and 300
JF-Expert Member
- Jun 27, 2012
- 26,398
- 36,406
Nipo tayari kuchangia gharama za mafunzo tajwaSiku moja mtu ajitolee kufundisha hii kitu na Mungu atazibariki Kazi za mikono yake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nipo tayari kuchangia gharama za mafunzo tajwaSiku moja mtu ajitolee kufundisha hii kitu na Mungu atazibariki Kazi za mikono yake
Ngoja nicheke kwanza[emoji1787][emoji1787][emoji23]
Umeusoma Uzi wake vizuri mkuu?
[/QU
Diana nimesoma rafiki.
Asante sana nduguJapo unahisi hukufanyiwa haki ila hiyo experience uliyoipata ni kubwa sana!! Mainjinia wengi wanajua theories tu lakini kazi za ufundi hawajui ila wewe tayri una theoury na una uzoefu full wa kazi za ufundi!!
Kitu cha muhimu zaidi ya yote ni kuhakikisha umesajiliwa na ERB either kama Gradute engineer au professional engineer!!
Then...
Wazo la kwanza, naamin unajua kutumia autocad na archcard/revit, anza kwa ku design simple houses then tumia mtandao wa kijamii kupost design zako... mtu akitaka una mchaji pesa plus akianza kujenga unaweza ongeza dau ili usimamie ujenzi na kuhakikisha jengo linajengwa kitaalamu!!
Wazo la pili, tafuta masela wako wawili watatu unao waamini then fungua kampuni ya ujenzi (hata class 6 si mbaya), hatua hii itaambatana na hatua ya kwanza, ukisha design jengo tumia kampuni yako kusimamia na kutekeleza ujenzi!!
Wazo la tatu...
Kama una ujuzi wa autocad na archcad tumia angalia fursa za freelancer... google "freelancer.com, upwork, fiverr" huko utakutana na freelancers wengine...go and compete, kama una ujuzi utapta tenda kwa kutumia ujuzi wako wa autocad/archcad!!
Wazo la mwisho!
Wazo lingine unaweza tafuta ajira kwenye kampuni ingine ya ujenzi, kwa ujuzi ulio nao unaweza pata dau zuri zaidi!!
Kila la heri mhandisi!
Well, wewe ni fundi wa nini? Kama fundi wa ujenzi, tumia akaunti zako za mtandaoni kujitangaza kwamba unajenga kwa ubora, uaminifu na bei nafuu.
Ukipewa kazi ya kujenga kuwa muaminifu kweli na fanya kazi nzuri. Utapata kazi hadi zitakushinda. Tatizo kubwa tulilonalo Tanzania ni mafundi wasio waaminifu. Ukiwa mwaminifu utakuwa tajiri ndani ya miaka mitano.
Huyo million 2 iweke vizuri, ili ukishafanikiwa utanipa kama malipo ya ushauri huu.
- Tafuta frem anzisha kampuni yako ya ujenzi hasa ukilenga wateja wa kawaida wenye kazi na mahitaji ya ujenzi
- Buni ramani za nyumba za gharama nafuu ambazo watu wengi hujenga kisha uza hizo ramani kwa bei nafuu ambayo hata mwenye ndoto ya kutaka kujenga miaka 10 ijayo anaweza kushawishika kujenga.
- Anza kutengeneza connection na wadau wengi kwenye tasnia hiyo ya Ufundi ili ikitokea fursa inayohitaji huduma ya taaluma yako wakupe fursa.
- Fungua social media accounts kwa ajili ya hiyo taaluma na ofisi yako (niliyokushauri ufungue) Kisha uwe unatoa ushauri mbalimbali kuhusu mambo ya ujenzi, pia kwa watakaotaka ushauri zaidi waambie wakuone ofisini kwako na uwape ushauri BURE, ili uweze kupata connection na wateja hasa wanapovutiwa na ushauri mzuri uliowapa.
- tembelea maeneo ambayo yana miradi mingi ya ujenzi kama Dodoma, Kigamboni nk kutafuta fursa (mkaa bure sio sawa na mtembea bure).
