Bongo senior
JF-Expert Member
- Nov 22, 2015
- 757
- 1,526
Ila habari za k/koo kuhusishwa na mauza uza sijaanza kusikia leo kuna mtu aliwahi nambia wale wanaouza asilimia kubwa si binadam kama tunavyowaona.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora hata nisome story maana jpili ishaanza kua ndefuMpaji Mungu kilinge hiki hapa😃
Babu ana chimbo lake boya yoyote hawezi ingiaWe bwana mdigo leta mambo hayo au bado unakula kamba wako ,kamba kutoka kidimbwi maalum anakijua babu yako tu hiko kidimbwi😅😅🤣
Kwetu msimu wa kamba zinakuja fuso za friji kuwabeba.Hii ni Story Kamba. Ni KAMBA MWANZO MWISHO.MPAKA KIKAPU KIMEJAA KAMBA
Babu yangu alijaaliwa maarifa siku nyingi sana. Alijichagulia hiyo sehemu ambayo watu wote walikua wanaiogoppa. ikawa kajichagulia katikati ya matawi mawili ya mto ambayo yote,a yanatoa kamba kwa wingi wakati wa msimu, lile tawi kubwala mashariki na lile lenye mapango ya kiajabu, yote yapo kwenye eneo la shamba lake. Ule mto wa Mashariki ndio kwa upande wa pili jamii wanapata kuvuna msimu wa kamba, mto ule ndio mpaka wa shambani kwetu, huu mto wa Magharibi ni tawi dogo tu lisilokauka, linapita katikati ya shamba letu, mapango mawili makubwa moja ni kama ukumbi tu mkubwa, hayakutani kwa ndani, yote yapo ndani ya shamba letu.We bwana mdigo leta mambo hayo au bado unakula kamba wako ,kamba kutoka kidimbwi maalum anakijua babu yako tu hiko kidimbwi😅😅🤣
Kamba.... Na wewe umeamua kutufunga kamba. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Mleta mada kaeleza mambo mengi makubwa ila juu juu (siwezi sema kakosea maana target yake ni kufikisha ujumbe kuhusu alichokiona baada ya kufunguka macho, na alhamdulillah ujumbe umefika,,,, japo utata umebaki mwingi kwenye vichwa vya watu)
Ngoja nisawazishe eneo dogo hapa kwajinsi ninavyoelewa!!
Mada kubwa mezani ni SPIRITUAL AWAKENING
Viumbe wa kiroho... Ni viumbe wote ambao hawaonekani kwa macho ya kawaida (malaika, majin n.k kila mtu anawafaham kwa mujibu wa imani yake) viumbe Hawa huwa na connection kwa watu maalum pekee
Watu maalum ni hawa 👉 Manabii na mitume, wachamungu sana, waganga wa kichawi na watu waliopendelewa
Ili uwe kwenye special group lazima uwe connected na source of power yoyote kati ya hizi
A. Mungu
B. Ibiris
Sasa viumbe wa kiroho wao pia wapo makundi mawili tu.... Kutokana na uanachama wao kweny hizo source of power (hapo either awe upande wa Mungu au Shetani🤝
Sasa hao special group pia wananamna yao ya kuwasiliana na hao viumbe.....
Baadhi ni hisia, ndoto, telepathy na kuona
(Hii njia ya kuona ndio njia ya juu zaidi tuseme ndio maqam ya mwisho.... Sasa huwa unaanza kwa kupanda daraja
Utaanza njia ya hisia, ndoto, telepathy mwisho utaona🤝
Mleta mada yupo kwenye special group upande wa watu waliopendelewa... Maana hajafata process wala hajaandaliwa ila karushwa daraja moja kwa moja
(Kwa imani ya kiislam huwa Kuna watu wanazaliwa wakiwa n mawalii wa Mwenyezi Mungu,,,,, kitu ambacho n nadra sana mtu kukipata
Au mfano mtu ufanye ibada mpk uwe nabii😁😁😁🏃
Ngum sana, nabii huzaliwa akiwa tayar ni nabii
(Dah mambo ya kiroho huwa yanamaelezo mengi sana...... Ila ukiweza kuwasiliana na viumbe wa kiroho hii Dunia umeiweza🤝
Njaa kwako sahau, kuonewa kwako sahau, kukataliwa kwako sahau,,, hii ni Siri ambayo wazungu wanaitumia sana
Ushuhuda:
Baba yangu alikuwa na uwezo wa kwenda kwenye mlima wowote au mto mkubwa, akifika anawaita watawala wa huo mto au mlima wanakuja live anawaeleza anataka nn kutoka kweny himaya yao halafu wakielewana kazi kwisha
(Anaenda kweny kaburi la mtu aliyekufa anamuamsha anaongea nae akimaliza anarudi kulala..... (Najua hapa ntaonekana muongo)
Anazama kweny maji anatoka mkavu bila kuloana
Anaweza kuchukua ile sarafu ya zaman inayotafutwa kila kona
SIMBA MBILI au Rupia (akafanya yake akamtoa yule Simba na king George wakakaa na kuanza mazungumzo
Alikuwa na uwezo wa ajabu sana.....
