Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Wasomi wengi wa dini hasa Sunni wanawachukulia sufi kama watu wasio katika usahihi hii ni kutokana na mambo yao hasa wengi kujihusisha na mambo ya uganga ijapokuwa wapo masufi wanaelimu kubwa tuu na ni wachamungu kwelikweli.
Moja katika masufi wakubwa ni huyu Ahmad Al Buni yeye aliandika kitabu maarufu kiitwacho Shams al maarifa inadaiwa ni kitabu cha uganga na mambo ya talasimu.
Shams al Maarif na Shams al Maarif al Kubra...
....

@};--

Tanzania imekuwa na watu ‘Wateule’ wachache walioitengeneza njia na misingi ya ‘mageuzi/mapinduzi’ ya mifumo inatawala ‘Dunia ya Leo’ na hali, KWA SASA 2024, tupo kwenye kipindi cha ‘Lala Salama’, siku za mwisho za mifumo inayovuna ujinga na upoyoyo wa umma ambao haujazinduka. Basi ndiyo amani ya dunia inalega lega na kupitia changamoto nyingi kwa kuwa ‘vita na machafuko huku na kule’ ni koroga koroga na kukorogana kwa ‘wahuni’ katika jamii – jamii zilizo kwenye ‘mazingira hatarishi’ ama hata pia ‘zilizoendelea’; mambo ya ‘vipakazio’ vya kuepa mielekeo ya midololo wa kiuchumi na mifumo/siasa mbovu za tawala.

Tanzania Mpya na basi ‘Afrika Mpya’, Afrika 2.0, haiwezi kujitenga na madhila ya upepo mbovu wa kiuchumi, tawala na amani Duniani. Kusudi la kujihami na mambo haya, kwa Tanzania, lilitaasishwa kwa shughuli ya siasa za Chama cha Watu, Chama cha Wananchi—Chama cha Mapinduzi.

Haya yatukumbushe ukweli wa dhahabu, Afrika 2.0—Afrika Mpya, ni ushindi wa wanadamu wa sura na rangi zote. Mwalimu Kambarage Nyerere, alipodhihiri tamko la Chama cha Mapinduzi kuhusu dhamira na mwongozo kwa ajili ya kushirikiana ili kuleta ‘Haki na Amani’ Duniani, nia yake ilikuwa moja na ‘Roho ya Ushindi’:

Kazi ya Chama Cha Mapinduzi ni kuwaongoza Watanzania washirikiane na Waafrika wenzao kuleta uhuru na umoja katika Afrika nzima. Kazi ya Chama Cha Mapinduzi ni kuwaongoza Watanzania washirikiane na binadamu wenzao kuleta haki na amani duniani; Chama Cha Mapinduzi ni Chama cha watu; Chama Cha Mapinduzi kitaongoza kutoka miongoni mwa watu na kitaongoza kikiwa ni sehemu ya Watanzania maana wananchi ndio waliokiunda Chama Cha Mapinduzi kiwe chombo chao na kiongozi wao”

Mwenge wa Uhuru, ni shughuli ya kuchochea ‘Utaamuliko Jamii’ kwa ajili ya Afrika na Dunia Mpya—kupitia ‘UTU Mpya’; Mwanzo wa ‘Jua la Maarifu’.

====

View: https://www.youtube.com/watch?v=Po2R9IbJCAE
====


Jua la Maarifu​


Imani ni safari kwa ajili ya Hakika ya UTU na Uisho.

Siku za zamani, faraja ya Msafiri ni Dua yake na Imani, kwamba ijapokuwa akatiza katika ukonde wa uvuli wa mauti hatahofia Uovu.

‘Utaamuliko Jamii’ pia ni saga ya Msafiri; jamii inahitaji nguzo za imani kwa ajili ya safari yake ya matumaini – matumaini ya kuenenda salama.

Ijapokuwa jamii tofauti zimepata kufikiwa na miongozo ya kheri kwa ajili ya maisha na kuishi, jamii ya leo, tuseme 2024, bado inahitaji lile lile la ‘funguo za Maarifa’ kwa ajili ya kheri na salama ya maisha ya kileo.

Kiuono na ufikirifu mifumo, safari ya kujitafuta kiroho ina hatua tatu (1) Ya Nje, (2) Ya Mpito, na (3) Hatma ilivyo basi ni (A) Miongozo/Sheria, (B) Mbinu/vitendo imani, na (C) matunda ya kuiva na kukomaa kiroho. Kwa mintarafu ya haya, mambo ya nje ndiyo muktadha akilifu wa mapokeo ya kimila, desturi na sheria; mambo ya mpito ni muktadha akilifu wa ‘kaida/sala/miditisha; na mambo ya hatma ni Utaamuliko, Kujitambua, Kuifahamu KWELI.

