Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Hayo mambo yapo, ni ushirikina mjubwa sana ambao utakufikisha uanza kutoa kafara za damu za watu.

Mimi napigana nao wanoyoyafanya hayo. Soma kisa cha Unguja, kipo humu, utayaona madhara yake kijuujuu, pia kisa cha Tanga. Utavipata hapa kwenye fahirisi ya uzi:

Mhh! Embu fafanua zaid Arsis iweje kuwatumia majini katika kukuza uchumi iwe shirk, Maana nabii suleiman aliwatumia na hapo naona Che mittoga amesema majini wazuri, Ina maana majini wazuri hawawezi msaidia mwanadamu kupata mali?
 
Naam ni mambo mazito sana, kinga ya kwanza ni salat na kulinda udhu wetu. Tusiziache wala kuzidharau sala zetu tano kwa siku, na kila tuwezapo kusali za ziada tuzisali. Ni kinga kubwa sana. Hii dunia ina mengi sana mabaya tusiyoyaona.
Simba wewe umepata bahati ya kufunguliwa macho na kuona mengi ambayo watu wengi hatuyaoni, Kwa uzoefu wako ukitoa masokoni ni maeneo gani mengine ambayo mashetani wanapenda kuwepo.
 
Vipi
Hayo mambo yapo, ni ushirikina mjubwa sana ambao utakufikisha uanza kutoa kafara za damu za watu.

Mimi napigana nao wanoyoyafanya hayo. Soma kisa cha Unguja, kipo humu, utayaona madhara yake kijuujuu, pia kisa cha Tanga. Utavipata hapa kwenye fahirisi ya uzi:

Mtu anaweza kushirikiana na mtu mbaya kufanya mambo mabaya.

Pia mtu anaweza kushirikiana na mtu mwema kufanya mambo mema.

Kutoka na uzoefu wako.
Hivi kuna shida gani kushirikiana na Majini wema kufanya mambo mema ?

Kama Majini wema wapo, kuna shida gani kuwashirikisha katika kufanya mambo mazuri ya ibada ya maendeleo ?
 
Mhh! Embu fafanua zaid Arsis iweje kuwatumia majini katika kukuza uchumi iwe shirk, Maana nabii suleiman aliwatumia na hapo naona Che mittoga amesema majini wazuri, Ina maana majini wazuri hawawezi msaidia mwanadamu kupata mali?
Asante kwa kunisaidia hili jambo.
Kama Majini wana nguvu na uwezo kuna haja sasa ya kuwashirikisha katika sekta ya maendeleo.
Kama waovu wanatumika kwa uchawi basi wale wema wanaweza kabisa kutumika katika maswala ya kujenga uchumi.
 
1000019674.jpg
 
Vipi

Mtu anaweza kushirikiana na mtu mbaya kufanya mambo mabaya.

Pia mtu anaweza kushirikiana na mtu mwema kufanya mambo mema.

Kutoka na uzoefu wako.
Hivi kuna shida gani kushirikiana na Majini wema kufanya mambo mema ?

Kama Majini wema wapo, kuna shida gani kuwashirikisha katika kufanya mambo mazuri ya ibada ya maendeleo ?
Hakuna jini mwema wa kukupa utajiri. Jini mwema anakushauri mema na kukukataza kufanya maasi.
 
Mhh! Embu fafanua zaid Arsis iweje kuwatumia majini katika kukuza uchumi iwe shirk, Maana nabii suleiman aliwatumia na hapo naona Che mittoga amesema majini wazuri, Ina maana majini wazuri hawawezi msaidia mwanadamu kupata mali?
Majini wema huna haja ya kuwatumia, wapo na wanafanya mema bila kutumiwa na mtu.

Kama ulivyo wewe binadam, kufanya mema mpaka utumiwe na mwingine?

Soma visa vya Arsis humu, hakuna hata kisa kimoja alitumiwa na mtu kufanya mema, bali yeye hufanya mema kwa wema wake tu.
 
Wapo kila mahali lakini wanogopa sana sehemu inaposomwa Qur'an na adhana.
Vipi kuhusu makazi yao je kuna tofauti ya kitabia na elimu kwa majini wanaoishi majini na kwenye miti mikubwa na wanaoishi milimani?
Na ni falme gani kati ya hizo ina nguvu kuliko falme nyingine ?
 
