Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upo vizuri kaka,...inatokea post namba 227
Arsis: Babu yako aliporudi nyumbani akaita jini wa bakora, Akamueleza yote kama alivyoelezwa kwa Sheikh Mgunya na wale wageni.
Jini Bakora akmwambia babu yako ampe muda alifanyie kazi suala, mpka siku ya pili amuite atamueleza kafikia wapi. Siku ya poili babu yako akamuita. Jini bakora akafika akaanza kumweleza babu yako.
Jini Bakora; Mbaruki umefungua mambo makubwa sana, jana nimeenda mpaka Amboni, unajua pango letu ndio hilo hilo linakwenda mpaka mlango wa Amboni, hakuna jini kwenye hayo mapango aliyewahi kuona hiyo sehemu isipokua wapo waliosikia sikia tu. Hao waliosikia tu nao hawana uhakika ya walichosikia, kwa hio ni kama hadithi tu.
Jini Bakora; Kwa hio kabidi niende nikaongee na majini wa baharini, nahati nzuri tunaheshimiana nao sana. Nikaonana na mkubwa wao kabisa kwa upande huu wa mlango wa Ambini, akanambia habari hizo hata yeye amezisikia tu lakini hana uhakika nazo hakuna aliemuuliza kabla. Lakini huyu akanipa ushauri. Akanambia kuna kazi nzito inabidi ifanyike, kuna jini ana kitabu, lakini huyu Jini yupo dunia ya tatu, dunia ya tatu inabidi lango lake lifunguliwe ili huyo jini apate kutoa kitabu na kurudi. Inabidi mumpate jini au mtu mwenye uezo wa kwenda dunia ya tatu na kurudi na yule jini mwenye kitabu, na jini asie na nguvu akienda huko harudi tena huku. Na hakuna anaeweza kuja na hicho kitabu isipokua huyo jini mwenye hicho kitabu. Kwa hio Mabruk niwache niendelee na hii kazi, wacha niendelee kutafuta jini mwenye uwezo huo. wapo tutawapata, usiwe na shaka, lakini inabidi kazi kubwa ifanyike. Hivi vitabu vya majini vina kazi na hatari kubwa sana kwetu sisi majini. Mbaruk ukikipata hicho kitabu utawamiliki majini wa dunia nzima, sio mchezo.
Mbaruki: Sasa wewe fnya njia zako na mimi nafanya njia zangu, tukutane hapa baada ya siku tatu. Mimi nitakuita.
Mabruki siku ya pili, akenda kwa Mgunya akamueleza kilichopo, Mgunya nae akaahidi atafanyia kazi baada ya siku tatu wakutane. Ikawa kazi sasa ipo pande tatu, Jini Bakora na Majini wa Mgunya na Babu yako na vitabu vyake na majini wake wengine.
Siku ya tatu wakutana wote watatu, kila mmoja akaeleza alichokipata. Akaanza Mgunya akasema mimi nimepata jina la hicho kitabu kinachoongelewa, na zipo nuskha (kopi) lakini sio nzuri zimechezewa sana na watu waongo waongo. Kwa kifupi hakifai, mpaka kipatikane kwa huyo jini.
Jini Bakora; Hata mimi nimepata jina la hicho kitabu na nimepata ufumbuzi mwepesi kidogo. Kuna mtu amefungwa na majini hapa hapa duniani, huyu akitolewa kifungoni anaweza kwenda na kurudi kuleta hicho kitabu, kazi ya kumtoa kifungoni sio ndogo lakini inawezekana, na anaeweza kumtoa huyo ni binadam tu, sio Jini, kwa sababu majini wote wanaogopa, atakae mtoa huyo atauliwa. Mimi nimeweza kupata jini ataetuonesha kafungwa wapi na vipi tutamtoa inabidi apatikane binadam asie na uoga na anaejua kusoma Qur'an, Qur'an ndio kinga pekee itakayo mkinga na majini wanaomlinda huyo mtu aliefungwa, akipatikana ndio atumike. Haya Mabruki wewe umepata nini?
Mabruki: Mimi nilichokipata hakuna zaidi isipokua ahadi za kufanyiwa kazi tu. Kwa hio naendelea kusikiliza. lakini kama anatakiwa binadam aifanye hio kazi kama ulivyosema, nipo mimi nitaifanya.
