Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Inatokea post namba 4.

Siku ya kwanzq ilikua haina pirika yoyote zaidi ya kusalimiana na ndugu jamaa na marafiki, walikua wengi wengi tu. Babu alikua bize sana na wageni wake, kwa hiyo nilipata muda mrefu wa kuongea na bibi. Bibi akanambia umekuja msimu wa kamba, keshi kutwa tutaanza kuvuna kamba, mti yote safari hii imeshona kamba, hivi wengine wameshaanza kuvuna huko. Sifahamu kwanini bibi alikua anasena "kuvuna" kamba wakati wapo kwenye maji, mimi najua kuvua.

Siku ya pili alfajiri babu akanigongea chumbani kwangu, nikajua kama kawaida yake, lazima uamke alfajiri muende mkasali msikitini, kuna msikiti hapo kwenye boima lake la ndio nyumba ya kwanaza kabisa kabla hujafika kwake ni msikiti, mzuri tu wa kisasa. Basi nikatoka na babu tukaelekea msikitini, tukasali,tulipomaliza akanambia sasa "bwana mkubwa" hakuna kurudi kulala nyumbani, tunaianza kazi yako wakati jua linapanda juu, tunaenda kwenye yale mapango upande wa pili. Nilikua nayajua hayo mapango, yapo upande wa pili wa mto ule wa Kaskazini, na kuyafikia lazima upite baharini uuzunguke mto ndio ufike.

Tukaenda na babu, na kija mmoja katika wale waliokuja kunifata na baiskeli. Huyo mwenyewe anasema ni "mwanafunzi" wa babu. Tulipoingia baharini akanambia zama mwili wote, piga mbizi maji ya chumvi yakupate kila sehemu. Na mimi ninavyopenda kuogelea, ikawa ndio kanifikisha. Babu alikua anacheka tu.

Kutoka hapo tukavuka tukatokea upande wa pili wa mto, kabla ya kuingia mapangoni akanambia, sasa kakoge mtoni, nikaenda, nilikua mwenyeji wa ule mto. Nikaingia nikakoga, nikaona kweli msimu huu kamba wengi mtoni, maana pale nilipoingia ni kama bwawa kubwa, mtoi umechanua. Sio kwenye mkondo wa mto, walikua kamba wamejaa. Nilipotoka kwenda angoni, babu akanambia umeona neema ya kamba mwaka huu? Nikamwambia nimeona babu, ni wengi sana. Akanambia imekua vizuri utapata zawadi ya kuwapelekea mjini.

Basi tukaingia pangoni, babu akaanza kunipa dawa akanambia hii jipake mwili mzima, kama mafuta ya nazi hivi yamechanganywa na majani majani ya kupondwa kupondwa, akanambia usiache sehemu. Nikafanya kama alivyoniagiza. Akanambia sasa hiyo dawa haitakiwi ukoge mpaka kesho, sana sana unachukua udhu. Fanya hima usitengue udhu. Nikamuelewa.

Akaniwachia dawa za kula, akanambia babu hapa usitoke kuja nyumbani leo, leo utalala hapaahapa, mimi ntakuja baadae, wacha nikashughulikie wageni. Wrewre na mwenzako huyo leo zungukeni upande huu huu. Mtaketewa chai na chakula hukuhuku. Msiende mbali na mapango wala msiende kuogelea. leo mpo kwenye himayta ya viumbe ambavyo hamvioni.


Itaendelea.
Sawa
 
Inatokea post namba 43.


Usiku huo ulikua hauna matukio yoyote, nililala usingizi mnono kabisa, isipokua niliamka alfajiri sana, kutoka kwenye ndoto iliokua ndefu kidogo.

Wakati najitayarisdha kuamka sawa sawa, nikasikia kwa nje sauti ya babu "hodi, hodi, hodi bwana mkubwa bado umelala? Amka tusali bwana. Fanya haraka bibi yako kanipa kahawa na visheti nikuletee".

Nikaamka nikiwa fresh kabisa, usingizi ulikua umenitosha kabisa na zaidi. Kutoka nje nikamsalimia babu nikaenda kwenye mto nikatawadha nikarudi, njiani nikakutana na mwanafunzi wa babu na yeye kishaamshwa na babu.

