Inatoka post namba 112.
Kabla ya kufika Dar nilichoanza kukiona Chalinze kilinitisha lakini nikavumilia kwa kujiamini.
Tumefika Chalinze mapema sana, kama saa mbili na nusu asubuhi. Mama akasema Chalinze tununue mananasi. Mzee hakufanya hiyana akaenda mpaka kwenye mananasi akapaki gari kwa pembeni kidogo ya wanapouza mananasi. Dada yangu akasema ngoija nishuke na kahawa ya mzee nilimtengenezea asubuhi, nikutilie na wewe? Nikamwabia nitilie. Tukatoka nje ya gari, wite, mimi na mzee tukaenda kuna kimkahawa kina viti, tukakaa na kahawa yetu, kumbe kile mkahawa, mwenyewe mwanamke mmoja wa Kisomali kamzowea mzee anamjuwa na mama. Akatusalimia, akamuuliza leo body guard yuko wapi? mzee akamwabia yule kule ananunua mananasi, mimi nikacheka, akasema huyu mdogo wako mbona mmefanana, Mzee akamwabia Sofia huachi zako? Unajifanya humjui huyu leo? Sofia akacheka akasema nilikua nataka nikuone, namjua sana, labda yeye ndio kanisahau, huyu aliekua analilia machungwa akipewa anayatupa nisimjue mimi? Nikacheka nikamwabia Abti Sofi nakujua sana, umesahau wiki iliopita nilikuja peke yangu hapa kukusalimia? Akasema nakumbiuka sana "ukaanza kunitongoza kama baba'ko", mrtoto wa nyoka ni nyoka tu. Mzee akamwanboia "mtoto ea simba huyu" Sofia aaha nilisahau simba mwenzangu. Sasa umeshamfundisha usimba mwanao. Baba aksema huyu mpaka akioa. Kwa ssa bado. Sofua "ada za simba wa kwenu kama za kwetu tu, hakuna mchezo mpaka mtu aoe au aolewe. Na yule malaya wako anaejishaua yuko wapi? Baba akacheka, yule kule na mamake wananunua mananasi. Sofia akanambia mimi "bwna mkubwa, nenda kwa yule mzee pale kwenye mananasi alievaa kofia, mwabie mimi namuita, mwambie na mamako aje, mimi namuigta akichelewa atamtafuta mumewe mpaka akome". Mimi nnikaenda nikafikisha ujumbe kama nilivyopewa kwa wote wawili.
Nikarudi nimeongozana na Dada yangu, kabla hatujafika akanambia ngja nimkere Anti Sofia, nikimkalia baba mapajani anaudhika kweli. Mimi kusikia hivyo nikamwabia siendi, mimi nakwenda pale kwenye machungwa, basi sister kufika kwa mzee kamkalaiza mapajani, Sofia: we malaya, ngoja uolewwee kwanza kisa cha kujishindilia nao, unamuumiza tu babako. Dah sikungpja kusikia, nikanyanyuka nikaondoka na mama na yule mzee wakawa washafika.
Sada hapo kwenye machungwa kabla sijafika, nikakuta wanawake wawili wanauza genge, mmoja ytupo uchi kabisa wa mnyama, yani hana nguo hata moja, kakaa kwenye kigoda na miguu kaichanua, mwenzake ndio anaongea na wateja. Yule mwanamke aknitazama sana, nikaona kanitazama mikonoi kuiona ile pete kama akastuka hivi, akanyanyuka akaingia kwenye mabanda yalikua karibu pale. Mimi nikaenda kwenye machungwa kufika kwenye machungwa, Nikamwabia mwenye machungwa nataka uniletee machungwa pale kwa Anti Sofia. Akanambia pale kwa Sofia simba msomali? Nikawa sijamuelewa akacheka, aksema yule simba mwenzako, hata wewe umenisahau? Babako machungwa huwa anachukua wapi akipita hapa. Nikamkumbuka ni rafiki sana ya mzee. Nikamwabia yeye yupo pale kwa Sofia. Mzee yule akasema machungwa anawalete huyu kijana wangu saa hivi. wewe simba usiwe na wasiwasi, machungwa mengine hapa yantoka shamba la bibi yako. Huku anacheka.
