Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Nimejikuta nimesmile kwa hili jibu...so ni wazi ulimaanisha methali ikiwa na maana ya mfano wa mafumbo, na co neno 'mfano' kwa maana mfano ni ufananisho wa wazi, basi Simba hili darsa lako kama una kichwa kibovu hutoboi
 
Nimejikuta nimesmile kwa hili jibu...so ni wazi ulimaanisha methali ikiwa na maana ya mfano wa mafumbo, na co neno 'mfano' kwa maana mfano ni ufananisho wa wazi, basi Simba hili darsa lako kama una kichwa kibovu hutoboi
In Shaa Allah tutatoboa. Nikimalliza kisa nitapitia upya kama kuna makosa ya kurekebisha hapa na pale nirekebishe. Na nyote humu mpo huru kihitilafiana nami, kunirekebisha, kuuliza, kushauri na kukosoa. Ninapoliona kosa naahidi kurekebisha.

Qur'an ni "software" ya ajabu, kila tunapozamia kina kirefu na yenyewe inaturekebisha tulipokosea.

Uzuri wa Qur'an imeungana kama kiota, unaweza kusoma aya moja ukaja kuielewa zaidi unaposoma nyingine kuleeeeee.
Mifano ni mingi, sitaki kuiingilia mada nyingine kwa sasa.
Simba.
 
Habari; Naomba kuuliza haya maswali

1.Nimeota ndoto ninafunga ndoa na jini, je ndoto kama hizi zina uhalisia???

2. Baada ya kuota ndoto hiyo nilishtuka kutoka usingizini lakini haikuchukua muda usingizi ukanipata nikaota tena nipo mahali fulani natambulishwa mtoto wa kiume niliyezaa na jini, wakanitajina hadi jina la huyo mtoto lakini nimelisahau, na umri wake kama miaka miwili au mitatu hvi. Je ndoto hii ina uhalisia??
 
Swali lako zuri sana, pia naomba unistahamilie majibu yangu, kwani ni muhimu tufahamishane kwa kina. Kabla sijaendelea kulijibu swali lako, huwa napenda sana kufikisha ujumbe wangu kwa kuuliza maswali, ili mtu ajaaliwe ajipatie majibu mwenyewe badala ya kujizoesha kungoja majibu ya wengine tu.

Ndoto ni kitu cha kawaida sana kwa binadam wote, wala sio muujiza wala ajabu. Ndoto zinadondokea katika elimu ya saikolojia na mabingwa wa elimu ya saikolojia ni wenye elimu ya masomo ya Kiislam. Saikolojia kwenye mafundisho ya Kiislam huitwa "elimu ya Nafsi" (Ilm nafs).

Nafsi zetu huupata uelewa kwa njia kadhaa, zikiwemo za elimu tunayoipata kwa kusikia, kuona, kunusa, kuhisi kwa kushika au kugusa, bila kusahau elimu ambayo tunajifunza na kufundishwa kwa njia mbali mbali, ikiwemo kujisomea wenyewe.

Na kubwa zaidi ni elimu anyotupa Muumba wetu daima. Ndio mpaka Waislam tunafundishwa dua "Rabi zidni ilman", ikimaanisha kumuomba Muumba wetu atuzidishie elimu.

Kwa hio ningependa kufahamu, wewe umefikiaje kuamua na kusema kua huyo uliemuota ni jini? kwanini sio binadamu?
Simba.
 
Ahsante kwa swali lako Simba.
Jibu:
1. Kwanza Mimi nina mke na mtoto mmoja wa kike. Naweza kusema niliyemuota ni jini kwa sababu nimeota ndoto ya mtu ambae simfahamu kabisa, kwenye ndoto nilikuwa naona sura ya huyo mwanamke kwa kufifia sana na hata mtoto wa kiume niliyemuota nae sura yeke nilikuwa naiona kwa kufifia sana.
2. Kwenye ndoto yule mwanamke akawa ananiambia yeye ni jini na wakati tunafunga ndoto alikuwa anatembea kwa kupaa na kushuka chini mimi nilikuwa natembea kawaida, tulipomaliza kufunga ndoa tukaenda hadi shule ya msingi niliyosoma akawa yeye anaigia shule kwa kupotea na mm nikawa naingia kwa njia ya geti la shule.
3. Baada ya hapo akanielezea kuhusu mdogo wangu wa kiume ambae ana dalili za kuugua uchizi kuwa alipata tatizo hilo kwa kujiingiza kwenye masomo mabaya( hapa nilikuwa sielewi masomo gani) ila alisema yeye atamsaidia.
Ndio maana nikasema niliyemuota ni jini, naamini nimeeleweka Simba.
 
Naomba nikufahamishe kitu cha muhimu sana; Kama ni jini kweli basi atarudi tena na kurudi tena na tena.

Ulizisoma njia za kumuita jini, juu huko?
Simba?
 
Hiki kisa cha Adam ni kizuri lakini kimefukuza watu wengi humu..... Watu wanavutika zaidi na elim iliyo kweny mfumo wa story, ila hiki kisa cha Adam ni elim ngumu inayohitaji kushughulisha akili kitu ambacho wengi hawapendelei

Kwenye visa vya Arsis popote alipozungumziwa
Jinn 1, 2 pamoja na Bakora... Hapo elim bubashara ilitolewa!!(hongera kwao)

MAFANIKIO NILOYAPATA KUPITIA ELIM KTK HUU UZI
a) kuwajua majinn na viumbe wa kiroho katika uharisia wao
b) kuijua mode of communication ya hao viumbe
C) kuweza zungumza nao kwa kupitia nafsi (telepathy)
D) kumchukulia jinn n kiumbe wa kawaida tu...