Babu akanambia kunywa kahawa wakati tunamsubiri mwenzako arudi tusali. Akanitilia kikombe cha kahawa, akanambia kuna visheti pia, nikamwambia visheti baadae babu, tukisha sali. Mwanafunzi aliporudi akakimu sala, tukasali pamoja.

Tulipomaliza kusali, tukatia kikombe cha kahawa tukaanza kunywa na visheti. Kimya kimya, baada ya kama dakika kumi, mwanafunzi wa babu akaaga, akasema atarudi baada ya muda si mrefu.

Alipoondoka tu, babu akaniuliza, vipi umelalaje pangoni? Nikamwambia nimelala hata sijijui kabisa. Babu akacheka. Nikaendelea, isipokua babu nimeota ndoto moja siielewi elewi, sasa hivi ndio inanijia kichwani. Babu akasema, kama unaweza nielezee ndoto yako. Nikaanza kumuelezea.

Nimeota kuna mtu kaja, lakini sura yake siikumbuki, anasema yeye kaja kwa ajili yangu. Yeye anafanya kazi na wewe babu kwa miaka mingi sana, na mimi inabidi nianze kuijua hiyo kazi kupitia kwako na yeye atakua ananisaidia katika hio kazi. Hapo babu sijamuelewa kazi ipi, kabla sijamuuliza ikawa nimeamka.

Babu akacheka, akasema "si nilikwambia wewe ndio mrithi wangu?". Nikamwambia, babu mimi nirithishe mali zako, kazi zako mimi siziwezi. Babu akacheka, akasema mali nikiondoka kabla ya wanangu watarithi wanangu, wacha tamaa. Nikacheka. Babu akaendelea, akanambia kazi zangu ni nyepesi sana Bwana Mkubwa, wewe unachotakiwa kufanya, akija mtu ana shida yake yoyote usithubutu kumwambia hapana au hujui. Usichokijua chochote niulize mimi. Kuanzia ukiondoka hapa wenye matatizo wataanza kukufata, usiwatoe njiani hata siku moja. Wewe wasikilize, nipigie simu, na yule aliekuja ni ruhani wangu, ana akili sana na anajua mambo mengi sana. Saa zingine atakutatulia matatizo ya watu bila wewe kunambia mimi. Lakini yatakujia mambo madogo madogo tu, yale makubwa mpaka ufikie miaka 35 mpaka 45 babu, usiogope. Mpaka wakati huo utakua umeshazowea.

Babu akaendelea, kama umemsikia na umekumbuka ina maana ushafunguka wewe. Huna haja ya kukaa hapa muda mrefu, tutatimiza ada ya siku chache kabisa za kukaa, nazo ni siku tatu. Lakini siku zijazo mwenyewe utataka uje pangoni hapa, utakua na mambo mengi ya kufanya. Leo usijitie dawa yoyote, kakoge maji ya chumvi halafu kakoge maji ya mtoni, ukimaliza njoo tumalizie kahawa.

Nikaenda nikaogelea baharini, nikakuta kuna kama watu watano wapo baharini wanaogelea kwa mbali kidogo na mimi, lakini nikaona wao hawajavua nguo, wapo maji yanawafika tumboni. Sikuwatazama sana nikatoka baharini nikaenda mtoni, nikakoga maji ya mto. Kamba walikua wamejaa tena wameshakua wakubwa wengine, nikatoka.

Nikamwambia babu, kamba naona wamekua wakubwa tayari, akanamabia, hao wa kuanzia kesho babu, kesho kwenye dimbwi lile kubwa hakuna pakukanyaga. Ndio msimu umeanza, kesho ndio watakua kamba wazuri. Tena mbele huko kuna wale wakubwa kabisa, nao kesho wataanza kuvunwa kwa wingi. Babu akaniuliza hujakutana na watu wanavuna kamba huko? Nikamwambia sijakutana na mtu babu isipokua nimeona watu wanaogelea baharini lakini kama wamesimama tu maji yameishia tumboni. Babu akacheka, akanambia wewe macho yashagfunguka hayo. Hao hata mimi niliwaona nilipokua nakuletea kahawa. Babu sasa utayoyaona usiogope, utaona mambo na viumbe vingi ambavyo kwa macho ya kawaida huwezi kuviona. Wale uliowana sio watu, wale ni viumbe vingine kabisa wamekuja kwa umbo la binadam tu.

