Kisa cha Adam 2.2
Kwanza tulitazame neno hili Q 2:26 إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسْتَحْىِۦٓ (A) “yastahyiy
Neno hilo pia tunalikuta kwenye Q 28:4 إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًۭا يَسْتَضْعِفُ طَآئِفَةًۭ مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَآءَهُمْ وَيَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُفْسِدِينَ ٤
Kama mnavyojionea hapo kuna “skun” kwenye “ha” حْ. "Skun" au wengine wanaita "sakna”, pia kuna “kasra” chini ya Ya, hizo zinamaanisha kuna Ya (Y) nyingine baada ya "Ya" (Y) inayotamkwa. Na hivyo ndio jinsi inavyoonyeshwa na hivyo ndivyo inavyotamkwa “stahiyiy”. Kama kuna wataalamu wa tajweed wananisoma lazima waseme "ndio ukweli".
Hata sisi tunaweza kutafuta audio au video ya wataalamu wa tajweed kwenye YouTube au popote ukajisikilizia.
Sehemu ya kuvutia (interesting) ni kwamba tahajia (spelling) zipo sawa na inavyotamkwa ni sawa kwa aya hizo zote mbili, aya Q 2:26 na katika aya Q 28:4.
Tuzipitie tafsir tofauti hapa chini kwa ufupi, tujionee wenyewe;
Atabari alilitafsiri neno hilo “haogopi” kwenye Q2:26 na kwa upande wa Q28:4 akatafsiri “kuwaweka” (keeping)
...wanawake wao hai, hii ndio kama maana ya msingi iliyompa Zamakshari (hii ni tafsiri pia) alitumie neno sawa na “hayat” ambayo ni uhai au kuishi.
Nimeweka hayo kwa ufupi tu lakini ukipitia ukajisomea, utajionea karibia tafsiri zote zipo kwenye kuhitilafiana kwa maana ya hilo neno kutoka aya moja na nyingine.
In shaa Allah ikifikia wakati wa kuitafuta maana kamili ya 28.Surat Al-Qas'as' tutajionea maana kusudiwa ya aya hiyo/hizo.
Kwenye maana yetu sisi ya “la yastahyiy” tumesema; ... “hatafuti” ; Mwenyezi Mungu hatafuti kuleta ugumu katika Maisha...
Baada ya neno hilo, sasa tuendelee kupiga mbizi, vipi tumeipata maaana kamili ya hizo aya kwa kutumia mbinu za tafsil, kiota na ndimi “lisan” kwa maneno mengine;
Tutazame neno mbu ”baudha” بَعُوضَة(C), tutaona kabla ya neno hilo kuna neno “ma” مَّا. Neno “baudha”.
Neno “baudha” ili kulifanyia tafsil inabidi tuingie kwenye elimu ya lugha ya Kiarabu kidogo, tukilitamka peke yake kama lilivyo andikwa inabidi tulitamke “baudhatun” kwa kua mwishoni mwake lina herufi “Ta” iliofungwa (Ta marbuta) ة.
Kwenye lugha ya Kiarabu kuna elimu inayoitwa “elimu ya “Sarf”, Kingereza chake ni “morpheme”, katika elimu ya sarf tunajifunza kua kuna maneno “mzazi” (parent words” ambayo hayabadili maana ya neno yanapongezewa kionjo bali hubadili matumizi ya hilo neno. Mfano mdogo ni neno “faul”, nikisema “hamala” ambayo inamaanisha “kubeba” nikisema “Hamil” inakua ni mbebaji, sarf yake ni “fail”, mtendaji, yule anaebeba “hamil”. Nikisema “mahmoul” ambayo ni sarf ya “maf’ul” inamaanisha “amebebwa”,
Kwa ufupi ndio utamu wa vionjo (sarf) vya lugha ya Kiarabu.
Tukirudi kwenye neno letu “baudha” bila herufi ya "ta" iliofungwa, linakua ni “baudh”
...
Kisa cha Adam 2.3
Baada ya kupitia "sarf" za maneno mbali mbali tumefikia tamati kua neno hilo halimaanishi mbu kwenye aya ya 26 na maana yake ni kama tulivoiweka kwenye ufafanuzi wetu juu hapo. Pia hakuna methali yoyote ya mbu au nyingine inayoongelewa hapo.
Pia naweza kusema hakuna hata mfano hapo bali kuna taarifa ya mbinu za ki qur’an zinazotumika Qur’an nzima. Ni tamko jema kutoka kwa Muumba wetu ambalo lipo mwanzo mwanzo wa Qur’an ili kutuongoza.
Neno "ma" liliopo kabla ya neno "baudh" ni la kukanusha, mfano mzuri na mwepesi kwa Kiarabu ni pale tunaposema nenpo "Fi" , maana hyake ipo. Na tukiiongezea "ma" kavbla ya "fi" inakua 'mafii" yaani 'hakuna.".
Cha kushangaza, sifahamu kwanini watafsiri walio wengi, kama si wote, hawakulitumia neno hilo katika tafsiri zao na mpaka wengine wamefikia kusema hilo ni neno la ziada. Hili tunaweza kulitolea ufafanuzi zaidi likiulizwa kipekee, kwani pia kuna baadhi ya watafsiri wamelipa maana nyingine.
Mimi naamini Qur’an haina neno au herufi ya ziada. Naamini kua kila neno au herufi iliotumika ndani ya Qur’an ina maana yake na sababu zake kamili kuwepo, labda iwe bado tu hatujajaaliwa kulijua. AlhamduliLlah sisi tumejaaliwa kuliona na kulitumia neno hilo na kufikia ufanunuzi tulioutoa wa aya hio.
Tukirudi juu hapo kwenye aya ya 27 inaweka wai kabisa kua hicho ni kikundi kimojawapo miongoni mwa vikundi vya Bani Israel, tafadhali rejea juu kidogo hapo tulipoweka ufafanuzi wa aya ya 27.
Natamani wasomaji waniulize kuhusu ahadi iliotajwa katika aya ya 27.
Kuna vitu muhimu sana vya kuvizungatia kabla hatujaendelea. Navyo ni kujionea wenyewe jinsi aya ya 26 na 27 zilivyoungana, yote yaliopo kwenye aya 26 ndio hayo hayo yanaendelea kuongelewa aya ya 27 na kuendelea. Qur’an tumesema ipo kama kiota, imeungana na kiushikana yote.
Tusifanye kosa la kama tunavyofanya wengi wetu, kufikia kutoa maamuzi ya aya fuani kuitengenisha na aya nyingine kabla hatujaielewa hata hio aya.
In shaa Allah tuendelee na aya ya 28 na tutajionea mambo yanaanza kua myepesi kila tunavyotumia mbinu ya kiota, kuunganisha ayat na sio kuziwachanisha.
...