bali ni ndoto za mchana kumshinda kwa gepu la 57%!!
Watu wenye akili wakiamua kutetea ujinga wakati wanajua ni ujinga dawa yao ni kuwapuuza tu!