Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Swali zuri sana.

Cha muhimu kabisa, mimi hapa sifanyi "tarjama" wala "Tafsir", ninachofanya ni "interpretation" au kama alivyonifundisha FF hapo juu kidogo, "exegesis", yaani kuipata maana kusudiwa kwa kutumia Kiswahili. Kwa hio sioni kama 'methali" au 'mfano' inaondoa maana kusudiwa.

Unataka tuweke "methali" kufata neno mathala, pia kwangu naona sawa.

Tunaweza ku edit kabla hatujaenda mbali, mnishauri. Hili ni letu sote.
Simba.
Nimejikuta nimesmile kwa hili jibu...so ni wazi ulimaanisha methali ikiwa na maana ya mfano wa mafumbo, na co neno 'mfano' kwa maana mfano ni ufananisho wa wazi, basi Simba hili darsa lako kama una kichwa kibovu hutoboi
 
In Shaa Allah tutatoboa. Nikimalliza kisa nitapitia upya kama kuna makosa ya kurekebisha hapa na pale nirekebishe. Na nyote humu mpo huru kihitilafiana nami, kunirekebisha, kuuliza, kushauri na kukosoa. Ninapoliona kosa naahidi kurekebisha.

Qur'an ni "software" ya ajabu, kila tunapozamia kina kirefu na yenyewe inaturekebisha tulipokosea.

Uzuri wa Qur'an imeungana kama kiota, unaweza kusoma aya moja ukaja kuielewa zaidi unaposoma nyingine kuleeeeee.
Mifano ni mingi, sitaki kuiingilia mada nyingine kwa sasa.
Simba.
 
Habari; Naomba kuuliza haya maswali

1.Nimeota ndoto ninafunga ndoa na jini, je ndoto kama hizi zina uhalisia???

2. Baada ya kuota ndoto hiyo nilishtuka kutoka usingizini lakini haikuchukua muda usingizi ukanipata nikaota tena nipo mahali fulani natambulishwa mtoto wa kiume niliyezaa na jini, wakanitajina hadi jina la huyo mtoto lakini nimelisahau, na umri wake kama miaka miwili au mitatu hvi. Je ndoto hii ina uhalisia??
 
Swali lako zuri sana, pia naomba unistahamilie majibu yangu, kwani ni muhimu tufahamishane kwa kina. Kabla sijaendelea kulijibu swali lako, huwa napenda sana kufikisha ujumbe wangu kwa kuuliza maswali, ili mtu ajaaliwe ajipatie majibu mwenyewe badala ya kujizoesha kungoja majibu ya wengine tu.

Ndoto ni kitu cha kawaida sana kwa binadam wote, wala sio muujiza wala ajabu. Ndoto zinadondokea katika elimu ya saikolojia na mabingwa wa elimu ya saikolojia ni wenye elimu ya masomo ya Kiislam. Saikolojia kwenye mafundisho ya Kiislam huitwa "elimu ya Nafsi" (Ilm nafs).

Nafsi zetu huupata uelewa kwa njia kadhaa, zikiwemo za elimu tunayoipata kwa kusikia, kuona, kunusa, kuhisi kwa kushika au kugusa, bila kusahau elimu ambayo tunajifunza na kufundishwa kwa njia mbali mbali, ikiwemo kujisomea wenyewe.

Na kubwa zaidi ni elimu anyotupa Muumba wetu daima. Ndio mpaka Waislam tunafundishwa dua "Rabi zidni ilman", ikimaanisha kumuomba Muumba wetu atuzidishie elimu.

Kwa hio ningependa kufahamu, wewe umefikiaje kuamua na kusema kua huyo uliemuota ni jini? kwanini sio binadamu?

