Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Habari za Alfajiri wana ukumbi?

Mtanisamehe sana kwa kupotea ghafla.

Kulikuwa na mambo ya kifamilia yaliyonifanya niwepo Tanga mjini na mahandakini kwa muda mrefu kiasi kuliko kawaida, na kutokea huko huko nikapata safari ya ghafla bin vuu ilionifikisha nchi mbili za Kiarabu bila kutarajia.

Pateni kionjo cha safari, mtaunganisha dots wenyewe kwa kufyatua codes:

View attachment 3141064
Nilichoweza kuunganisha hapo na huu uzi ni hizo bakora tu.
. Funguka, wachana na mambo ya codes.
 
Nikusaidie, tena kwa elimu ya kusoma, si ya mazingaombwe! Kasha la Agano (Ark of Covenant) ambalo katika Qur'an limeitwa 'Tabuut' liko katika Kanisa moja la zamani sana kule Ethiopia. Kanisa hilo limechimbiwa chini ardhini. Au lilijengwa kutokana na kupasuliwa kwa mwamba. Hakuna ruhusa ya yeyote kulifungua kasha hilo isipokuwa makuhani watatu tu, hivi kwamba Condoleeza Rice, Waziri wa Marekani wa zamani wa Usalama, aliwahi kulifungia safari kutaka afunguliwe aone mabaki ya waliyaacha watu wa Musa (Moses), kama ilivyosema Qur'an.....lakini hata yeye alikataliwa!
Ukiinukuu Qur'an uweke na hizo aya unazonukuu.
 
Hivi majini yanawezaje au yanamdai mtu pesa kwa misingi ipi ?
Yani mtu anatakiwa apeleke pesa sehemu yanayomwambia akifika hapo pesa zinakwenda na maji ndio Mhusika anashtuka Ila hela ndio bhasi tena.
 
Mambo yanaweza kuonekana ya ajabu sana kwa wengine, lakini kwa kua naishi nayo kwa muda nrefu sasa, kwangu yanakua si ajabu tena bali ni mikasa na vituko.

Nilikwenda Tanga mjini kwa mambo ya kifamilia, siku ya pili usiku, mapema tu, kama saa tatu za usiku niliingia kupumzika, mlango ukagongwa, ile staili ya kugongwa nikajua ni Jini 1 huyo. Nikasema, ingia. Jini 1 akaingia.

. Baada ya kusalimiana nae, Jini 1 akanambia nimekuja na mgeni wako, Bakora yupo hapa anataka kuongea na wewe peke yako, aingie? Nikamwambia, aingie tu. Jini 1 akafungua mlango, Bakora akaingia, Jini 1 akaaga, akatoka zake.

Bakora alipoingia nikashangaa kumuona ana bakora yake na mbili zingine.

Bakora; hii fimbo yako, nimeona nikuletee.

Kweli, bakora yangu niliiacha Dar nikaona ndio moja kati ya tatu alizonazo. Siku hizi mara nyingi huwa sisafiri nayo.

Bakora; Usishangae, kuna kazi muhimu sana ndiyo maana nimekuletea, inahusiana na hii bakora nyingine niliokuja nayo. Kesho unatakiwa uje mahandakini mapema, kuna mambo muhimu sana.

Mimi; Mambo gani?

Bakora; Usiulize sasa hivi, utayajua yote ukija mahandakini kesho, usiwe na wasiwasi ni mema tu. Hizi bakora zote mbili nakwenda nazo.
Bakora yako utaikuta mahandakini utapokuja kesho. Atarudi Jini 1 kama una maswali yoyote atakujibu yeye. Kwaheri.

Akaondoka zake.
 
Yapo majini yenye tabia zote mbya walizo nazo watu.

Wapo wezi, majambazi, matapeli malaya, mashoga na wapo kila aina ya wema.

Majini hayana tofauti na watu kitabia. Mbele huko tutakuja kutambua kua majini wengi zaidi, kama si wote, ni watu.
 
Arsis dr tulia alikusoma humu nini akakuchek akakuelezea shida zake ukaenda msaidia si ndio ivo
Hapana. Ana njia zake mwenyewe zilizomfikisha wakajuana na shangazi yangu wa Mahandakini, akajulishwa kwa Bakora, wamejuana na Bakora akazawadiwa Bakora na hapo alikwenda rasmi kwenye sherehe za wenye Bakora, mimi na shangazi yangu pia tulikuwepo.

Haya majini yana mitandao yao mipana sana.
 
Heri,

Wote tulizaliwa tukijua tumegawanyika sehem tatu yaani roho,nafsi na mwili kwa mujibu wa kitabu.Ila kusudi la Muumba lilikuwa wote tuwe MOYO (moyo safi)
kwa mujibu wa
mathayo 5:8 (Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.) na

mithali 4:23 (Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.)

Muumba alituumba tuweze kumiliki na kutawala vinavyoonekana na visivyoonekana kwa mujibu wa

Zaburi 8:4-6

4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?

5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;

6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

Badala yake baada ya dhambi visivyoonekana ndio vikawa na nguvu na ndo vikawa vinatutawala na kuendesha uumbaji.

