Inatokea post namba 200.
Nikalala fofofo, sikumbuki hata kama niliota. Kabla ya alfajiri mshikaji dereva kanigongea mlango, akanambia twende mwanangu, usijali mimi nililipia vyumba, hata chako nimekilipia, mimi ndio nimekuchelewesha.
Nikajimwagia faster. Maji ya moto, safi kabisa kwenye shower. Tukatoka mpaka kwa Gadafi ile tunafika ndio wanakimu sala, Tukasali pale tukaondoka, nikaona hatujachelewa sana, mapema tupo Manyoni, tukapita faster tu. Dereva leo alikua haongei sana.
Dereva; Mshikaji tutapiga chai Singida.
Mimi; poa.
Dereva; Saa hizi tunaambaa vizuri, mapema tu Singida, leo mshikaji Inshallah mimi nalala Buja.
Mimi; In sha Allah.
Hayukupita muda sana tukawa tupo Singida, imetuchukua kama masaa mawili na nusu hivi. Akaiingiza gari mitaa ya mjini. Kaacha njia kuu akaingia kulia, ndio kuendea katikati ya mji wa Singida.
Dereva: Twende mwanangu, kuna kihoteli kina chakula kizuri sana, kama cha nyumbani. Kufika akanambia hapa ndio ukisikia "utemini", kuna wanawake wazuri hapa kuliko Dubai.
Tukashuka, mimi nikanywa maziwa kwanza, halafu kulikua na mzee nje ya hoteli ameweka mapande ya steki ya ng'ombe anaoka kwenye oven la kienyeji, inatamanisha.
Nikamwambia nikatie nyama, akasema bado kidogo. lakini subiri nikutazamie.
Mwenzangu alikua kishaagiza chai, sambusa na mandazi anapiga, Mimi nikapiga ile nyama ya kuoka na maziwa Nilippomaliza nikawahi kulipa bill yote ili mshikaji asinione mtu wa mserereko. Tukaondoka pale mapema tu, mchana mchana hivi tukaingia Shinyanga.
Nimeiona safari kama fupi, tukaenda moja ka moja kwa kaka yake Jamal wa wimpy ya Dodoma, mzee Ali. Mshikaji akasema nakuwacha hapo utaenda kwenye gari kutokea hapa, gari walipoiweka itanitoa mimi njiani mshikaji; haujali sio?
Mimi; Nashukuru sana, nimefika Shinyanga salama, nakutakia safari njema.
Dereva; Usijali mwanangu, tuwasiliane bwana, mimi nakuja sana Dar kufata haya magari.
Mimi; tutawasiliana, usijali, tuko pamoja mwanangu.
Dereva; umemuonaje lakini yule dada wa Gairo, si anafaa kuolewa yule?
Nikacheka, tu. Mzee Ali akasema mleteni mgeni kahawa, alikua mzee fiti sana, michapo yake akanikumbusha nyumbani. Ikaletwa kahawa pale, nikamwambia zmzee kuna machungwa na mananasi haya imekuwa ndio zawadi yako, ya chalinze haya.
Mzee Ali akasema ahsante sana. Ngoja nikupeleke mimi mwenyewe kwenye gari lenu, nimeshajua wapi, sio mbali ni karibu tu, sema yule dereva sio mwenyeji hapa.
Nikaenda na gari yake Mzee ali, ana Rav 4, anaendesha mwenyewe Tulipofika nikamwambia, ahsante sana Mzeew Ali, wewe unaweza kwenda tu.
Mzee Ali; hapana, sina haraka fannya kazi zako pengine ytahitaji kitu bwana.
Dereva wa truck nilikua nishampigia simu ikawa ananingoja pale, nikashuka nikatinga ovaroli langu, nikachukua mashine yangu nikaibandika kwenye poti yake, iakawa haisomi kitu kabisa, nikacheki betri za gari, terminal zote zipo poa, nikiweka switch on gari inakaa switch on.
Dereva; Bro hii gari mafundi wa Shy wameshindwa, wamesema mpaka ije kompyuta, sasa kompyuta kwani inakwambia nini?
Mimi; Gari hakun mawasiliano baina ya kompyuta ya garii yako kabisa. Kuna fundi waya alikuja hapa?
Dereva: ndio.
Mimi; Unaweza kumwita nijue kafanya nini hapa ili iwe wepesi, itakua kacheza na waya.
Dereva; Ngoja nimpigie simu
Wakati anampigia simu na mimi nikampigia mee nikamueleza tatizo nililokuta.
Mzee wangu kama mchawi wa magari, akanambia huyo fundi kacheza na harness muulize alisafisha ile soketi ya harness mwisho kule yenye kama swichi ndani? Nikamwambia akija nitamuuliza, ngoja jae, mimi bado sijafanya kitu mzee.
