Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Tutarudi tena hivi karibuni na somo la namna ya kuita na kukamata majinni.

Tahadharini sana, kuita kukamata majini haomaanishi kuwakamata na kuwafuga. Ni kuwakamata kuteketeza mambo yao ya uchawi na kuwaonesha nia njema, wanaposalimu amri wanakuwa huru. Wanapokaidi kuna mawili tu, au wanauliwa muda huohuo au wanapelekewa jela za majini.

Tutakapoanza asjaribu kuita mtu jini mpaka amalize somo lote kamili, ambalo lina sura (chapters zaidi ya 13.
Tutaleta sura moja moja ili kila mmoja aelewe kwa kina na kama kuna maswali tutajibu kila sura kivyake.

Ni hatari sana kujifanya umeshaelewa ya kufanya kabla hujamaliza somo zima. Ni hatari kubwa sana, nasisitiza.
 
Huyo "mkinda wa buguruni" simfahamu. Unataka ushahidi kwenye lipi?
 
Upo sahihi kwa kiwango fulani.

Maneno anayonukuu Arsis ya Qur'an nayo huyafati kwa kuwa kayaleta Arsis?

Kwa kukujuza hata maulamaa waliojitahidi zamani na wao waana makosa yao waliyoyafanya, hawapo sahihi kwa asilimia zote. Iliyo sahihi na isio na shaka ni Qur'an pekee.
 
Unaharibu uzi wa watu kwa kuweka mabandiko marefu yasioeleweka, fungua uzi wako unaohusiana na makanisa, hapa tunasoma habari za majinni.
 
Mtoa mada unaonekana unayajua majini vizuri.
Hebu nitaftie Jini Moja Jema linalo shika dini vizuri kwa ajiri ya kuniletea pesa mimi ili zinisaidie kutatua changamoto mbalimbali za maisha.
Nadhani kwa utaalamu wako utanifanikishia hili.
 
Karibu Arsis pole na majukumu, Darsa za kumalizia ni nyingi sana nakukumbusha tu.
Hili somo la kuwakamata majini ni la muhimu sana lini utaanza kulitoa?
 
Unaharibu uzi wa watu kwa kuweka mabandiko marefu yasioeleweka, fungua uzi wako unaohusiana na makanisa, hapa tunasoma habari za majinni.
Habari Dada faiza FaizaFoxy
Samahani Sana Kwa kukukwaza kwa Bandiko Langu ambalo wewe Umeona Halina Maana..

Ufafanuzi:

Kama Ukiangalia Vizuri Bandiko hilo Limeandikwa Tarehe 05 December 2024 Obviously Lina Miezi Miwili Tangu liandikwe..
Na kama Umenotice Ni kwamba Baada ya Bandiko Hilo Sikuwasilisha Bandiko jingine tena kwenye Uzi huu..

Nini Kilitokea!

Watu waliomba Niongelee hiyo Mada na Nilikataa (Maana kwa Kawaida Huwa Sianzishi Mada Kwenye Mada ya Mtu mwingine unless Inahusiana na Jambo husika..

Ikabidi nimtafute Mwenye Uzi wake na Kumuuliza Kuhusu Maoni ya Watu kuongelea Kuhusu Muktadha Wa makanisa saba kama Ilivyoongelewa kwenye Ufunuo Na Ku Decipher the massage Behind nikapata Baraka Zote za Mtoa mada Kuwa ninaweza Kuliongelea..

Nilipoliongelea Baada ya Wiki moja Nikapokea Maoni Tofauti kutoka kwa Watu tofauti wengine ni watu ninaowaheshimu Sana kuniambia Nisitishe jambo hilo na Nilikubaliana nao na Nikasitisha Kuongelea Swala Hilo kwa muktadha wowote huku Wasomaji Nikiwaadaa Kuwa Nitawaletea Somo hilo nikipata Muda (Siri nyuma ya Kuahirisha Kila siku Kuleta somo hilo)..

Samahani Sana Kwa Kukereka lakini Kwa bahati mbaya Ni kwamba Kero yako Imechelewa Kufika kwa sababu Kero zote ziliwasilishwa ndani ya Wiki Moja huenda Ningeijibu kwa Muda..

Asante sana
 
Mkuu .. What's wrong ukiendelea na hiyo mada kama mwenye uzi kakuruhusu?
Hata hivyo naheshimu maamuzi yako mkuu just i want to know.
 
Kumbe ni Mjinga kiasi hiki.
Mjinga kivipi ?
Kama Sulemani aliyatumia Majini mema katika kumsaidia kufanyia kazi mbali mbali, kwanini mimi nisiichukue hiyo fulsa ili kujiongezea kipato?

Tambua kua kiumbe chochote duniani kinaweza kutumika katika shughuri za kuinua uchumi.

Punda anatumika kubeba mizigo, Ng'ombe anatumika katika shughuri za Kilimo.

Kwanini wewe umekasirika sana niliposema mtoa mada anisaidie kunipa majini kazi kama anauzoefu kwa upande huo?

Je ni kwanini wewe hupendi mimi kupata msaada toka kwa majini wema ?

Kumbuka ni Juzi Dr. Sule alitamka kuwa;

"Kuwatumia Majini wema kujiongezea kipato sio dhambi"

Ni kwanini wewe hutaki mimi kutumia hiyo fulsa?
 
Karibu Arsis pole na majukumu, Darsa za kumalizia ni nyingi sana nakukumbusha tu.
Hili somo la kuwakamata majini ni la muhimu sana lini utaanza kulitoa?
In shaa Alah tutaliaza wiki hii, hili ndio kwa kiwango kikubwa lilinifanya nisitishe mada ya Comorro, kwani huko ndio nilipoanza kuliona mubashara. Ni very interesting, tutagusia kidogo nimalizie kipande cha Comorro japo kwa summary ili nikinza hili nidumu nalo nilimalize haraka, watu wasiende wakajidai mafundi wakajiumiza wao na wengine. Ni somo refu kiasi.
 
Sawasawa
Naona umeweka tahadhari sana watu wasijaribu mpka somo liishe, Mwenye masikio na asikie.
 
Hayo mambo yapo, ni ushirikina mjubwa sana ambao utakufikisha uanza kutoa kafara za damu za watu.

Mimi napigana nao wanoyoyafanya hayo. Soma kisa cha Unguja, kipo humu, utayaona madhara yake kijuujuu, pia kisa cha Tanga. Utavipata hapa kwenye fahirisi ya uzi:

 
Sawasawa
Naona umeweka tahadhari sana watu wasijaribu mpka somo liishe, Mwenye masikio na asikie.
Naam ni mambo mazito sana, kinga ya kwanza ni salat na kulinda udhu wetu. Tusiziache wala kuzidharau sala zetu tano kwa siku, na kila tuwezapo kusali za ziada tuzisali. Ni kinga kubwa sana. Hii dunia ina mengi sana mabaya tusiyoyaona.
 
Nakushauri ulifungulie uzi wako kama alivoshauri dada yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…