Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Sawa
 
Inatokea post namba 43.


Usiku huo ulikua hauna matukio yoyote, nililala usingizi mnono kabisa, isipokua niliamka alfajiri sana, kutoka kwenye ndoto iliokua ndefu kidogo.

Wakati najitayarisdha kuamka sawa sawa, nikasikia kwa nje sauti ya babu "hodi, hodi, hodi bwana mkubwa bado umelala? Amka tusali bwana. Fanya haraka bibi yako kanipa kahawa na visheti nikuletee".

Nikaamka nikiwa fresh kabisa, usingizi ulikua umenitosha kabisa na zaidi. Kutoka nje nikamsalimia babu nikaenda kwenye mto nikatawadha nikarudi, njiani nikakutana na mwanafunzi wa babu na yeye kishaamshwa na babu.

Babu akanambia kunywa kahawa wakati tunamsubiri mwenzako arudi tusali. Akanitilia kikombe cha kahawa, akanambia kuna visheti pia, nikamwambia visheti baadae babu, tukisha sali. Mwanafunzi aliporudi akakimu sala, tukasali pamoja.

Tulipomaliza kusali, tukatia kikombe cha kahawa tukaanza kunywa na visheti. Kimya kimya, baada ya kama dakika kumi, mwanafunzi wa babu akaaga, akasema atarudi baada ya muda si mrefu.

Alipoondoka tu, babu akaniuliza, vipi umelalaje pangoni? Nikamwambia nimelala hata sijijui kabisa. Babu akacheka. Nikaendelea, isipokua babu nimeota ndoto moja siielewi elewi, sasa hivi ndio inanijia kichwani. Babu akasema, kama unaweza nielezee ndoto yako. Nikaanza kumuelezea.

Nimeota kuna mtu kaja, lakini sura yake siikumbuki, anasema yeye kaja kwa ajili yangu. Yeye anafanya kazi na wewe babu kwa miaka mingi sana, na mimi inabidi nianze kuijua hiyo kazi kupitia kwako na yeye atakua ananisaidia katika hio kazi. Hapo babu sijamuelewa kazi ipi, kabla sijamuuliza ikawa nimeamka.

Babu akacheka, akasema "si nilikwambia wewe ndio mrithi wangu?". Nikamwambia, babu mimi nirithishe mali zako, kazi zako mimi siziwezi. Babu akacheka, akasema mali nikiondoka kabla ya wanangu watarithi wanangu, wacha tamaa. Nikacheka. Babu akaendelea, akanambia kazi zangu ni nyepesi sana Bwana Mkubwa, wewe unachotakiwa kufanya, akija mtu ana shida yake yoyote usithubutu kumwambia hapana au hujui. Usichokijua chochote niulize mimi. Kuanzia ukiondoka hapa wenye matatizo wataanza kukufata, usiwatoe njiani hata siku moja. Wewe wasikilize, nipigie simu, na yule aliekuja ni ruhani wangu, ana akili sana na anajua mambo mengi sana. Saa zingine atakutatulia matatizo ya watu bila wewe kunambia mimi. Lakini yatakujia mambo madogo madogo tu, yale makubwa mpaka ufikie miaka 35 mpaka 45 babu, usiogope. Mpaka wakati huo utakua umeshazowea.

Babu akaendelea, kama umemsikia na umekumbuka ina maana ushafunguka wewe. Huna haja ya kukaa hapa muda mrefu, tutatimiza ada ya siku chache kabisa za kukaa, nazo ni siku tatu. Lakini siku zijazo mwenyewe utataka uje pangoni hapa, utakua na mambo mengi ya kufanya. Leo usijitie dawa yoyote, kakoge maji ya chumvi halafu kakoge maji ya mtoni, ukimaliza njoo tumalizie kahawa.

Nikaenda nikaogelea baharini, nikakuta kuna kama watu watano wapo baharini wanaogelea kwa mbali kidogo na mimi, lakini nikaona wao hawajavua nguo, wapo maji yanawafika tumboni. Sikuwatazama sana nikatoka baharini nikaenda mtoni, nikakoga maji ya mto. Kamba walikua wamejaa tena wameshakua wakubwa wengine, nikatoka.

Nikamwambia babu, kamba naona wamekua wakubwa tayari, akanamabia, hao wa kuanzia kesho babu, kesho kwenye dimbwi lile kubwa hakuna pakukanyaga. Ndio msimu umeanza, kesho ndio watakua kamba wazuri. Tena mbele huko kuna wale wakubwa kabisa, nao kesho wataanza kuvunwa kwa wingi. Babu akaniuliza hujakutana na watu wanavuna kamba huko? Nikamwambia sijakutana na mtu babu isipokua nimeona watu wanaogelea baharini lakini kama wamesimama tu maji yameishia tumboni. Babu akacheka, akanambia wewe macho yashagfunguka hayo. Hao hata mimi niliwaona nilipokua nakuletea kahawa. Babu sasa utayoyaona usiogope, utaona mambo na viumbe vingi ambavyo kwa macho ya kawaida huwezi kuviona. Wale uliowana sio watu, wale ni viumbe vingine kabisa wamekuja kwa umbo la binadam tu.

Nikacheka, nikamwambia babu, mambo yenu nyinyi wazee, ya kiajabu ajabu tu. Babu akanmbaia yashakua yako sasa, usiogope tu. Lakini usiwe na wasi wasi bwana mkubwa, wewe una kinga zote kuanzia utotoni, hii tunakufanyia kama ada tu, wewe ulikua huna sababu ya kuja kama sio ada kukuleta.