Nikamwabia poa. nikaondoka kurudi, yule mwanamke aliekua uchi nikamuona kavaa nguo lakini hajarudi pale, kasima kule banadani anaongea nini sijui huku ananitazama halafu anatazama chini na mwanamke mwingine, ni vijana tu. Ile narudi kwa mzee, nikasikia sauti ya Arsis masikioni, yule ulimtazama mara tatu, akaelewa umemuona kua ni mwanga. mjinga tu yule, hivi anakuogopa na yule anaeongea nae na yey alikua uchi dukani, ndio wanashauriana wakufanye nini lakini walichokiona hata banada wanaliona baya kukaa, wanataka kuondoka waende kwa wakubwa zao, wamezuiliwa kutoka. Ngoka nikuoneshe kitu kitu ujifunze dunia hgii Bwna Mkubwa.
Mie nikaka kwa mzee pale kwa sofia Dada yangu akasema kahawa yako imeshapoa. Sofia aksema ngoja nimepe kahawa yangu, wewe unajauje kutengeza kahawa? Akaja na chupa ya kahawa na vikombe vya kahawa. Mzee akasema aah, nilisahau kahawa yako Sofia. Sofia akamwambia ulisahau au unajizuzua tu upo na boy guard? Hujamwambia kua kila ukipita hapa lazima nikupikie kahawa uondoke nayo? Mama aksema anambie wakati nayajua sana, siku zigine mpaka kahawa ya nyumbani haitaki, anasema ntakunywa kwa sofia akiwa anakuja njia hii.
Sofia: kumbe unayajua eeh?
Mama; hanifichi kitu mimi.
Sofia; madawa yenu ya kidigo ymemwivia mwilini mwake. lakini humuwezi wewe huyu ukoo kubwa, dawa zako zinadunda hapo.
Wakati wanaongea wanatiana pale, Sofia kaleta kahawa na visheti, mama akamwabia hivi visheti hujatia limbata ya Kisomali?
Sofia: Wasomali sio wachawi sisi, sisi ni machezo tu.
Mara akaja yule mzee wa machungwa na na apu zima la machungwa.
Mzee wa machungwa: Simba isingekua bwana mkubwa kunambia uko hapa nisingejuakama umekuja.
Baba: Nisingethubutu kuondoka bila kuja machungwa yangu mnayiniibia shambani.
Wakacheka wote.
Sofia; Kumbe machungwa yako, mimi ananiuzia kama myeja wa kawaida, hata wakipita wageni zangu ndio anawapiga kweli.
Mzee wa machungwa: Wasomali wana pesa, utawafananisha na sisi wadigo.
Sofia: Nilikua sijui kama machungwa yanatoka shmani kwa simba.
Baba: Tena simba, ukichukua machungwa shambani hakikisha unamletea sofia kapu lake.
Mzee: Ngoja nianze kuletea sasa hivim haya yametoka kwenu, tena shmaba la bibi yajomkabisa. Mwaka huu bibi yule atatajirika, hizo Fuso za Wakenya zilizokua zinaingia kuvuna machungwa, Mashaallah. Sasa simba njoo huku wakati namletea machumgwa Sofia, wewe njoo tunong'one kidogo.
Mze akaamka akaenda nae kwenye machungwa.
Sofia: Babako Chalinze nzima wanamjua.
Mama: Hapa si wamejaa watu wa Tanga na muheza, lazima wamjue. Si kama wewe, wanagu huyu Sofia tumekua Tanga, msimuone hivi huyu, malkia huyu wa Tanga huyu.
Sofia; wasinione hivi nini "once a malkia always a malkia". Kama unabisha muulize mumeo. Una bahati upo na makinda wako hapa, ningemiuingiza ndani mumeo na wewe unayaona.
Mama ; Yule mzee wako wa Kisomali aliekuja kukuchakaza Chalize hapa yuko wapi?
Sofia: Huna habari ndugu yangu, kafariki zaidi ya miaka sasa. Nipo singo. Hivi unavyoniona nahamia Dar karibuni, namngoja huyu mtu nimemuuzia nyumba na hii shehemu hapa aje nondoke anakuja siku yoyote kuanzia sasa. Utanikoma nikija Dar.
Mama: Simu zangu si unazo, ukija nijulishe ulipo nije kukuonesha jiji.
Sofia: Mbona mumeo anapajua mpoaka kwangu, mimi siku nyingi nna nyumba yangu Dar, toka mume wangu yupo hai hatujakaa nyumba ya kupanfga sisi.