Note: source yake ya Power haikuwa GOD
(Kwenye hii Dunia ukitaka kuwa mtu hatari we chagua njia moja upite hiyo kikamilifu utaona balaa lake.... Kama n Mungu swali sana acha dhambi kwa ukamilifu wake utaona utavyokuwa hatari
Kama n upande wa shetwani... Roga sana, usisite kutoa mtu kafara Yani kuwa nyambisi haswaa utaona ibiris atavyokupenda😂
Fanya juu chini upate mapenzi either ya Mungu au Ibiris.... Usikubali kukaa katikati maana utakuwa mtumwa
Hivi hilo jina .... Arsis ndo hili Osiris (au hao ni wawili tofautiInatokea post namba 155.
Baada ya kuagana na Arsis nikaenda kwenye gari, nikaondoka bila kukuta na yeyote, nilipofika nyumbani, mlinzi akanifungulia geti bila kuita au kupiga honi, nikaaiweka gari, nikaingia chumbani kwangu kulala. Usingizi ukawa hauji haraka. Nikaanza kuitazama ile pete, nikachukua mkebe wake nikautazama vizuri. Ulikua ni mkebe wa kizamani sana, ulikua na maandishi maatatu kama michoro yale ya Kimisri ya zamani. Nikasema nikikutana na Arsis nitamuuliza kimeandikwa nini. Nikarudisha mkebe, nikaichukua bakora nikawa naichezea, nailaza chini inanyanyuka yenyewe, naiweka upande inajisimamisha yenyewe. Mpaka nikawa nacheka tu mimi mwenyewe, Bakora haikubali kulala chini kabisa. Nikaiweka pembeni ya kitanda changu. Nikalala.
Maisha yakaendelea kama vile kabla sijaenda Tanga, haikupita muda nrefu nikawa noimeshafu ga ndoa, ilikua ndoa ya surporise kubwa kwangu, lakini hapa sio pahala kwake kuielezea.
Kuna siku, baada ya kama miezi miwili mitatu ya kuoa, nikasema leo ngoja nikamtembelee "mama mkwe" wa kwenye vitumbua asubuhi subuhi, lakini toka siku niliyoyaona Chalinze na pale kwao nikawa naogopa kula kwa mama lishe. Nikajisemea wacha niende tu nikawagtembelee. Kufika, mama mkwe akawa na bashasha kweli, "Ah bwna harusi, leo umefunguliwa?" Nikamwambia "mboina jamani saba iliisha siku nyingi/". Aaah huonekani nikajua "honey moon zenu, mwezi umekwisha bwana harusi huonekani" Nikamwabia aah si unajua tena, maisha ya ndoa tofauti na ya zamani. Akanambia "tena yafurahie bado ungali una nguvu mwanangu, usicheze na furaha yako hata kidogo> Nikamwambia 'poa".
Akanambia haya nikjupe vingapoi leo? Nikamwambia nimekuja kulusalimia tu, nyumbani si wameshakuja kuchukua? Akanambia haya kula viwili, imi ingawa hukumngoja bintoi yangu lakini najua kuna siku uytamuoa tu, ukwe uko pale pale. Nikamwabi tulikua nae harusini, kumbe ni partner mkubwa wa mke wangu. Khaa, nyinyi mmetufanyia voituko vinaogelewa Ilala nzima hii, miaka yote sisi tunajua yule dadako kumbe mmelelewa pamoja tu. Nikamwabia hata mimi nilikua najua tumezaliwa pamoja. Kumbe ni watoto wa mjomba na shangazi.