Mgunya akasema shabash, mimi naahidi kuwapa ushirikiano wowote mtakao uhitaji kutoka kwangu tumpate huyo mtu.
Mabruki; Haya tunafanya baada ya hapa?
Jini Bakora:; Wacha nikaandae majeshi kwanza tupapate alipofungwa huyo mtu, halafu tujue namna kufika na kutoa kifungoni.
Mgunya: Tukijuwa kafungwa wapi, kama ni dunia hii, namna ya kufika niwachieni mimi, kuna elimu ya kupafika hata kuwe na ulinzi vipi wa majini, mradi isiwe dunia nyingine tu. Dunia yetu hii halafu jini aytushinde ujanja kwetu? Sisi ni viumbe bora kabisa. Mimi nasema tukutane kesho, wewe Bakora, kafanye uchunguzi wko, umeleta habari nzuri sana, na mimi nitafanya uchunguzi wangu, na wewe Mabruki usichooke, kesho njooni tukutane hapa. sasa tuna muelekeo.
Wakaondoka, ikabidi mgunya amueleze yule kijana wa Kipemba, kua haya mambo ni marefu inabidi aende gtu kwao, yakoiwiva atapelekewa habari aje.
Mpemba: Sasa nitapataje habari?
Mgunya: usiwe na shaka utapata tu habari, usofikiri kuna mtu ataifanya hio kazi akudhulumu, umetupa mtihani mkubwa sana. Mimi nakuonea huruma kuendelea kukaa hapa. Wewe nakushauri neda tu.
Mpemba; Mimi nakenda lakini baada ya mwezi kama sikusikia kitu nitarudi kuja kusikiliza.
Mgunya" Inshallah utapata habari kabla hya mwezi kwisha ili tukupunguzie gharama za nenda rudi, ukija hapa inatakiwa ujue iunakuja unaondoka na mali sio mikono mitupu.
Basi wakaubaliana Mpemba aondoke na wao wakutane siku ya pili yake.
Itaendelea.
Kabisa story nzuri sanaExactly hapa sasa nazani tunaelewana ndugu mwandishi, Inavutia sana hii mikasa na natamani isiishe kabisa hii story yako yaani iendelee mpaka mwakani.
🤣🤣Muulize arsis hivi hii CCM itatoka madalakani Kwa anavyo ona yeye au tuendelee kuwatumikia wabakaji???#
Kweli nina maswali mengi sana,,lkn ngoja tuendelee kupata story zaidiNimefurahi sana kwa hilo swali lako, hilo amenielezea zamani sana. Ni kisa kirefu kidogo,
Kwanza alikua ananielezea kuhusu dunia, kwanza yeye anakataa kua dunia haipo duara kama tunavyoaminishwa na sayansi. Pili anasema hiz nyita wanasema ni kubwa ni waongo wana sayansi, hizo nyota anasema ni kama ilivyosemwa kwenye Qur'an ni mapambo kwa hii dunia. Pia anasema hakuna nyoita inayozidi tani kumi ukubwa wake, wanasayansi ni waongo. Na vimondo ndio hizo nyota. Ka ufupi sana jibu ndio hilo, mbele huko kisa kikifika sehemu hiyo nilipouliza utakisikia kwa kina.
Majibu ya Arsis yanaweza kukuachia maswali mengi sana. Ni vizuri kua hilo alinijibu zamani.
Kuna uwezekano watu mkifa mnahamia dunia nyingineHapo kwenye Dunia ya SITA naelewa kiasi kwanini Hana mamlaka ya kuongelea..sijui ndo hiyo sixth dimension sijui
Anyway story yako Iko very interesting
Arsis alisahau ku editKikapu kikajaa kamba............
Hii stori kamba wametajwa kuliko kitu kingine chochote
WE tulia tuendelee kula kambaKikapu kikajaa kamba............
Hii stori kamba wametajwa kuliko kitu kingine chochote
KIkubwa tu Arsis haja mind, bas hakuna shidaTypos zimekuwa nyingi mpaka inakuwa vigumu kusoma kwanini usipitie spelling errors na kuzirekebisha watu wengi sio waandishi wazuri lakini hawaandiki kwa kutojali kama wewe inaonekana una haraka mno ya kuandika
Ulivyotaja whimpy na Jamal nimeamini.Inatokea post namba 197.
Safatri yetu ya kuelekea DOM ikawa nzuri sana haina pirika wala vituko Dereva akawa anaendelea kunipoiga story tu.