- Tafuta location nzuri fungua duka la Hardware hata kama una 50,000 Nunua mfuko mmoja wa cement na misumari uza, kadiri siku zinavyoenda bidhaa kwa ajili ya kuuza zitaongezeka.
- Nunua vifaa muhimu vya ujenzi ambavyo mara nyingi watu hupenda kukodisha ili uwe unakodisha.
- Kifupi Fanya biashara zinazoendana na taaluma uliyosomea kwani ina wigo mpana sana na ina fursa nyingi.
- Kama kweli umeweza kupata uchungu kwa malipo hafifu ya kuajiriwa, basi jua kuwa una roho ya biashara tena yule mfanyabiashara mwenye mafanikio. Jiandae kwa changamoto lakini usikate tamaa wala kurudi nyuma.
Sina ujuzi na biashara ya mise Ila babu zangu wameifanya Sana hii tena bila kuwa na elimu yoyote, nachokiona ni kwamba watu toka miaka hiyo ya 90 mpaka leo bado wanafanya hivyo. Nachojua Tu soko la mafuta ya mise lipo tayari. Na Kwa kigoma dumu moja halishuki 45000. Muhimu fanya research kidogo Ila ni idea Tu niliyokupa ambayo ukiifanya kwa kutumia elimu yako utatoka.Asante sana, je unafahamu zaidi kuhusu biashara ya mise? Je yenyewe ina msimu? Unaweza kuichanganua zaidi kama ulivyochanganua ishu ya tofali?
Sijawahi ona comment ya kipuuzi kama hiiWewe ni boya! Kama ungekuwa so valuable sokoni, basi ungekuwa ushapata kazi kwenye kampuni nyingine. Kama kwa mwaka mmoja umeshindwa kupata kazi ingine ukiwa kazini tegemea kula jeuri yako kitaa.
Kwanini usifungue kampuni yako mtafute mdau mwenza mjoin muanze na class 7 huku ubapamabana na mambo mengine.Habari zenu wana jamvi,
Nimeacha ajira kwa hasira. Nimefanya maamuzi ya kipuuzi? sijui! Ngoja nianzie mbali kidogo kuwasimulia:
Nilihitimu Shahada yangu ya Uhandisi mwaka jana na baada ya kukaa mtaani kwa miezi mitatu tu nilifanikiwa kupata ajira. Nilipata ajira kama fundi mchundo (Technician) na sio Muhandisi kama nilivyotegemea. Kwa kweli nilivunjika moyo kwa hilo kwa kuwa wakati huo naingia kazini niliingia na jamaa mmoja naye akaajiriwa kama Technician ila yeye amesoma Veta Level 2.
Kilichoniuma mimi ni kwamba nina Stashahada Ya Uhandisi Pamoja na Shahada ya Uhandisi alafu bado nalipwa sawa sawa na mtu mwenye cheti cha Veta, tena kiuhalisia yeye analipwa kiasi kikubwa kwa kuwa yeye hana makato ya Bodi ya Mkopo ila mimi bodi wananinyoosha.
Wakati naanza kazi nilimuuliza bosi wangu kwa nini naajiriwa kama Technician na sio Engineer, akanijibu kwamba nitaweza kupandishwa huko mbeleni kulingana na utendaji. Basi mimi nikaanza kazi.
Kwa kweli kazi ilikuwa na changamoto kwa sababu nilikuwa na majukumu mengi. Nikiwa ofisini nilikuwa nikihusika katika usanifu na kuandaa mpango kazi na nikiienda site nilikuwa napigika zaidi maana nilikuwa nahusika kwenye kusimamia kazi, ununuzi wa materials, na pia nilikuwa nikihusika katika kazi za kufanya kwa mikono.
Yaani kwa ufupi nilikuwa nikifanya kazi za fundi mpaka za muhandisi mimi mwenyewe. Katika mradi wangu wa kwanza nikagundua hata dereva analipwa pesa nyingi kuliko mimi, nikazidi kuumia.