Ahsante kwa swali lako Simba.
Jibu:
1. Kwanza Mimi nina mke na mtoto mmoja wa kike. Naweza kusema niliyemuota ni jini kwa sababu nimeota ndoto ya mtu ambae simfahamu kabisa, kwenye ndoto nilikuwa naona sura ya huyo mwanamke kwa kufifia sana na hata mtoto wa kiume niliyemuota nae sura yeke nilikuwa naiona kwa kufifia sana.
2. Kwenye ndoto yule mwanamke akawa ananiambia yeye ni jini na wakati tunafunga ndoto alikuwa anatembea kwa kupaa na kushuka chini mimi nilikuwa natembea kawaida, tulipomaliza kufunga ndoa tukaenda hadi shule ya msingi niliyosoma akawa yeye anaigia shule kwa kupotea na mm nikawa naingia kwa njia ya geti la shule.
3. Baada ya hapo akanielezea kuhusu mdogo wangu wa kiume ambae ana dalili za kuugua uchizi kuwa alipata tatizo hilo kwa kujiingiza kwenye masomo mabaya( hapa nilikuwa sielewi masomo gani) ila alisema yeye atamsaidia.
Ndio maana nikasema niliyemuota ni jini, naamini nimeeleweka Simba.
 
Naomba nikufahamishe kitu cha muhimu sana; Kama ni jini kweli basi atarudi tena na kurudi tena na tena.

Ulizisoma njia za kumuita jini, juu huko?
Simba?
 
Hiki kisa cha Adam ni kizuri lakini kimefukuza watu wengi humu..... Watu wanavutika zaidi na elim iliyo kweny mfumo wa story, ila hiki kisa cha Adam ni elim ngumu inayohitaji kushughulisha akili kitu ambacho wengi hawapendelei

Kwenye visa vya Arsis popote alipozungumziwa
Jinn 1, 2 pamoja na Bakora... Hapo elim bubashara ilitolewa!!(hongera kwao)

MAFANIKIO NILOYAPATA KUPITIA ELIM KTK HUU UZI
a) kuwajua majinn na viumbe wa kiroho katika uharisia wao
b) kuijua mode of communication ya hao viumbe
C) kuweza zungumza nao kwa kupitia nafsi (telepathy)
D) kumchukulia jinn n kiumbe wa kawaida tu...

Kiufupi faida humu ipo,,,,, pia mengi yanayozungumzwa humu n kweli
(Hasa ile story ya vibuki ile ni ukweli mtupu 🚶🚶

Pia nimeweza kumhudhurisha kiumbe kukusaidia kufanya shughul zako (Kama ambavyo Arsis anaweza jibu maswali hum kupitia kwa Simba yani mnakuwa two in one🤝🤝

Ilianza kama udadisi mwisho ikawezekana.. Yani unaweza ita kiumbe kikajaa nafsin hlf mkaanza kufanya Jambo jema kwa pamoja!!!

Yote haya Asante kwa mleta uzi, maana katoa elim ya mambo mengi kwa maelezo, story na vitendo
 
Ahsante kwa kufatilia huu uzi.

Nikuhakikishie, kisa cha Adam tukikifatilia vizuri, tunakoelekea tutaelewa kidogo zaidi kuhusu majini.

Visa vyote nilivyoleta ni vya kweli tupu, hao watu wapo na wengi wao bado wanaishi.
Simba.
 
...

Kisa cha adam. 2.1

Je, malaika walimuuliza Mwenyezi Mungu?

Katika sehemu hii tunaanza na swali hilo, la kwenye kichwa cha Habari, ambalo In shaa Allah tutalizungumzia kwa kina.

Je, Malaika waliuliza kweli?

Wakati tunaendelea, kwanza tukumbushane kitu ambacho tulikiongelea huko nyuma nyuma kiasi, kijuujuu, nacho ni kua asilimia kubwa sana ya Qur’an, nadiriki kusema zaidi ya asilimia 60 ni visa na hadithi mbali mbali zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa kusisitiza; ikiwa hakuna visa na hadithi ndani ya Qur’an basi hakuna Qur’an.

Tunapata na istilahi nyingine “dhikr”, ambayo kama tutavyojionea, mara nyingi inapotajwa “dhikr” katika haya maandiko yetu, inamaanisha kisa, fumbo au hadith ya Qur’an. Hili tutaliongelea kwa kina na kuonesha Ushahidi uliopo ndani ya Qur’an na tutajionea tunavyoweza kujifunza kutokana na dhikr, ambayo ni hadith za Qur’an.

