Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Hakuna tabu kabisa, unaonesha posts unaziruka, kasome hii, binya link: Umeziona aya za Qur'an?

Msiwe na haraka, elimu kubwa haitaki haraka. Someni kwa umakini tu. Huu sio uzi wa kuufanyia haraka.
Simba.
Ili twende sawa aya unaweza ukasoma na usielewe vizuri sidhani kama Quran inakataza kumpa mtu ufafanuzi.

Hiyo aya iko wazi mashetani yamtumikie mtume, vipi kwa waislamu?
 
Arsis,

Nimeyakuta haya kwenye uzi huko jukwaa lingine, tupe ujuzi wako kuhusu haya mambo👇🏾

 
usishau tu kua Mtume Muhammad alikua ni Mtume kwa majini pia. Ai sivyo?
Ni kweli , swali langu linarudi kwako.. je aliwatumia kuagua watu, aliwafuga ? alikuwa na rafiki ambaye ni jini? aliwahi kukaa kumuita jini amtume mahali ? je hao wanaofanya hivyo na kuhusisha na uislam wameyatoa wapi hayo ?

Hoja hii nilishajibu hapo Juu huo ni uwezo alipewa suleiman tu, na kumbuka ombi lake kwa Allah unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu Je wewe ni nani ujimilikishe majini na kuyatuma au kuagua watu Ndio maana Mtume hakuvuka huo mstari sio kwamba hawezi alikuwa na uwezo wa kuyafanya lakini hakuyafanya na hakuwahi wafundisha maswahaba zake kuyafanya hayo...

Napenda kukufahamisha, kua tusifikie kuhukumu watu kwa elimu chache tulio nayo.
Haki lazima isemwe na Batili lazima ikemewe , na uzushi katika dini lazima upingwe VITA , tusipofanya hivyo hawa wachawi wanaovaa mapete ya rangi za kila aina , wasoma nyota , wafuga majini ndio wataonekana mashekh mwisho wa siku watakuwa watoaji fatwa katika jamii ya kiislam na kuzidi kuwapoteza ...

Uislam ni Rahisi sana Kufuata mafundisho ya Mtume pamoja na matendo yake na matendo ya wajawema waliotangulia katika zile karne tatu .. kabla hujafanya jambo jiulize JE MTUME ALIFANYA KAMA HAJAFANYA NI BIDAA NA KILA BIDAA NI UZUSHI NA KILA MZUSHI KATIKA DINI ATAINGIA MOTONI...

RASOOL ALLAH S.W.A ALIWAHI FUGA MAJINI, AU KUWATUMIA MAJINI KATIKA KUSAMBAZA UISLAM AU TIBA ..? SIMPLY HAPANA NA ,KILA MWENYE KUYAFANYA HAYO NI MCHAWI
 

Uchawi umekatazwa kwa Waislam na viumbe wote.

Mtume Muhammad katuletea Qur'an ambayo ni mwongozo wetu.

Unafahamu maaana ya jini?

Mimi nakushauri, kama nilivyoandika nyuma huko, wakati tunaendelea na kisa cha Adam tutaleta habari za majini kutokea kwenye Qur'an, kama hujui majini ni nini nakushauri uwe na subira, una mengi sana ya kufaidika nayo.

Maswali ya kielimu hayawi kama utakavyo wewe, labda uwe unajua unachokiuliza ni nini na una ushahidi nacho. mfano unauliza kuhusu kufuga majini, wewe uliona au ulisoma wapi majini yanafugwa? Au ndio kinachoitwa "heresy" Kingereza?
Simba.
 
Maswali yako yamenikumbusha, niliwahi kuuliza haya kwenye post aliyoileta Lidafo, nikaomba yeyote anayeweza kujibu ajibu👇🏾
Binafsi naona suala la Majinni linaenda sambamba na suala la Adam.

Kwa mtazamo wangu zote ni lebo tu.

Naomba kuuliza swali, kwako au yeyote yule anaeweza kujibu, ikiwemo Arsis.

