Nimeacha kazi: Nianzie wapi kwenye biashara?

Asante sana ndugu
 
Mkuu naona maamuzi yako hayakuwa sahihi, kwasababu hata wewe hilo umeshalitambua. Milioni mbili nipesa nyingi endapo wakati unaacha kazi ungejua unaenda kufanya nini, vilevile nindogo sana sanaaaa tena sanaaaa kwasababu bado ujajua utaifanyia nini ili iongezeke huku nawewe ukila, ukivaa, nakulala.

Milioni mbili uliyoipata ndani yamwaka mmoja haikuwa ndogo kwasababu ndio ilikuwa kazi yako yakwanza toka umalize chuo. Vilevile umeweza kuweka akiba hiyo yamilion mbili hali yakuwa ulishakula, ukalipia room, ukavaa, umeonga, navitu vingine vidogovidogo umeshavifanya.

Hali yamaisha kwasasa ningumu sana na biashara ningumu sana mtu asikudanganye nasio kama nakukatisha tamaa ila ndio ukweli huo. Kwamazingira yaTZ mtu aliyetoka familia yahali yachini ukimkuta kajiajiri ujue kuna mawili hana elimu/vigezo vyakuajiriwa au kakosa ajira kabisa. Ila sikufichi ndoto zawengi nikuajiriwa nahuo ndio ukweli nayote hiyo nikutokana namazingira magumu yaupatikanaji mitaji namazingira magumu ya kibiashara.

Ndani yamwaka mmoja umeweza kumake milioni mbili inamaana ndani yamiaka mitano kazi hiyo hiyo ungeifanya vizuri bila kuongeza majukumu basi ungekuwa namilioni kumi!!! Miaka mitano unaweza kuiona mingi namilioni kumi unaweza kuiona ndogo kwakuipata ndani yamiaka hiyo mitano ila amini nakwambia miaka mitano inaweza kufika usiwe nahiyo milioni 10 ukawa hivyo hivyo ulivyo sana sana ukawa umenunua vitu vyandani tu ambavyo thamani yake isizidi milioni 1.5

Naamini kama umeacha kazi ukiwa namilioni mbili hiyo hiyo basi naamini tayari imeshapungua sio tena milioni mbili nakama ujaipunguza hiyo Milion mbili yako basi tayari umeshapunguza pocket money yako bila kuingiza kitu so namilioni mbili yako soon utaichokonoa2.

USHAURI: biashara ndio kama unaianza nakama ujawahi kufanya biashara naumetokea familia zetu hizi zakajamba nani, mara nyingi tunachoangalia katika hatua zamwanzo wabiashara ikuingizie faida yakula, kulipia room, na mengine mambo madogomadogo. Biashara ikishakuwezesha hayo hapo juu ndio utapata matamanio yakuiwezesha ili ikupatie pesa nyingi kwaajili ya maendeleo yako mwenyewe najamii nzima iliyokuzunguka yaani ndugu zako.

So angalia katika mazingira hayo uliyopo utafanya biashara gani unayoipenda nakuimudu kuifanya kwamoyo wako wote mpaka isimame ili iweze kukuletea maendeleo. Kisha wafate moja kwamoja wazoefu wahiyo biashara ili wakupe A-Z yahiyo biashara nawala usione aibu. Nahuo ndio ushauri wangu.

Poleni kwagazeti hili lanipashe.
 
Nanukuu "hiyo milioni mbili iweke vizuri utakuja kunipa kama malipo ya ushauri huu" [emoji23][emoji119]
Umekua boss ushauri wa hela yote huu!
Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Bonge la ushauri aisee, japo ni wa filed tofauti ila nmeona kuna mahala na mimi naweza u-apply!
Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Asante sana, je unafahamu zaidi kuhusu biashara ya mise? Je yenyewe ina msimu? Unaweza kuichanganua zaidi kama ulivyochanganua ishu ya tofali?
Sina ujuzi na biashara ya mise Ila babu zangu wameifanya Sana hii tena bila kuwa na elimu yoyote, nachokiona ni kwamba watu toka miaka hiyo ya 90 mpaka leo bado wanafanya hivyo. Nachojua Tu soko la mafuta ya mise lipo tayari. Na Kwa kigoma dumu moja halishuki 45000. Muhimu fanya research kidogo Ila ni idea Tu niliyokupa ambayo ukiifanya kwa kutumia elimu yako utatoka.
 
Ungekuja kuomba ushauri kabla ya kuacha hiyo kazi, yaani kabla ya kumtunishia kifua huyo mwajiri wako; huenda ungepata mawazo mengi sana, yakiwemo hasi na chanya. Binafsi naona uliwahi sana kuacha hiyo kazi uliyokuwa ukiifanya. Ulitakiwa uvimilie miaka miwili au mitatu mbele kabla ya kuchukua uamuzi uliouchukua.

Siku zote wenzako tunaamini kwenye ile methali ya "mvumilivu hula mbivu" na pia ile ya "Haraka haraka haina mbaraka". Umeingiwa na wivu kumuona dereva analipwa mshahara mkubwa kuliko wewe! Unalipwa mshahara sawa na mtu wa level 2 huku ukiwa na stashahada na shahada juu!

Je, unafahamu amefanya kazi kwenye hiyo kampuni kwa muda gani? Unazifahamu changamoto alizopitia? Uvumilivu na uaminifu wake kwenye kampuni unaufahamu? Mahusiano yake na mwenye kampuni unayafahamu?

Mimi naona kiburi cha elimu kilikuponza na hivyo kuamua kuacha kazi eti ukajiajiri kwa kitu ambacho hata hukifahamu na kwa mtaji mdogo wa milioni 2 (Pesa hii ni nyingi kwa mjasiriamali aliyeanza na mtaji wa laki tano kushuka chini ila siyo kwa yule aliyekurupuka kama mtoa mada)

Ushauri wangu; Tafuta kazi nyingine ili urudi kwenye fani yako huku ukiendelea kujipanga kwa lengo la kuja kujiajiri siku za usoni.

Kwa sasa nadhani muda bado! Kama huamini, ingia kitaa halafu uone hiyo milioni mbili itakavyo pukutika ndani ya siku chache tu na kubakia huna kitu.
 
Wewe ni boya! Kama ungekuwa so valuable sokoni, basi ungekuwa ushapata kazi kwenye kampuni nyingine. Kama kwa mwaka mmoja umeshindwa kupata kazi ingine ukiwa kazini tegemea kula jeuri yako kitaa.
 
Kwanini usifungue kampuni yako mtafute mdau mwenza mjoin muanze na class 7 huku ubapamabana na mambo mengine.
 
Ushauri wangu japo mimi siyo mfanyabiashara

Popote pale ulipo jaribu kununua vyombo vya ndani vikombe bakuli sahani majagi vijiko n.k halafu peleka kauze huko mawilayani. Anza na laki sita tu nunua robo dazenidazeni ujaribu uone.

By the way wewe uko mkoa gani
 
Mh Kasulu, nimepakumbuka sana nilikuwa huko juzi kati tu.

Kasulu Pale unaona nini pale? Ingawa mtaji wako si mkubwa sana ila still unaweza fanya kitu.

Kwenda mikoa ya mbali sio ishu pia unaweza jongea Kibondo au Kakonko. Bado huko kumelala sana.

Sema kuna baadhi ya Furusa zinahitaji mitaji mikubwa kama Kilimo, au ununuani wa mazo.

Nipo Kigoma, Kasulu kwa sasa.
 
Hizi ni akiwa huko kwa Waha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…