Nikacheka, nikamwambia babu, mambo yenu nyinyi wazee, ya kiajabu ajabu tu. Babu akanmbaia yashakua yako sasa, usiogope tu. Lakini usiwe na wasi wasi bwana mkubwa, wewe una kinga zote kuanzia utotoni, hii tunakufanyia kama ada tu, wewe ulikua huna sababu ya kuja kama sio ada kukuleta.

Babu akaag, akaondoka zake, ile anaondoka tu akaja yule mwanafunzi wake, kumbe hajaenda mbali alikua anangoja babu aondoke tutu arudi. Kukaa kidogo akaja na yle mwingine na kapu lina chupa ya chai, akasema leo bibi yako kaanza kukupikia kuanzia usiku, kuna mikate ya sinia humu na rosti la kamba. Nikamwambia, lete, maana najisikia njaa, kweli, tukaanza kula weote pale. Bibi yangu alikua anasifika kwa kupika. Wale vijana wakasema wewe usiondoke mapema huku tufaidi vyakula vya bibi yako. Huwa anavifaidi babu yako tu ukiwa haupo, sisi hatuvioni. Nikacheka.


Itaendelea.
Simba.
 
Inatokea post namba 43.


Usiku huo ulikua hauna matukio yoyote, nililala usingizi mnono kabisa, isipokua niliamka alfajiri sana, kutoka kwenye ndoto iliokua ndefu kidogo.

Wakati najitayarisdha kuamka sawa sawa, nikasikia kwa nje sauto ya babu "hodi, hodi", hisi bwana mkubwa bado umelala? Amka tusali bwana. Fanya haraka abibi yako kanipa kahawa na visheti nikuletee".

Nikaamka nikiwa fresha kabisa, usingizi ulikua umenitosha kabisa na zaidi. Kutpoka nkje nikamsalimia badu nikaenda kwenye mto nikatawadha nikarudi, njiani nikakutana na mwanafunzi wa babu na yeye kishaamshwa na babu.

Babu akanambia kunywa kahawa wakati tunamsubiri mwenzako arudi tusali. Akanitilia kikombe cha kahawa, aknambia kuna visheti pia, nikamwambia visheti baadae babu, tukisha sali. Mwanafunzi aliporudi akakimu sala, tukasali pamoja.

Tukipomaliza kusali, tukatia kikombe cha kahawa tukaanza kunywa na visheti. Kimya kimya, baada ya kama dakika kumi, mwanafunzi wa babu akaaga, akasema atarudi baada ya muda si mrefu.

Alipoondoka tu, babu akniuliza vipi umelalaje pagoni? Nikamwambia nimelala hata sijui kabisa. Babu akacheka. Nikaendelea isipokua babu nimeota ndoto moja siielewi elewi, sasa hivi ndio inanijia kichwani. Babu akasema aksema, kama unawza nielezee ndoyto yako. Nikaanza kumuelezea.

Nimeota kuna mtu kaja, lakini sura yake siikumbuki, anasema yeye kaja kwa ajili yangu. Yeye anafanya kazi na wewe babu kwa miaka mingi sana, na mimi nabidi nianze kuijua hiyo kazi kupitia kwako na yeye atakua ananisaidia katika hio kazi. Hapo babu sijamuelewa kazi ipi, kabla sijamuuliza ikawa nimeamka.

Babu akacheka, akasema "si nilikwambia wewe ndio mrithi wangu?". Nikamwambia babu mimi babu nirithishe maki zako, kazi zako mimi siziwezi. Babu akacheka, akasema mali nikiondoka kabla ya wanangu watarithi wanangu, wacha tamaa. Nikacheka. Babu akaendelea, akanambia kazi zangu ni nyepesi sana Bwana Mkubwa, wewe unachotakiwa kufanya, akija mtu anashida yake yoyote usithubutu kumwabia hapana au hujui. Usichokijua chochote niulize mimi. Kuanzia ukiondoka hapa wenye matatizo wataanza kukufata, usiwatie njiani hata siku moja. Wewe wasikilize, nipigie mimi, na yule aliekuja ni ruhani wangu, ana akili sana na anajua mambo mengi sana. Saa zungine atakutatulia matatizo ya watu bila wewe kunambia mimi. Lakini yatakujia mambo madogo madogo tu, yale makubwa mpaka ufikie miaka 345 babu, usiogope. Mpaka wakati huo utakua umeshazowea.