Hivi ni nini tofauti ya Iblis, afrit, jinni, jaan, insan, bashar, shetan, adam, Khalifa, malaika, ruh, nafs qareen, nabii, rasul?

Yote hayo yapo kwenye Qur'an.
 

Bwana Simba ... Rasool Allah ameshushiwa quran na kutuachia kama muongozo nakubali kabisa. Hakuna muislam asiyejua tofauti ya majini na mashetani.. Ulimwengu wa majini ni moja ya aina ya ulimwengu ambao unaozungukwa na uwezo wa Allah, na kuamini kwake ni sehemu ya imani ya ghaibu.. Majini ni viumbe kama walivyo viumbe wengine wa Allah ,wapo waliowema ambao hawajihusishi kabisa na maisha ya wanadamu wana maisha yao kadri Allah alivyowakadiria na shetani ni sifa anaweza akawa nayo binadamu au Jini ..
Majini wana majukumu kama wanadamu na wataulizwa juu ya matendo yao, kama watakavyoulizwa wanadamu, kama ilivyoelezwa katika Qur'an katika aya hizi: {Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii.} [Al-Anaam: 130], nakatika aya nyingine Mwenyezi Mungu anasema: {Tutakuhisabuni enyi makundi mawili} [AR-RAHMAAN: 31].
Mwenyezi Mungu alisema katika Quraani kwamba majini wanasema: {Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.} [AL-JINN: 11].
Na jini lolote linaloingia mwilini mwa binadamu basi hilo lishakua ni adui wa Allah na usitarajie mazuri toka kwake zaidi ya kuzidi kukupoteza...

Tatizo unarukaruka yote hii kutaka kunasabisha utumikishaji wa majini na uislamu ukishavuka huo mpaka Hui tena muislam bali ni mshirikina .. na ni mchawi

Haqi itabaki kubwa haqi na batili itabaki kuwa batili ..
 
Ni kweli , swali langu linarudi kwako.. je aliwatumia kuagua watu, aliwafuga ?
Kwanza kabla sijakupa jibu, nikupe elimu ndogo tu. Ngoja nikukate maswali yako niwache swali moja tiulijadili, tukimaliza tutaenda lingine. Hatuna haraka wala "time limit". Uzi upo hapa na posts zipo hapa.

Nilikujibu juu kidogo hapo lakini naona hukuelewa. Maana unachanganya mambo ya uzushi (heresy) mengi mengi kwa pamoja.

Usidhani kuuliza maswali mengi ya kuzusha ndio kuelewa au kujuwa sana. Hiyo kingereza inaitwa "ignorance fallacy" Kiswahili chake ni uongo wa ujinga.

Ili kukuonesha kua huo wako ni "uongo wa ujinga", inatakiwa kwanza utueleze na ijulikane umelitoa wapi hilo swali kielimu; Nani "aliwafuga" na "waliofugwa" ni nani?

Raha ya elimu ya Uislam, ni lazima kipatikane chanzo (source), kama hauna chanzo inabaki kua ni uzushi wako b9nafsi.
Simba.
 
Nimekupata, ndiyo ile "iliterate people of the 21st century are not those who can't read or write. illiterate people of the 21st century are those who learn but can't unlearn and relearn".
Kabisa, umeiweka vizuri kabisa kuliko ninavoiweka mimi Kiswahili.

Naamini hata njiwa ameelewa maana yake.
Simba.
 
Nakumbuka kama nilikwambia usubiri, naendelea kukwambia usubiri. Kuna mada yake inakuja kama ulivosema wewe, inaenda sambamba na ya adam, kwani kwenye kisa cha adam baadhi ya hayo yametajwa.

Kuwa na subira, mambo mazuri hayataki haraka,
Simba.
 

Umejitahidi lakini bahati mbaya unajichanganya sana na badot unahitaji elimu zaidi.

Ili kuendelea kuelimishana; Umeelewa maana ya Qareen na walivoielezea waliojibu wawili ulipokua bado hujaielewa? kutoka watafsiri wa Qur'an, wengne wamesema "Jini", wengine "Malaika", wengine "shetani". Au sivyo?