Dareva: Waarabu wa Morogoro wana pesa bwana, ule mzigo wao, Halima kanilipa na wao wamenilipa, tena nimewaambia nimeshapewa nauli ya huu mzigo na Halima, wakanambia hiyo sio nauli, hizo zako, Kafurahi na wewe. Wakanambia siku wakiambiawa mimi ndio naleyta mzigo wanafurahi, maredereva wengine wanawakata mirungi yao wanaenda kuuza juu kwa juu ghiyo.
Mimi; Mbona wewe unakula?
Dereva; Mimi yangu ananipa Halima, tena toka Sofi yupo pale ndio alizowesha, mimi nilikua sili mirungi mshikaji, Sofi kila nikienda ananipa, sema nashukuru siili hii mpaka nbipewe pale, sijawahi kununua wala kuwachomolea mirungi yao Waarabu. Mie nimelelewa kwetu mshikaji. Siijui jaa mimi, kwetu masikini lakini hatukosa riziki, tunakula wali na mboiga nne mshikaji wangu.
Nikawa nacheka jinsi anavyoongea.
Dereva: Mshikaji wewe kama mimi hupendi kula kula njiani, mimi bwana nyama nyama sijui kuku, sijui nani kachinja, sili kabisa, tutalishwa vibudu njiani, Humu. Hivi hapa kula yangu mimi Dodoma, kwa Sharifu, uhindini au wiumpy, na yeye sharifu vile vile, Kule tena nikimkuta habiba Jamal pale wimpy silipi kitu, Mwenye ananiita sheikh wake. Unajua mwenye wimpy Dodoma?
Mimi; Hapana sikjui, mimi nimeahi kupita tu Dodoma, sijuani na watu.
Dereva: basi leo nitakupeleka ukamjue Al Habiba Jamal wa wimpy. Mimi nilijuana nae kuna siku walikua wanagawa sadaka, wakaja chuoni kwetu nyumbani, nikawapiga dua, pale hajanisahau toka siku hiyo. Ananniita Sheikh wangu. Tena unaweza kuwajua wewe, wanasema alikua na wimpy Dar wakaiuza.
Mimi; Labda mzee wangu atawajua, mi isiwafahamu.
Drereva; Usijali mshikaji, mradi upo na mimi utawajua watu wa maana nia hii, wananijua mimi kama shilingi.
Nikawa nacheka tu uongeaji wake, haikupita muda tukafika Gairo, akanambia hapa mshikaji hatuingii mjini huko, tutasimama pembeni hapo kuna kituo cha mafuta na kuna shehemu ya chai nzuri tu, ukitaka kula pia, hakuna wasiwasi.
Mimi; Mimintamenya nanasi na machungwa nile, sijisikii kula sasa hivi.
Dereva: Mwili ra tizi huo, kula mshikaji usione haya.
Akapaki vizuri kituo cha mafuta, kunajamaa pale akamwabia, wewe kila ukija hapa nakwambia paki kule pambeni unajifabya huelewi sio?
Dereva; Nashau mshikaji wangu, mhapa najiona nimefika nyumbani, nipo huru.
Yule jamaa akamwabia, hapo nakwambia kwa usalama, wako wagtakukwangua, madereva wengine walevi.
Dereva: kwli mwanagu wacha niiweke pembeni.
Akaiweka pembeni akafungua buti nyuma akanambia lete hayo machungwa kama kumi hivi watatumenyea hapa, leta na manasi mawaili, moja lako moja langu. Mshikaji usiwe na wasi wasi na wasiwasi tutakula martinda tu leo kama timbiri, sem mananasi na machungwa tutakojoa sana njiani.
Mimi:; Nimeona msikiti pale, wacha nikapige safar kidogo nakiuja, sasa hivi sichelewi.
Dreva' Nenda mshikaji wangu dua kwa wingi tu usiwe na wasi wasi. dua muhimu sana. Mimi nikishaunganisha zangu, ningekuja na wewe. Utakuta hapo kwenye kiduka hicho, kun mrfembo humo ndani, halafu naambiwa kawachwa na mumewe.
Mimi nikaondoka, nikajua huyu hanyamazi sasa hivi. Nikasali nikarudi nikaingia kwenye kimgahawa, dah kweli, nikamkuta mwanamke mzuri kweli sio mchezo. Mshikaji wangu sikumuona.
