Niliyoyashuhudia Jeshini

hakuna jeshi laini duniani nasema hakuna. nilikutana na dogo mkorea kusini wao service kwa mujibu ni 2 years. mwendo wa shuluba yaan baruti bin cheche bin kujamba.
Lakini tofauti na majeshi ya nchi zilizoendelea huku kwetu bado tunachapana kama punda, kule kwa wenzetu ni matusi tu kama kawa lakini drill instructors hawaruhusiwi hata kumkunja recruit, huku kwetu afande anamnyuka kuruti utasema anapiga mtoto wake
 
Nahisi ulikuwa Op Magufuli, kama ulimkuta Private Kwaro alikuwaga na msemo wake mmoja "kuruti kama hujashiba wahi bombani", maana yake usirudie msosi we kabwie mimaji tu utashiba
 
Hahaha mkuu umenichekesha sana aisee, mdogo wangu wa kiume alipangiwa maramba Tanga, Sasa yeye ni mweupe, siku amerudi ile wiki moja wanayopewa ya kuapply chuo na mkopo aisee kawa mweusi, kakondaa, mama alipomuona akamkumbatia tu huku machozi yanamlenga, kila saa tunampa mara matunda, mara supu, hafokewi yaani tulimhandle with care, baba na mama wote wamepita jkt ile mujibu ya mwaka mmoja na kaka etu mkubwa yupo jwtz wakampa mbinu mbinu na kumtia moyo hapo akarudi Tena.Ile program ilimtransform Sana dogo kwanza alirudi ile miezi mitatu ilipoisha ana furaha, self discipline ilikua juu sana, zamani kusafisha tu chumba chake mpaka mgombane, maji anaoga ya Moto lakini alipotoka kule anaoga mara 2 kwa siku bila kuambiwa Tena maji baridi anafanya mambo yake kwa wakati, yupo active, nilimfurahia Sana nikasema Jeshi kumbe linabadilisha watu.Mpaka leo anasoma MD mwaka wa 3 yeye ni mtu wa mazoezi tu , anacheza mpira wa miguu na kukimbia hizi mbio fupi, yupo kwenye timu ya chuo.Nilisema nikipata mtoto wa kiume lazima aende JKT mwaka mmoja.
 
Lakini tofauti na majeshi ya nchi zilizoendelea huku kwetu bado tunachapana kama punda, kule kwa wenzetu ni matusi tu kama kawa lakini drill instructors hawaruhusiwi hata kumkunja recruit, huku kwetu afande anamnyuka kuruti utasema anapiga mtoto wake
hapo ndipo chanzo cha kuambukizana ukimwi...fimbo imchape yule, huyu...na yule...😭😭😭

jeshi limeoza...asilimia 75 wapo kwenye grid ya Taifa😭😭😭​
 
Hapo kudoj Tpdf elezea kidogo mkuu kwamba hutoboi vp?kwa maana kwamba Kuna msako mkali au vipi
 
Mmh nisingeweza uwiii
Hongera
 
Karibu upande wa pili, huku hakuna kuchimba visiki wala hutaenda kuvuna mahindi.
 
Duuh asee hakuna kitengo ninachokipenda na ninachokiona rahisi jeshini kama kwata huwa sielewi kwanini watu wanakichukia na kukiona kigumu

Yani mimi kwangu kwata ndio ilikuwa sehemu ya kupoozea machungu ya jeshi, maana mimi sipendi mabio wala mazoezi nakumbuka mwishoni mwa six weeks za kwanza, nilikosa kuwepo kwenye pass of square tu roho iliniuma sana

Nikasema kwenye graduu lazima niingie kitengo cha kwata, na kweli graduu nilikuwa kwata coy sema kimbembe kuweka silaha begani, hadi mfupa wa bega ukaanza kuuma nikawa naweka handkerchief

Yani mimi kiujumla jeshini vitu nilivyovipenda ni chenja, kwata, range (japo niliishia kulenga mijusi), syndicate na route march (kutembea tu), ila ukishaniambia nikimbie daah nilikuwa najionea tabu tu

Na yale maovyoovyo mengine nilikuwa siyapendi kabisa
 
Mimi kitu pekee ambacho kilikua kinaniudhi ni kuhesabu namba Kila dak. As ware nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…