rafiki sijasema habari ya uwongo hapana , uwe na amani. bali kawaida mtu akidunduliza na kuona ana wazo flani na na anona laweza timia ndio anaacha kazi, sasa wewe umefanya kinyuma umedunduliza mwaka mzima , je wakati unadunduliza ulikuwa wadunduliza kwa ajili gani? si unaona lazima ulikuwa na wazo. maana biashara nayo ni passion , kuna biashara nyingi lakini lazima uwe na passion ya biashara flani tuanzie hapomilioni mbili hiyo nimeikusanya kwa mwaka mzima sio kwamba nimeipata kwa mara moja. Ni kweli nimeacha kazi nikiwa bado sina detailed plan ya nini cha kufanya. ila ndo nimeshaacha na nnaamini nitasavaiv, hapa nimekuja kuomba ushauri kwa watu wenye uzoefu. Kama wewe unahisi nimeleta habari ya uongo ni siwezi kukuaminisha tofauti ila kama unaweza kunisaidia kwa mwongozo, nitakushukuru sana.
ni kweli ila niliona tuanzie hapo, maana lazima at back of his/her mind alikuwa anawaza kitu tukianzia hapo tunajenga hoja ya kusaidia, hata Dr ukienda huanza kukuliza historia then anajua aanzie wapiSijaona haja ya kumuuliza hili Swali
Biashara ya kuingiza nyanya mjini kutoka mkoa inalipa sana kwa maelezo zaidi sogea mabibo kwa madalaliHabari zenu wana jamvi,
Nimeacha ajira kwa hasira. Nimefanya maamuzi ya kipuuzi? sijui! Ngoja nianzie mbali kidogo kuwasimulia:
Nilihitimu Shahada yangu ya Uhandisi mwaka jana na baada ya kukaa mtaani kwa miezi mitatu tu nilifanikiwa kupata ajira. Nilipata ajira kama fundi mchundo (Technician) na sio Muhandisi kama nilivyotegemea. Kwa kweli nilivunjika moyo kwa hilo kwa kuwa wakati huo naingia kazini niliingia na jamaa mmoja naye akaajiriwa kama Technician ila yeye amesoma Veta Level 2.
Kilichoniuma mimi ni kwamba nina Stashahada Ya Uhandisi Pamoja na Shahada ya Uhandisi alafu bado nalipwa sawa sawa na mtu mwenye cheti cha Veta, tena kiuhalisia yeye analipwa kiasi kikubwa kwa kuwa yeye hana makato ya Bodi ya Mkopo ila mimi bodi wananinyoosha.
Wakati naanza kazi nilimuuliza bosi wangu kwa nini naajiriwa kama Technician na sio Engineer, akanijibu kwamba nitaweza kupandishwa huko mbeleni kulingana na utendaji. Basi mimi nikaanza kazi.
Kwa kweli kazi ilikuwa na changamoto kwa sababu nilikuwa na majukumu mengi. Nikiwa ofisini nilikuwa nikihusika katika usanifu na kuandaa mpango kazi na nikiienda site nilikuwa napigika zaidi maana nilikuwa nahusika kwenye kusimamia kazi, ununuzi wa materials, na pia nilikuwa nikihusika katika kazi za kufanya kwa mikono.
Yaani kwa ufupi nilikuwa nikifanya kazi za fundi mpaka za muhandisi mimi mwenyewe. Katika mradi wangu wa kwanza nikagundua hata dereva analipwa pesa nyingi kuliko mimi, nikazidi kuumia.
Sasa bwana mwezi uliopita, mwisho wa mkataba wangu ukafika, bosi akaniita akanikabidhi mkataba mpya, lakini baada ya kuupitia nikagundua mshahara ni ule ule na cheo ni kile kile. Basi mimi nikamuomba bosi anipe siku moja nikafikirie alafu nitakuja kusaini au la. Baada ya siku moja nilirudi na nikaamua kuweka dau la mshahara ninaloona mimi ni sahihi. Kwa kifupi bosi alikataa na mimi nilikataa na mimi nikaishia hapo kufanya kazi.
Sasa turudi kwenye kichwa cha uzi huu. Naomba mnishauri niazie wapi maisha ya biashara maana kazi nimeshaacha (na sijui kama lilikuwa wazo la busara), hapa nina 2 million ambayo nilifanikiwa kuikusanya kwa mwaka huo mmoja niliokuwa nikifanya kazi.
Sijawaambia wazazi wangu wala watu wangu wa karibu kwamba nimeacha kazi na ninafikiria kwenda mkoa ambao nitakuwa mbali nao nikaaendelee kujifunza maisha huko.
Nipo tayari kufanya biashara ya hali yoyote, nakaribisha ushauri.
Asanteni.
Mkuu mimi nina skills kwenye pc repair and maintenanceMobile phone an PC repair and maintenance, sale ukiwanazo hizo skills mzee utaona kweli kuajiriwa ni ujinga sana na uoga.