Majini wema huna haja ya kuwatumia, wapo na wanafanya mema bila kutumiwa na mtu.

Kama ulivyo wewe binadam, kufanya mema mpaka utumiwe na mwingine?

Soma visa vya Arsis humu, hakuna hata kisa kimoja alitumiwa na mtu kufanya mema, bali yeye hufanya mema kwa wema wake tu.
Kwamaana hiyo jini mwema anaweza kutoa msaada kimyakimya tu akiona kuna haja ya kufanya hivyo.
Na vipi kuhusu wachawi, Wanaweza kuwakamata hao majini wema kichawi na wakawatumia katika shughuli zao za kichawi? au wao wanaweza kuwatumia mashetani tu?
 
Habari Dada faiza FaizaFoxy
Samahani Sana Kwa kukukwaza kwa Bandiko Langu ambalo wewe Umeona Halina Maana..

Ufafanuzi:

Kama Ukiangalia Vizuri Bandiko hilo Limeandikwa Tarehe 05 December 2024 Obviously Lina Miezi Miwili Tangu liandikwe..
Na kama Umenotice Ni kwamba Baada ya Bandiko Hilo Sikuwasilisha Bandiko jingine tena kwenye Uzi huu..

Nini Kilitokea!

Watu waliomba Niongelee hiyo Mada na Nilikataa (Maana kwa Kawaida Huwa Sianzishi Mada Kwenye Mada ya Mtu mwingine unless Inahusiana na Jambo husika..

Ikabidi nimtafute Mwenye Uzi wake na Kumuuliza Kuhusu Maoni ya Watu kuongelea Kuhusu Muktadha Wa makanisa saba kama Ilivyoongelewa kwenye Ufunuo Na Ku Decipher the massage Behind nikapata Baraka Zote za Mtoa mada Kuwa ninaweza Kuliongelea..

Nilipoliongelea Baada ya Wiki moja Nikapokea Maoni Tofauti kutoka kwa Watu tofauti wengine ni watu ninaowaheshimu Sana kuniambia Nisitishe jambo hilo na Nilikubaliana nao na Nikasitisha Kuongelea Swala Hilo kwa muktadha wowote huku Wasomaji Nikiwaadaa Kuwa Nitawaletea Somo hilo nikipata Muda (Siri nyuma ya Kuahirisha Kila siku Kuleta somo hilo)..

Samahani Sana Kwa Kukereka lakini Kwa bahati mbaya Ni kwamba Kero yako Imechelewa Kufika kwa sababu Kero zote ziliwasilishwa ndani ya Wiki Moja huenda Ningeijibu kwa Muda..

Asante sana
Ila nami nakulaumu kwa jambo moja kama ishu ndio hiyo ni bora ungekuwa wazi kwamba kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu nasitisha mada

Sasa ndugu Lidafo kila wakati alikuwa anakukumbusha unapiga kimya kumbe unajua unachofanya

Doktori huu sio uungwana
 
Kwamaana hiyo jini mwema anaweza kutoa msaada kimyakimya tu akiona kuna haja ya kufanya hivyo.
Na vipi kuhusu wachawi, Wanaweza kuwakamata hao majini wema kichawi na wakawatumia katika shughuli zao za kichawi? au wao wanaweza kuwatumia mashetani tu?
hukulia mfano wa binadam tu, hakuna tofauti kabisa.

Tunavyoendelea na visa na mikasa ya SArsis tutayaona mengi sana. Mliyoyasoma mpaka sasa ni mwaka au miaka miwili tu ya mwanza yo kujuana nae, sasa ni zaidi ya miaka 30.

Kuna mengi sana ambayo nina uhakika wengi wetu hatujawahi hata kuyawaza. Ulimwengu wetu una mengi sana. Tusiache kusoma na tusidhani kila tunachokijua sisi ndicho hicho hicho.
 
hukulia mfano wa binadam tu, hakuna tofauti ka isa.