Elimu 1.0 inahusu ‘Ya nje’; inaweza kusadifu mengi ya ‘maarifa ama/na kujua’ lakini kiufundi ni uelewa wa juu juu wa mambo. Elimu iliyotamalaki duniani—ya kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, kiufundi, bado ni Elimu 1.0; inakidhi fahamu za mawazo na fikra kwa sura za juu juu lakini ‘haina kina hasa’ cha ukweli wa mambo… Hili ndilo linalotaka hata ‘Maarifa ya Dini’ yaje kujaribu kukamilisha ‘kiu cha maarifa’ ya Kweli.

Elimu 2.0 inahusu ‘Ya Mpito’; ni njia ya hekima kwa kuwa Uono na Ufikirifu Mifumo ni shughuli ya kutangamanisha kinachojulikana na kile kisichojulikana pasipo ‘Kasumba’ bali ‘Ushahidi’ wa Muktadha Akilifu wa Ushahibiano wa Mambo. Hili ndilo linalotengeneza nasibu ya ‘Kuipa Kina’ Elimu 1.0 kwa yale yafahamikayo kwa ufasaha. Basi ndiyo yawa, Elimu 2.0 ni daraja la ‘yenye ukomo’ na ‘yale yasiyo na ukomo’ kwa kuwa ‘mapengo ya maarifa/maarifu’ daima yanakubalika; kilicho ni fumbo kinabaki kuwa fumbo na kinachojulikana kinayakinishwa kwa mapana, marefu na kina cha mashauri.

Elimu 3.0 inahusu ‘Hatma’; ni hitimisho la mafikara na mwanzo wa ‘Kuya-JUA’ yote. Kiufundi kuyajua yote, ni uweza na upeo wa kutangamanisha yanayojulikana na yasiyojulikana kwa ‘Taamuli’ na ‘Umbonishaji fahamu Sahihi’ wa mapana, marefu na kina ya mafikara/kujiwazia Utu—ili kupata kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wa ‘Uzabibu 13’, upitao ufahamu wa kawaida -- kwa jinsi ulivyo mwingi, kupata kutimilika kwa utimilifu wote wa kile kilicho ni khasa ‘Roho ya Uzima wote’.

Elimu 3.0 ni ‘Jua la Maarifu’--mwanzo wa kujua yote kwa jinsi ya ndani na nje ya dhahiri.

Elimu 1.0 na Elimu 2.0 ni ‘uwanja wa mafikara’ na hali Elimu 3.0 ni usikirifu na maarifu kwa siri za miundo/mageuzi na uzima wa miili. Kwa mintarafu ya haya, Elimu 3.0 ni ‘Maarifu’ ya halisia za ‘Mwezi na Nyota’ na pia ‘Msalaba’ wa fizikia na metafizikia ya mambo. Elimu 3.0 huleta madaraja ya nishani ya utu, kujichagulia na Matendo Makuu. Elimu 3.0 ndiyo ufunguo wa Ukamilifu wa Hekalu la Mwili—Mambo ya ‘Uimamu’ ama kusema ‘Uteule’ kwa huduma za kuongezea wengine njia katika ‘Safari za Kujitafuta Kiimani na Uisho’.

Katika ulimwengu halisi wa mambo, watu wa ‘Uimamu’ na ‘Uteule’ huandamwa na uhasimu wa ‘Mapokeo’ na ‘Taratibu’ kutokea kwa Wahifadhina wa hayo kwa kuwa, kiufundi, mapokeo na taratibu ni mambo ya usukaji miundo jamii kwa ajili ya ‘usawa wa kimashirikiano’; kuyatishia hayo usalama wake inaweza kuwa ni ‘msala’.

Miundo yote inayonasibu ya kubadilika palipo na ‘Nuru’/’Ujio wa Nuru’; kwa kuwa nuru ya ‘Jua la Maarifu’ daima husukuma ‘mageuzi’ ya utu na jamii’-- ‘ mwenye nuru’ na ‘jamii’ katika kukutana uso kwa uso. Basi, Nuru ya Mtu wa Daraja, huleta chachu mpya ya utamaduni na kujichagulia ambavyo inaweza kuwa rafiki ama si rafiki na ‘hali ilivyo’/Statusi Kwou.

Na hili ndiyo adha iliyowakumba watu wa ‘Mwangaza’ katika nyakati na jamii mbalimbali; jambo linalotaka ‘Mtu wa Mwangaza’ kuzicheza karata zake kwa uangalifu kwa kuwa ‘kiza cha utu’/statusi kwou si rafiki kwa ‘Mvinyo Mpya’. Hili pia ndiyo daima limefanya ulazima wa faragha ama ‘sanaa ya kujichanganya na hali usijulikane’; kwa watu wa Elimu 3.0 kuishi hivi. Kwa hivyo, kiufundi, watu wengi wa rizayati ya Elimu 3.0 wamekuwa ni walinzi wa ‘maarifa ya Kazi’ ya kuleta ‘Utaamuliko Jamii’ kwa ‘Subira’ na ‘Faragha’.