Tutaona pia ndimi “lisan” ya Ibrahim (Abrahamic locution) inavyotolewa kwenye dhikr wakati tunaongelea suala hili la Malaika ambao, eti wamemuuliza maswali Muumba wetu, kama tulivyoaminishwa na watafsiri wengi katika aya Q 2:30.

Raha ilioje kila tunapogundua njia mpya na za kipekee ambapo Qur’an yenyewe inatufundisha na kuturekebisha mithili ya “advanced software” ya kompyuta kila tunapoendelea kugundua kuisoma kwa kufata mifumo yake ya kutuelimisha.

Kwa hakika ni muujiza kuelewa hayo kutoka kwenye Qur’an yenyewe, ni ya kushangaza na kustajaabisha. In shaa Allah Tutajionea wenyewe kila tunavyoendelea.

Hivi tunaviita moja ya vibainisho “bayyinah” au viashiria vipya tunavyojifundisha kwa pamoja.

In shaa Allah uwe ni ujuzi na elimu yenye manufaa kwetu na kwa wengine wote pia iwe ni sadaka njema kwetu na kwa Waislam wote, waliopo na waliotutangulia.

Tueleweshena na tuelewe kua, hii ni elimu na sio starehe, raha yake isio na mfano ni pale tunapojitambua kua tunaupata ujuzi wa kina wa kuulewa mwongozo wetu wa Qur’an kwa mbinu za Qur’an yenyewe.

Qur’an ni muujiza ambao huwezi kuufananisha kitabu cha mtu yoyote au chochote au mshairi yoyote duniani. Hakuna mbinu za kujifundishia za mtu yeyote zinayoweza kufanana au hata kuzikaribia mbinu za Qur’an.

Kwa kujikumbusha haraka haraka, tulipoipitia aya ya 26 na 27 ya Suratul Baqara tuliona kuhusu (baudhatun) بَعُوضَةًۭ au mbu kwa Kiswahili. Tukajikinaisha kua kilichokusudiwa sio mbu wala mfano wa mbu bali ni moja ya kikundi cha watu katika vikundi vya bani israel ambavyo vimegawanyika lakini daima wako kazini kuwagawanya wengine kwa kuwadunga sumu kama mbu, yaani mradi wawapotoshe tu.

Kutajwa kwa mbu wala kusitustue kwani kwenye Kiswahili pia kwa ulimi (lisan) au “locution” ya Tanzania tuna mifano kama hio mingi tu. Mmojawapo maarufu sana ni pale tunaposema ‘wanyonyaji wenye mirija”, naamini hakuna Mtanzania asiejua maana yake, lakini, anaweza kutokea mtu anaejifundisha Kiswahili au wa kutoka nchi nyengine kabisa yenye Kiswahili lakini haina msamiati huo, asielewe maana ya mirija na wanyonyaji.

Kwaa ufupi, natumai maana ya “locution” au ulimi au “lisan” kwa Kiarabu imeeleweka. Ni msamiati au aina ya neno au maneno yanayotumika sehemu fulani au na watu fulani. Wengine hata kwenye familia tu kuna maneno fulani wakiyaongea, ingawa ni ya Kiswahili lakini kama si mwanafamilia unaweza usielewe kinachoongelewa.

Hii imenikumbusha mfano wa kwetu Tanga, ukiwa baraza za bao, chakula kikiwa tayari nyumbani anaweza kutumwa mtoto akaambiwa “kamwambie babako, kabati limeanguka aje haraka kusaidia kulibeba”. Baba na wanaolewa “lisan” hio wanakua wameshaelewa, chakula tayari.

Au ule utani maarufu wa Ilala; Mume alishikwa na hamu na mkewe alikuwa Jirani na mashoga zake wana sherehe yao. Baba akamtuma mwanae “kamwambie mamako aje haraka kuna nguo za kufuliwa nyumbani”, Mama nae hali ilikua sio nzuri, akamwambia, kamjibu babako “mama anasema washing mashine leo mbovu”. Ni matumaini yangu tumeelewa maana ya “locution”.