Tunavtyoendelea na visa na mikasa ya SArsis tutayaona mengi sana. Mliyoyasoma mpaka sasa ni mwaka au miaka miwili tu ya mwanza yo kujuana nae, sasa ni zaidi ya miaka 30.

Kuna mengi sana ambayo nina uhakika wengi wetu hatujawahi hata kuyawaza. Ulimwengu wetu una mengi sana. Tusiache kusoma na tusidhani kila tunachokijua sisi ndicho hicho hicho.
Kikubwa usipotee sana,wengine hupenda kujifunza mambo tofauti tofauti
 
hukulia mfano wa binadam tu, hakuna tofauti ka isa.

Tunavtyoendelea na visa na mikasa ya SArsis tutayaona mengi sana. Mliyoyasoma mpaka sasa ni mwaka au miaka miwili tu ya mwanza yo kujuana nae, sasa ni zaidi ya miaka 30.

Kuna mengi sana ambayo nina uhakika wengi wetu hatujawahi hata kuyawaza. Ulimwengu wetu una mengi sana. Tusiache kusoma na tusidhani kila tunachokijua sisi ndicho hicho hicho.
It's been a long time sir but thats okay now am here with a new indentity

Sio mbaya ninajifunza mambo mapya
 
Habari Dada faiza FaizaFoxy
Samahani Sana Kwa kukukwaza kwa Bandiko Langu ambalo wewe Umeona Halina Maana..

Ufafanuzi:

Kama Ukiangalia Vizuri Bandiko hilo Limeandikwa Tarehe 05 December 2024 Obviously Lina Miezi Miwili Tangu liandikwe..
Na kama Umenotice Ni kwamba Baada ya Bandiko Hilo Sikuwasilisha Bandiko jingine tena kwenye Uzi huu..

Nini Kilitokea!

Watu waliomba Niongelee hiyo Mada na Nilikataa (Maana kwa Kawaida Huwa Sianzishi Mada Kwenye Mada ya Mtu mwingine unless Inahusiana na Jambo husika..

Ikabidi nimtafute Mwenye Uzi wake na Kumuuliza Kuhusu Maoni ya Watu kuongelea Kuhusu Muktadha Wa makanisa saba kama Ilivyoongelewa kwenye Ufunuo Na Ku Decipher the massage Behind nikapata Baraka Zote za Mtoa mada Kuwa ninaweza Kuliongelea..

Nilipoliongelea Baada ya Wiki moja Nikapokea Maoni Tofauti kutoka kwa Watu tofauti wengine ni watu ninaowaheshimu Sana kuniambia Nisitishe jambo hilo na Nilikubaliana nao na Nikasitisha Kuongelea Swala Hilo kwa muktadha wowote huku Wasomaji Nikiwaadaa Kuwa Nitawaletea Somo hilo nikipata Muda (Siri nyuma ya Kuahirisha Kila siku Kuleta somo hilo)..

Samahani Sana Kwa Kukereka lakini Kwa bahati mbaya Ni kwamba Kero yako Imechelewa Kufika kwa sababu Kero zote ziliwasilishwa ndani ya Wiki Moja huenda Ningeijibu kwa Muda..

Asante sana
Not fair at all mkuu.... Tumengoja sana ili mwisho wa siku tusikie hiki? But once a decision is made there is nothing we can do to change it
 
Arsis (simba) habari za siku ya leo mkuu natumai u mzima kabisa

Ukiniuliza hali yanguu ata sielewi asee yaani sijielewi mambo ya ajabu ni mengi mkuu

Wiki hii j3 kama sio j4 kuna mambo ya ajabu yamenitokea ndo nakuja kushtukia leo.... iko hivi mimi naumwa na nina rafiki yangu ambayr anakujaga kunitembelea nyumbani anaweza ata kukaa pia mwezi mzima na zaidi innshort amekuwa kama ndugu.
Sasa hiyo siku ilikuwa jioni kama saa kumi na moja hivi huyo rafiki yangu alikuja na mimi nilikuwa nimelala si unajua usingizi ulivyo mtamu bhana