‘Maarifa ya Kazi’ ni upanga—ukiwa katika mikono salama, ni kheri ya ‘Haki’ na ‘Mapenzi Mema’ kuifikia jamii pana, kwa namna zinazofaa na wakati muafaka. Ukiwa katika mikono isiyo salama, ni ‘mkosi’ wa ‘Madhalimu’ na ‘Dhuluma’--mambo ya kufumbana ukweli wa mambo ili basi kutumiana katika mabatili ya ‘Kujilisha Upepo’. Kwa mintarafu ya haya, mambo ya faragha daima ni Utaasisi ndani ya Taasisi kwa kuwa Muundo wowote wenye kujishikilia kwa uadilifu wa mafikara/shauri, dhamira na matendo ni ‘Taasisi’.

Basi ndiyo yawa, si kwa kuwa kuna jumuiya inayodhaniwa kuwa na ‘faragha’ basi kuna nia ovu nyuma yake… Kuna namna hata ulimwengu wote umefanyika kwa mambo ya muktadha akilifu wa uwaziwazi na tena vile vile muktadha uliyositirika—jambo hili linalazimu uhitaji wa ‘Roho wa Busara ya Utambuzi’ kumaizi ni yepi ya kushiriki kwa kheri na kutoshiriki kwa kheri vile vile—mambo ya ‘kutotupia lulu kwa shuwaini’…

Katika kipindi hichi ya ‘Mavuno’, busara ni kutangamanisha yale yote ambayo yamejitokeza katika dini na miongozo yote ya UTU na kujichagulia--kuyatangamanisha kwa kusudi la ‘kuijengea jamii/jumuiya ya kimataifa uwezo wa kulivuka vuguvugu la upoteaji wa Amani na Tumaini’ Duniani. Hili linalazimu kulingania ‘Utaamuliko Jamii’ kwa minajili ya kuleta umahiri wa jamii yote nzima katika ugani wote wa Elimu 1.0, Elimu 2.0 na Elimu 3.0. Kuleta wepesi kwa jamii kutambua dini zote na mafundisho ya kiroho, hasa hasa yanayotawala idadi kubwa ya waumini, yana ‘Hazina’ ijayo ni ‘mafumbo ya Kiimani’ kwa ajili ya ‘Liberti’--kweli yenye kumweka mtu huru kweli kweli…

Kujengea jamii uwezo wa fumbua mafumbo ya imani kuna leta ‘kinga’ na ‘ulinzi’ dhidi ya migogoro inayoweza kuchochewa na ‘ujuaji wa juu juu wa mambo’--ujuaji mbovu unaoweza kuchochea dhamira, jitihada na matendo ya uhasama na machukizo dhidi ya ‘Ubinadamu’.

Shams al Maarif’, Jua la Maarifu, ni moja ya kompendiamu ya ‘Maarifa ya Kazi’ inayovutia wengi wenye nasibu ya Rizayati ya Elimu 3.0 na hali hapo hapo ‘inaogopwa’ na wengine wengi wasio na ‘msuli’ wa kuyakabili ‘Maarifa’ yake. Rizayati ya Elimu 3.0 ni uzao wa ‘shughuli za faragha’ za watu wa Maarifa na Maarifu. Katika mikono isiyo salama, huwa ni zana ya ‘Shetani’ na katika mikono salama huwa ni zana ya ‘Malaika’. Basi ndiyo yawa, katika ‘wakati muafaka’ ukweli wa hili hauna budi kuwekwa wazi ili kumalizana na ‘kasumba’ ama/na ‘nongwa’ ya ‘kujua mambo kwa sehemu’.

Hisia na Kujisikia ndiyo asili ya cheche ya ‘Utu’, ambavyo tena ni asili ya nukta na duara la utukufu wa ‘Roho ya Uzima wote’. Kiuno na ufikirifu mifumo, hili linashahibiana na ‘nukta’ ya ‘andiko’ la (1)Kauli/NENO la kuanza yote kwa Jina la Rehema na Fadhili. (2) Kushukuru na Kutukuza ni ‘ombi’ la kijiweka sawasawa na ‘Mapenzi na Kheri’ ya kile kilicho ni asili ya Uzima wote na Amali zote za ‘Mbingu’ na ‘Nchi’. Kwa mintarafu ya ‘Mamlaka’ na ushahibiano wa Utaasi wa UTU na Utamaduni, asili ya yote hutajwa ni ‘Bwana wa Ulimwengu’.

Kiuono na ufikirifu mifumo, ‘Ufunguo wa Imani’ ni ‘Vesika Paisisi’ ya ‘Uzabibu 13’ ambavyo (3) Mbegu ya Miongozo ya Utu bora inakiriwa na kundanishwa(Rehema na Fadhili), (4) Utambuzi wa Utaasisi wa ‘Mtu/jamii katika Imani’ na hatma ya ‘Nyakati’ unakiriwa na kundanishwa (Eskatolojia—Siku ya ‘Hesabu’), (5) Kujisalimisha katika ‘Nishani ya Utu Bora’ – udhamirifu wa jitihada za kustahiki ‘kheri ya utukufu’ katika ‘Safari ya Kujitafuta’ (Sifa za kutosha Kuabudiwa kile kilicho ni Khasa asili ya ‘Mbegu ya Utu’ wetu kama ‘watu’, (6) Udhamirifu wa ‘Jitihada Sahihi’ kwa ajili ya kupata uongozeaji wa njia – njia za kujichagulia yaliyo na kheri ya ‘utimilifu wa kusudi la UTU’, (7) Udhamirifu wa ‘Kutumainia Mema’ na kuwa ndani ya ‘Mapenzi Mema’ ya fahari ya UTU.
.....
Hmmmm​
 
Hapa mimi iutabidi unielimishga zaidi. Mimi ni Nyislam, Sufism shirk yake ni ipi wakati jina "sufi" linaashiria wepesi na usagfi wa kuwa karibu na Allah.

