Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Uzi huu umeongelea mambo mazito sana ambayo wengi hawakuwahi kuyajuwa, lakini FF kuleta porojo za Manara na Mobeto na Simba unajaa kwenye 18 zake ni kuukosea adabu uzi huu wenye platinum zake.

Siasa za Simba na Yanga zinajulikana wazi, mechi za Yanga zinachezwa nje ya uwanja na wapinzani wake kuipunguza Yanga nguvu.

Yanga kuhama uwanja wa Azam wapo sahihi wanahujumiwa, tatizo la kocha anafuata utaratibu wa ulaya wachezaji wana muda wa maisha yao binafsi na vaada ya mechi wanapewa ruhusa warudi nyumbani siyo kukaa kambini muda wote.

Zama za Manara zimekwisha, Ally Kamwe ndio mahitaji ya wakati, huyo chizi Manara wamemshindwa ccm.

Kwenye uzi huu ukituletea porojo za machizi kama Manara utakuwa unatukosea sana.
 
Hakuna haja ya ushahidi wa mazingira, Huo ni ukweli kabisa.

Kumbuka, Kiislam mtu anaweza kuolewa umri wowote kwa ridhaa ya walii wake, ambae mara nyingi huwa ni wazazi wake wa kuumeni. Lakini ndoa haitimii (wanakuwa hawajaoana) mpaka msichana atimize kua mwanamke kamili anaeweza kuingiliwa kimwili na akubali yeye mwenyewe kuolewa na fulani. Ndipo inakuwa wameoana.

Hayo yote yalitimia kwa Bi Aisha.
Hujamalizia maswali yake.
 
Niko na swali kuhusu hadithi kadhaa,
1. Naomba kufaham kuhusu Anunaki, je kweli wapo??
Je ni kweli ndio wameumba binadamu??
Je ni kweli wametokea sayari inayoitwa Nibiru??

2. Naomba kufaham kuhusu na Enki na Enrili.

3. Je kuna vita yoyote ya kiroho iliyopo Kati ya majini na binadamu? Nauliza hvyo kulingana na uelewa wa kibinadamu. Rejea changamoto za watoto wa kike wengi kuanguka au kuumwa wakiwa mashulen kibinadamu hali hiyo tunaihusisha na matendo ya majini.

Nataman kufaham kama kuna bifu Kati yetu nn chanzo chake??

Ahsante
 
Sikiliza Lidafo, nilikupa zoezi la kufanya sijui liliishia wapi lakini elimu uitakayo inaitwa "ladoun" imetajwa katika Qur'an, sehemu kadhaa.

Kwa bahati mbaya, sio elimu ambayo unajifundisha moja kwa moja au kuna mtu atakae kufundisha. Ni elimu inayotoka kwa Allah pekee, na yeye kuchagua wa kumpa.

Wewe unachotakiwa kufanya ni kuzidisha kusoma, kila fursa unayoipata, soma kila kitu kutoka kwa kila mtu na omba sana dua ya Allah akuzidishie elimu. Ukikuta boksi lisome, ukikuta pakti ya maziwa isome, ukiona mti usome, ukiona mnyama msome.

Ukitaka niielezee zaidi, nitaielezea mpaka jina lake linavyojulikana kwa maulamaa wengine.
Uliniambia nitafute ni sura ngapi zilizoanza na alif, lam na miim kisha nitafute jumla yake kwa kutumia abjad, Alafu nitafute sura zilizoanza na alam.
Nilikujibu ila ukanambia idadi ya abjad nimekosea, Nimejaribu kutafuta njia nyingine nimekosa zaidi ya ile niliyotumia.
Elezea hiyo elimu ya Ladoun ni ya namna gani na aya zipi katika quran zimeelezea, Hili ni jipya kwangu kabisa.
 
Uzi huu umeongelea mambo mazito sana ambayo wengi hawakuwahi kuyajuwa, lakini FF kuleta porojo za Manara na Mobeto na Simba unajaa kwenye 18 zake ni kuukosea adabu uzi huu wenye platinum zake.