Wewe umeelewa vipi mpaka sasa kuhusu Qareen?
Simba.
 

Simba unazunguka sana haya kutokana na tafsiri za watu tofauti Quran ina jibu moja tu kwa waumini Surat Baqara aya ya pili simply ni ghaibu " the unseen " nimescreen shot Aya ya pili ... Basi mimi ni miongoni mwao hilo kundi .. naamini Ghaibu lakini sipetuki mipaka inatosha kwa muumini kuamini na hakuna muislamu asiyeamini katika ghaibu so simply kwangu mimi qareen naiweka katika kundi la ghaibu ..

Narudia tena hauna elimu mpya itakayotoa RasoolAllah amemaliza kila kitu na yeye ndio kiigizo chetu .. unless ukatae kwako wewe si kiigizo ... mipaka yake katika viumbe hao wengine inajulikana na hakuwa na rafiki upande wa majini wala kuwatumikisha vyovyote vile ... Kwani kufanya hivyo ni kupetuka mipaka ...
 

Attachments

  • Screenshot_20240922-223729_Quran - Swahili Translation.jpg
    218.8 KB · Views: 7

Salaala , umeng'ang'ana kufuga .. bahati nzuri mimi ni mwenyeji na mzaliwa wahukuhuko ulipokwenda kulazwa pangoni na babu yako ..... Nadhani pia uliongea jambo kwamba sijui ulikuta pete chini ya mto na hiyo pete ili isiibiwe unaweka kwenye kasha fulani ... Ndio mifugo wako huo ....

Simba Basi achana na maswali yooote naomba ujibu hili nipe dalili katika Quran na Sunna Mtume Mohamad SAW kuwa aliwahi kuwatumia au kutumikisha Majini ?! Nielimishe mwalimu..
 
Naona umerudia tena "ignorance fallacy".

Hayo yote unaoyasema hayajajibu swali langu. Au huelewi unachokisoma hata nilipoacha swali moja tu? Rudia;

Kwanza kabla sijakupa jibu, nikupe elimu ndogo tu. Ngoja nikukate maswali yako niwache swali moja tiulijadili, tukimaliza tutaenda lingine. Hatuna haraka wala "time limit". Uzi upo hapa na posts zipo hapa.

Nilikujibu juu kidogo hapo lakini naona hukuelewa. Maana unachanganya mambo ya uzushi (heresy) mengi mengi kwa pamoja.

Usidhani kuuliza maswali mengi ya kuzusha ndio kuelewa au kujuwa sana. Hiyo kingereza inaitwa "ignorance fallacy" Kiswahili chake ni uongo wa ujinga.

Ili kukuonesha kua huo wako ni "uongo wa ujinga", inatakiwa kwanza utueleze na ijulikane umelitoa wapi hilo swali kielimu; Nani "aliwafuga" na "waliofugwa" ni nani?

Raha ya elimu ya Uislam, ni lazima kipatikane chanzo (source), kama hauna chanzo inabaki kua ni uzushi wako binafsi.
 
Sijakuelewa wewe kama nani?

njiwa
Sielewi mwenzetu kama nani ki ilm mpaka uamue "unaiweka... "?

Kwa ilm ipi ulionayo mpaka ukafikia kufanya hivyo?

Isijekuwa tuna Alim wa kiwango cha kutowa fatwa hatukuelewi?
 

Kisa cha Adam 1.

Salamoun Alaykum!

Leo katika muendelezo wetu wa Kisa cha Adam nitaanza na mada ambayo nilisita sana kuiwasilisha jukwaani kwa sababu mbili kuu.

Sababu ya kwanza; ni kua mada hii ni ndefu na inabidi mnivumilie kwani inabidi tuifanyie tafsil kwa kina bila kuacha kitu kikielea (hangig). Tutaitumia sana mbinu ya kiota, kufata na kuonesha maana kusudiwa katika aya zingine au lilipotumika neno kama tunalolifanyia ‘tafsil”.