Warumi 7:17
Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

Isaya 26:13-14
13 (Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.)

Je ni nini kilisababisha hayo yatokee?

Wote tulizaliwa tukijua tumegawanyika mara tatu yaani Roho,nafsi na mwili, maana yake nini?
Ukiwa roho ilikuwa ni kuugua tu

Warumi 8:23

Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

Ukiwa nafsi ilikuwa ni kubeba uchafu tu

Marko 7:21-22

21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Ukiwa mwili ilikuwa kuwa na uadui na Muumba wako.

Warumi 8:7
7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.

Utendaji wa roho, nafsi, mwili na asili ilikuwa ni kuibiana vipawa na viwekezo hasa wale wenye maarifa,kuishi maisha ya mwengine huku yeye akiteseka,unafunga nyumba yako mtu anajigeuza mjusi au panya au kutoonekana anaingia na kufanya yake.

Ilikuwa haiwezekana kuwa msafi wa moyo kama ukiwa ni roho,nafsi na mwili maana ulikuwa huwezi kutenda kile unapenda.Ni Muumba peke yake ndiye anayeweza kutufikisha kwenye usafi wa moyo ili aishi yeye ndani yetu.

Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye umilele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na moyo uliotubu na kunyenyekea, ili kuifufua mioyo ya wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.

Ukiwa roho,nafsi,mwili na asili ulikuwa huwezi tenda vile unapenda sababu kulikuwa na wanaokumiliki(mizimu,ruhani,asili,mauti,majini,wachawi,watu, n.k) na kukufanya wewe kiti chao kwa kujua ama kutokujua.

Warumi 7:15
15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.

18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

19 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

Hupendi uzinzi ila unajikuta umezini,hupendi kutoka nje ya ndoa yako unajikuta umeshachepuka,hupendi uongo ila unajikuta unadanganya,hupendi ulevi ila unajikuta unakunywa pombe,hupendi wizi ila unajikuta unaiba,hupendi umalaya ila unajikuta unajiuza

Je haya yote yamekujaje?

Ni kutokana na uumbaji wote kuwa kwenye uteka ndo maana watakatifu wote walishindwa kufikia kwenye usafi wa moyo (MOYO SAFI).

Warumi 8:20
20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;

Je KUSUDI ni nini?
Muumba alitukusudia tuwe MOYO yaani wasafi wa Moyo( Clean heart) hapo mabaya hayakai.Bila ya kukaliwa na mzimu wowote au jini lolote au maruhani yeyote,uwe wewe kama wewe ulivyoumbwa bila kuning’iniwa na uchafu wowote au mtu yeyote.

Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Mathayo 5:8
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Muumba.

Je Moyo maana yake nini?
Nikisema Moyo sio huu unaopelekwa India kupasuliwa lahasha bali ni muonekano wako wote ndio ulikusudiwa uwe MOYO na yale mema na mazuri uyapendayo.
 
Mambo yanaweza kuonekana ya ajabu sana kwa wengine, lakini kwa kua naishi nayo kwa muda nrefu sasa, kwangu yanakua si ajabu tena bali ni mikasa na vituko.

Nilikwenda Tanga mjini kwa mambo ya kifamilia, siku ya pili usiku, mapema tu, kama saa tatu za usiku niliingia kupumzika, mlango ukagongwa, ile staili ya kugongwa nikajua ni Jini 1 huyo. Nikasema, ingia. Jini 1 akaingia.

. Baada ya kusalimiana nae, Jini 1 akanambia nimekuja na mgeni wako, Bakora yupo hapa anataka kuongea na wewe peke yako, aingie? Nikamwambia, aingie tu. Jini 1 akafungua mlango, Bakora akaingia, Jini 1 akaaga, akatoka zake.

Bakora alipoingia nikashangaa kumuona ana bakora yake na mbili zingine.

Bakora; hii fimbo yako, nimeona nikuletee.

Kweli, bakora yangu niliiacha Dar nikaona ndio moja kati ya tatu alizonazo. Siku hizi mara nyingi huwa sisafiri nayo.

Bakora; Usishangae, kuna kazi muhimu sana ndiyo maana nimekuletea, inahusiana na hii bakora nyingine niliokuja nayo. Kesho unatakiwa uje mahandakini mapema, kuna mambo muhimu sana.

Mimi; Mambo gani?

Bakora; Usiulize sasa hivi, utayajua yote ukija mahandakini kesho, usiwe na wasiwasi ni mema tu. Hizi bakora zote mbili nakwenda nazo.
Bakora yako utaikuta mahandakini utapokuja kesho. Atarudi Jini 1 kama una maswali yoyote atakujibu yeye. Kwaheri.

Akaondoka zake.
Tatizo lako Simba humaizii kisa, una alama zakuuliza nyingi.
 