Yule mwanamke akaniuliza wewe ndio umekuja jna yue dereva wa IT?
Mimi; Ndio sister
Alikua anaonesha ana umri mkubwa kwangu lakini bado ni kijana. mafa mshikaji akaja, bumetoka mumenya vitu, pale, hawa wakaguru hapa hawajui kumenya machungwa wala mananasi.
Dada: Kw akujidai huyu, wewe uje na machngwa yako nani akumenyee? Unaleta ujanaja wa mitaani hapa?
Dereva: Usisemee mbovu, ningepajua kwenu ningeshapelka posa. mtoto mzuri kama wewe unaka poarini huku? Ningekuweka mjini wewe.
Dada; Nipishe huko, nani alikwambia ana shida ya kuolewa? Una maneno ya kijinhga jinga.
Dereva: basi poa, nimekuletea zawadi, ngoja nikuletee.
Akatoka akaenda kwenye gari akarudi na nanasi moja kubwa na machungwa kwenye bakuli kubwa tu.
Dada; Nilifikiri utalisahau bakuli langu.
Dereva; Sina akili ya kusahau mimi. Ukila nanasi tu hilo, nimelisomea hilo, ujue hunikatai tena.
Dada: tna ndio nalila kwanza hilo, hariufu yake tu linaonesha limewiva, sasa weewe unajida zawadi kumbe kinanasi kimpoja tu?
Dereva; Mwanangu, hiku kanielekea mimi, hakuna mwanamke mwenye shukurani duniani isipokua mama yako mzazi tu. Si unamuona huyu mwanamke, mimi nimemuwazia zawadi, nilikua sina sababu ya kusimama hapa zaidi ya kukuletea wewe zawadi, halafu unaiponda zawadi yangu. Na siku ingine.
Dada: Kwani leo hukusimama kwa ajili ya kusali?
Dereva: Mimi nimeshaunganisha sala ya safari, unajua sala ya safari wewe? Nimesimama kwa ajili yako tu.
Dada; Haya ahsante, Mungu akuzidishie.
Dereva; Hayo ndio maneno, twende zetu mshikaji wangu, anaweza kunizuwia huyu nisiondoke hapa, anajidai tu.
Dada; Nipishe huko, nani akuzuwie wewe. Tena usimfundishe huyo kijna, mwenyewe anaonesha mpole.
Dereva: Mpole? Simba mwenda kimya huyo. Au nimwache yeye mimi nitangulie?
dda: Huyu, mwache ahamie hapahapa patapendeza hapa, sio wewe. Haya kwaherini.
Aaingia ndani. na sisi tukaondoka zetu.
Dereva: mwanangu lazima ujue nituo vyua njiani, sio unajisimamia hovyo tu. Usione tabu mwanangu, umenabia wewe fundi, unaweza kufata migari mibovu huku ujue wapi pa kula, wapi pa kupumzika. Hapa kuna wajjaguru, wachawi kama nini.
Tukaendelea na safari pka nje nje ya Dodoma akanambia mshikaji kuna mawili, au tutafute sehemu gtulale hapa Dom au tutembee mpaka Singda, unasemaje?
Mimi; Mimi vyoivyote vile niko poa tu.
Dereva; usijali mwanangu, tulale hapa, alfajiri tuondoke haina haja ya kukimbizana barabra usiku.
Tukaenda moja kwa moja mpaka ki gesti kimoja kipo mjini kabisa, gari inaingia mpaka ndani, akiweka gari akanambia mshikaji, Sasa kama kukoga kutawadha, tukutane hapa nje kama nusu saa hivi twenda kwa wimpy tulkle mapema, halafu tuke kupumzika mapema, alfajiri sana tukijaaliwa tuondoke. Tutasali kwa Gadafi. Kuna msikiti mkubwa mbele hapo unaitwa kwa Gadafi.
Akaingia chumbani kwake na mimi nikaingia chumbani kwangu, ilikua ndio mara ya kwanza kulala gesti namna ile. Kilikua k9i gesti fukani kidogo lakini ksafi. Nikakoga kuna choo ndani, nikagtoika nje. Baada ya muda akaja, tukaondoka tukaenda wimpy, bahati akamkuta rafiki yake anaitwa Jamali, tukaulizana pale, tukala, Jamali akakataa kabisa kupokea pesa, akasema nyie wageni wangu, Huyu Sheikh wangu. Mtakuepo Dodoma?