Babu akaendelea, kama umemsikia, umekumbuka ina maana ushafunguka wewe. Huna haja ya kukaa hapa muda mrefu, tutatimiza ada ya siku chache kabisa za kukaa, nazo ni siku tatu. Lakini siku zijazo mwenyewe utataka uje pangoni hapa, utakua na mamboi mengi ya kufanya. Leo usijitie dawa yoyote, kakoge maji ya chumvi halafu kakoge maji ya mtoni, ukimaliza njoo tumalizie kahawa.

Nikaenda nikaogelea baharini, nikakuta kuna kama watu watano wapo baharini wanaogelea kwa mbali kidogo na mimi lakini nikaona wao hawajavua nguo, wapo maji yanawafika tumboni. Sikuwatazama sana nikatoka baharini nikaenda mtoni, nikakkoga maji ya mto. Kamba walikua wamehaa tena wameshakua wakubwa wengine, nikatika.

Nikamwambia babu, ikamba naona wamekua wakubwa, tayari, aknamabia, hao wa kuanzia kesho babu, kesho kwenye dimbwi lile kubwa hakuna pakukanyaga. Ndio msimu umeanza, kesho ndio watakua kamba wazuri. Tena mbele huko kuna wale wakubwa kabisa, nao kesho wataanza kuvunwa kwa wingi. Babu akniuliza hujakutana na watu wanavuna kamba hiuko? Nikamwambia sijakutana na mtu babu isipokua nimeona watu wanaogelea baharini lakini kama wamesimama tu maji yameishia tumboni. Babu akacheka, akanambia wewe macho yashagfunguka hayo. Hao hata mimi niliwaona nilipokua nakuletea kahawa. Babu sasa utayoyaona usiogope, utaona mambo na viumbe vingi ambavyo kwa macho ya kawaida huwezi kuviona. Wale uliowana sio watu, wale ni viumbe vingine kabisa wamekuja kwa umbo la binadam tu.

Nikacheka, nikamwabia babu, mambo yenu nyinyi wazee, ya kiajbu ajabu tu. Babu akanmbaia yashakua yakjo sasa, usiogope tu. Lakini usiwe na wasi wasi bwana mkubwa, wewe una kinga zote kuanzia utotoni, hii tunkufanyia kama ada tru, wewe ulikua huna sababu ya kuja kama sio ada kukuleta.

Babu akaag, akaondoka zake, ile anaonfdoka tu akaja yule mwanafunzi wake, kumbe hajaenda mbali alikua anangoja babu aondoke tutu arudi Kukaa kidogo akja na yle mwingine na kapu lina chupa ya chai, akasema leo bibi yako kaanza kukupikia kuanzia usiku, kuna mikate ya sinia humu na rosti la kamba. Nikamwabia, leyte, maana najisikia njaa, kweli, tukaanza kula weoite pale. Bibi yangu alikua anasifika kwa kupika. Wale vijana wakaema wewe usiondoke mapema huku tufaidi vyakula vyua bibi yako. Huwa anavifaidi babu yako tu ukiwa haupo, sisi hatuvioni. Nikacheka.


Itaendelea.
Wamekupa mkoba?
 
Inatokea post namba 64.

Tukala na wnafunzi wa babu, baada yta kumaliza kula mmoja akasema vipi, mshikaji, sisi tunaelekea kijijini kwenye vishughuli vyetu, sisi hatuna mwiko wa kuondoka hapa. Nikawaambia poa. Wakaondoka na vyombo vingine, wakaniwachia chupa ya chai na kahawa na mikate ya sinia.