Qur’an muujiza wake mmojawapo ni huu wa lisan au “locution”, mfano, miaka mingi sana imepita tokea wakati wa Nabii Ibrahim (Alayhi salaam) mpaka wakati ilipokuja Qur’an, lkini imetumika sana ‘lisan” ya Ibrahim (Abrahamic locution ) ndani ya Qur’an.

Pia zimetumika “locution” za Mussa, Firauni na nyenginezo, tutaziona kila tuvyoendelea, kiasi ni muujiza ulio wazi mpaka leo hii, wa kujiuliza, vipi Mtume Muhammad (Sala Allahu Alayhi Wasalaam) alizijua ndimi hizo za zamani sana? Aliwashangaza sana Mayahudi wa Madina wa wakati wake alipokua akitamka mambo mengine kwa ndimi zao. Hadi leo hii Qur’an inaendelea kuwashangaza mabingwa wa tafiti za kugha kwa jinsi ilivyoandikwa.

Kwenye “table” nilipozichambua (tasil) aya mbili za 26 na 27, nimeziwekea herufi za kwenye mabano (a), (B), (C)... na baadhi ya maneno nimeyawekea rangi (highlight) ya njano ili iwe wepesi kuzirejea tunapozielezea.

Kumbuka kua hatuongelei bani Israel wote bali ni baadhi ya vikundi tu na hivyo ndivyo aya ya 28 na 29 za Suratul baqara zinavyowaelezea;

Ili tuipate maana kusudiwa ya aya za 28, 29 na kuendelea, kwanza tujikite kwa kina kwenye tafsil ya aya ya 26 na 27 na tuipate maana kusudiwa ya aya hizo.

Nakumbusha hapa kwa kubandika tafsiri ya kawaida ya Sheikh Ali Mohsin barwani, ya aya hizo, ambayo inatumika sana kwenye mtandao;

Q 2:26. Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walio amini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, lakini wale walio kufuru husema: Ni nini analo kusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini hawapotezi ila wale wapotovu, 26

Q 2:27. Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara.
27

Baada ya kuiona hio tafsiri, hapa chini tunaweka ufafanuzi (interpretation) ambayo Mwenyezi Mungu ametujaalia kuiona kwa kutumia mbinu za ki Qur’an za "tafsil" kwa kina, ili kupata maana halisi. Mbinu ambayo tutaitumia kwa kina katika episode hii ya adam na nyinginezo zitakazofata.

Tutajionea kua tumeweka maana tu iliokusudiwa na tumeachana na tarjama na tafsiri kama ilivyozoeleka.

Baada ya huu ufafanuzi wetu, tutapiga mbizi, kuzamia kwa kina kwa tafsil ili tujionee jinsi tulivyoweza kuipata maana hii kwa kutumia mbinu (methods) za Qur’an. Tuanze;

Tafsil (syntactic segmentation) ya Qur’an 2:26 na 27
Mwenyezi Mungu hatafuti kuleta ugumu katika Maisha.
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسْتَحْىِۦٓ (A)​
kwa kupiga mfano wowote
أَن يَضْرِبَ مَثَلًۭا مَّا (B)​
kwa vikundi miongoni mwa Bani Israeli ambao huchochea vikundi kutokubaliana (yaani, watu wanaopanda mgawanyiko kwa kuuma na kuingiza habari za kupotosha).
بَعُوضَة(C)​
Kwa maana hawakubali kitu chochote juu yao! (Hakika kundi hili liliwakataa kwa kiburi wale wote walioinuliwa na Mwenyezi Mungu juu yao.)
فَمَا فَوْقَهَا ۚ (D)​
Na wale walio amini wanaelewa kua hio ni haki itokayo kwa Mola wao Mlezi
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ​
Na wale walio kufuru wanasema Mwenyezi Mungu anataka nini kwa methali hii?
وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَـٰذَا مَثَلًۭا ۘ​
(Allah) anaitumia kuwapotosha wengi na kuwaongoza wengi.
يُضِلُّ بِهِۦ كَثِيرًۭا وَيَهْدِى بِهِۦ كَثِيرًۭا ۚ​
Lakini (Allah) hapotoshi kwayo ila wapotoshaji (Alfasiqin).
وَمَا يُضِلُّ بِهِۦٓ إِلَّا ٱلْفَـٰسِقِينَ
(Q 2:26)

