Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1 B.


Usiku nikaenda Ocean Road kama kawaida, nikamwita Arsis;

Aysis: Simba, vipi hali uako
Mimi; Sipo sawa kabisa leo.
Arsis: Nafahamu sana, hii habari ni nzito sana. Subiri nikueleze kilichopo na nini kifanyike.
Mimi: Sawa.
Srsis: Sikia simba, Ali asingekupigia simu kabisa wala asingetoa namba yako lakini sisi ndio tulifanya akupigie.
Mim; Nyinyi kivipi?
Arsis: Please subiri usiulize maswali maka nimalize kukufahamisha, usiumize kichwa, acha mimi niwe niulize maswali.
Mimi; Sawa.
Arsis: Unakumbuka ulimuona mke wa Sharifu ulipokua Shinyanga?
Mimi; Namkumbia sana.
Arsis: :lazima umkumbuke, kwa sabu yupo tofauti na watu uliozowea kuwaona. Si unafahamu kua yule ni Muindonesia?
Mimi: Nafahamu hilo, alinambia mzee hapa. Alinambia "Ali alikwenda Indosia, kwa ami yake, ndio akaozwa yule binti kule na yeye ni Sharifu vilevile.
Arsis; sawa kabisa, yule mwanamke ni mwema sana na alijaaliwa Qareen, wqengine wanaita Ruhani, lakini ni Qareen., mwema mwema sana. Wale Ali na mewe kwenye ukoo wao ni watu wa Ilmu na wa tiba, lakini Ali yeye watu wanasikia Sharifu wanakwenda anawaombea dua na anawasome Qur'an inakuwa kubul, alipokuaja mkewe, alkua hata Kiswahili hajui kabisa, kajifundisha haraka sana kaelewa. Qareen wa mkewe ni wa tiba, za ilm na dawa za Kiarabu, binadamu wengine wanadanganya za sunna, sunna ya nani, waongo tu.

Sasa wakija watu kusomewa dua, mkewe anaobeshwa na Qareen wake wana matatizo gani na watibiwe vipi anamwabia Ali, Ali akawa hata hizo dawq HAJUI apate wapi. akawa anaagoza mafduka ya dawa kutokea Dar. Zikifika yule mwanamke anatzama zingine anazikubali zingine anazikataa. Anasea hizi sawa, hizi sio swa. Ali hakuwa na wasiwasi sana kwa sababu anajua kule kwao Ami yake ni mtu wa ilm sana na anasaidia watu wengi, hakujua kua ni Qareen mwenye kufanya yote yale sio mkewe peke yake. Ikaenda mpaka akazowea. Ba watu wkawa wanapata habari wanafanikiwa wakienda kwa Ali. Nina uhakika hilo ulikua hujui.

Ulipoenda wewe yule Qareen wake alimuona yule mwanamke kijinni ulienda nae, tulimwabia awe na wewe safari yoite. Yule mwanamke akaongea na huyu Jini wetu. hawa majini huwa wanaongea wenyewe kwa wenyenyewe, hio ni kawaida kabisa.
MImi: Nafahamu hilo lakini la yule mke wa Ali sikujua.
Arsis; nafahamu hukujua, ilikua haina sababu ya wewe kujua, lakini sasa nimeona nikueleze, aana alipokuja huyu mama, yule mwanamke ya Ali akamuhurumia sana, akaona yeye kua mtoto wake yupo lakini hajui wapi kwa sababu amefichwi na wachawi wakubwa, siuo rahisi mtu au jinni au Qareen ambae sio kazi yake akajua. Basi yule mwanamke akakumbuka huyu Jini wetu, akawa anamwita, huyu akatuuliza sisi tukampa rukhsa aende akasikilize anaitiwa nini ndio yule mwanamke akamuonesha yule mama akamwabia matatizo yake ndio wakanifahamisha kwa kua wao haiwezi ile kazi peke yao. Ndio tukaamua wamwambie yule mke wa Ali amkubushe mumewe wakawambie ili tuifanye kwa idhini ya mumewe. Umeelewa?
Mimi; Nimeelewa.
Arsis: Sfi sana, usiulize kitu sasa hivi najua una maswali mengi sana. Mimi nikaanza hii kazi kabla yule mwanamke hajaja, tukaweka ulinzi iliwasoiweze kuendelea kumdhuru, aKawa ameanza kupwa dawa na Jini Bakora, zakuua uchawi kwenye mwili wake. Jini Bakora ni hodari sana, anampa dawa bila wachawi kujua na majini waowachafu.

Tulipona anaweza kukolewa na anaweza kupona ndio tukaamua sasa kazi ifanyike. Simba, kazi itafanyika hivi, lazima yule anaefanya hii mambo apatikane, sisi tumeshamjua, lakini amefanya mengi sana kwenye ukoo wao, tunataka wajue na wapo wengine kwenye ukoo kama yeye. Tunataka tusafishe ukoo mzima wasisumbuliwe tena na hawa watu wabaya, mashetani wakbwa sana hawa.