Dereva: hapana mjomb Jamal. sisi tuombee dua sharofu, alfajiri ytunachoma.
Jamal: Woi safari hii?
Dereva" Mimi kule kule Burundi, huyu mshikaji anaishia Shinyanga.
Jamal": Kuna kaka yangu pale Shinyanga, chukua namba zake, nhgoja nikuandikie, ukiwa na mwenyeji ni vizuri zzaidi. Jamal alikua namwili wa unene na mtu mzima makamo ya mzee wangu akanipa namba, SAkasema mimi nitamoigia na wewe ukifika usiache kwenda kumuona, au mwenyeji wewe Shinyanga. Nikamwambia hapana, mimi nafata gari tu limeharibika huko.
Jamal; Wrewe fundi au unapeka spea, unaonesha bado kijana mdogo sana?
Mimi: Mimi fundi, tuna gereji kwetu, nimekulia gereji.
Jamal; Basi uone kaka yangu anaitwa Ali, maarufu sana Shinyanga.
Mimi; sawa nitampigia nikifika.
Jamali: Mwambie hata huyu mwezako akupeleke kama hana haraka, anapajua nishampa mizigi ya Ali matra nyingi ampelekee.
Dereva; Nitamuonesha Sharifu, siwezi kukuvunja hata siku moja kijukuu cha mtume.
Tukala pale tiukaondoka, tukatembea mwendo kido mpaka kwa gadafi tukakuta wamesha sali isha, sisi tikasali, tukaunganisha jamaa na wengine waliochelewa kama sisi. Tukarudo hoiteli
Ikawa mimi nimekosa usingizi na sijachoka nikatoka nje, niliona shemu kama garden hivi wakat tunaenda na kurudi msikitini, nikaenda pale, kinyaa hakuna mtu kabisa, nikasema ngoja nimwite Arssis. Nikamwita kimya kimya akaja kweli, nikaanz akusikia sauti.
Asis; Vipi hali yako?
Mimi: Salama, sikutegemea kama utakuja.
Arsis; Hakuna neno, sehemu nzuri hii umechagua sema washenzi wanakojoa kojoa hovyo hapa. nenfda pale ulipfikia nje kuna baraza zuri, tutaonea pale. Najua una maswali. Titaonana baadae kidogo.
Nikaondoka pale, kweli nikaanz akusikia harufu ya mikojo, nikarudi hoteli, nikakaa nje pembeni kibarazani, kumwita tu Arsis akaja.
Arsis; Vipi hali? Unaona hapa pazuri, unasemajje?
Mimi: Arsis; leo nilikua naongea na yule jini mwanamke, mboina yeye anakubali ni jini, wewe unasema sio jini?
Arsis: Mimi nimekwambia naweza kua chochoite kile, naweza kua mtu, naweza kua jini, naweza kua mti. Wewe hilo usijali, amini ninachokwambia.
Mimi; Sijui nianzie wapi?
Arsis: Anza popte tu usiwe na wasiwasi.
Mimi; Yule jini wa kike kasema yeye yuko na mimi ananifundisha, ananifundisha nini? Nani kampa hio kazi ya kunifundusha?
Arsis: Mimi nimempa kazi, kuna mengu sana hayajui. Anayoweza yeye atakujulisha asioweza mimi nitakufundisha.
Mimi; Kwanini mimi?
Arsis: haya mambo yanakua kiukoo, ni viapo vua ukoo kabla ya babu yako kuzliwa sisi tuko kwenye ukoo wenu.
Mimi: Unasema sisi, una maana mko wengi?
Arsis: Hapana, mimi niko peke yangu, yule jini wa kike na mamake, ndio wanafanya kazi kwangu, wapo chini ya himaya yangu. Babu yako sijawahi kufanya nae kazi, zema namfahamu sana nimemsaidia mara nyingi. Yeye ruhani wake aliekurithisha ni yule mwenye ile bakora. Mimi ni mkuwaba wao, eote wapo kwenye himaya yangu, kwa hio hawawezi kupinga na mimi. Mi i nasaidia tu mpaka ulipokabidhiwa wewe kwa yule mwenye bakra nikaona ujuzi ulionao usipotee bure, tulikua tunatafuta binadam siku nyingi wa kumfundisha tunayojua. Wewe ndio nimekuchagua nikufundishe.
Mimi; Mbina unasema "sisi" kama mpo wengi halafu unasema uko peke yako, unanishanganya.