Mzee; Akichelewa mimi nitakwambia nini ufanye. Kuna rafiki yangu hapo Shinyanga, nitakurushia namba zake ukimaliza kazi umsalimie. Ukimuona mwambie nataka mchele, nikamwambia poa, nirushie namba, mzee akanirushia namba nikashuka chini ya lori kairbu ya mzee Ali, ile napiga simu nasikia inalia ya mzee Ali, Duh, maajabu haya, nikaona kumbe ni yeye alienileta kwenyue gari.
Mzee Ali; Hii simu umenipigia wewe? Namba yangu alikupa yule dereva?
Mimi ; Hapana kanipa babangu sikujua kama ni wewe, ndio nakupigia hivi,
Mzee Ali; Babako nani?
Nikamfahamisha, akanambia aah, kumbe mwanangu, ngoja nimpigie babako, akampigia palepale, akamweleza kilichotokea wakacheka pale. Mara fundi umeme akaja, akanionesha alichofanya, kweli alikichezea kile kile kitu alichosema mzee.
Mimi; Fundi umekifungua hiki?
Fundi: hapana nimekisafisha tu kwa kutumia spray ya dawa ya mbu.
Nikampigia mzee nikamfahamisha. Akanambia huyo fundi mjinga, hivyo kweli huwa vinakwama, lakini hicho ni plastiki na spray ile ni mafuta makali, amaekiharibu zaidi.
Sasa cha kufanya hapo, hicho kinataka zile bisibisi ndogo za mafundi saa ukifungue ndani, ukikwangue plastiki yote. Halafu kukiosha kwake, hicho chukua baking soda dukani tia maji gilasi moja, weka baking soda vijko viwili vya chakula. Mwambie mzee ali akutafutie fundi saa ukimpata mimi nitamwelekeza namna ya kukifungua. Akifungua kiingize chote kwenye baking soda, iwache kama robo saa, ikaushe vizuri. Hakikisha haina uchafu hata tone, angalia vi swichi vyake vya shaba vidogo sana humo ndani, msivichangue.
Nikamwambia mzee Ali, akanambia twende, tukaingia Shinyanga mjini kabisa, akanipeleka kwa fundi saa mmoja mzee wa kichaga. Kumuona Mzee Ali, Ahha Sharifu upo?
Mzee Ali' Nipo baba, msikilize kijana wangu huyu ana tatizo dogo.
Nikamuelekeza yuke mzee, akasema huna haja ya ya kumpigia mtu, nimeshaona namna ya kuifungua hiyo, akaiweka juu ya meza yake akaanza kuingiza vibisibisi vyake vile vidogo kabisa, kama dakika tu, akanambia kitu hicho. nikusafishie? Kina taka Z plastiki nyingi ndani. Nikamwabia, kisafishe lakini sio kwa mfuta aina yoyote.
Akanambia, mimi sio mjinga, mpira huo ukisafisha na mafuta unaiua hiyo, tena kuna mtu kaisafisha na mafuta, sema kidogo sana. Hiyo tunasafisha na cocacola kijana.
Mzee Ali akacheka, nikamwambia tumia baking soda mangi. Akasema hpo duka la chakula utapata, kumbe wewe fundi kijana, sisi tunatia coca cola inasafisha kama baking soda, nikaleta baking soda. Mzee wa Kichaga ni hodari sana. Vile anavofanya kazi zake kwa utulivu bila wasiwasi, nikaiona kama staili ya mzee wangu, hawana haraka kabisa.
Akachanganya na maji akajaza gilasi, akitia ile swith yote ndani ya yale maji ya baking soda, akanambia haya fundi, hii nusu saa itakua tayari. imeshapona hii, unaona swichi hizo sipo ndani? hiHzi zilikwamishwa na vumbi la plastiki na shaba, zililika sana kwenye plastiki.
Imehapona hii, iwache nusu saa, nitakisafishia ndani hiyo, inakua mpya kuliko ulaya. kama kuna swith haifai tutaibadili, usijali
Tulipomaliza akairudishia vizuri kabisa, akanambia nenda kaijaribu, hiyo ikifanya kazi ilete tuipige sili na super glue.
Tukarudi nacho kwenye gari, njiani nikampigia Mzee nikamueleza kuhusu fundi saa, Mchaga na cocacola, akasema huyo anajua. Basi usiwe na wasiwasi ulivyonieleza tu nimejua huyo fundi mzuri. Nikamwambia anatengenea mpaka saa za betri. Akasema, haya testi sasa italeta moto kwenye komputa, ikileta fanya test zako muiwashe.
Dah kuiweka komputa ikasoma kama kawaida, ikawa inainipa error ya swith ya injection. hizo nazijuliamnikaichomoa switch ile ya injection, nikaiweka sawa dakika mbili tu, kuiridishia, komputa kusoma, ikatoa majibu kila kitu bomba.
Kuipiga gari start, nusu kiki tu, chuma kikanguruma , nikamwambia Mzee. Akanambia, haya bwana gfundi mwache dereva wa watu aanze safari yake, gari ishapona hio.
Nikarudi kwa mzee Ali akanizuia nilale pale. ndio mambo ya majini yakaanza pale kwake. Kama Mungu alinipeleka pale.
Itaendelea.