Kwa hio ni lazima ukoo mzima ule uende Tanga kwa babu yako, sio shamba, pale kwake mjini.

Kwa hio wewe leo ukirudi usowaambie kitu, ongea na babu yako, na labada tayari anayo habari lakini wajib wako umfahamishe kwa mdomo wako, ukishaongea na babu yako kesho asbuhi utamwambia Ali amwambie yule mama lazima wote waje, ndugu wote, wakubwa,wadogo, kina mama, kina bibi, kina shangazi waliopo Mwanza< Shinyanga, Tabira na kokote pale lazima waje. Umeelewa?
Mimi: Imekua vizuri Mzee Ali amwabie. Na wewe wakiku[pigia na Ali akikuuliza mwabi hujui chochote hii tulioongea mwambie tu lazima waje Tanga, yeye afanye hima awaambie, waje na basi, wanazo basi kubwa za safari kwenye ukoo wao. Waje hata basi tatu au nne, mbona nyinyi binadam kwenye harusi na kwenye kuzika watu wenye pesa wote wanakenda kwa gharama kubwa popote. Hawa gharama hio kuja, kula kulala ni juu yao, usiwe na wasi wasi, wale wapo vizuri. Mengine tutapanga na babu yako na wewe. Mimi kazi hii nitakua karibu sana lakini mawasiano itakua wewe nayule Jini mwanamke. Sawa?
Mimi: Sawa/.

Arsis: Una swali lolote?
Mimi: Sasa ...
Arsis usiulize hilo swali, wewe waambie tu ndio kwenye ufumbuzi.Mengine tutaongea kesho. Kwaheri.

Mimi: haya kwaheri.

Arsis akaenda zake na mimi nikaondoka, nikarudi nyumbani, nikampigia babu saa hiyo hiyoi, akanisiliza, akanambia hakuna shida nijulishe lini wanakuja na wakiondoka huko waseme watu wangapi ili tufanyue mipango ya Tanga. Wewe uje siku moja au mboili kabla yao.
Mimi: Babu ndio hilo nilitaka kusema, mimi, kuna sababu ipi ya mimi kuja?
Babu: Sbabu ipo kubwa sana, ukija utaiona, utaelewa.
MIMI; Babu kai za watu huku.
Babu; Atazifanya baba'ko, mimi nitangea nae ukiwa tayari, hukai huku, wewe mwabie wiki moja tu, sasa usinambie mkeo sijui mwanao. Hao wazoeshe kuwa peke yao. Kwaheri babu saa nyingi.

Ka heri babu, keshonitakupigia.
abu; Okay.

Nikajua babu hataki kuongea zaidi ujumbe kisha nipa.


Itaendelea.
Kwenye hii story kuna mambo mengi ya kujifunza hasa kuhusu majini na wachawi.
Wachawi wanaweza ku summon majini na wakawatuma lakini pia waganga wanaweza ku summon majini na wakawatuma utofauti itakuja tu unawatuma kwa kazi gani?
Ila haya mambo yanataka yanataka uwe na msingi wa imani vinginevyo utaangukia kwenye shirki, bwana Arsis story yako ina mambo mengi ya ulimwengu usionekana endelea kushusha vitu.
Muulize Arsis ni mambo gani mwanadamu ukiyafanya unakuwa umejiingiza kwenye rada za wachawi yaani wachawi wataanza kukufuatilia? Ili tujifunze hapa jinsi ya kuwakwepa hawa wanga maana wamezidi
 
Bwana Arsis huu uzi wako unafuatiliwa sana kila nikikatiza more than 15 people are here naamini kuna watu wengi wanafuatilia na wana elimu kubwa tu juu ya mambo ya kiroho ila hawa comment.
Comment ziongezeke jamani tujifunze simmesikia Arsis anapenda challenge ila nimegundua kuna vitu ata Arsis anaweza kujifunza kutoka kwetu na anawapenda binadamu
 
Kwenye hii story kuna mambo mengi ya kujifunza hasa kuhusu majini na wachawi.
Wachawi wanaweza ku summon majini na wakawatuma lakini pia waganga wanaweza ku summon majini na wakawatuma utofauti itakuja tu unawatuma kwa kazi gani?
Ila haya mambo yanataka yanataka uwe na msingi wa imani vinginevyo utaangukia kwenye shirki, bwana Arsis story yako ina mambo mengi ya ulimwengu usionekana endelea kushusha vitu.
Muulize Arsis ni mambo gani mwanadamu ukiyafanya unakuwa umejiingiza kwenye rada za wachawi yaani wachawi wataanza kukufuatilia? Ili tujifunze hapa jinsi ya kuwakwepa hawa wanga maana wamezidi
Mchawi hana sababu hata usifanye lolote wakiamua wakuharibue maisha wataharibu unadhani walo haribiwa maisha na wachawi waliingia rada zao??