Tupe ilm na ushahidi siyo kurusha tuhuma.

Mimi ni Muislam nisiyekuwa na dhehebu isipokuwa Uislam tu, naamini sufism" siyo dhehebu bali ni lugha tu ikimaanisha njia za wenye kuabudu(tariqa t ibadi). Madhehebu ni yale yenye kufata majina ya watu kama Ukristo.

Mtazamo wangu huo.
Endelea kutetea shirk ,ukristo umeingiaje hapo
 
Jambo lingine kuna mtu sikutaka kuanzisha nae ligi,alipinga au anakataa kutokuwepo kwa majini wakristo.

Iko hivi binadamu ndio kiongozi wa hii dunia,hivyo mitume na manabii wote walikuwa wanadamu na sio majini,maana yake ni kwamba majini walisikia ujumbe wa Mungu kupitia mwanadamu na wao kazi yao ni kusikia na kufuata amri za Mungu

Kwahiyo kwa kila nabii walimsikia na lufuata ujumbe wake,hivyo walifuata mafundisho yake na kifuata hukumu zake,je walio mfuata Yesu walikuwa nani?

Na baada ya kuja Mtume Muhammad rehema na amani ziwe juu yake,walisikia qur'aan na mafunzo ya Mtume na kufuata uislamu,kama njia sahihi ya kumwabudu Mungu mmoja,je cha kushangaza ni nini?

Ni viumbe wa aina mbili tu majini na watu watahukumiwa siku ya kiyama na kuingia peponi au motoni

Viumbe wengine wote watahukumiwa,kisha baada ya hukumu kupita na kila mmoja kupata haki yake,itahukumiwa wageuke kuwa mchanga period
Hakuna cha ligi wala nini.

Sisi Wakristo tunatambua kuwa hakuna Majini Wakristo.
Na Kuna Aya nyingi sana zinazo tueleza kuwa Majini ni pepo wachafu fullstop.

Na sijui ni kwa nini baadhi ya Waislamu wanashinikiza kwa nguvu zote kuwa kuna Majini Wakristo.

Kwani Majini wakiamua wenyewe kumwabudu Mungu wao kupitia Dini ya Kiislamu kuna shida gani ?

Nasema tena Wakristo wote kupitia mafundisho ya Manabii wao wanafundishwa kuwa Majini yote ni maovu.

Kama Majini waliamua kutubu na kuwa Waislamu sisi Wakristo hatuna shida na Hilo.

Ila kauli ya baadhi ya Waislamu kuwa kuna Majini Wakristo bila kuleta ushahidi wowote wa kimaandiko tunaiona ni kauli ya kupuuzwa tu.

Narudia tena, hakuna Mkristo anaye amini kuwa kuna Majini Wakristo. Ndivyo tulivyo fundishwa na Manabii wetu.

Mambo ya Walawi (Lev) 17:7 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.

Huu ndi msimamo wa Wakristo wote.
Naomba ieleweke hivyo.

Majini ni Waislamu na Aya Zipo nyingi tu.
وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ ۖ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا

(AL - JINN - 14)
Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.

NB:
Kama Kuna kauli tofauti tunaomba ushahidi wa Kimaandiko na sio kuongea hewani tu.
 
Vionjo Vya Arsis 2
Hilo la Yesu binafsi niliwahi kumsikiya msomi wa Kipalestina, namfatilia sana huyu kwa kuwa anaongea lecture zake kwa Kingereza kizuri na anafundisha. yupo kwenye mtandao. Na hivi juzi sijuwi jana, ndiyo nimemuona Arsis akilileta kivingine. Sema kanusa tu, hatupi vitu kwa kina, sifahamu Arsis anabana bana au Corazon Espinado anatubania vitu. Tafadhali simba kamba, usome uzi kwenye link hiyo ya chini hapo ili Arsis au wewe mtujazie manyama. Tuwekee kamba wale wanene wanene kabisa.

Hilo mimi niliwahi kuandika humu JF, nikakosa watu wa kupasha moto uzi. Pitieni hapa:

https://www.jamiiforums.com/threads...ni-hata-waislam-wengi-hawayajui-haya.2227017/
Nimeiona, mimi huko sina ujuzi kabisa, mambo ya Arsis jinayaleta kama alivyonielezea. Akiongeza nyama au chumvi nitaleta.
 