Kiufupi faida humu ipo,,,,, pia mengi yanayozungumzwa humu n kweli
(Hasa ile story ya vibuki ile ni ukweli mtupu 🚶🚶

Pia nimeweza kumhudhurisha kiumbe kukusaidia kufanya shughul zako (Kama ambavyo Arsis anaweza jibu maswali hum kupitia kwa Simba yani mnakuwa two in one🤝🤝

Ilianza kama udadisi mwisho ikawezekana.. Yani unaweza ita kiumbe kikajaa nafsin hlf mkaanza kufanya Jambo jema kwa pamoja!!!

Yote haya Asante kwa mleta uzi, maana katoa elim ya mambo mengi kwa maelezo, story na vitendo
 
Ahsante kwa kufatilia huu uzi.

Nikuhakikishie, kisa cha Adam tukikifatilia vizuri, tunakoelekea tutaelewa kidogo zaidi kuhusu majini.

Visa vyote nilivyoleta ni vya kweli tupu, hao watu wapo na wengi wao bado wanaishi.
Simba.
 

Kisa cha Adam 2.2

Kwanza tulitazame neno hili Q 2:26 إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسْتَحْىِۦٓ (A) “yastahyiy

Neno hilo pia tunalikuta kwenye Q 28:4 إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًۭا يَسْتَضْعِفُ طَآئِفَةًۭ مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَآءَهُمْ وَيَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُفْسِدِينَ ٤

Kama mnavyojionea hapo kuna “skun” kwenye “ha” حْ. "Skun" au wengine wanaita "sakna”, pia kuna “kasra” chini ya Ya, hizo zinamaanisha kuna Ya (Y) nyingine baada ya "Ya" (Y) inayotamkwa. Na hivyo ndio jinsi inavyoonyeshwa na hivyo ndivyo inavyotamkwa “stahiyiy”. Kama kuna wataalamu wa tajweed wananisoma lazima waseme "ndio ukweli".

Hata sisi tunaweza kutafuta audio au video ya wataalamu wa tajweed kwenye YouTube au popote ukajisikilizia.

Sehemu ya kuvutia (interesting) ni kwamba tahajia (spelling) zipo sawa na inavyotamkwa ni sawa kwa aya hizo zote mbili, aya Q 2:26 na katika aya Q 28:4.

Tuzipitie tafsir tofauti hapa chini kwa ufupi, tujionee wenyewe;

Atabari alilitafsiri neno hilo “haogopi” kwenye Q2:26 na kwa upande wa Q28:4 akatafsiri “kuwaweka” (keeping)

...wanawake wao hai, hii ndio kama maana ya msingi iliyompa Zamakshari (hii ni tafsiri pia) alitumie neno sawa na “hayat” ambayo ni uhai au kuishi.

Nimeweka hayo kwa ufupi tu lakini ukipitia ukajisomea, utajionea karibia tafsiri zote zipo kwenye kuhitilafiana kwa maana ya hilo neno kutoka aya moja na nyingine.

In shaa Allah ikifikia wakati wa kuitafuta maana kamili ya 28.Surat Al-Qas'as' tutajionea maana kusudiwa ya aya hiyo/hizo.

Kwenye maana yetu sisi ya “la yastahyiy” tumesema; ... “hatafuti” ; Mwenyezi Mungu hatafuti kuleta ugumu katika Maisha...

Baada ya neno hilo, sasa tuendelee kupiga mbizi, vipi tumeipata maaana kamili ya hizo aya kwa kutumia mbinu za tafsil, kiota na ndimi “lisan” kwa maneno mengine;

Tutazame neno mbu ”baudha” بَعُوضَة(C), tutaona kabla ya neno hilo kuna neno “ma” مَّا. Neno “baudha”.

Neno “baudha” ili kulifanyia tafsil inabidi tuingie kwenye elimu ya lugha ya Kiarabu kidogo, tukilitamka peke yake kama lilivyo andikwa inabidi tulitamke “baudhatun” kwa kua mwishoni mwake lina herufi “Ta” iliofungwa (Ta marbuta) ة.

Kwenye lugha ya Kiarabu kuna elimu inayoitwa “elimu ya “Sarf”, Kingereza chake ni “morpheme”, katika elimu ya sarf tunajifunza kua kuna maneno “mzazi” (parent words” ambayo hayabadili maana ya neno yanapongezewa kionjo bali hubadili matumizi ya hilo neno. Mfano mdogo ni neno “faul”, nikisema “hamala” ambayo inamaanisha “kubeba” nikisema “Hamil” inakua ni mbebaji, sarf yake ni “fail”, mtendaji, yule anaebeba “hamil”. Nikisema “mahmoul” ambayo ni sarf ya “maf’ul” inamaanisha “amebebwa”,

Kwa ufupi ndio utamu wa vionjo (sarf) vya lugha ya Kiarabu.

Tukirudi kwenye neno letu “baudha” bila herufi ya "ta" iliofungwa, linakua ni “baudh”

...
 
Naona n nahau na balagha tupu🤔
Ambao hatuna ilm mnatuonea
 
Naona n nahau na balagha tupu🤔
Ambao hatuna ilm mnatuonea
Sarf, tena kijuujuu tu. Lengo kuu ni kupeana elimu. Tufikishe ujumbe japo kwa aya moja tuliojaaliwa.

Kama kuna sehemu inakutatiza, uliza tu.
Simba.
 
Hiyo ni aina madda ya aljaaizu munfaswilu kama cjakosea, kutoka katika kundi la madda za far-i'yyu...utavuta vya kutosha tu hapo, harka 5 kama nitakuwa sawa. Unaturudisha madrasa Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…