Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Endelea kutafta mahali wakristo wamepata jina Yesu lakini kwa jina hilo mapepo yanatoka.. viwete wanatembea.. wagonjwa wanapona.. wafu wanafufuliwa..

Mnafocus na vitu visivyo na maana as if mkionyeshwa mtaamini.. msipoteze wakati
Siku za usoni utayaona mengi sana kuhusu majini kwenye uzi huu. Usidhani ndio tumemaliza, ndio kwanza tunaanza.
 
Wale wanaokuja pm (dm) kwa mambo yao, tafadhali ongeeni hapahapa jukwaa la wazi, huu uzi wa mafunzo hatuwezi kuongea siri, tunataka iwe faida kwa wengi.

Usidhani tatizo lako ni lako peke yako.
 
"Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israel uulize neno kwake, hata unaenda kuuliza kwa Baal ze bubu, Mungu wa ekron?"
EWaislam tunaamini Mwenyezi Mungu ni mmoja tu, hakuna wa taifa fulani au kabila fulani. Kumgawa Mwenyezi Mungu Kimataifa au kikabila ni kumshirikisha na kufuru Kiislam.

Iwe kikauli au kiitikadi, yote ni kukufuru.
 
Mjinga kivipi ?
Kama Sulemani aliyatumia Majini mema katika kumsaidia kufanyia kazi mbali mbali, kwanini mimi nisiichukue hiyo fulsa ili kujiongezea kipato?

Tambua kua kiumbe chochote duniani kinaweza kutumika katika shughuri za kuinua uchumi.

Punda anatumika kubeba mizigo, Ng'ombe anatumika katika shughuri za Kilimo.

Kwanini wewe umekasirika sana niliposema mtoa mada anisaidie kunipa majini kazi kama anauzoefu kwa upande huo?

Je ni kwanini wewe hupendi mimi kupata msaada toka kwa majini wema ?

Kumbuka ni Juzi Dr. Sule alitamka kuwa;

"Kuwatumia Majini wema kujiongezea kipato sio dhambi"

Ni kwanini wewe hutaki mimi kutumia hiyo fulsa?
Majini wa kishetani ni laghai na waongo sana. Lengo lao uwache kumwabudu Mwenyezi Mungu uwaabudu wao. Sijaisikia kauli ya Dr. Sule, siwezi kuijibu.
 
Mie mbona Aris kashindwa kukupa taarifa zangu.. au kapofuka
Arsis hafanyi kazi za kujua au kuchunguza taarifa za watu. Huo ni umbea. Hairuhusiwi Kiislam:

Q 49:12. Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu
 
Arsis (simba) habari za siku ya leo mkuu natumai u mzima kabisa

Ukiniuliza hali yanguu ata sielewi asee yaani sijielewi mambo ya ajabu ni mengi mkuu

Wiki hii j3 kama sio j4 kuna mambo ya ajabu yamenitokea ndo nakuja kushtukia leo.... iko hivi mimi naumwa na nina rafiki yangu ambayr anakujaga kunitembelea nyumbani anaweza ata kukaa pia mwezi mzima na zaidi innshort amekuwa kama ndugu.
Sasa hiyo siku ilikuwa jioni kama saa kumi na moja hivi huyo rafiki yangu alikuja na mimi nilikuwa nimelala si unajua usingizi ulivyo mtamu bhana

Alivyokuja hakuniamsha bali mimi ndo niliamka licha kutoosikia mtu kuingia yaani nimefumbua macho na kugeuza kichwa jamaa huyu hapa akaniambia "fresh" kwa ishara na mimi nikajibu then nikagonga tano nikarudi kulala huku nikijua rafiki yangu huwa haondoki nikiwa nimelala badala yake atabaki akicheki zake muvi au aniamshe tupige story za hapa na pale ila hakuniamsha basi nikafumba macho kama nusu saa hivi then nikasema acha nizinguane naye tu maana sio fair mtu anakuja kukuona wewe unalala tu

Ile kufumbua macho hayupo kuwauliza madogo wakasema kaondoka nikasshangaa mbona hajaaga sio kawaida yake hiyo
. Nikajisemea atakuwa ameenda kumsalimia mpenzi wake ambaye ni jirani na kwetu so atarudi tu ila cha ajavu mpaka iinafika saa tatu usiku jamaa hoka


Kuja kumuuliza kwenye simu mbona hakuaga plus lawama leo ndo anajibu anasema hakuja kabisa asee nimeshtuka pengine ni jini amechukua sura yake kuja kuniona, nimefikia hata hatua ya kuwaza pengine mwamba Arsis amekuja kuniona(sorry sir for suspecting you)