Nikakaa kaa kidogo pale uvivu ukaanza kunijia, nikaamka nikakimbia kimbia kidogo, leo nilikua sina mwiko wa dawa, nikaenda kujitupa baharini nikaanza kuogelea kwa kasi, mpaka kama dakika kumi hivi nikajisikia kuchoka nikarudi ufukweni, Ile narudi kwa mbali nikaona mtu yuko pale kwenye lango la pango kwa nje, kasimama na bakora moja nzuri. Kufika karibu nikatoa salam, akitikia, akanambia mimi mgeni wako bwana mkubwa. Nikashangaa, hakuna anaenitta bwana mkubwa isipokua babu yangu tu. Nikamwambia karibu, kwema?

Akanambia, kwema sana, nikamwambia subiri nilete kahawa tunywe, hakunijibu kitu, nikaingia kwa ndani ya pango nikatoka na chupa ya kahawa na vikombe viwili. Nikavitia kahawa, akanambia, samahani, mimi sinywi kahawa hiyo. Nikamwambia ngoja nikuletee chai, akanambia hapana, usilete, kaa kunywa nikueleze kilichonileta. Nikakaa nikaanza kunywa kahawa yangu, nikahisi anitazama mimi halafu anaishika fimbo yake anaitazama.

Akaniuliza "umeupata mzigo wako pale unapolala?", nikamwambia ninapolala wapi? Akacheka, akanambia si hapo ulipolala jana? Nikamwambia sijapata mzigo wowote, nikawa napiga dua za sura ndogo ndogo za Qur'an, kimoypomoyo, nikaanza kuhisi huyu sio mtu wa kawaida. Ikawa kama kanielewa kua nimeingiwa na hofu fulani, akanambia usiwe na hofu, mimi ni rafiki wa babu yako, nenda pale ulipolala kwenye mto wako tazama vizuri utakuta mzigo wako, njoo nao.

Nikaingia ndani kwenye mto wangu wa rundo la mchanga niliojitengenezea, hikaona kuna kama kimkebe cha bati hivi, nikakibeba, kukitazama kilikua na nakshi nzuri sana, na kilikua sio bati, nilipotoka nacho nje nikaona ni chuma kinang'aa nikawa nakishangalia, kinaonesha cha zamani kweli kweli. Yule mzee alikua anitazama tu, huku antabasamu. Kumtazama sana akasema fungua hicho kimkebe uone kina nini ndani, kukifungua nikakuta kina pete moja ina jiwe jekundu lakini limekooza sana linakwenda kwenye weusi. Akanambia "ivae hiyo kidole chochote utachopenda, nikaiva ile pete kwenye kidole cha shahada. Ikawa imenikaa sawaswa kama imepimwa.

Akanambia huo mzigo wako na huu mzigo wako, akanipa ile bakora aliokua amishoika. Akanambia hii bakora ni yangu, ukiwa nayo hii ujue na mimi sipo mbali, usiniulize kwanini. Ukitaka kujua zaidi muulize babu yako. Hiyo pete ni ya kiumbe mwingine . na yenyewe muulize babu yako mambo take, mmi nakueleza kitu kimoja tu kuhusu hio pete. Hio pete usiivue ukaiacha nje, ukiivua hakikisha unaitia kwenye huo mkebe na unauweka vizuri. Hawezi kuufungua mtu huo isipokua wewe na mwenye hio pete, ukiiweka nje ya huo mkebe kama hujaiva, inaweza kuibiwa au inaweza ikapotea usiione tena. Ikiibiwa, huyo akatakaeiiba atapata madhara makubwa sana na itakua ni kwa uzembe wako. Umeelewa? Kabla sijamjibu akanambia, mambo mengine muulize babu yako, kwa heri. Mimi njia yangu napitia humu ndani ndio inakua karibu na kwangu, akaingia pangponi na mimi nikamfata nyuma, lakini alikua anakwenda ndani zaidi pangoni ile natazama pembeni kumtazama tena sikumuona, nikarudi zangu nje ya pango. Nikakaa nakunywa kahawa huku naitazama ile pete, nikaona ina michoro pete yote na hata lile jiwe kwa ndani lilikua kama lina muhuri ambao sijauelewa maana yake. Nikaitazama fimbo, nikakuta na yenyewe ina alama fulani kabla ya pale ilipopinda kushikiwa na chini kabisa huko kama vidole vinne kutoka chini kabisa ilikua na kama alama za nyaya zilizoingizwa kwa ndani lakini zipo sawa sawa na ile fimbo. Ilikua ni nzuri sana kwa uchache. Nikawa nawaza ya kumuuliza babu kuhsu pete na fimbo.