Sababu ya pili hii mada itakua na mshtuko (shocker) utaotutikisa kidogo uelewawetu, hususan kwa wale wote ambao hawapendi kuisoma Qur’an kama ilivyo na hupenda kuongezea maneno ya watafsiri hata kama hayamo kwenye Qur’an.

Mtikisoko utakua wa ziadsia kua kwa miaka mingi tumefata na kuamini mambo kwa kufata watu ambao wamefanya makosa kataika tafsser zao au wamefata vitabu vingine ambayo visa au mafundisho yake ni ya kibinadam tu, hayana hata chembe na uhusiano na Qur’an.

Nawaasa wote tustahamili kuisoma hii elimu kidogo kidogo, kwani ina mengi ambayo tutayaleta kidogo kidogo ili yatuingie kwa mitindo (methods) ambayo inatokana na Qur’an yenyewe na wala sio ubunifu wa mtu.

Msiniulize mtayoyasoma hapa kwanini wengi wetu hatujayaona kabla na au kwanini “Maulamaa wetu hawajayaona kabla?”. Tustahamili kuuliza hayo kwani naamini kila tutavyoendelea Qur’an yenyewe itatupa majibu,


Tunakusudia kuanza kuifanyia tafsil aya ya 30 na kuendelea, lakini kabla hatujaingia kwenye aya ya 30 itabidi tupitie aya ya 28 na 29.

Ni muhimu sana tujifunze mbinu mbili tofauti za kutusaidia ufahamu wa Qur’an kutokana na Qur’an yenyewe.

Alhamdulillahi, Mwenyezi Mungu ametujaalia kutupa elimu na mwongozo ulio bora kabisa kuliko wowote ule na usio na shaka ndani yake, Qur’an.

Hatuna budi tufanye hima tujikite kwenye Qur’an kama msingi wetu mkuu wa kuielewa Qur’an yenyewe. Maneno ya watu binafsi tuliofundishwa, haijalishi yanatokea kwa mwenye jina kubwa vipi, kama katumia yake binafsi kuongezea ambayo hayamo kwenye Qur’an au kutumia akili yake, ambayo haiwezi kua na ujuzi wa kumpita Allah kwa lolote li;e, tuyapuuze.

Ikiwa kuna Alim au mwanazuoni yeyote yule, kupunguza kitu au kusema kua hiki hakina maana kilizidi tu, kwa sababu yoyote atakayoitoa, huyo au hao tuwatazame mara mbili mbili, kwani naamini hakuna neno au herufi itokayo kwa Muumba wetu isiyo na kazi yake au maana yake kuwepo kwenye Qur’an.

...2
 

Kwa jibu lako hilo una maana hujaridhika na majibu ya wote waliojibu kwa kutumia Qur'an na watafsiri na hadeeth, kwa kua kwako ni ghaib na huielewi ghaib au sivyo?

Ni suala ambalo badala ya kuzunguka sanq, ningekuelewa ungesema kua kwako hilo ni jipya na hauna ujuzi nalo zaidi.
Simba.
 
Sijakuelewa wewe kama nani?


njiwa
Sielewi mwenzetu kama nani ki ilm mpaka uamue "unaiweka... "?

Kwa ilm ipi ulionayo mpaka ukafikia kufanya hivyo?

Isijekuwa tuna Alim wa kiwango cha kutowa fatwa hatukuelewi?

Faiza mimi ni mwanafunzi , sijafika kiwango cha kutoa fatwa .... nilichosema haki katika dini inajulikana na batili inajulikana hayo mambo yalishawekwa wazi kitambo sana katika quran na Sunna
 

Raha ya elimu ya Uislam, ni lazima kipatikane chanzo (source), kama hauna chanzo inabaki kua ni uzushi wako binafsi.
Ni kweli kabisa ... Nipe chanzo au source kutoka kwenya mafunzo ya Mtume ya kuunasibisha uislam na kutumia majini kwenye TIBA au kutaka usaidizi wa majini ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…