Mama mkwe; Aaahmkeo na binti yangu umesahau toka wadogo wako pamoja? Mimi nimewaambia na huyo mume atawaoa wote mkae pamoja.
Mimi; Mimi poa tu, wakikubaliana wenyewe mimi nipo. Niakbadilisha topis, vipi mama wa mandazi, sijamuona toka siku ile ya pirika?
Mama Mkwe: Kwani yaliompta madogo mwanangu, si kashikwa anawanga huko buguruni. Kututukana na kutuita sisi wachawi, kumbe yeye ndio mchawi.
Mimi; hatari kubwa, sina habari.
Mama mkwe: Makubwa mwanangu hata hayasemeki. Alikua anaongea huku ananong'ona. Tena hapa mwezi ujao hatupo tena, hii nyumba imeshauzwa, tunatafuta kijiwe kingine hivi sasa. lakini mimmisina wasiwasi, nitakua nyumbani kwangu palepale, hakuna wa kunihamisha, pale kwangu mwenyewe. Nitapika pale nitakwenda kuuza vitumbua vyangu pale nje ya msikitini mpaka tupate kijiwe.
Mimi: Kumbe tuko wote, hakuna tabu. Usihame kijiwe kipya bila kunijiulisha.
Mama mkwe: Kumbe huna habari? Wenye nyumba hii washama wote, wameiuza nyumba haraka haraka kwa aibu, kumbe walikua chama kimoja nayule muuza mandazi. Wameaibishwa wote, kwa aibu na jiji wamelihama.
Mimi; Kasheshe.
Mama mkwe, lakini toka wameondoka, hata uzito na mazonge zonge yamepungua, kumbe tunaishi na wanga hapahapa, sasa hivi baba kijiwe kimesafoshwa hiki, mbao walikua hawaji sasa wanakuja.
Mimi; Kwani aliepanunua kawaambia muhame?
Mama mkwe; Wala hajatwambia tena mteja wetu mzuri, anakaa hapo mtaa wa nyuma, shogake mamako , yule mwanamke mpambe wa Kiarabu? Aaah, nimeshamjua, ndio nilisikia kanunua nyumba nyingine, kumbe ndio hii?
Mama mkwe; Pesa imetulia pale kachukua hii na ya nyuma yake, zote kwa pamoja, pesa cash nq sisi wotw hapa tukapata sadaka yetu nono, tenono kweli kweli. Hatuna manug'uniko wala masikitiko. Hatutaki tumewekee kiza akianza ujenzi, mwenyewe kasema hachelewi ataanza ujenzi. Sisi tumeona wala hana ya kutwambia tuhame, tumeishi nae kama ndugu miaka yote. tena mwenzetu sana yule Mwarabu, sisi tumefurahi kununua yeye hizi nyumba, maana yule na mamako ndio kimbilio letu tukiwa na shida zetu. mwenyezi Mungu awajaalie kila heri, akapiga dua ndegu hapo. Kabla hajamaliza, mama muuza uji akasema bwana harusi kombe lako hili la uji, usiseme umeshiba nimekuongezea pilipili manga njia za mkojo zifunguke vizuri.
Mama mkwe: Kwani alikwambia ana shida na njia yake?
Uji: Koma bibi wee, sisi tunajua kutunza mabwana harusi, Watanga mwenzangu huyi, ulikua hujui?
Mama mkwe: Nawaju, wote wadigoi nyinyi.
Uji: Kwa hio usituingilie kabisa, tuwachie wenyewe. Bwana harusi usimsikilize huyumzaramo, hana alijualo zaidi kutingisha makalio tu.
Mama mkwe; Mboina unamwaga razi kwa mkwe wangu?
Uji; Tupishe huko, tukaoe mzaramo sisi hatuna akili? Nyie ndio mje kuoa kwetu msiojua kupika nyinyi.
Mama mkwe: Mkwe wangu usimsikilize huyu bibi, hata huko kwao Tanga kapasahau, toka aolewe hajaenda hata kutemnbea kwao, mzaramo alivyo mdhibiti.
Mimi; Jamani nilikua nataka kuwauliza kitu.
Wakakaa kimya wote wananisukiliza.
Mimi; Hivi kwanini hamuweki kijiwe kwenu pale msikitini kwa pembeni pale, uwanja mkubwa tu, hata mkiwa ishirini mtaenea pale.