Huo ni ukweli usiopingika, mimi naamni sisi ni 100% bora ingawa Arsis nimesoma anasema kuna viumbe wa dunia nyingine wapo 12 tu.

Dah hao wa kufikirika.

Corazon Espinado ongea na Arsis atujazie nyama ya hao viumbe wanaoitwa "Ramadiyin", nimepekuwa mtandao wote sijakutana nao hao. Ngoja niendelee kuwatafuta kwa kutenguwa "code" za maana ya majina. Sijapata kitu, isipokuwa kitu cha karibu ninachokipata ni Ramadhan, kuwa kwa Kiarabu asili yake ni jina la msimu wa joto kali.
Kwanza Arsis hajawahi kusifu posy ya yeyote tok tumenza huu uzi, hii yako kaisifu sana. Kasema kuniambia mimi lakini naona ni ujumbe unaotakiwa ufike hapa. Anaanambia nisome "vedic" nitakuta Rama na daya, niwasome sana hao nitapa muangaza wa Ramadiyin.

Nipo msibani Bagamoyo rafiki ya mzed wangu ambae mimi nimemzowea kuanzia mdogo namuita Ami, ametutoka leo, ndio nipo na mzee huku. Inna li Llahi wa inna ilayhi rajiun.

Wengi mnaweza kumfahamu alikua mcheza mpira maarufu kabla sijazaliwa anaitwa Abuu Marwaa, aliwahi akucheza Cosmo na Yanga, mzee anasema inawezekana huyukachukua ubingwa wa ligi ya Tanzania akiwa na Cosmo na Yanga za Kariakoo Dar. Zamani miaka ya60 na ngapi sijui 70 na ngapi sijui. Wa zama hizo mtueleze.
 
Kingine majini wote wanajua kiongozi wa dunia hii ni mwanadamu,kwahiyo wanatuogopa sana,unaambiwa hata jini mkubwa anaweza kumuogopa mtoto wa kibinadamu kama atajiamini kwakuwa nature iko hivyo

Mfano kama mimi na wewe tunavyomwogopa simba au chui,hata mtoto wa simba ukimuona unaweza kukimbia

Hawa viumbe hawana mamlaka juu ya mwanadamu,sijui tunafeli wapi
Hilo ni asilimia zote, wengi hawaelewi kuwa sisi tuna uwezomkubwa kuliko majinni.
 
Kwanza Arsis hajawahi kusifu posy ya yeyote tok tumenza huu uzi, hii yako kaisifu sana. Kasema kuniambia mimi lakini naona ni ujumbe unaotakiwa ufike hapa. Anaanambia nisome "vedic" nitakuta Rama na daya, niwasome sana hao nitapa muangaza wa Ramadiyin.

Nipo msibani Bagamoyo rafiki ya mzed wangu ambae mimi nimemzowea kuanzia mdogo namuita Ami, ametutoka leo, ndio nipo na mzee huku. Inna li Llahi wa inna ilayhi rajiun.

Wengi mnaweza kumfahamu alikua mcheza mpira maarufu kabla sijazaliwa anaitwa Abuu Marwaa, aliwahi akucheza Cosmo na Yanga, mzee anasema inawezekana huyukachukua ubingwa wa ligi ya Tanzania akiwa na Cosmo na Yanga za Kariakoo Dar. Zamani miaka ya60 na ngapi sijui 70 na ngapi sijui. Wa zama hizo mtueleze.
Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

Niimesikia kuhusu huu msiba, mimi namfahamu Abuu na family yake zamani walikuwa wakiishi mitaa ya Jangwani, nyumba moja ya/na Bi Mariam Sehel.
 
Kwa hivyo karibu na Ikulu kuna ‘worm hole’ into other time dimension and time travel is possible.

Wazungu watakupa hela mingi sana ukiwaonyesha hiyo sehemu, “Einstein Field Equation” predicted that lakini mpaka leo hawajui zipo wapi.

Not to dismiss story yako entirely ila kama vile chumvi ni nyingi sana.

Vinginevyo I certainly believe kuna mambo mengi ya dunia binadamu hatuyaelewi. Ila chumvi nyingi sana ambazo hazi-add-up.​
Inawezekana...

Kuna kila dalili na ishara yapo malango mengi tu ya 'Maingiliano' ya 'dhahiri-macho' na 'dhahiri--kiini macho' Pwani yote ya Afrika Mashariki--pia maeneo mbalimbali ambayo labda utapata kusikia ni ya 'Matambiko'...

Siku za mbele kidogo, haya tunakwenda kufahamu kiufundi na weledi; ni hapa tu katikati siku hizi za katikati; tathmini inaendelea: 'udadisi' kuhusiana na utayari wa jamii zetu, muktadha akilifu, katika 'usahihi wa dhamirii' ya 'kujiongeza'-- ili waondokane na 'kasumba' na pia 'ushamba' wa 'visomo shobo' vya sayansi ya kimadarasani...

