Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Habari Simba Arsis
Kuna visa vingi sana umeishia njiani na baadhi ya mada ambazo Arsis hajamalizi, Rudi kama mwanzo mkuu.
Nakukumbusha tuu
1. Kuna kisa cha adamu ulikianza tukaishia njiani na kuna sehemu Arsis aligusia kuwa Abu jafar Muhammad ibn Jarir ibn yazid (Attabar) ndio aliyeleta wazo la Adam ni binadamu wa kwanza lakini vitabu vingi kuhusu kazi zake viliandikwa baada ya yeye kuondoka, Hivyo swali likabaki ni nani aliyeviandika na kwa malengo gani?, Arsis alisema hii pia ni mada nyingine hivyo nawakumbusha.

2.Kuhusu kisa cha adam pia, Arsis alianza kufanya Tafsil kuchambua neno kwa neno akasema ataelezea ile kauli ya Allah kuwaambia malaika wamsujudie Adam ila hakuelezea hilo nalo namkumbusha.

3. Lingine ni visa vyako ujamalizia baadhi na ulisema ndani ya wiki hii utaanza somo la jinsi ya kuwakamata majini, Pia nakukumbusha.
 
Arsis Mkuu tukumbuke mimi kwa kumbukumbu zangu kuhusu kisa cha comorro nadhani ulimaliza haina haja we leta tu hiyo elim mpya watu wajifunze and me too

Looking forward for your knoeledge!🥂
 
Arsis,
Swali
Kuna waganga wa mitishamba huwa wanaoneshwa dawa za matibabu na Majini.
Na dawa hizo zinawatibu watu magonjwa yao hadi wanapona kabisa.
Hapo tuna pata mambo mawili matatu.

1. Huyo mganga wa mitishamba anajiingizia kipato kwa kutibu watu

2. Wagonjwa wanapona magonjwa yao baada ya kutibiwa na hizo dawa asili

3. Waganga hao wanalipa kodi serikalini.

4. Mchango wao kwa jamii unathaminiwa.

Swali.
Ushirikiano huu wa mganga asili na Majini una nafasi gani kwenye dini unayo ijua?

Je ni ushirikiani mzuri au mbaya ?

Je Jini anayesaidia kumwonesha dawatiba mtabibu asili ni Jini mbaya au mzuri?

Nipo nasubiri majibu yako mtaalam.
 

Wewe umepeqa pingiri unavuta mua mzima.

Huna maana hata chembe.
 
= fursa
 
Arsis leta vitu.

Atakayejidai mjanja yakimkumba ya kumkumba ndiyo ataelewa kilichomtowa kanga manyoya ni nini.
 
Naona huchezi mbali na hii mada,
Kuhusu lugha mimi nakuacha mbali sana.
Tizama michango yako kwanye mada za DP World uone jinsi ulivyokuwa unachapia.
Na tulikuwa tunakuacha tu.
Nitawachaje inipite na Qur'an imetufundisha kuwa elimu ya roho wamepewa wachache sana na kwa uchache sana. Soma...

Q.17:85. Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu.85
 
Nitawachaje inipite na Qur'an imetufundisha kuwa elimu ya roho wamepewa wachache sana na kwa uchache sana. Soma...

Q.17:85. Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu.85
Niulizie kwa Arsis, kama anasema Majini wazuri hawana msaada kwa binadamu.
Vipi kwa baadhi ya Mashehe ambao wamewaomba Malaika na Majini ili mtu ashinde uchaguzi ujao ?
Inamaana yeye ana elimu ya dini kuwapita Mashehe wake ?
 
Niulizie kwa Arsis, kama anasema Majini wazuri hawana msaada kwa binadamu.
Vipi kwa baadhi ya Mashehe ambao wamewaomba Malaika na Majini ili mtu ashinde uchaguzi ujao ?
Inamaana yeye ana elimu ya dini kuwapita Mashehe wake ?
Wengi wnadanganya wanadanganywa.
 
Nipo hapa Mkuu Arsis kupata muongozo sahihi maana hao watu siwawezi kwa lolote ila Mimi haki yangu naitaka. Najua nafuatiliwa sana mpaka mtaani. Roho inaniuma kwanini wale jasho la Mnyonge kama Mimi wakati wao wana kila kitu wanachokitaka?
Mkuu ulijuaje kama vyeti vyako vinatumiwa? Ulifanikiwa kupata msaada? Isije kuwa majina yanafanana.
 
Arsis umeisusa mada yako au vipi ?
upo kimya tu na hujawaaga wasomaji wako.
Au umerudi Tanga kuongeza maarifa?
Kwa ukimya huu nina uhakika kuna kundi la watu wamekuja DM kwako na kukuzuia usiendelee kueleza vile ulivyoona baada ya kufumbuliwa macho.
Ili usije ukawaumbua zaidi na zaidi. mimi nishajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…