Qur’an 2:27

Waliokadhibisha ( ni mbu /baudha) ahadi ya Allah baada ya kuthibitika.
ٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مِيثَـٰقِهِۦ​
Na wanayakata (tenganisha) yale aliyo amrisha Allah yasikatwe (yasitenganishwe)
وَيَقْطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ​
Na wanayafisadi maandiko
وَيُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ​
Wao hao ndio wenye hasara
أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ ٢٧​

Itaendelea.

...

Kisa cha Adam 2.2

Kwanza tulitazame neno hili Q 2:26 إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسْتَحْىِۦٓ (A) “yastahyiy

Neno hilo pia tunalikuta kwenye Q 28:4 إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًۭا يَسْتَضْعِفُ طَآئِفَةًۭ مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَآءَهُمْ وَيَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُفْسِدِينَ ٤

Kama mnavyojionea hapo kuna “skun” kwenye “ha” حْ. "Skun" au wengine wanaita "sakna”, pia kuna “kasra” chini ya Ya, hizo zinamaanisha kuna Ya (Y) nyingine baada ya "Ya" (Y) inayotamkwa. Na hivyo ndio jinsi inavyoonyeshwa na hivyo ndivyo inavyotamkwa “stahiyiy”. Kama kuna wataalamu wa tajweed wananisoma lazima waseme "ndio ukweli".

Hata sisi tunaweza kutafuta audio au video ya wataalamu wa tajweed kwenye YouTube au popote ukajisikilizia.

Sehemu ya kuvutia (interesting) ni kwamba tahajia (spelling) zipo sawa na inavyotamkwa ni sawa kwa aya hizo zote mbili, aya Q 2:26 na katika aya Q 28:4.

Tuzipitie tafsir tofauti hapa chini kwa ufupi, tujionee wenyewe;

Atabari alilitafsiri neno hilo “haogopi” kwenye Q2:26 na kwa upande wa Q28:4 akatafsiri “kuwaweka” (keeping)

...wanawake wao hai, hii ndio kama maana ya msingi iliyompa Zamakshari (hii ni tafsiri pia) alitumie neno sawa na “hayat” ambayo ni uhai au kuishi.

Nimeweka hayo kwa ufupi tu lakini ukipitia ukajisomea, utajionea karibia tafsiri zote zipo kwenye kuhitilafiana kwa maana ya hilo neno kutoka aya moja na nyingine.

In shaa Allah ikifikia wakati wa kuitafuta maana kamili ya 28.Surat Al-Qas'as' tutajionea maana kusudiwa ya aya hiyo/hizo.

Kwenye maana yetu sisi ya “la yastahyiy” tumesema; ... “hatafuti” ; Mwenyezi Mungu hatafuti kuleta ugumu katika Maisha...

Baada ya neno hilo, sasa tuendelee kupiga mbizi, vipi tumeipata maaana kamili ya hizo aya kwa kutumia mbinu za tafsil, kiota na ndimi “lisan” kwa maneno mengine;

Tutazame neno mbu ”baudha” بَعُوضَة(C), tutaona kabla ya neno hilo kuna neno “ma” مَّا. Neno “baudha”.

Neno “baudha” ili kulifanyia tafsil inabidi tuingie kwenye elimu ya lugha ya Kiarabu kidogo, tukilitamka peke yake kama lilivyo andikwa inabidi tulitamke “baudhatun” kwa kua mwishoni mwake lina herufi “Ta” iliofungwa (Ta marbuta) ة.