Na kama sio jini ni nani sasa huyo maana braza hapa anasema hajaja

Yaani sielewi ata mkuu hapa itakuwa nini sasa?
Ni nafsi zinatembeleana.
 
kingine ni kuhusu leo baada ya jana usiku kukesha naangalia series moja ya kichina "fangs of fortune" kwenye simu na kutafuta nyuzi za kusoma kuhusu mambo ya kiroho hatimae nikachoka basi nikalala na kama sikosei nimelala saa kumi na mbili asubuhi nikaota ndoto nyingi za ajabu tofauti ila iliyoniamsha yaani kunishtua ni moja nimeota nikiwa nimelala chumbani ghafla kwenye ndoto nikamnasa mchawi uchi kapaka maunga meupe nimembamba analoga chumbani kwangu sijui ndo alikuwa anaanza au amemaliza au ameishia njiani baada ya kumuona(ni mwanamke) basi akataka kutoroka akawa ananinyooshea kidole kama ananisema hivi basi na mimi ikabidi nikemee potelea mbali uoga


Nikaanza kumkemea "kwa jina la yesu shindwaa, fireeeee!! Moto wa yesu unguaaaaa!!" Lakini wapi(kumbuka bado nomelala hapo na ata ndotoni navyokemea nilikuwa nimelala uwezo wa kuamka sina) alafu kama kuna nguvu flanì inanizuia nisiamke yaani nilikuwa najua kabisa naota ila sasa kuamka ndo shida yaani mwili mzima kama unatetema hivi au tuseme kama ganzii flani nimenasa kitandani

WAkati naendelea kukemea mchawi akawa anataka kutoroka dirishani mara akanasa dirishani na ajabu hapo dirishani kuna kiumbe mwingine kanasa ata sijui kama ni mtu ila umbo ni la binadamu na ni mkubwa kiumbo ila yeye hakuwa uchi lakini amenasa
yeye na mwenzake wananiangalia basi mimi nazidisha kukemea na mwisho wa siku nikaweza kuamka ila kichwa kinauma asee

Nini hiyo mkuu na ina maana gani?
Endelea kuusoma huu uzi utapata majibu ya kina, lakini kwa ufupi; Ndoto zetu ndio uhalisia "reality ya nafsi zetu na roho zote".
 
Huu uzi kuna visa vya Unguja sivioboi, viumechakachuliwa na nani Moderator?

Ilikuwa nianzie hapo nimalizie kisa cha Comorro, mwenye kupaona tulipoishia Unguja aniponeshe.
 
EWaislam tunaamini Mwenyezi Mungu ni mmoja tu, hakuna wa taifa fulani au kabila fulani. Kumgawa Mwenyezi Mungu Kimataifa au kikabila ni kumshirikisha na kufuru Kiislam.

Iwe kikauli au kiitikadi, yote ni kukufuru.
Kitu kimoja umewaambia ukweli hawa maamuma ni kuwa Allah sio Mungu ni jini mwenzio, watu wasimuombe Allah, wanatakiwa kumwomba "Illah", huyo ndio mwezi Mungu kwa kiarabu, lakini naona maamuma wamekomaa kumwabudu jini mwenzio Allah
 
Kitu kimoja umewaambia ukweli hawa maamuma ni kuwa Allah sio Mungu ni jini mwenzio, watu wasimuombe Allah, wanatakiwa kumwomba "Illah", huyo ndio mwezi Mungu kwa kiarabu, lakini naona maamuma wamekomaa kumwabudu jini mwenzio Allah
Expert wangu si kila uzi ni wa kila mtu, haikusaidii chochote kuleta kashfa hapa na heshimu imani za wenzio

Jf ni kubwa sana,tembelea majukwaa mbali mbali utakutana na mambo yenye hadhi yako
 
Kitu kimoja umewaambia ukweli hawa maamuma ni kuwa Allah sio Mungu ni jini mwenzio, watu wasimuombe Allah, wanatakiwa kumwomba "Illah", huyo ndio mwezi Mungu kwa kiarabu, lakini naona maamuma wamekomaa kumwabudu jini mwenzio Allah
Hewala mtaalaamu wa Qur'an na Kiarabu.

Wewe tuwache sisi na ujinga wetu tumuabudu Allah, wewe abudu umpendae.
 
Vipi m@moderator, nani kaupunguza huu uzi, kisa cha Arsis cha Unguja sikioni. Kama mmekifuta si mnatakiwa mtujulishe?
Hii tabia ya mods kufuta nyuzi za watu inakera sana... sijui wanafaidika na nini. Wanasema eti where we dare to talk openly na tukiongea vya maana wanafuta ilihali sheria haijakiukwa.

Kama sio kukosesha watu maarifa ni nini?? Maana kuna wengine hawajasoma
 
Back
Top Bottom