Siasa za Simba na Yanga zinajulikana wazi, mechi za Yanga zinachezwa nje ya uwanja na wapinzani wake kuipunguza Yanga nguvu.

Yanga kuhama uwanja wa Azam wapo sahihi wanahujumiwa, tatizo la kocha anafuata utaratibu wa ulaya wachezaji wana muda wa maisha yao binafsi na vaada ya mechi wanapewa ruhusa warudi nyumbani siyo kukaa kambini muda wote.

Zama za Manara zimekwisha, Ally Kamwe ndio mahitaji ya wakati, huyo chizi Manara wamemshindwa ccm.

Kwenye uzi huu ukituletea porojo za machizi kama Manara utakuwa unatukosea sana.
Vionjo muhimu, hata kwenye mchuzi, leo ndimu, kesho limao, jesho kutwa embe mbichi.
 
Ndio hio ern
Uliniambia nitafute ni sura ngapi zilizoanza na alif, lam na miim kisha nitafute jumla yake kwa kutumia abjad, Alafu nitafute sura zilizoanza na alam.
Nilikujibu ila ukanambia idadi ya abjad nimekosea, Nimejaribu kutafuta njia nyingine nimekosa zaidi ya ile niliyotumia.
Elezea hiyo elimu ya Ladoun ni ya namna gani na aya zipi katika quran zimeelezea, Hili ni jipya kwangu kabisa.
Mimi nadhani anayomaanisha Ndiyo hiyo wengine hudhani kuna jina la Allah la siri.
 
Sikiliza Lidafo, nilikupa zoezi la kufanya sijui liliishia wapi lakini elimu uitakayo inaitwa "ladoun" imetajwa katika Qur'an, sehemu kadhaa.

Kwa bahati mbaya, sio elimu ambayo unajifundisha moja kwa moja au kuna mtu atakae kufundisha. Ni elimu inayotoka kwa Allah pekee, na yeye kuchagua wa kumpa.

Wewe unachotakiwa kufanya ni kuzidisha kusoma, kila fursa unayoipata, soma kila kitu kutoka kwa kila mtu na omba sana dua ya Allah akuzidishie elimu. Ukikuta boksi lisome, ukikuta pakti ya maziwa isome, ukiona mti usome, ukiona mnyama msome.

Ukitaka niielezee zaidi, nitaielezea mpaka jina lake linavyojulikana kwa maulamaa wengine.
Majibu yako yamenipa maswali zaidi, Nivumilie tu.
1. Je jina Hilo lipo katika yale majina 99
2. Nimejaribu kupitia baadhi ya hadith nimeona viashiria kuwa jina la AL HAYYU AL QAYUMM huenda ndio ismul adhwam je hilo ni kweli? Kama sio kweli kuna uhusiano wowote wa jina Hili na ismul adhwam ?
Mwisho, Naomba ueleze jina Hilo linavyojulikana na maulamaa wengine?
 
Hatuyawezi yote, ukiona kuna vita vinavyoonekana elewa pia kuna vita visivyoonekana. Tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu aliotujaalia Allah.

Kikubwa ni wewe binadam, kufanya mema na kuepukana na maovu.

Soma sana. usiwe na mipaka katika kusoma isipokuwa elewa mipaka ya mema na maovu.

Nafsi yako itakueleza hili ovu,ukishajua ni ovu, lisome kupingana nalo, kama unaweza lizuwie kwa mkono wako, ukishindwa lizuwie kwa mdomo wako, ukishindwa lizuwie kwa kulichukia.

Tuko pamoja.
Arsis tafadhali kwa mara nyingine nakuomba utuelekeze tiba ya kuondoa sheitwan wa kukufanyisha zinaa(jini mahaba) kwa sababu hii changamoto itapelekea kuvunja ndoa za watu wengi kwa sababu watu wenye uwezo wa kutatua jambo hilo ni wachache na kuwajua ni mtihani!, Ulieleza kikubwa ni taqwa,adhkar na istighfar nakubali lakini kumbuka vyote hivi vifanyike vikiambatan na matendo mema na subra na wakati huo huo mwenza wako anaona hutimizi wajibu wako kwa kushindwa kumfikisha(upungufu wa nguvu uliosababishwa na sheitwan huyo wa kijini) mwisho wa siku huwezi ukawa na taqwa ya kweli kama una stress,tafadhali nakuomba iwe ni wewe au sheikh bakora kwa idhini ya Mungu unisaidie kuundoa mtihani huu mimi na wenzangu unaotutesa.
 