Atrsis: Usichanganyikiwe, wotew wanaofanya kazi chini yangu ina maana ni sisi. Mimi kiukoo nipo peke yangu ni tofauti kabisa na jini wa bakora na hawa majini wa kike, Wao wana ukoo wao mkubwa. Bado wewe pia unakoo mwengine, huo sana upande wa mama yako, ukoo wa simba. Lakini na babu yako yupo ukoo huo, sema yeye hapendi mamboi ya uasherati yeye ameshika dini, alifanya mcheo kidogo akafanya toba yeye sasa akita anaoa tu. Unajua babu yako kishaoa, wake wangapi mpaka sasa?
Mimi: Sijamuuiza lakini zee kanambia wengi tu.
Arsis" Mkionana muulize, wengi kwacha lakini kabaaki na wawili unawaju wewe na mmoja humjui.
Mimi; Kwa hio babu sasa anawake wa tatu?
Arsis: ndio, mullize mwenyewe atakwambia.
Mimi; Hii poete ya nini> N yule mwanamke naona inafanana na hii laikini yeye kiti cha duara.
ARSIS: hiyti pete ni zawadi yako, ni ya kwangu mimi, ipo moja tu dunaiani. Kwa ajili ya mawasiliano tu mimi na wewe. na walw wanawake ni mawasiano tulakini vyao ni vito nadhahabu yawaida tuliwatengeneza alipoana kufanyua kazi na mimi, sio siku nyingi sana, walikiua wanafanya kazi na yiule mwenye bakora, sasa kanipa mimi wanisaidie kwa ajili yako. basi hakuna zaidi.
Mimi: nyinyi ni wachawi?
Arsis: Hapana mimi sio mchwawi kabisa, na wale wanawake yule mama yake zamani alikua mchawi miubwa sana, sasa hana yena uchawi, amefanya toba na sasa nimwema kabisa, akiwa mchawi watamuua wenzake. Na huyu mwanae anaekuja sana kwako, hajawahi kua mchawi, sema anajua mambo mebgi ya kichawim kwa sababu anpiugana sana na wachawi katika kazi zake. Anjua mengi yule, usione anaongea na wewe kiupole nihatari sana ytule kwa wachawi, ana jeshi kunbwa sana wanamuogopa yule. Yule anakufundisha na anakulinda. Mradi wewe unaoete hiyo, wewe ndio boss wake sasa.
Mimi: Sasa wewe nani hasa?
Arsis; Mimi nimwalimu tu ninaekufundusha vile utaweza. Hatuwezi kukufunsisha mabaya wala sina mabaya. Wewe hukukabidhwa kwangu, mimi nimekuja kwako mwenyewe. Baada ya kukuchunguza sana, yule jini wa nakora ndio jini umekabidhiwa, miubwa sana yule, usione vile.
Mimi: Naona kwa leo inatosha, maana inabidi niamke alfajiri sna, tunaondoka.
Arsis: Sawa, sema Inshaallah.
Mimi; In shaa Allah. Haya kwaheti Arsis.
Arsis; Kwaheri, siku nyingine mitakundisha kitu leo nenda kapumzike.
Nikaingia zangu kulala.
Itaendelea.
Ulifikiri ni "kamba"? Hiki ni kisa cha kweli kadiri ya uwezo wangu wa kukumbuka, sana sana kuna vionjo tu, kwa sababu siwezi kukumbuka kila neno au kila kitu. Isipokua, kuanzia kisa cha Mahojiano yangu na SArsis, yote yana kumbukumbu za kurekodi. Nilianza kurekodi kabla ya hizi smart phones, nilianza kwa kurekodi na tape ndogo ya mkononi, kwa muda mchache sana, nikapata "digital recorder" ndogo sana ya mkononi, hio nilikaa nayo muda kiasi mpaka zilipoingia simu za kuweza kurekodi, ndio mpaka sasa.Ulivyotaja whimpy na Jamal nimeamini.
Kula, kwa jina la Mwenyezi Mungu, hautopata madhara ya kula visivyofaa.maeneo yote ya kweli.wimpy hapo nimekula sana ice cream.we jamaa mwarabu mwarabu nin? usagara huko kote napajua. leo nimesjindwa kula mjini.kila mtu namuona yupo uchi. tena mama mmoja mtu mzima kaniangalia sana nikawa namkazia macho