Alivyokuja hakuniamsha bali mimi ndo niliamka licha kutoosikia mtu kuingia yaani nimefumbua macho na kugeuza kichwa jamaa huyu hapa akaniambia "fresh" kwa ishara na mimi nikajibu then nikagonga tano nikarudi kulala huku nikijua rafiki yangu huwa haondoki nikiwa nimelala badala yake atabaki akicheki zake muvi au aniamshe tupige story za hapa na pale ila hakuniamsha basi nikafumba macho kama nusu saa hivi then nikasema acha nizinguane naye tu maana sio fair mtu anakuja kukuona wewe unalala tu

Ile kufumbua macho hayupo kuwauliza madogo wakasema kaondoka nikasshangaa mbona hajaaga sio kawaida yake hiyo
. Nikajisemea atakuwa ameenda kumsalimia mpenzi wake ambaye ni jirani na kwetu so atarudi tu ila cha ajavu mpaka iinafika saa tatu usiku jamaa hoka

Kuja kumuuliza kwenye simu mbona hakuaga plus lawama leo ndo anajibu anasema hakuja kabisa asee nimeshtuka pengine ni jini amechukua sura yake kuja kuniona, nimefikia hata hatua ya kuwaza pengine mwamba Arsis amekuja kuniona(sorry sir for suspecting you)

Na kama sio jini ni nani sasa huyo maana braza hapa anasema hajaja

Yaani sielewi ata mkuu hapa itakuwa nini sasa?
 
kingine ni kuhusu leo baada ya jana usiku kukesha naangalia series moja ya kichina "fangs of fortune" kwenye simu na kutafuta nyuzi za kusoma kuhusu mambo ya kiroho hatimae nikachoka basi nikalala na kama sikosei nimelala saa kumi na mbili asubuhi nikaota ndoto nyingi za ajabu tofauti ila iliyoniamsha yaani kunishtua ni moja nimeota nikiwa nimelala chumbani ghafla kwenye ndoto nikamnasa mchawi uchi kapaka maunga meupe nimembamba analoga chumbani kwangu sijui ndo alikuwa anaanza au amemaliza au ameishia njiani baada ya kumuona(ni mwanamke) basi akataka kutoroka akawa ananinyooshea kidole kama ananisema hivi basi na mimi ikabidi nikemee potelea mbali uoga

Nikaanza kumkemea "kwa jina la yesu shindwaa, fireeeee!! Moto wa yesu unguaaaaa!!" Lakini wapi(kumbuka bado nomelala hapo na ata ndotoni navyokemea nilikuwa nimelala uwezo wa kuamka sina) alafu kama kuna nguvu flanì inanizuia nisiamke yaani nilikuwa najua kabisa naota ila sasa kuamka ndo shida yaani mwili mzima kama unatetema hivi au tuseme kama ganzii flani nimenasa kitandani

WAkati naendelea kukemea mchawi akawa anataka kutoroka dirishani mara akanasa dirishani na ajabu hapo dirishani kuna kiumbe mwingine kanasa ata sijui kama ni mtu ila umbo ni la binadamu na ni mkubwa kiumbo ila yeye hakuwa uchi lakini amenasa
yeye na mwenzake wananiangalia basi mimi nazidisha kukemea na mwisho wa siku nikaweza kuamka ila kichwa kinauma asee

Nini hiyo mkuu na ina maana gani?
 
Mjinga kivipi ?
Kama Sulemani aliyatumia Majini mema katika kumsaidia kufanyia kazi mbali mbali, kwanini mimi nisiichukue hiyo fulsa ili kujiongezea kipato?

Tambua kua kiumbe chochote duniani kinaweza kutumika katika shughuri za kuinua uchumi.

Punda anatumika kubeba mizigo, Ng'ombe anatumika katika shughuri za Kilimo.

Kwanini wewe umekasirika sana niliposema mtoa mada anisaidie kunipa majini kazi kama anauzoefu kwa upande huo?

Je ni kwanini wewe hupendi mimi kupata msaada toka kwa majini wema ?

Kumbuka ni Juzi Dr. Sule alitamka kuwa;

"Kuwatumia Majini wema kujiongezea kipato sio dhambi"

Ni kwanini wewe hutaki mimi kutumia hiyo fulsa?
"Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israel uulize neno kwake, hata unaenda kuuliza kwa Baal ze bubu, Mungu wa ekron?"
 
Back
Top Bottom