Uji: Hwa wazaramo hawataki msikitini, wanga wakubwa wanapaogopa, mimi uji wangu nauanza na watu wa msikitini alfajiri, wakitoka tu msikitini wapo hapa. Hawa wanakua bado wamulalia.
Mama mkwe: Wewe mboina una mdomoi mchafu mbele ya mkwe wangu?
Uji: Nisamehe baba, mimi uji niytauuzia pale pale msikitini nikiondoka hapa, nimeshaongea na imamu kasema mradi nisipike pale tu, msikiti unatakiwa uwe msfi njje na ndani. Kai kwa hawa wachoma vitumbua na wapika chapati, watapoikia wapi pale?
Mama mkwe; Tutaongea na msikiti nyum aple tutapajenga wenyewe.
Uji; Hilo wameshakataa kama ulikua hujui, wanasema muda si mrefu msikiti unaongezwa ule unakua mkubwa na tena wagorogfa.
Mama mkwe: Hili nimesikia hata kimi, lakini hawajui lini utaanza lini.
Uji; Umelala wewe, msikiti kabla nyinyi hamjaondoka hapa utakua umeshaanza kujengwa.
Mama mke: basi poa, tutawauzia hao hao wanaokuja kujenga, tutabanana nao hapo hapo, watakula wapi?
Uji; Tena pla cheyameni wa wauzaji chkula mimi, mtanilipa mimi kila siku, mkitaka biashara pale.
Mama mkwe: Mdigo wacha utapeli wa mali ya msikiti, huo u cheyameni akupe nani wewe mwenzangu na mimi, nipishe huko.
Nikaona niage. Nikaaga nikapondoka zangu, uji kweli ulikua na pilipili manga ya ziada.
Utaendelea.
😂😂😂😂😂😂😂..... Haya mambo huwa yapo hvyo, ukisikia lazima uone ni kamba!!!Kamba.... Na wewe umeamua kutufunga kamba. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Ni tofauti kabisa, umewahi sana kuliuliza, niliwahi kumuuliza Arsis akanijibu;Hivi hilo jina .... Arsis ndo hili Osiris (au hao ni wawili tofauti
Tutafurahi kukusoma kisa chako. Hivi vitu vya viumbe visivyoonekana, ambao hawajakutana navyo hawawezi kuamini.😂😂😂😂😂😂😂..... Haya mambo huwa yapo hvyo, ukisikia lazima uone ni kamba!!!
Siku nikiamka vizuri ntaleta kisa changu hapa.
(Maana mm nilikabidhiwa kwa mashetwan toka nikiwa mdogo, baadae wakasalitiwa nikanyang'anywa mikononi mwao ilikuwa n vita kali sana..... Wakamgeuka mzee wangu wakamuua kikatili, mzee akaona ni bora yeye afe kuliko mwanae awe mfalme wa mashetwan na wachawi🚶🚶
Siku moja nikiamka vizuri ntaisimamisha jf kwa muda😂
Maana ni visa vya mfululizo kwanzia miaka 4 mpk Sasa hivi nnavyoandika hii comment bado vita inaendelea 🏃
Daah shukran sana ndo namaliza kusoma hapa ulipoishia alfajir hii, napata funzo kubwa sana kuhusu ulimwengu usioonekana. Naamini kabisa hasa kulingana na uzoefu wa nloyapitia mpaka Sasa. NakusubirInagtokea post namba 174.
Maisha yakaendelea, koo za ki simba na mambo na nidhami, zake ambazo sitaki kuzihusisha sana na hiki kisa cha viumbe wasioonekana.
Kitu kimoja kingine muhimu kilinitokea safarini, nilikua nasafiri na gari kubwa, nimepewa lift na mteja wetu mmoja tunaemtengezea gari zake, alikua anaelekea Mwanza na mimi naelekea Shinyanga kwa kazi nilotumwa na mzee, kazi zetu za ufundi.
Tumeondoka Dar vizuri Alfajiri sana, dereva akanmbia ana mke mdogo hapo mbele kidogo ya Kongowe , Kibaha.ka hiyo atasimama hapo kwa muda awasalimie, mimi kama ninaharaka sana atanitafutia lifti hapo check point ya TRA ndipo alipo paki gari, alisema hapo kuna usalama zaidi kwa gari. Nikamwabia, wewe nenda tu, nikiondoka nitakupigia simu. Akachukua boda boda akamwacha kwenye gari utingoi wake na mimi nikashuka, kuna vijimgahawa vingi vingi tu, pako na heka heka nyingi za hapa na pale.