Babu akaag, akaondoka zake, ile anaondoka tu akaja yule mwanafunzi wake, kumbe hajaenda mbali alikua anangoja babu aondoke tutu arudi. Kukaa kidogo akaja na yle mwingine na kapu lina chupa ya chai, akasema leo bibi yako kaanza kukupikia kuanzia usiku, kuna mikate ya sinia humu na rosti la kamba. Nikamwambia, lete, maana najisikia njaa, kweli, tukaanza kula weote pale. Bibi yangu alikua anasifika kwa kupika. Wale vijana wakasema wewe usiondoke mapema huku tufaidi vyakula vya bibi yako. Huwa anavifaidi babu yako tu ukiwa haupo, sisi hatuvioni. Nikacheka.


Itaendelea.
Simba.
 
Wamekupa mkoba?
 
Inatokea post namba 64.

Tukala na wnafunzi wa babu, baada yta kumaliza kula mmoja akasema vipi, mshikaji, sisi tunaelekea kijijini kwenye vishughuli vyetu, sisi hatuna mwiko wa kuondoka hapa. Nikawaambia poa. Wakaondoka na vyombo vingine, wakaniwachia chupa ya chai na kahawa na mikate ya sinia.

Nikakaa kaa kidogo pale uvivu ukaanza kunijia, nikaamka nikakimbia kimbia kidogo, leo nilikua sina mwiko wa dawa, nikaenda kujitupa baharini nikaanza kuogelea kwa kasi, mpaka kama dakika kumi hivi nikajisikia kuchoka nikarudi ufukweni, Ile narudi kwa mbali nikaona mtu yuko pale kwenye lango la pango kwa nje, kasimama na bakora moja nzuri. Kufika karibu nikatoa salam, akitikia, akanambia mimi mgeni wako bwana mkubwa. Nikashangaa, hakuna anaenitta bwana mkubwa isipokua babu yangu tu. Nikamwambia karibu, kwema?

Akanambia, kwema sana, nikamwambia subiri nilete kahawa tunywe, hakunijibu kitu, nikaingia kwa ndani ya pango nikatoka na chupa ya kahawa na vikombe viwili. Nikavitia kahawa, akanambia, samahani, mimi sinywi kahawa hiyo. Nikamwambia ngoja nikuletee chai, akanambia hapana, usilete, kaa kunywa nikueleze kilichonileta. Nikakaa nikaanza kunywa kahawa yangu, nikahisi anitazama mimi halafu anaishika fimbo yake anaitazama.

Akaniuliza "umeupata mzigo wako pale unapolala?", nikamwambia ninapolala wapi? Akacheka, akanambia si hapo ulipolala jana? Nikamwambia sijapata mzigo wowote, nikawa napiga dua za sura ndogo ndogo za Qur'an, kimoypomoyo, nikaanza kuhisi huyu sio mtu wa kawaida. Ikawa kama kanielewa kua nimeingiwa na hofu fulani, akanambia usiwe na hofu, mimi ni rafiki wa babu yako, nenda pale ulipolala kwenye mto wako tazama vizuri utakuta mzigo wako, njoo nao.

Nikaingia ndani kwenye mto wangu wa rundo la mchanga niliojitengenezea, hikaona kuna kama kimkebe cha bati hivi, nikakibeba, kukitazama kilikua na nakshi nzuri sana, na kilikua sio bati, nilipotoka nacho nje nikaona ni chuma kinang'aa nikawa nakishangalia, kinaonesha cha zamani kweli kweli. Yule mzee alikua anitazama tu, huku antabasamu. Kumtazama sana akasema fungua hicho kimkebe uone kina nini ndani, kukifungua nikakuta kina pete moja ina jiwe jekundu lakini limekooza sana linakwenda kwenye weusi. Akanambia "ivae hiyo kidole chochote utachopenda, nikaiva ile pete kwenye kidole cha shahada. Ikawa imenikaa sawaswa kama imepimwa.

Akanambia huo mzigo wako na huu mzigo wako, akanipa ile bakora aliokua amishoika. Akanambia hii bakora ni yangu, ukiwa nayo hii ujue na mimi sipo mbali, usiniulize kwanini. Ukitaka kujua zaidi muulize babu yako. Hiyo pete ni ya kiumbe mwingine . na yenyewe muulize babu yako mambo take, mmi nakueleza kitu kimoja tu kuhusu hio pete. Hio pete usiivue ukaiacha nje, ukiivua hakikisha unaitia kwenye huo mkebe na unauweka vizuri. Hawezi kuufungua mtu huo isipokua wewe na mwenye hio pete, ukiiweka nje ya huo mkebe kama hujaiva, inaweza kuibiwa au inaweza ikapotea usiione tena. Ikiibiwa, huyo akatakaeiiba atapata madhara makubwa sana na itakua ni kwa uzembe wako. Umeelewa? Kabla sijamjibu akanambia, mambo mengine muulize babu yako, kwa heri. Mimi njia yangu napitia humu ndani ndio inakua karibu na kwangu, akaingia pangponi na mimi nikamfata nyuma, lakini alikua anakwenda ndani zaidi pangoni ile natazama pembeni kumtazama tena sikumuona, nikarudi zangu nje ya pango. Nikakaa nakunywa kahawa huku naitazama ile pete, nikaona ina michoro pete yote na hata lile jiwe kwa ndani lilikua kama lina muhuri ambao sijauelewa maana yake. Nikaitazama fimbo, nikakuta na yenyewe ina alama fulani kabla ya pale ilipopinda kushikiwa na chini kabisa huko kama vidole vinne kutoka chini kabisa ilikua na kama alama za nyaya zilizoingizwa kwa ndani lakini zipo sawa sawa na ile fimbo. Ilikua ni nzuri sana kwa uchache. Nikawa nawaza ya kumuuliza babu kuhsu pete na fimbo.

Itaendelea.
Simba.
.
 
Hii ni tungo au stori ya kweli?
 
Stori Yako inatufundisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…