Sasa, swali la maudhi--ikiwa wanajamii hata kuotea visomo vyao vya uchumi na fedha/utaifa na jamii; kwamba vyote vimegubikwa na 'msiba wa kiroho'; kweli wanastahili kuongozewa njia kwenye 'mambo yaliyositirika' kama habari za 'SHIHATA'--ili iweje?

Kwanza, wananchi wanahitaji kufahamu maana na kusudi la 'Mwenge wa Uhuru'... Mengine yatafuatia kwa nafasi yake...

Sasa, unaweza kusikia habari za 'malango ya asili'; mengi yapo mapangoni, ardhini ama sehemu sizizoingilika kwa mwili wa nyama; hayo yanayoweza hata kukutobozesha, uingie na kutokea, siyo tu 'ndani kwa ndani'/'uso kwa uso' mwa 'vitovu vya mwili wa Dunia yetu' bali hata kungine 'nje ya Dunia'--lakini 'malango' yanaweza kutengenezwa kokote na popote na mtu mwenye 'Maarifa/Visomo/Maarifu' na 'Ujuzi Sahihi'...

Lakini, moja--Kuutafuta 'Ufalme wa Mbingu/Mungu na Haki yake, mengine kuzidishiwa' ndiyo ufunguo wa 'Mawalii' wote, na tena kwa ajili ya kustahiki kuyafahamu yote kadiri ya utimilifu wa UTU Bora--Kuutafuta ukaribu na 'Allah'...
 
Inawezekana...

Kuna kila dalili na ishara yapo malango mengi tu ya 'Maingiliano' ya 'dhahiri-macho' na 'dhahiri--kiini macho' Pwani yote ya Afrika Mashariki--pia maeneo mbalimbali ambayo labda utapata kusikia ni ya 'Matambiko'...

Siku za mbele kidogo, haya tunakwenda kufahamu kiufundi na weledi; ni hapa tu katikati siku hizi za katikati; tathmini inaendelea: 'udadisi' kuhusiana na utayari wa jamii zetu, muktadha akilifu, katika 'usahihi wa dhamirii' ya 'kujiongeza'-- ili waondokane na 'kasumba' na pia 'ushamba' wa 'visomo shobo' vya sayansi ya kimadarasani...

Sasa, swali la maudhi--ikiwa wanajamii hata kuotea visomo vyao vya uchumi na fedha/utaifa na jamii; kwamba vyote vimegubikwa na 'msiba wa kiroho'; kweli wanastahili kuongozewa njia kwenye 'mambo yaliyositirika' kama habari za 'SHIHATA'--ili iweje?

Kwanza, wananchi wanahitaji kufahamu maana na kusudi la 'Mwenge wa Uhuru'... Mengine yatafuatia kwa nafasi yake...

Sasa, unaweza kusikia habari za 'malango ya asili'; mengi yapo mapangoni, ardhini ama sehemu sizizoingilika kwa mwili wa nyama; hayo yanayoweza hata kukutobozesha, uingie na kutokea, siyo tu 'ndani kwa ndani'/'uso kwa uso' mwa 'vitovu vya mwili wa Dunia yetu' bali hata kungine 'nje ya Dunia'--lakini 'malango' yanaweza kutengenezwa kokote na popote na mtu mwenye 'Maarifa/Visomo/Maarifu' na 'Ujuzi Sahihi'...

Lakini, moja--Kuutafuta 'Ufalme wa Mbingu/Mungu na Haki yake, mengine kuzidishiwa' ndiyo ufunguo wa 'Mawalii' wote, na tena kwa ajili ya kustahiki kuyafahamu yote kadiri ya utimilifu wa UTU Bora--Kuutafuta ukaribu na 'Allah'...
Uandishi wako kuelewa ni sawa na vitabu fulani kuna kaka yangu mmoja (ni rafiki tu kwa umri namwita kaka).

Alikuwa anapenda au anayajua haya mambo (kabla ya social media) kuhusu untold human history. For some reason known to him akawa ananipa vitabu vyake ambavyo ni rare kuhusu human history kwa nadharia za mada kama hizi nijifunze.

Mkitabu wenyewe umeandikwa kwa kizungu ila lugha ngumu balaa (sio kwamba siwezi kusoma standard English). Ndio kama wewe jamaa unavyoandika Kiswahili chako inahitaji kamusi na kufikiria sana kukuelewa.

Either way mimi sibishii spiritual world kabisa (I have my own life, experiences which don’t make sense) hilo la worm holes jamaa nilimchomekea tu. Kama kashindwa kuona hoja yake inanguvu gani academically to tie it with the question nimeona nimuwache abaki na elimu ambayo anapewa arsis na kuwapa wengine.

Iła kuna vitu unasoma unaona fix mingi sana.
 
Uandishi wako kuelewa ni sawa na vitabu fulani kuna kaka yangu mmoja (ni rafiki tu kwa umri namwita kaka).

Alikuwa anapenda au anayajua haya mambo (kabla ya social media) kuhusu untold human history. Akawa ananipa vitabu vyake ambavyo ni rare kuhusu human history kwa nadharia za mada kama hizi.