Tatizo lako Simba humaizii kisa, una alama za kuuliza nyingi.
ni kweli hamalizi kimoja kikaisha atarukia kingine chenye maudhui tofauti kabisa..jamaa ana visa vingi sema upangiliaji wake tu ndio maaa mm nilimshauri aanzishe thread nyingi za visa tofauti tofauti ili kuwa na wigo mpana wa elimu anayotoa ila yeye uzi mmoja vimepandana visa kibao visivyoungana kimaudhui basi mparanganyiko tena ukiongeza na mabishano ya wafia dini basi vurugu tupu hadi uzi umepoteza ladha na kutoka nje ya lengo vile tulivyoanza.!
 
Usifikiri sote tutakua na namna moja katika uandishi wetu, kila mmoja na namna yake.

Namna yangu inalenga kwa makusudi kabisa kuacha watu wawe na maswali.
Kama hukuelewa kitu uliza, naweza kukujibu mimi au mwengine yeyote, ni uzi wa wazi huu.

Hakuna kisa humu cha kukianza na kukimaliza moja kwa moja. Hilo sahau.
 
Heri,

Wote tulizaliwa tukijua tumegawanyika sehem tatu yaani roho,nafsi na mwili kwa mujibu wa kitabu.Ila kusudi la Muumba lilikuwa wote tuwe MOYO (moyo safi)
kwa mujibu wa
mathayo 5:8 (Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.) na

mithali 4:23 (Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.)

Muumba alituumba tuweze kumiliki na kutawala vinavyoonekana na visivyoonekana kwa mujibu wa

Zaburi 8:4-6

4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?

5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;

6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

Badala yake baada ya dhambi visivyoonekana ndio vikawa na nguvu na ndo vikawa vinatutawala na kuendesha uumbaji.

Warumi 7:17
Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

Isaya 26:13-14
13 (Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.)

Je ni nini kilisababisha hayo yatokee?

Wote tulizaliwa tukijua tumegawanyika mara tatu yaani Roho,nafsi na mwili, maana yake nini?
Ukiwa roho ilikuwa ni kuugua tu

Warumi 8:23

Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

Ukiwa nafsi ilikuwa ni kubeba uchafu tu

Marko 7:21-22

21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Ukiwa mwili ilikuwa kuwa na uadui na Muumba wako.

Warumi 8:7
7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.

Utendaji wa roho, nafsi, mwili na asili ilikuwa ni kuibiana vipawa na viwekezo hasa wale wenye maarifa,kuishi maisha ya mwengine huku yeye akiteseka,unafunga nyumba yako mtu anajigeuza mjusi au panya au kutoonekana anaingia na kufanya yake.

Ilikuwa haiwezekana kuwa msafi wa moyo kama ukiwa ni roho,nafsi na mwili maana ulikuwa huwezi kutenda kile unapenda.Ni Muumba peke yake ndiye anayeweza kutufikisha kwenye usafi wa moyo ili aishi yeye ndani yetu.

Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye umilele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na moyo uliotubu na kunyenyekea, ili kuifufua mioyo ya wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.

Ukiwa roho,nafsi,mwili na asili ulikuwa huwezi tenda vile unapenda sababu kulikuwa na wanaokumiliki(mizimu,ruhani,asili,mauti,majini,wachawi,watu, n.k) na kukufanya wewe kiti chao kwa kujua ama kutokujua.

Warumi 7:15
15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.

18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

19 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

Hupendi uzinzi ila unajikuta umezini,hupendi kutoka nje ya ndoa yako unajikuta umeshachepuka,hupendi uongo ila unajikuta unadanganya,hupendi ulevi ila unajikuta unakunywa pombe,hupendi wizi ila unajikuta unaiba,hupendi umalaya ila unajikuta unajiuza

Je haya yote yamekujaje?

Ni kutokana na uumbaji wote kuwa kwenye uteka ndo maana watakatifu wote walishindwa kufikia kwenye usafi wa moyo (MOYO SAFI).

Warumi 8:20
20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;

Je KUSUDI ni nini?
Muumba alitukusudia tuwe MOYO yaani wasafi wa Moyo( Clean heart) hapo mabaya hayakai.Bila ya kukaliwa na mzimu wowote au jini lolote au maruhani yeyote,uwe wewe kama wewe ulivyoumbwa bila kuning’iniwa na uchafu wowote au mtu yeyote.

Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Mathayo 5:8
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Muumba.

Je Moyo maana yake nini?
Nikisema Moyo sio huu unaopelekwa India kupasuliwa lahasha bali ni muonekano wako wote ndio ulikusudiwa uwe MOYO na yale mema na mazuri uyapendayo.
Nakushauri punguza mahubiri, yafanye yawe mafupi.

Kuhusu swali lako la moyo, natumai Waislam watakujibu, kwani kimeongelewa sana katika Uislam na mimi nimeligusia kidogo huko nyuma.

Kwa ufupi; moyo ni kiini (core) ya utu. Unaendesha ubongo wetu ili tufanye yote tuyafanyayo.

Ni kweli, moyo kusudiwa sio huu waanaoufanyia upasuaji pale Jakaya heart Institute. Lakini naamini Dr. Janabi anafahamu sana kuhusu moyo uliokusudiwa kwenye maandiko ya imani, kwani nao hupatwa maradhi vile vile, kwa mujibu wa Quran.
 
Back
Top Bottom