Arsis naomba msaada wako mkuu Mimi ni mzaliwa wa bombo hospital nimekulia tanga usagara mabangi kingstone kama unapafahamu niko na mdogo wangu anaenifatia badala yangu alipata ajali ya pikipiki alipelekwa muhimbili kwa uwezo Mwenyezimungu alimbariki akapona lakini shida inakuja kauli hana kama mwanzo aongei vizur kama alivo kuwa mwanzo maneno hayamtoki vizuri kabisa hakuna tiba itayoweza msaidia arudi kama mwanzo naitaji msaada wako Bro
 
marahaba.
Sasa anko Arsis sijaelewa vizuri uliposema nimeoteshwa kazi yangu bila mimi kujijua

Ni kweli inaweza kuwa hivyo ila sasa ni kazi gani hiyo? Ndoto nyingi niotazo huwa sikumbukagi niamkapo

Naomba Arsis aniambie ni kazi gani hiyo Tafadhari🙏🙏
 
Usipo taja ukristo unapungukiwa nini kama unaona uislamu unafaa acha kushupaza shingo komaa na dini yako mkuu itakupeleka peponi
Hiyo itakuwa 'the peak of selfishness' Tumeumbwa tumtakie mazuri binadamu mwenzangu. Mimi naona Uislamu ni dini mustakim sana na inakidhi matakwa na majaribio ya akili. Nisimtakie mwingine hilo? Maana unajuaje kama huyo ameingia huko kutokana na kutofikiria au bila kupenda? Halafu sisi Waislamu tuna msemo mmoja: ' Naamini niko katika ukweli lakini pengine nakosea. Na naamini mwengine yuko katika upotevu, lakini pengine amepata!' Ndiyo maana nina vitabu sita vitakatifu vya dini na falsafa nyingine nyumbani kwangu navitalii mara kwa mara, ingawaje binafsi nimefasiri Qur'an Tukufu!
 
Nadhani
Umefanya utafiti? 😆 Tueleze Hypothesis yako iliitwaje? Methodology ni zipi na sample ni zipi? Wakristo wapi, maana wako matabaka mengi kuna Catholics na Protestants, katika Protestants kuna Adventists, Lutherans, Anglican na mengine mengi sana.
Uli base wapi au uliwapitia wote, marejeleo yako ni yapi? Kama hauna hivyo vichache basi mkuu umetumia hisia na mihemko, na maneno ya kuskia skia.

Kama ulivyosema wakristo wengi ni wajinga hasa linapokuja suala la uislamu, pia na mimi naona waislamu wengi ni wajinga vilevile linapokuja suala la ukristo.

Mkuu mimi case yangu na wewe ni pamoja na matumizi ya neno utafiti, wewe hauna resource za kufanya jambo hilo.
Nipe hata list ya vitabu vya kufafanua uislamu na vinavyounga mkono uislamu ambavyo umesoma ukiondoa kitabu kikuu Koran takatifu.

Pia nipe chapisho au kitabu ulichosoma kinachoupinga uislamu, haya mambo yangekuwa mepesi kama unavyoamini watu wasingekuwa katika mkanganyiko wa kiimani unaouona.

Kwa hiyo mkuu na wewe kuhusu ukristo bado hauujui,na pengine haupaswi kuusoma ukifatilia dini yako vizuri usije ukachanganya mambo. Ndio maana mataifa yanayoendeshwa kiislamu hayaruhusu pengine kirahisi shughuli za dini tofauti na yao.