Mkitabu umeandikwa kwa kizungu ila lugha ngumu balaa kama wewe unavyoandika Kiswahili chako inahutaji kamusi kukuelewa.

Either way mimi sibishii spiritual world kabisa, hilo la worm holes jamaa nilimchomekea tu. Kama kashindwa kuona hoja yake inanguvu gani academically nimeona nimuwache abaki na elimu ambayo anapewa arsis.
NKNS

Vitabu vya Dolores Cannon labda?

Huyu mama ameandika mengi hasa kuhusu haya yote--kwa kweli; wengi tu huko Magharibi na Mashariki ya Mbali wameandika 'habari za ajabu' za mtu, watu na maisha.

Mazoezi !, mazoezi !--maarifa ni pamoja ujuzi na uwezo wa matumizi bora ya lugha na maneno; hili linakuja kwa nidhamu na udhamirifu wa fasaha na miundo ya semi/udadavuaji...

Maarifa yana 'Mbegu ya Ujuaji', siyo porojo tu na kuhorojoka. Ukifanyika uwezo ndani yako wa kuzibaini 'mbegu za ujuaji uliobora' basi unaweza kusoma mashauri yoyote na juu ya kisomo chochote--ilihali uwasilisho wake umesukika kiufundi.

Kwa hivyo yapo mengi humu, katika huu uzi, yanoyohitaji 'Kunyooshwa'--kutengenezewa koherensia ya ufikirifu; lakini hili linakuja kulingana na 'chachu' ya washiriki na uwezekano wa manufaa katika kuingiliakati mazungumzo.

In Shaa Allah, kadiri inavyofaa, kidogo kidogo 'tutayapatia sura rasmi' yote yanayohusiana na 'Ulimwengu wa Kiroho' kwa lugha yetu ya Kiswahili; kwa manufaa ya wale wote wenyebidii ya visomo na pia udhamirifu wa jitihada/ufundi wa uwasilishaji wa habari za maisha na maajabu ya maisha/uisho...

Hili siyo suala la starehe tu, hili ni suala la Utamaduni na Umahiri wa mambo... Kwenye 'kujichagulia ilivyobora', 'hakuna kazi nyepesi'...

Kila mtu anaubeba mzigo wake.

Hmmm
 
NKNS

Vitabu vya Dolores Cannon labda?

Huyu mama ameandika mengi hasa kuhusu haya yote--kwa kweli; wengi tu huko Magharibi na Mashariki ya Mbali wameandika 'habari za ajabu' za mtu, watu na maisha.

Mazoezi !, mazoezi !--maarifa ni pamoja ujuzi na uwezo wa matumizi bora ya lugha na maneno; hili linakuja kwa nidhamu na udhamirifu wa fasaha na miundo ya semi/udadavuaji...

Maarifa yana 'Mbegu ya Ujuaji', siyo porojo tu na kuhorojoka. Ukifanyika uwezo ndani yako wa kuzibaini 'mbegu za ujuaji uliobora' basi unaweza kusoma mashauri yoyote na juu ya kisomo chochote--ilihali uwasilisho wake umesukika kiufundi.

Kwa hivyo yapo mengi humu, katika huu uzi, yanoyohitaji 'Kunyooshwa'--kutengenezewa koherensia ya ufikirifu; lakini hili linakuja kulingana na 'chachu' ya washiriki na uwezekano wa manufaa katika kuingiliakati mazungumzo.

In Shaa Allah, kadiri inavyofaa, kidogo kidogo 'tutayapatia sura rasmi' yote yanayohusiana na 'Ulimwengu wa Kiroho' kwa lugha yetu ya Kiswahili; kwa manufaa ya wale wote wenyebidii ya visomo na pia udhamirifu wa jitihada/ufundi wa uwasilishaji wa habari za maisha na maajabu ya maisha/uisho...

Hili siyo suala la starehe tu, hili ni suala la Utamaduni na Umahiri wa mambo... Kwenye 'kujichagulia ilivyobora', 'hakuna kazi nyepesi'...

Kila mtu anaubeba mzigo wake.

Hmmm
Yaleyale japo nimetumia nguvu sana walau safari hii nimekuelewa kidogo.

Haya mambo yenu, ni ya kujifunza taratibu kwa sisi wakawaida (ni somo) Iła sio jepesi kwa sisi wengine kama ilivyo kwa uelewa mpana.
 
NIonavyo mimi huyu mleta hadithi, katoka kwenye hadithi yake na kaanza kujibu maswali, tungejaliwa uvumilivu tumuache aalete hadithi yake kama alivyokuwa kakusudia mwanzo.

Sasa naona kai kata kata, ananza kuandika hadithi kufuatia maswali ya watu badala kuleta mfululizo wake kama alivyokusudia mwanzo, kwa ufupi katoka kwenye reli sasa ana puyanga kwa kufuata maswali badala ya kuleta hadithi.

Kakiri yeye siyo muandishi mzuri, nimeona FAIZAFOXY kamshauri aache kupuyanga, arudi kwenye hadithi lakini hajasikia.

