Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

Nakumbuka nilienda kambi ya Kanembwa Kigoma kulikuwa na afande wanamwita " Cyborg" yule mwamba alikuwa hacheki alooh na anaogopeka balaa.

Mazoezi ya kule acha tuu kuna afande alikuwa anaitwa John Magesa na mwingine Dakanyama walifanya maisha yetu ya jeshi yawe magukumu.

Nilipata rafiki basi kwenye mchakamchaka alikuwa anapenda sana kuniimba " Sio lako Trudie la mchina hilooooo, umechoma sindano la mchina hilooooo, umepaka mafuta la mchina hiloooo" Nimekumbuka mbali sana
Binamu nami nije nilione trudie 😀😝😝
 
HII imenikumbusha siku niliyoripoti JKT mimi nilinyoa kipara Sasa wakati nafika kwenye gari la kuelekea kambini nilikutana na wadada wawili wao walikuwa hawajanyoa, Ile tunafika nikaulizwa Hawa unawafahamu nikajibu ndiyo, wakaniambia kwahiyo wewe umewadanganya wasinyoe alafu ukanyoa peke yako, aisee palepale getini nilianza kuroll na kurukishwa vichura, nikamwagiwa maji, Kisha nikaambiwa niwapake poda usoni yaani vumbi, alafu niwanyoe yaani palepale hamu yote ya JESHI iliisha
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]daahh asee nimegundua kambi niliyoenda ilikuwa ya kawaida sana!!
 
Mimi maisha niliyapenda vitu vingi bado nakumbuka...

Nilikuwa napenda sana maelekezo ya mabio

Utasikia kuruti utanyoosha njia hii utakuta kibao kimeandikwa shule fulani hujaja kusoma hapa utapita kushoto utakata njia ya kwenda messi sio muda wa kula huu utanyoka wazi kuruti[emoji2][emoji2]
pale ruvu utasikia kuruti uelekeo ni hivi utapita huku nyuma kama unaenda kwa dosa, utarudi hadi road block uelekeo kilima nyege[emoji3]
 
Huko sijawahi pangwa mkuu yani kwa kifupi kitengo cha mifugo sijawahi kuwa na zali nacho ni siku moja tu nilipangwa kule poultry kuokota mayai ya kuku basi, mimi shamba langu lilikuwa kule jkt club karibu na barabara ya kwenda mikoani, tulikuwaga tunanunua vitafunwa kule kule mtu unarudi kikosini ushashiba zako
dah umenikumbusha jkt club, lile tengo nililipenda sana full utawala mapema tu kazi zimeisha mnaanza kufua wengine wanalala. Wakipita wenzenu wanaoenda guantanamo (shamba la vitunguu) wanawaangalia kwa huruma. Jioni mnarudi kambini wasafi na nguo safi!!
 
Mimi maisha niliyapenda vitu vingi bado nakumbuka...

Nilikuwa napenda sana maelekezo ya mabio

Utasikia kuruti utanyoosha njia hii utakuta kibao kimeandikwa shule fulani hujaja kusoma hapa utapita kushoto utakata njia ya kwenda messi sio muda wa kula huu utanyoka wazi kuruti[emoji2][emoji2]
Umenikumbush 823KJ[emoji1787]
 
NITAKUJA KUWAPA NILIYOYAONA KWENYE UWANJA WA DAMU.

UTAMBULISHO WA KAMBI (WELCOME TO THE CAMP)

BULOMBORA 821KJ

KUJITOLEA SIYO MUJIBU WA SHERIA.

WANA WALIVYOPATA MAGONJWA YA AKILI.

RAFIKI ZANGU VIPANDE(MIILI MIKUBWA) WALIVYOESCAPE KAMBINI BAADA YA MATIZI MAKALI.

NILIVYOOGELEA KWENYE SHIMO LA MAJI MACHAFU (DOSO) MTALO ULIOKUA UNATOKA BAFUNI BAADA MAKURUTI KUOGA.