Hakuna njia ya kukwepa mwanga mchawi Ila ucha Mungu jitakase na madhambi jenga urafiki na Mungu hakuna mchawi jinn atakusogelea.
 
Corazon Espinado.

Siyo utani. Kisa chako ni kizuri sana. Siyo kwa huo usimba ushuzi wako.

Kuna mengi yanaingia akilini. Ushauri wangu kwako, usiwe na haraka ya kupost ulichoandika. Andika post yako, tulizana, isome mara mbili tatu, rekebisha makosa ya kiuandishi kadri ya uwezo wako, kisha ndiyo post.

La pili ni ombi, naona kuna masuala ya dini yamejitokeza, natamani uniruhusu niyajibu ninavyoelewa mimi.

Mambo yako na majinni wako sikuingilii, nikiwa na swali huko ntauliza.

Ombi langu la mwisho kwako, tafadhali sana wachana na u foxy wangu na usimba wako. Tumekutana kwenye mtandao yaishie kwenye mtandao na mada zilizopo. Mjmi sikujuwi kabisa. Nikisema nakujuwa ni kwa kukutania tu. Ispokuwa, umemtaja mtu wa Shinyanga ambae nafahamiana nae toka utotoni, wamekuwa pamoja na mume wangu kwa ukaribu kabisa. Nawahamu ukoo wake wote. Ulichoelezea kijuujuu kuhusu huyo mtu wa Shinyanga ni ukweli mtupu.

Tafadhali nielewe, maana naona uzi umeshaingia watu wa jazba, wewe "remain cool" utupe kisa au visa vyako. Narudia, nimekipenda kisa chako, wachana na vile visa vyako vya usimba ushuzi.
Kama umekimbia kujihami mno Bimkubwa.
 
Safi kwa kuwa muwazi.
Kwanini uliacha uislamu mkuu?
Kama swali hili litakukwaza unaweza ku ignore tu be free
Ilitokea tu nilifanya kazi misheni ya Wakatoriki kule Peramiho.
Jinsi walivvokuwa wana nihudumia vizuri kimahitaji ya maisha na nikaanza kushirikiana nao kama kwenda kanisani kusali nao, kusoma Biblia na kuitafakari, nikayapenda mazingira yote kwa ujumla na kuamua kuwa Mkristo.
 
Nilikua sijaiona hii ruksa.

Arsis anasema wewe ni Muislam, ila ni asi tu.

cc; FaizaFoxy
Jamaa kashaumbuliwa!🤣 Ishu ni kwamba viumbe vingi visivyoonekana(malaika, majini e.t.c) ni vina uwezo au kiwango fulani za kujua siri za ulimwengu wa roho ambapo kule kila mtu yupo uchi. Ndo maana binadamu hata tufanye nini tayari mihuli ilishagongwa kwenye ulimwengu wa roho.
Ndo maana magonjwa, ukiua, ukizini ukijifanya hutaki mambo yako yajulikane watu wakienda kwenye watu waliopewa access ya ulimwengu wa roho kule hakujifichi kitu. Kule Unasoma maisha ya mtu hata kabla ya kuzaliwa, e.t.c

Nb; Ni rahisi kutabiriwa kuwa huyu mtu atakuja kuwa na mafanikio makubwa lakini atapitia changamoto kubwa. Laiti tungekuwa tunajua siri za ulimwengu wa roho tusingekua tunacheza na maisha ambapo shetani nae anaingia hapo kuvuruga maisha ya watu..kuna watu Leo hii walitakiwa kuwa watu wa nyazifa za juu, matajiri, e.t.c wamefariki kwa kucheza na maisha mfano kwa magonjwa ndoto hazijatimia. Ulimwengu wa roho unaweza ukatuelekeza ni namna gani tuishi na kuja kufanikiwa.Sema ndo hivo tumefungwa macho hatuoni yambeleni.

Aiseeh; ukijua siri za ulimwengu wa roho utamiliki na kutawala..yaani umeshatoboa...
Ndo maana hata leo hii mtu mwenye access ya ulimwengu wa roho ana uwezo wa kujua hata kubaini manabii feki, utajiri wa mtu kama ni halali au sio, kila kitu unachokitaka.
 
Ilitokea tu nilifanya kazi misheni ya Wakatoriki kule Peramiho.
Jinsi walivvokuwa wana nihudumia vizuri kimahitaji ya maisha na nikaanza kushirikiana nao kama kwenda kanisani kusali nao, kusoma Biblia na kuitafakari, nikayapenda mazingira yote kwa ujumla na kuamua kuwa Mkristo.
Nimependa jinsi ulivyo muwazi
Ukipata muda jaribu kuisoma na kuitafakari quran pia. Naamini utajifunza kitu ila huyu Arsis jini anabalaa.
 
Back
Top Bottom