Kuna waarabu wakristo pale Lebanon zama na zama na wao pia unafikiri kwa miaka yote ya mwamko wa uislamu mbona wanabaki katika ukristo wao? Unataka kusema kule pia wanafundishwa na wajinga
Nadhani tatizo lako kubwa ni elimu. Hii simaanishi kukutweza bali kukutia hamasa uanze kujisomea. Juu ya utafiti, suala hilo nimeshalijibu. Vitabu nilivyosoma juu ya Uislamu kwa Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa ni vingi hata sijui nikuongoze kwa kipi. Binafsi nimefasiri Qur'an kwa Kiswahili. Kama una idea tu juu ya uwezo hu, utakisia uelewa wangu nilionao. Huwezi kufasiri Qur'an kwa ustadi bila kupitia Bible. Hadithi nyingi zilizomo kwenye Bible zinaelezewa vizuri katika Qur'an. Mary, mama wa Yesu, nadhani ametajwa mara mbili tatu kwa jina katika Bible. Katika Qur'an ana chapter nzima iitwayo Mary!
Tafuta kitabu "Mohammad, the Natural Successor to Christ' by Ahmed Deedat, au 'Muhammad' by Karen Armstrong.
Juu ya Waarabu kuendelea kuwa Wakristo, hilo ni ushahidi kwa Uislamu haukuwalazimishi watu kwa nguvu kujiunga nao pale ulipofik mjini. Kuna Wamisri milioni 22 Wakriso, Walebanon milio3 Wakristo, Wapalestina, Wa Iraq hata Wairan wengi tu. Waislamu waliitawala India kwa karne kadhaa, lakini hadi leo kuna Mabaniani! Sidhani kama Wakristo wangelikubali hilo. Sehemu zote ambako majeshi ya Kiislamu yalifika yaliwapa hiari wakazi, aidha kusilimu au kulipa kodi. Kodi hii ilikuwa ni gharama ya ulinzi wao, vile hawakulazimika kuingia jeshini au kupigana na adui.
Kama wewe umeusoma Ukristo vizuri, kwanza nieleze nini maana ya ' Conquistadors' na jee unajua stori ya Joan of Arc? Na kwa nini Latin America yote wamekuwa Wakristo? Ambapo kabla ya kufika Wa Spanish walikuwepo Wahindi na Waislamu? Wamekwenda wapi Waislamu na Wayahudi wote wa Spain, wakati Spain kwa miaka 600 iikuwa chini ya Waislamu? Jibu nikujue umesoma!
 
Mkuu

Mkuu wakristo waafrika wa dhehebu gani?
Ndiyo maana nikasema huo uliouita ujinga, upo kila upande juu ya dini ya mwenzake. Isingekuwa hivyo probably watu wangefuata imani moja.

Mfano unaanzaje kuufanya uislamu thabiti ukiri dhana ya utatu mtakatifu na haipo katika kitabu chao, na unaanzaje kuufanya ukatoliki ukiri Mtume Mohammed (S.A.W) ni mtume wa mwenyezi Mungu na hayupo katika biblia, na kama yupo hawaoni jina?
Au Wayahudi na dini yao wakubali Yesu ni kristo, na hawakubali habari zake?

Jambo kama hili utaweza kulifanya kirahisi kwa muislamu mmoja mmoja na mkristo mmoja mmoja.

Biblia ina mistari mingi inazuia ushirikiana na viumbe wengine wa kiroho bila kujali ni wazuri au wabaya, sasa utawezaje kumfanya mtu alieshika biblia akubali kuwa ni sawa.

Hata humu unaona kuna baadhi ya waislamu nimeona kama wanasita pia kukubaliana na hii issue ya Arsis.

Lakini ukija kwa mtu mmoja mmoja kama mimi, napenda kujifunza maarifa naweza kusoma na kusikiliza nikiwa katika neutral ground
Kwanza katika Kiswahili hakuna neno 'dhehebu' ni 'madhehebu' hata likiwa moja.
Pili: tunapozungumzia Uislamu na Ukristo hapa hatutazami madhehemu gani. Hayo ni masuala ya ndani mtajuana nyie wenyewe. Kwetu Ukristo ni Ukristo tu, kama ambavyo ukizungumzia Uislamu unazungumzia wote.
 
Back
Top Bottom