NITAWASIMULIA NILIVYOENDA KUFANYA FUJO KWA KIJIJINI KWA DOSA HAPA NI RUVU JKT.

NITAWASIMULIA NILIVYOKUA NAKAZA MATRONI (DATE) NILIGUNDULIKA NA KUPATA TABU SANA.
duuh! Hii ya kiumeni itakuwa balaa
 
SEHEMU YA 11

2. NGOMA COY

Nilimwambia Anna mimi kwata nishafukuzwa, akanishauri nihamie ngoma coy.
Ngoma coy wanajihusisha na sanaa kuimba, kucheza, kuigiza hivyo.

Nikapiga picha mimi kuigiza, kucheza, kuimba siwezi nitafanyaje sasa? Nikajipa moyo kesho nikaongozana na Anna kitengo.

Nimefika pale bakabaka akaniambia bora umekuja ngoma coy huku utawala kama wote! hamna jua wala kutumia nguvu. Sasa kuna mchujo humu huingii bure, wote unaowaona hapa wamefanya vizuri kipindi cha mchujo.

"Aya imba tukusikie sasa ndo mchujo huu usifanye masihara"
Mimi kuimba sijui
"Sasa hujui kuimba, hapa umefata nini? Aya cheza tuone"
Kuna mziki kabisa kwenye lile hall! Navyokwambia ngoma coy utawala ujue utawala kweli!!
Mziki unapiga nicheze! Anna ananiangalia anacheka tu, nikajikaza kucheza[emoji1]

Naona kuruta wananicheka na mimi najua hapa naharibu tu.
"Weeee! Kuruta kucheza unajua lakini sasa hapa tumeshajaa tupo wengi, jaribu vitengo vingine" akaniambia bakabaka

Majibu hayo tu nikajua nimeboronga kucheza hivyo kanikataa kiaina kama walijua wamejaa kwanini hakuniambia tokea mwanzo?......

Sasa niende wapi! Ngoma coy sijafit ila ningekubaliwa hapa ingekua utawala kama wote.
Nikarudi hangani mapema, sababu muda ulikua umebaki mwingi kuruta wapo vitengoni.
Hairuhusiwi kwenda hangani muda wa kazi hivyo nililala chini ya deka ili bakabaka wakipita wasinione.

Usiku kama kawaida kombania! Ukifika unakaa chini vumbi kama lote. Kipindi hiki tushamaliza zile first weeks za mateso hivyo tukawa hatupewi mazoezi magumu hivyoo!

Tunanyanyua viroba (squats) tukichoka tunaimba chenja mambo yakizidi tunaekewa mziki tucheze bakabaka wetu alikua na speaker ndogo.


3. KITENGO CHA KAZI MCHANGANYIKO
Nilivyotoka ngoma coy nikaja huku sasa.
Kazi mchanganyiko wanadeal na kufyatua tofali na kubeba, kuchimba visiki, kuvuna machungwa na kupukuchua mahindi, kumwagilia bustani ya mbogamboga bondeni, kusafisha vyoo, kufyeka nyasi.

Mwanzo nilijitahidi nikaekwa kundi la kuvuna machungwa! Bakabaka walituambia kula machungwa hadi usaze kubeba hairuhusiwi hivyo nilikula utawala sana shambani.

Mpaka shamba likawa jeupe tumevuna kila kitu
Hivyo kazi ya machungwa baada ya kama wiki ikafa tukawa hatuendi tena.

Nikawa najila ili niende kundi la bustani nikafanikiwa, kule pia utawala sana tunamwagilizia michicha spinach ila tatizo likaja bustani kwenda ni asubuhi na jioni tu. Mchana tunaambiwa twende shambani kung'oa visiki.

Huko shambani mbali kama 2km nikaona hiki kipengele kila siku kubeba visiki nikawa nalalamika sana.
Anna akaniambia kwanini usiende kitengo cha karate?

Nikafunga ukurasa na kazi mchanganyiko nikahamia karate rasmi!

Itaendelea.

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini

Pole wewe ni general sasa
 
Back
Top Bottom