Kwenye lugha ya Kiarabu kuna elimu inayoitwa “elimu ya “Sarf”, Kingereza chake ni “morpheme”, katika elimu ya sarf tunajifunza kua kuna maneno “mzazi” (parent words” ambayo hayabadili maana ya neno yanapongezewa kionjo bali hubadili matumizi ya hilo neno. Mfano mdogo ni neno “faul”, nikisema “hamala” ambayo inamaanisha “kubeba” nikisema “Hamil” inakua ni mbebaji, sarf yake ni “fail”, mtendaji, yule anaebeba “hamil”. Nikisema “mahmoul” ambayo ni sarf ya “maf’ul” inamaanisha “amebebwa”,

Kwa ufupi ndio utamu wa vionjo (sarf) vya lugha ya Kiarabu.

Tukirudi kwenye neno letu “baudha” bila herufi ya "ta" iliofungwa, linakua ni “baudh”

...
 
Kisa cha Adam 2.2

Kwanza tulitazame neno hili Q 2:26 إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسْتَحْىِۦٓ (A) “yastahyiy

Neno hilo pia tunalikuta kwenye Q 28:4 إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًۭا يَسْتَضْعِفُ طَآئِفَةًۭ مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَآءَهُمْ وَيَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُفْسِدِينَ ٤

Kama mnavyojionea hapo kuna “skun” kwenye “ha” حْ. "Skun" au wengine wanaita "sakna”, pia kuna “kasra” chini ya Ya, hizo zinamaanisha kuna Ya (Y) nyingine baada ya "Ya" (Y) inayotamkwa. Na hivyo ndio jinsi inavyoonyeshwa na hivyo ndivyo inavyotamkwa “stahiyiy”. Kama kuna wataalamu wa tajweed wananisoma lazima waseme "ndio ukweli".

Hata sisi tunaweza kutafuta audio au video ya wataalamu wa tajweed kwenye YouTube au popote ukajisikilizia.

Sehemu ya kuvutia (interesting) ni kwamba tahajia (spelling) zipo sawa na inavyotamkwa ni sawa kwa aya hizo zote mbili, aya Q 2:26 na katika aya Q 28:4.

Tuzipitie tafsir tofauti hapa chini kwa ufupi, tujionee wenyewe;

Atabari alilitafsiri neno hilo “haogopi” kwenye Q2:26 na kwa upande wa Q28:4 akatafsiri “kuwaweka” (keeping)

...wanawake wao hai hii ndio kama maana ya msingi iliyompa Zamakshari (hii ni tafsiri pia) alitumie neno sawa na “hayat” ambayo ni uhai au kuishi.

Nimeweka hayo kwa ufupi tu lakini ukipitia ukajisomea, utajionea karibia tafsiri zote zipo kwenye kuhitilafiana kwa maana ya hilo neno kutoka aya moja na nyingine.

In shaa Allah ikifikia wakati wa kuitafuta maana kamili ya 28.Surat Al-Qas'as' tutajionea maana kusudiwa ya aya hiyo/hizo.

Kwenye maana yetu sisi ya “la yastahyiy” tumesema; ... “hatafuti” ; Mwenyezi Mungu hatafuti kuleta ugumu katika Maisha...

Baada ya neno hilo, sasa tuendelee kupiga mbizi, vipi tumeipata maaana kamili ya hizo aya kwa kutumia mbinu za tafsil, kiota na ndimi “lisan” kwa mananeno mengine;

Tutazame neno mbu ”baudha” بَعُوضَة(C), tutaona kabala ya neno hilo kuna neno “ma” مَّا. Neno “baudha”.

Naona n nahau na balagha tupu🤔
Ambao hatuna ilm mnatuonea
 
Naona n nahau na balagha tupu🤔
Ambao hatuna ilm mnatuonea
Sarf, tena kijuujuu tu. Lengo kuu ni kupeana elimu. Tufikishe ujumbe japo kwa aya moja tuliojaaliwa.

Kama kuna sehemu inakutatiza, uliza tu.

Hiyo ni aina madda ya aljaaizu munfaswilu kama cjakosea, kutoka katika kundi la madda za far-i'yyu...utavuta vya kutosha tu hapo, harka 5 kama nitakuwa sawa. Unaturudisha madrasa Simba
 
Back
Top Bottom