Sasa bwana mwezi uliopita, mwisho wa mkataba wangu ukafika, bosi akaniita akanikabidhi mkataba mpya, lakini baada ya kuupitia nikagundua mshahara ni ule ule na cheo ni kile kile. Basi mimi nikamuomba bosi anipe siku moja nikafikirie alafu nitakuja kusaini au la. Baada ya siku moja nilirudi na nikaamua kuweka dau la mshahara ninaloona mimi ni sahihi. Kwa kifupi bosi alikataa na mimi nilikataa na mimi nikaishia hapo kufanya kazi.
Sasa turudi kwenye kichwa cha uzi huu. Naomba mnishauri niazie wapi maisha ya biashara maana kazi nimeshaacha (na sijui kama lilikuwa wazo la busara), hapa nina 2 million ambayo nilifanikiwa kuikusanya kwa mwaka huo mmoja niliokuwa nikifanya kazi.
Sijawaambia wazazi wangu wala watu wangu wa karibu kwamba nimeacha kazi na ninafikiria kwenda mkoa ambao nitakuwa mbali nao nikaaendelee kujifunza maisha huko.
Nipo tayari kufanya biashara ya hali yoyote, nakaribisha ushauri.
Asanteni.
Ushauri wangu japo mimi siyo mfanyabiasharamilioni mbili hiyo nimeikusanya kwa mwaka mzima sio kwamba nimeipata kwa mara moja. Ni kweli nimeacha kazi nikiwa bado sina detailed plan ya nini cha kufanya. ila ndo nimeshaacha na nnaamini nitasavaiv, hapa nimekuja kuomba ushauri kwa watu wenye uzoefu. Kama wewe unahisi nimeleta habari ya uongo ni siwezi kukuaminisha tofauti ila kama unaweza kunisaidia kwa mwongozo, nitakushukuru sana.
Nipo Kigoma, Kasulu kwa sasa.
Kama we sio muoga na afya yako ni nzuri,na unae passport kazi hiyo apo nchini Dubai
Pima afya yako I mean HIV, TB and hepatitis B and C
Visa 630000 for 3 month
Air ticket 610000
Try your luckyView attachment 1249814View attachment 1249815
Biashara ya kuingiza nyanya mjini kutoka mkoa inalipa sana kwa maelezo zaidi sogea mabibo kwa madalali
Sikiliza moyo wako
Japo unahisi hukufanyiwa haki ila hiyo experience uliyoipata ni kubwa sana!! Mainjinia wengi wanajua theories tu lakini kazi za ufundi hawajui ila wewe tayri una theoury na una uzoefu full wa kazi za ufundi!!
Kitu cha muhimu zaidi ya yote ni kuhakikisha umesajiliwa na ERB either kama Gradute engineer au professional engineer!!
Then...
Wazo la kwanza, naamin unajua kutumia autocad na archcard/revit, anza kwa ku design simple houses then tumia mtandao wa kijamii kupost design zako... mtu akitaka una mchaji pesa plus akianza kujenga unaweza ongeza dau ili usimamie ujenzi na kuhakikisha jengo linajengwa kitaalamu!!
Wazo la pili, tafuta masela wako wawili watatu unao waamini then fungua kampuni ya ujenzi (hata class 6 si mbaya), hatua hii itaambatana na hatua ya kwanza, ukisha design jengo tumia kampuni yako kusimamia na kutekeleza ujenzi!!
Wazo la tatu...
Kama una ujuzi wa autocad na archcad tumia angalia fursa za freelancer... google "freelancer.com, upwork, fiverr" huko utakutana na freelancers wengine...go and compete, kama una ujuzi utapta tenda kwa kutumia ujuzi wako wa autocad/archcad!!
Wazo la mwisho!
Wazo lingine unaweza tafuta ajira kwenye kampuni ingine ya ujenzi, kwa ujuzi ulio nao unaweza pata dau zuri zaidi!!
Kila la heri mhandisi!
Engineer uchwara ataweza kuosha magari? Labda kuwa Admin group za Whatsapp