Mkuu wala huja offence kwani naamini ufahamu wangu haujakamilika pia najifunza kitu kupitia kwa wengine kama wewe hivi.
Niliposema dini ni imani niliweka mabano(belief), lugha ya kiswahili tunatafsiri yote kama imani lakini kuna tofauti kati ya belief na faith. Imani(faith) ni sifa, hivyo inakuhitaji u qualify kupitia matendo yaliyobeba nia, ila imani(belief) mtu yeyote anaweza kuwa believer bila hata kuwa na matendo yanayoongozwa na nia yake as long as anafuata taratibu na miongozo ya dini fulani, ambapo misingi hiyo inakuwa influenced na asili. Hope nimekujibu paragraph 1.
Sijasema dini zingine, ILA hakuna dini yoyote ile inakupeleka katika utakatifu bali imani inakupeleka. Lengo la dini ni zuri sana maana dini zina hubiri haki, amani na upendo hivyo kupitia miongozo yake ile ndio itakuhitaji wewe usikie neno na kulielewa baada ya kulielewa utakuwa ni believer mwenye faith kupitia matendo yako, hivyo matendo yako ndio yatakuhesabia haki na sio wewe kujiona una haki na wengine wasio amini kama wewe hawana haki. Hapo tunaona dini imekusaidia kukupa njia ila imani yako kupitia matendo ndo yatakufikisha unakokwenda. Natumai nimekujibu paragraph 2.
Matendo ya namna ya kuishi yamejumuisha imani na dini. Mfano namna ya kuvaa, vyakula hii inakuwa inachangiwa na asili ya mazingira, upatikanaji, hali ya hewa na vitu vingi vinavyotokana na mazingira. Ukisoma vitabu vya dini utaona vyakula vilivyoelezewa ni vile vilivyopatikana eneo husika kwa wakati huo. Pia tunaona kuna matendo ya imani, mfano namna ya kuishi na majirani hii inatokana na imani, maana uhalisi wa mtu ni upendo(dhahiri yake ni kuwa na furaha). Huwezi kuwa na imani kama huna upendo hivyo swala la kuishi na majirani ni inatokana na imani ndio maana katika kila jamii kuna watu wenye upendo na watu wenye kinyume chake maana hii haihusiani na asili ya mtu bali halisi yake(imani). Natumai nimekujibu paragraph 3.
Kwa nielewavyo mimi Mungu akuhesabu wewe katika label ya msabato, mkatoriki ama muislam. Anakuhesabu wewe kama kiumbe chake mtu(aliyekupa upendeleo na mamlaka) hivyo hayo maswala ya usabato na ukatoliki tunayajua sisi yeye anachoangalia ni imani yako kwake iko vipi, ni zaidi ya mzazi awaonavyo wanae bila matabaka.
Ibada kwa maana yangu ni ku surrender kila kitu, na kuonyesha kuwa wewe si kitu na huwezi chochote bila ya huyo unaye mwabudu.
Umenena vizuri, nikipata mda siku yoyote nitarudi kuendelea tulipoishia.
Ila kuna haya kama utayapenda yazingatie, kwani nakuona uko na fikra huru kiasi chake.
1. Kitu kizuri, ni kile kilicho kwenye asili yake. Ubora wa elim au maarifa ni yale yapatikanayo katika asili yake hasa upande wa lugha. Hizi tafsiri za kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine kisha lugha nyingine ndio zilizo tufikisha hapa tulipo.
Kwani mtafsiri hua anatafsiri uelewa wake, hivyo utashi wake unaingizwa ndani ya tafsiri. Utashi ambao unaweza kua sawa au usiwe sawa. Wakiwa watafsiri watatu na kila mmoja akaweka uelewa wake ambao unatofautiana na mwingine basi chap yashakua makundi matatu kwani katika hao kila mmoja atakua na wafuasi wake wanamuamini kila asemalo haijalish yuko sawa au laa.
Neno moja linapokua na maana tofauti kwa watu huleta mkanganyiko, mkanganyiko huzaa makundi. Na mfano wa makundi ni haya unayo yaona leo hii. Bahati mbaya hakuna aliye radhi kuondoa mkanganyiko kwa kurejea kwenye asili ya elim husika...
2. Hakuna elim au maarifa yasiyo na asili, au marejeo (reference). Kila ujualo, uzungumzalo lina marejeo. Mfano huezi jua yale ni "Maji" kama hukuwahi kufunzwa kua yale ni "Maji". Of course unaweza usijinasibishe na dheheb lel say msabato wala mkatoliki ni jambo zuri, lakini ni uhalisia usioweza kuupinga kua ufaham wako ulionao una marejeo. Kuna sehem ulipojifunza, either katika vitabu au kwa kusikia watu ambao unawaamini.
Udhaifu ambao binafs nauona kwako ni pale kuna wakati kunakua na hisia zako zinachanganyana na marejeo yako. Nirudie tena kusema samahani kama nitakua nimetumia lugha ngum hapa juu yako.
Kila ulichozungumza hapo kina marejeo, na marejeo umeyapata katika dini. Na huezi kupinga kua ni katika Ukristo. Sio jambo baya kwani huo ndio mwongozo wenyewe wa maisha yako unaokuweka karib naye Mwenyezi Mungu.
Nasema hivyo kwanini? Upande wangu mie wala sijifichi. Ni Muslim na najivunia hilo hakika. Huku Dini na Imani vinazungumzwa katika nyanja mbili huku Imani ikiwa ni daraja la juu zaidi. Viwili hivi yani Dini na Imani kila kimoja kina nguzo zake. Kuna nguzo za dini pia kuna nguzo za Imani vile vile. So hata katika matendo, kuna matendo ya kidini, na kuna matendo ya kiimani pia. Nikizitaja nitarefusha sana hii post but ingekupa maana ambayo binafs naifaham juu ya Dini na Imani.
Mfano kama kwenye hiki hapa chini, sijui reference yako ni nini ya kauli hii, kwamba umeitoa wapi? Au ni just hisia zako? Ningependa kujua ingawa sio lazima.
Kwa nielewavyo mimi Mungu akuhesabu wewe katika label ya msabato, mkatoriki ama muislam.
Kingine hapa chini sijafurahia jambo moja, hapo uliposema kua Mwenyezi Mungu hajui Usabato, Ukatoliki. Unamdogosha Mola wetu mlezi. Anajua kila kitu kutuhusu, tunayoyaficha na tusio yaficha. So vyema kumuenzi kwa Ukubwa wake.
Anakuhesabu wewe kama kiumbe chake mtu(aliyekupa upendeleo na mamlaka) hivyo hayo maswala ya usabato na ukatoliki tunayajua sisi yeye anachoangalia ni imani yako kwake iko vipi, ni zaidi ya mzazi awaonavyo wanae bila matabaka.
Cha mwisho ni hapa 🤣
Ibada kwa maana yangu ni ku surrender kila kitu, na kuonyesha kuwa wewe si kitu na huwezi chochote bila ya huyo unaye mwabudu.
Unaona hapo umetumia neno la kingereza "Surrender" ambalo kiswahili ni Kujisalimisha na upande wa kiarab ni kusilim na ndipo neno Islam likapatikana. Utaona ni neno moja kwenye tatu lugha tofauti. Hapa pia nieleweke vizuri, SIKUSHAWISHI kitu ila ujionee utofauti wa lugha, utofauti wa kimaana katika neno moja ndio umetufikisha hapa tulipo. Makundi kwa makundi tuna kitu kimoja ila maana kila mmoja na yake. Na hiki ndio kilikua dhumuni la kuuliza Dini ni nini, Imani ni nini.