Tafadhali mleta mada achana na mwaswali yetu, leta hadithi kisha maswali utayajibu ukimaliza kuhadithia.
 
Yaleyale japo nimetumia nguvu sana walau safari hii nimekuelewa kidogo.

Haya mambo yenu, ni ya kujifunza taratibu kwa sisi wakawaida (ni somo) Iła sio jepesi kwa sisi wengine kama ilivyo kwa uelewa mpana.
SAHIHI,

Hata kiingereza watu wanaliwa danzu na (1) 'ugeni wa maneno' na (2) 'kukosa mazoea' ya matumizi ya lugha yenyewe husika ya kigeni.

Bado hatuna wadau wakutosha kufanya bidii ya kuandika, kwa Kiswahili, mambo mbalimbali kiufundi na ule ujuzi khasa wa misamiati na umahsusi wa matumizi yake; hili likija kuimarika ninakuhakikishia yapo yatakayoanza kuzungumzwa hapa, tuseme JF, hata kwa wanaozungumza lugha ya Kiingereza bado hayajazungumzwa...

Kamwe usiidharau lugha yoyote--ila washangae wenyelugha wanaojibeza na vile vile 'kutojiongeza'; lugha yoyote inakuzwa ama/na kuboreshwa na wanajamii wenyewe wanaohusika nayo--ubunifu, utundu, uthubutu na kukomaa; siyo kughairi ghairi ule muktadha wa jitihada za kuikuza na kuijenga lugha husika.

Inaanza na udhamirifu na kujichagulia; siyo kufuatisha mkumbo wa 'waliojisahau' ama tuwaite 'wale wenye kujichagulia fungu la kukosa'...

Hmmm
 
Kwahiyo kwa kila nabii walimsikia na lufuata ujumbe wake,hivyo walifuata mafundisho yake na kifuata hukumu zake,je walio mfuata Yesu walikuwa nani?
Hakuna manabii wala mitume wa Mungu (Yehova/Elohim) waliohubiria majini. Waka hajuna majin waliofuata mafundisho ya Kristo wala mitume wake hivyo hakuna majini yansyofungamana na ukristo. Huku we casting out the demons kwa mamlaka Ya jina kuu la Yesu. Hatupungi waka kupandisha pepo maaba hatuna ushirika nao wowote.
Ukiona mkristo anafanya hayo, tambua huo ni ushirikina wake binafsi wala hatuna doctrine za kijinga jinga hizo, our God is holly n pure, hachangamani na mapepo wala sisi tunaomuamin na kumfuata hatuna time na mapepo waka majini, si mazuri si mabaya kama myaitavyo.
 
Unataka nikujibu Arsis alisema nini kuhusu hilo? Sitaki jazba lakini, ni majibu ya Arsis.

Arsis aliwahi kusema"Yesu mwenyewe kajua siku hizi kua kuna watu wanamuita Yesu". Nikamuuliz kwanini? Akanambia Yesu hajawahi kuitwa hivyo duniani. mama yake Yesu alikua anaongea Kiaramu (Aramaic) na Kimisri. Nilipomuuliza zaidi akanambia "wewe hupendi kusoma. Hizo lugha zote mbili zinafanana sana na Kiarabu cha zamani".
Hapa nakubaliana nawewe.. probably YESU liko jina lake la Siri lenye nguvu kuliko walilongangania walokole Sasa hivi
 
Kwa hivyo karibu na Ikulu kuna ‘worm hole’ into other time dimension and time travel is possible.

Wazungu watakupa hela mingi sana ukiwaonyesha hiyo sehemu, “Einstein Field Equation” predicted that lakini mpaka leo hawajui zipo wapi.

Not to dismiss story yako entirely ila kama vile chumvi ni nyingi sana.

Vinginevyo I certainly believe kuna mambo mengi ya dunia binadamu hatuyaelewi. Ila chumvi nyingi sana ambazo hazi-add-up.
Swali zuri sana hilo. naamini wengi hawatokuelewa.

Mimi binafsi niliandika jana atuongezee nyama kuhusu hiyo dunia ya "Ramadiyin". Nimeona alichojibu, ni kama nisome, nimepitia alichoambiwa akispome nimekikuta mtandaoni, ni kitabu cha imani za Kihindu cha zamani sana, kweli nikakugta "Rama" bado napitia, nimeona kuwa huyo Rama ni kiumbe kutoka nje na walikuja na mashine yao "UFO". bado nasoma, niseme ni "interesting" - theboss.

Nahisi kama kuna "coce" fulani inafunguka kwa maana ya majina na si lazima jina lote kamili. Hii wwanatumia sana Waarabu, Wayahudi na sasa nimefahamu Wahindu pia wanayo hiyo, tena wao wanaenda mbali zaidi mpaka kutumia herufi moja moja ya kwenye jina kumaaanisha vitu vingi kwa pamoja.

Naendelea kubukuwa.

cc; Corazon Espinado
 
Back
Top Bottom