Nikaingia kwenye kimgahawa kimoja, nikaagiza maziwa ya moto Nikaletewa, kulikua na mtu mje hapo anakaanga chips kuku wanaukia, ikanijia hamu, nikasema ngoja nile kuku, kumtazama vizuri yule mtru nikaona mwiko anaoopolea kuku umekaa kiajabu ajabu, kuutazama umekaa kama mikono ya mtu iliokauka kaboisa kwa moto. Nikataka ku panic, ikanijia sauti ya Arsis, ikanambia tulizana, kawaida tu hiyo. Nikanyamaza, nikatazama kimgahawa kingine nikaona kuna mwanamke kakaa kama namfahamu hivi, nikasema ngoja nikamuone, kufika nikamuona ni yule mwanamke wa kijini nilijulishwa nae mapangoni kwa babu. Akacheka, akanambia kaaa tuongee. Nikakaa.
Jini 1; Umeoina maboi yale?
Mimi: Dah, nini kile?
Jin1: mkono wa mtu ule wa siku nyingi sana umekaushwa ndio umegeuzwa mwiko wa chipsi.
Mimi; na zile chipsi kweli?
Jini 1; pale hakuna kisicho cha kweli isipokua huo mkono tu.
Mimi: Makubwa haya, na maziwa nimeshjindwa kuyamalizia.
Jini 1; Maziwa mazuri yale, maziwa mazuri yale, hayahusiani kabisa na yule mchawi anaechoma chipsi. Uchawi wa kijinga hauna faida yoyote kwake, basi kuamini tu, mkono ule wa maiti, kabla haijaoza, umekaushwa, wanajua wenyewe wachawi wanavyoukausha. Wanawauzia hawa wanaopenda ushirikina, lakini hauna maana yoyote.
Mimi; Sasa kwanini anautumia?
Jini 1; Wanasema unazidisha ladha ya chakula kiki[pikiwa na ukipakuliwa na ule mkono basi mlaji huwezi kuisahau ladha yake, siku nyingine utarudi tu kula tena.
Mimi; Na inakua hivyo?
Jini 1; Ule una faida moja tu kwake, lakini haelewi, faida yake ni wale wanga na wachawi, wakija kununua chpsi wakiuona wanaelewa ndio wanakua wateja wakubwa, maana wao kula nyama za watu ni kawaida kabisa, lakini kwa mtua siye mwanga wala mchawi hauna lolote zaidi ya kiini macho tu, hauoni wala hajui.
Mimi; Hatari hii.
Jini 1; utayaona mengi, mimi sikuja kwa ajili ya huo mkono, mimi nimekuja kukwambia usiende na hii gari, huyu dreva kaenda kufanya mamboi ya kishirikina, asafiri mpaka apite kwa huyo bibi yake aliekwenda amtzamie safari itakuwaje. Ni ushirikina tu, Nilikua nasubiri ushuke nikufahamishe hilo, wewe chukua mzigo wako uondoke. Mimi nilikua na nyinyi kwenye gari, sikutaka hata wewe unione, ungestuka.
Mimi; Ngoja nikachukue vutu vyangu safari imekua chungu hii.
Jini 1; Mwombe Mungu atakjulinda, sisi ni msaada tu lakini mwenye kukulinda wewe na sisi ni Mwenyezi Mungu tu. Tazama kule upande wa pili wa barabara kwenye ile bar.
Nikatazama snikawa siamini ninachokiona.
Mimi; Masanamu yale?
Jini 1; wati wale, kuna sanamu linaongea namna ile, nenda kawatazame vizuri, utawaona watakukaribisha, wenzako wanataka wateja wale.
Mimi; Wateja wa nini?
Jini 1; Wewe nenda ukajionee, usishtuke na jifanye hujui kitu. Mimi nipo nakungoja urudi nikusindikize upande gari.