Itaendelea.
Simba.
.
 
Ilikua ni siku chache kabla sijatimiza miaka 18. Nilipelekwa Tanga, kijiji kimoja kipo karibu sana na mpaka wa kwenda Kenya. Kabla ya kuingia huko kijijini ndani kuna kimji kinaitwa Duga. Ilikua sio mara yangu ya kwanza kupelekwa huko kwa mambo ya kimilla na jadi.

Lakini hii ya safari hii ilikua kidogo yakutisha. Kijiji chenyewe kipo ufukweni kabisa na kina mito miwili inapita, mmoja Kaskazini mashariki ya kijiji, huu mkubwa kiasi na mmoja mdogo unapita kusinii ya kijiji. Kwa hio kijiji ni kama kimezungukwa na maji, maana mashariki yake ni bahari ya hindi, Kaskazini mto na kusini mto. Magharibi tu ndio kuna njia ya kwenda mpaka barabara kubwa ya lami, ambayo ipo kama kilomita 3 au 4 kutokea hapo kijijini.

Safari hii ilikua ni nzito kidogo kwa sababu niliambiwa unaweza kukaa kijijini huko wiki moaja au mbili itategemea na "babu" huko ataamua kama mambo yako tayari au bado.

Nilifatana na Baba na Mama yangu kwenye gari la nyumbani mpaka hapo barabara kuu kutokea Tanga, hapo nikakuta vijana wawili wakubwa kwangu, wananingoja na baiskeli mbili, moja ya kunipakia mimi na moja ya kupakia mizigo yangu.

Mizigo yangu kweli ilikua mingi, yangu binafsi lilikua ni begi kubwa na racksack ya mgongoni, lakini kuna mabiksi kama matatu makubwa yalia ya mama akanambia haya yote mkabidhi babu yako mifika.

Basi tukaagana pale, wao wakanambia ukimaliza kazi yako watakuleta hapa barabarani utapanda gari za kuja Tanga, sisi utatukuta Tanga, tutakuja baada ya wiki mbili, kama utakua umemaliza kabla ya wiki mbili ukifika Tanga tusubiri. Wakaondoka zao, na mimi kapakiwa kwenye baiskeli kama abiria, na nyingine ikafungashwa ile mizogo yetu yote ikatangulia.

Hatukuchukua muda sana, tukafika kijijini, moja kwa moja mpaka kwa babu yangu. Babu yangu tunajuana sana, na alikua ni sahiba yangu sana, ni mtu ma story ya kizamani na mimi nilikua mdadisi sana. uzuri wa babu alikua hakwepi swali lolote utalomuuliza na alikua hamumunyi maneno, anakujibu mpaka likuingie. Nilikua namshangaa sana, kwani hakuna swali lilililokua gumu kwake. Hata niwe na swali, mwenyewe naliona gumu kweli, nikimuuliza bau ananijibu huku ananisifia "swali zuri sana hilo", ananijibu kiurahisi kabisa, mengine huwa anavhukua muda kuyajibu, mtindi wake wa kuibu ulikua kama anakusimulia hadithi, anaweza akatoka kabisa nje ya swali ulilomuuliza lakini atakuhadithia mpaka utalipata jibu. Mara nyingi akikujibu basi lazima utakua na maswali mengine mawili matatu ya kuuliza. Kwa ufupi alikua anaelewa kufungua "kichwa" kwa mujibu baba yangu.

Tutaendelea baadae.
Hii ni tungo au stori ya kweli?
 
Inatokea post namba 7.


Haukupita muda mrefu, tumekaa karibu na mlango wa pango kwa ndani. Mlango wa pango ulikua ni mkubwa sana, na chini ulikua ni mchanga mweupe wa pwani, Kulikua na kivuli kizuri na upepo mzuri sana.