Kwangu Kwa hiyo million mbili ni nyingi Sana na nitakushauri ifuatavyo Ila kabla ya yote pesa tamu huja Kwa maumivu na kudhalilika. Kuna tuliomaliza hizo degree tukadharaurika nyumban mpaka kuondoka Kwa hasira pasipokujua na plan.Nipo Kigoma, Kasulu kwa sasa.
Ngoja nicheke kwanza[emoji1787][emoji1787][emoji23]bado taarifa zimepinda. unafanya kazi, unapata million mbili huyo! unatimka na kuanza kuplan uifanyike kazi gani!! nilihani inaacha kazi una mikllion mbili tayari umepata fursa sasa unaona million mbili kwa mradi wako ukizifanyia zitakuwa a faia kuliko kazi hiyo.
hapo hajafunguka! unless hakuwa na kazi sasa kakwapua pahala anajikuta ana million mbili na hajui azifanyire nini!! Lakini wafabnya kazi , unalipwa unapata million mbili unaamua kupumzika kazi halafu unaleta jamvini hapo kwanza tuambie wewe una mawazo gani tuanzie hapo
Fungua banda la chips Mabibo hostelAsingejipanga maana yake hata hiyo milioni mbili asingekuwa nayo. Anachoomba hapa ni wazo la biashara kwa mtaji wa milion mbili.
Asante sana, je unafahamu zaidi kuhusu biashara ya mise? Je yenyewe ina msimu? Unaweza kuichanganua zaidi kama ulivyochanganua ishu ya tofali?Kwangu Kwa hiyo million mbili ni nyingi Sana na nitakushauri ifuatavyo Ila kabla ya yote pesa tamu huja Kwa maumivu na kudhalilika. Kuna tuliomaliza hizo degree tukadharaurika nyumban mpaka kuondoka Kwa hasira pasipokujua na plan.
Kwa kigoma fursa nitakupa fursa mbili.
Ya Kwanza hiii inapendeza hasa kipindi kuanzia mwezi wa tano kuelekea wa tisa.
Utengenezaji wa tofali za kuchoma kibiashara tena za quality nzuri.
Kwa ujumla kama umefanya KAZI kwenye ishu za ujenz utakuwa unajua jinsi tofali zinavosumbua hasa kipindi cha ujenz Sana Sana kigoma mjini. Na challenge kubwa inatokana na uhaba wa miti ya kuchomea na wengi wanaoifanya hiyo KAZI hawana Ile munkari ya kupata pesa ya kufa mtu.
Mfano ukiwa kigoma mjini vile vitofali vidogo saiz ya tako vinaenda Kwa bei ya 100 mpaka hamsini. Lakini kuna wanaotengeza kubwa kidogo wanauza mpaka 250.
Kukodi lorry mfano toka kidahwe mpaka kigoma mjini la tofali1000 ni kama 80000.
SASA wewe unaweza amua tafuta site nzuri yenye upatikanaji wa maji na udongo wa mfinyanzi mzuri unatafuta vijana wako hata watano na ukapiga hesabu zako labda wafyatue hata tofali 100000 huku wewe ukiwa unahudumia chakula na malazi . Pia kuhangaikia kuni za kuja chomea.zaid ya hapo ukadili pia kutafuta wateja wa kuwauzia kusud utapoivisha tanuri lako uuze na kuwalipa wafanyakazi wako. Ukifanikiwa fyatua tofali hata 100000 nzuri zile kubwa kubwa unauza hata Kwa bei ya 200 huwez kosa pesa.
Mradi wa pili huu ni mgumu sana nao ni kuingia vijijin ukawa unatafuta Mise ya hasa vijijin vya mwambao MWA ziwa Tanganyika ukipata unabangulisha kabisa unasafirisha kuleta kigoma mjini. Ukifika unakamulisha na kuuza mafuta na mashudu
Japo unahisi hukufanyiwa haki ila hiyo experience uliyoipata ni kubwa sana!! Mainjinia wengi wanajua theories tu lakini kazi za ufundi hawajui ila wewe tayri una theoury na una uzoefu full wa kazi za ufundi!!Witmak255,
Hapana ndugu mimi ni Civil Engineer. Karibu lakini uniambie hicho kitu.
safi mkuu umejibu kwa upeo mkubwa makofi kwako......Asingejipanga maana yake hata hiyo milioni mbili asingekuwa nayo. Anachoomba hapa ni wazo la biashara kwa mtaji wa milion mbili.
Engineer uchwara ataweza kuosha magari? Labda kuwa Admin group za WhatsappUsichelewe fungua Car wash mlimani City nasema usichelewe the rest is history.
Siku moja mtu ajitolee kufundisha hii kitu na Mungu atazibariki Kazi za mikono yakeskills economy