Niaksogea, kuna bar pale, wasicha watatu wamekaa nusu uchi kabisa, lakini kwa kawaida unawaona wapo vizuri, kuatazama kwa macho yaliofunguliwa, ndio nikaona, wana makucha marefu, wachafu sana, nywele zao zipo hovyo hovyo, kwa ufupi wanatisha. Kufika, mmoja akaanza, "kaka karibu ukae hapa, kuna huduma zote hapa", nikamwabia mimi nilikua namtafuta mtu, kanambia atakua maeneo haya. Akasema "msubiri mpenzi, kaa na mimi hapa" kaa nikununulie kinyaji gani, usijali mimi nataka mtu wa kuongea nae tu. Wale wengine wananitazama huku wananishekea, chekea, mara mmoja anioneshe maziwa yake, yamelala kabisa, mwengie ajipapase papase mapaja.
Nikatazama kule kwa kwa jini sikumuona lakini nikaona kuna watu wengine wamekaa pale. Nikawaambia ahsanteni niliokua namtafuta nimemuona. Yule mwanamke akanambia, kamuone uje nae basi. mimi sina haja ya poesa zako, nataka nikakufurahishe tum nafanya hata masaji, nitakunyoa, kama unasafiri nikutoe mchoko wote. Nikamwabia pao, wacha nimuone mwenzangu, nitafanya bidii nijae nae. Nikaondoka, ile nakaribia pale kwenye imgahawa naona tule jini anatokea barabata kubwa huku anacheka anacheka.
Jini 1: bado upo? Nimeshkupati mtu atakupakia kwenye gari ndogo. Nimetoka kukutafutia lifti.
Mimi; Wapi?
Jini 1; Pale barabara kubwa kwenye kona, hujaona wale polisi, mmoja wa kikwe mmoja wa kiume?
Mimi; Nakumbuka niliwaona tulivyokua tunaingia hapa.
Jini 1; Yule mwanamke ana jini la kiume la kichawi linamlinda, nimeongea nalo, majini wa kichawi mimi wananiogopa sana usinione hivi Akacheka. Taayari kasema anajua cha kufanya yule mwanamke akusimamishie gari uende, mimi nimeshaongea nae yule askari, anajua mimi binadam, tena dada yako, haya twende.
Nikaondoka nataka kuelekea kwenye gari nikaona yule msaidizi wa dereva anakuja na begi langu, jini akanambia nishamwambia akuletee begi lako, mwache alibebe mpaka barabarani, nikamwabia, hapana, ni jepesi halina uzito wowote.
Nikachukue begi langu nikamwabia ahsante, nikachukua simu nimpigie yule dereva, nikapiga simu ikawa haipatikani kabisa. Nikaanz akufatana na jini kuelekea barabara kubwa, kufika nakuta yule askari wa kike anaongea na gari iko pembeni, gari ndogo tu.
Askari: Haya mwabie aje, gari hii hapa, mdogo wako handsome, kwanini ulimficha huko?
Jini 21; Wacha utani bwana.
Askari; Sitanii, ataniwachia namna zake, ukiwa unarudi nipigie utakua mgeni wangu.
Mimi ; Nikacheka, unaitia aibu mbelke ya dada hapa.
Askari: usijali, mbo9na dadako yupo poa tu. Hya dereva huyu ndugu yangu, asije kunambia mmemtoza pesa, tena uhakikishe anakula vizuri njiani.
Dereva" Poa afande, leo mbona hujanipa bahasha ya kwenda kwenu?
Askari; Sikupi muhuni wewe, unataka kunichapa.haya nendeni bwana, nipo kazini.
Mimi: Ahsante afande.
Askatri, huondoki hapa nila muiniwachia namna nilizotaka. Nikamtajia namba zangu akapiga wakati huo huo nikawa nimeipata namba yake, Jini akasema mimi jamni mtanishusha Mlandizi hapo, akapanda nyuma. Tukaondoka.
Kufika Mlandizi yule dreva akasimama Jini 1 akashuka, aksema nipe dakika moja tu niongee na mdogo wamgu. Nikashuka.
Jini1; Haya niliingia kuhakikisha kuna usalama, ytuko poa, hehe mwenzzako huyo, safari njjema. Akaondoka huyo, nikaingia kwenye gari tukaanza safari. Nikawa anongea ongea na dereva, akanambia bro tutasimama kidogo Chalinze ninunue zawadi pale kama kuna mananasi na machungwa. Mie kwetu Dodoma, lakini napeleka hizi garu za transit Bujumbura. Sikai sana Chalinze,
Mimi; Poa, usijali tuko pamoja.
Itaendelea.