Mwanafunzi wa babu alikua ananieleza lile pango, ni refu sana na huko ndani lina kama vyumba vyumba, vingine ukiingia unakutana na sehemu za kwenda chini zaidi.

Wakati tunaendedlea kuppiga story tukasikia, hodi, mara akaingia yule kijana mwengine waliokuja kunipokea na baiskeli. Kabeba kapu akasema haya, jamani chai ya asubuhi, na mimi mgeni wenu, bibi huko kanitoa mbio, anasema nimwahishie chai mumewe, katoka nyumbani bila kula.

Tukala pale tukamaliza, ilikua samaki wa kuchemsha na vipande vya mihogo. Chai ya rangi imekolea viungo na chupa mbili tatu za maji ya kunyea. Tulipomaliza, jamaa akakusanya vyombo, kulikua na samaki na mihogo imebaki, akasema hii mtakula mkisikia nja. Akaondoka. Nikamuita, nimueagize vitu vyangu juu, akasema, huku ndio hairuhusiwi kuja na chochote ambachoi hujaja nacho kwanza, labda akuletee babu mwenyewe. Akaondoka.

Sisi tuka kaa kaa pale kama kiusingizi kizito killinipipitia, ile nastuka, namuona babu kaja na yule kijana wana kapu lingine. Hiyo kama saa tisa mchana. Akasema haya, chakula chenu. Mmelala sana. Sisi tumekuja kama nusu saa hivi, tukasema tusiwaamshe. Wewe bwana mkubwa nafahamu ukilala, ni zile dawa ulizopakwa, zina nguvu sana. Lakini huyu mwingine, inaonesha kala mihogo mingi. Mihogo inaleta usingizi sana, hasa hii ya mbegu ya bibi yako, mwenyewe aniita dawa ya usingizi. Na kweli, imewasaidia watu wengi weye matatizo ya usingizi.

Babu akasema haya, njoo kuna dawa zingine hapa, sisi tunataka kuondoka. Babu akanipa chupa ya mfuta yenye dawa, kama inachenga inachenga. Akanambia hii utajipaka mwili mzima kikisha ingia kiza kabla hujalala. Na mizizi mingine akanambia hii utatafuna tafuna kila unaposikia mdomo mchungu. Mizizi yenyewe ilikua kama ina sukari fulani hivi kwa mbali unapoitafuna tafuna. Ina harufu nzuri sana.

Babu akatuaga, akasema mshatafuta sehemu ya kulala, pango kubwa sana hili, unaweza kulitenbea mpaka joni hujafika mwisho, linaungana na lile la Amb0ni, mkiingia nia zingine mnaweza kufika Mombasa na njia nyingine mnaweza kufika handeni. Lakini nyie tenbeeni tu ndani msijali. Huyo mwenzako mwenyeji kiasi, sema muoga. Na wewe "bwana mkubwa" muoga? Nikamwambia babu mimi si unajia "komancho" akasema "wewe ndio mroithi wangu", najua wewe uoga huna kabisa, wala sina wasi wasi na wewe simba. Wakaondoka zao.

Tukaamka pale tukaanza kuzunguka ndani pangoni, tukaenda tunaingia vinjia vya vyumba vingine, tunatoka, tunaingia kwengine, mradi tupoteze muda tu, hatujauacha mbali mlango tunayona mwangaza, mwangaza ulipoanza kufifia tukarudi. Tukakuta kiza kimeshaanza kuingia. Hakuna jipya, tukala tukakaa tunapoiga story, jamaaa ananipa story za kijijini na watu wanavyopitisha magendo kutokea Kenya, na jindi wanavyopata pesa kuwavusha wati na mizigo. Wanaingiza poesa nyingi sana, kuliko wangakua mjini. Akanambia kesho nitakuonesha tunapicha mizigo tukija nayo. Kuna oango lingine, hilo lkina kamlango jadogo na kamejaa kichaka, huwezi kujua kama kunapango. ndani pakubw sana. Mie nikajipaja dawa yangu baada ya kula nikakusanya michanga kama mtoi , nikajitupa kulala. Mwenzangu nimemwacha macho anapiga story hata simsikii kwa usingizi, sijui alilala saa ngapi.

Itaendelea.
Stori Yako inatufundisha nini?
 
Back
Top Bottom