Mama: Eeeh nimekumbuka, uliolewa Dar, ytena nilija mpaka kwako pale Upanga,
Sofia: Sasa ulifikiri nyumba ya msajili ile, ile nyumba yangu na hivi nimeshawahamisha wapangaji, nangoja nije kuikarabati nihamie. Mwanagu mmoja yupo Dar ni Pilot wa Aur Tanzania, yule wa kike aliolea na Msomali wa QWatar huko, ana watoto watatu sasa. Yule mwengine wa kume anafanya kazi za baba'ke za malorry, hivi kila siku njiani, namwabia awachane nazo hataki. Anapita hapa kila siku mbili tatu, yeye ndio anakaa hapa sasa hivi na mkewe, wanawe wapo Dar wanasoma, wanakaa kwa yule mdgo wangu wa kiume unamkubuka?
Mama " Nisimkumbuke muhuni yule? Yule hatoki nyumbani hata hawa wanamujua, MImi nikauliza Anko Abdi? mama aksema ndio yeye hiyo, huyu dada yake mama mmoja baba mmoja.
Dada: Yule anaonesha alikua bonge la handsome alivyokua mdogo.
Sofia: Muulize mamako.
Mara mzee akarudi akaniita pembeni, kumbe na yule mzee wa machungwa yupo. Mzee.
Baba; Mwambie mwenyewe kilichotokea.
Machungwa: Mwanangu, kwanza pole sana. Haya mamboi si madogo mpaka yamefika kwangu, nimemueleza babako, yule mwanamke kumbe ni mwanga, mwenyewe kakiri, mimi wamekuja wakubwa zake kunieleza nije kukwambia umasamhe. Mimi nikajifanya kushangaa, kama sijui kitu kabisa.
Mimi; Kwani kuna nini?
Machungwa; Tule mwanamke anasema ulimuona akiwa hana nyuo, akaenda kumjulisha mwenzake ndani na yeye akawa hana nguo, wakataka waje kukukomesha sasa wameganda mule ndani hawawezi kutoka ingawa sasa hivi wamevaa nguo lakini hawawezi kutoka wakawaiata wenzao ndio wakawasiliana wakubwa zao, wakubwa zao wakataka kukufata hapa wakutie adabu, wakaishia njiani wakja kwangu walivyoona mimi naonge na ongea na wewe ndio wamebifata nije niwaombee msamaha. Uwawachie waendelee na mambo yao, wapo tayari kulipa fidia ypoyote.
Baba: Umefanya nini simba. Sijafanya lolte baba hata sijui nini kinaendelea.
Kidogo wakati bado baba namzu)ee wa machungwa wanaongea ikanijia sauti ya Arsis,
Arsis: wewe waambie hujui kitu, tena wasikufate tena kuletea mambo ya kipuuzi, sisi tutawatia dabu hawaji tena kufanya vbiasha )ra uchi. Umenielewa.
Mzee: Sasa tufanye nini jamani, mimi mjumbe tu? mjumbe hauawi. Mimi mwenyewe nashangaaa ujanja wangu wote sikuyajua haya. Wapumbavu wale wanakuja kutulisha uchafu wao hapa, ndio mimi sili kwa hawa mama ntilie nisiowajua. Sasa niwaambie nini wale jamaa zao?
Mimi; Waambie mimi sijui kitu na wasimisumbue, sijanywa hata kawahawa yangu. Sijui kinacheoendelea.
Baba; Haya bwana ahsate kwa kuniita, umesikia mwenyewe, ansema hajui nini kinaemdelea anajiponea ajabu. Waambie kama wana maneno zaidi wanifate mimi Dar. Lakini waje wamejitayarisha.
Mzee: Wacha utani bwana, alilosema huyu simab, ndio neno, wasimsumbue yeye na wasimsumbue mtu. Na mi nipeni ryuksa niondoke, nitajua cha kuzungumza nao. Samahani sana ,wajinga wale sasa watakoma wasikiri kila mtu wakucheewa. Aaondoka ake. Akasema na yale machungwa ni ya bibi yako zawadi ytangu kwako.
Tukaridi na mzuu tukanywa kahawa yetu na visheyi, akipakia machungwa kwenye gari, yule mzee wa mananasi nae alikua amyaleta kibao, Sofia akachagua, akasema mpeni elfu ishorini kwa ajili yangu. Mama akatoa akampa. Tukaondoka zetu., Nilikuja kujua siku ya pili nini kiliendelea na wale wachawi.
Itaendelea.