Swali langu
Arsis
Kwanini nashindwa kupata msaada kwa watu kwenye suala langu la jamaa kutumia vyeti vyangu na anapata mshahara mzuri,posho, na marupurupu mengine?
Nimejaribu kufuatilia mpaka baraza la mitihani (NECTA) Kujua jina langu au vyeti vyangu vinatumika ofisi gani au idara gani iii nipate kuchukua hatua za kisheria?
Ukiwa kama unayeona mpaka mambo yasiyoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu au kwa sisi watu ambao hatuna Mamlaka yoyote kwenye hii nchi. Kinachonisumbua ni kupata upinzani kila mahali, hata watu ambao wana nafasi za kunisaidia lakini bado sifanikishi? Nilienda mpaka NECTA kuhakiki lakini nilikuta upinzani na yule niliyemkuta sehemu ya ukaguzi wa vyeti ikaonesha alijua naenda kufanya nini pale na ananijua. Ninapambana kwa sababu ni haki yangu Chuo ada niliilipa kwa jasho langu mwenyewe hata kuijenga na kuitengeneza CV yangu ni jitihada zangu. Nimeomba msaada kwa ndugu zangu ambao wana nafasi ya kutoa amri mara moja tu lakini nao wanapuuzia. Halafu mtu ambaye hakusoma wala hakupata uzoefu wa kutengeneza wasifu anakula kupitia jina langu. Nikifanya interview kwenye ofisi zingine nafaulu vizuri usaili lakini kuitwa kuanza kazi hakuna. Mpaka nimeamua kufanya mambo yangu binafsi tu na Alhamdulillah nayamudu lakini kwanini nadhurumiwa haki yangu? Na kwanini sipati ushirikiano kutoka kwa Ndugu, marafiki au watu niliosoma nao ? NECTA ni pagumu na UTUMISHI nako ni vikwazo na nimejiapiza sikubali haki yangu ipotee hivi hivi. Ingawa kuna mazingira fulani ya kutishia usalama wangu nayaona au kuhisi hatari ya kufuatiliwa na watu wasiojulikana. Ushauri wako na mwongozo wako nauomba.