Nimeacha kazi: Nianzie wapi kwenye biashara?

Maisha sio kuajiriwa tu. labda riziki yake haiko huko kwenye kuajiriwa na Mungu alimpangia apewe mshahara mdogo ili aondoke huko make maisha yake hayako huko bali yako kwenye kuajiri.

Hivyo si kwamba kuajiriwa ndo kila kitu mkuu kwenye Dunia hii ya leo na pia hayo ni maamuzi yake binafisi sasa unapo anza kumpinga kwa maamuzi yake binafisi inakuwa sio kabisa
 
Huwezi Mshauri bila kutukana? Au bila kitukana huwezi jenga hoja?

Kwa hiyo wewe unaamini walio ajiriwa ndo wajanja na wasio kuwa na kazi ni mafala na wajinga.
Wewe ni boya! Kama ungekuwa so valuable sokoni, basi ungekuwa ushapata kazi kwenye kampuni nyingine. Kama kwa mwaka mmoja umeshindwa kupata kazi ingine ukiwa kazini tegemea kula jeuri yako kitaa.
 
Pamoja na pongezi zote unazopata ..
Ulikosea kuacha kazi na kuanza upya maisha mengine , Ni makosa makubwa mno
Acha kazi ukijua unaenda kuendeleza kitu na sio kuanza upya .
Nakupa Pole ila nakuombea kuelekea safari mpya ulioamua kuanza , japo haitakuwa rahisi hvyo
 

Kiongozii me naona bado mapema sana kwa career yako ulioitafuta kwa miaka kama 7 afu kuitosa kwa ajili ya mshahara mdogo sidhan bado kuna firm nyingi hata kama unataka kujiajirii angalia wazo ambalo utaweza kuliendesha hata ukipata chance nyingine ya kazi...iyo 2milions wekeza ila bado pigania career yako una kitu kikubwa sana nasema hiv kwa sababu tayar una uzoefu na pia. Juu hapo kuna mahalii unasema huna uhakika kama kuacha kazi lilikua wazo sahihi...hayo tuu mkuu
 
Pole sana mkuu, nipo kwenye hiyo field mwaka wa 5 huu na kampuni binafsi, utofauti wa mshahara kwa kampuni binafsi ni jambo la kawaida sana na mara nyingi hua inategemea uliingia vipi mara ya kwanza...
Natamani kuandika mengi hapa ila usikate tamaa na nafasi mbele unayo tena kubwa tuu
 
hujaonesh achochote kuonesha kama wewe ni engineer unataka ulipwe kama engineer. umeona wapi ukiacha serikalini
 
Ushauri wangu chezea kuwekeza kwenye mambo ya taaluma yako mkuu hapo hutajuta.
Sababu tayar umeshafanya kazi na pia umesomea hiyo huo ndo mtaji wako mkubwa.
 
FANYA PROFFESSIONAL ENTREPRENEURSHIP,ZA UJUZI KOSA KUBWA ULILOFANYA NI KUTOFANYA SOCIAL CAPITALIZATION KWA WATU ULIOWAPA HUDUMA KULE SAITI,WALE NDIO WATEJA WAKO WA KUANZIA AMBAO WANGEKUPA CONNECTION YA KAZI,HIVYO YOU HAVE TO USE MORE SKILLL OF HOW TO SELL YOUR SELF,B'SE YOOU ARE THE PRODUCT YOUSELF.WEWE NI UJUZI NA UJUZI NI BIDHAA,INGIA SOKONI,NAJUA WEWE KAMA ENGINEER UMEFUNDISHWA SOMO LA MARKERTING NI AIUBU KWA INJINIA WA MAJENGO KULIA MITANDAONI WAKATI KUNA DRS LA PILI WANAPATA TENDA ZA KUJENGA.
ANZA KUJIUZA HAPA HAPA JF,WASAP,FACEBOOK NA MARAFIKI ZAKO WOTE ULIOSOMA NAO NA WA MTAANI WAJULISHE KUWA SASA UNATOA HUDUMA YA KUJENGA NYUMBA,KUSIMAMIA NK.
FUNGUA KAOFISI MSHENZI KAMA HAPO KASULU WANAJENGA KWA KASI KAMA SIO HAMA NENDA MWANZA DAR DOM HUKO KUNAJENGWA KWA KASI.
KUUZA UJUZI NI RAISI ZAIDI KULIKO BIDHAA,ILA USHINDANI NI MKUBWA NA KUJUANA KWINGI ILA WAPO WANAOTAKA UBORA NA WANAPESA.
 
Dah....una 2m...Dah...umewahi kubeti?[emoji2960]
 
Mkuu umemaliza kila kitu
 
Kama kijana ninaetafuta life huu ujumbe nimeusoma kwa dhati kwakua unanigusa,muda mwingine unajifananisha na wengine inakuumiza sana moyo unaona unachelewa hivi.asante mkuu
 
Nmependa koment yako, hasa ya kwanza ambayo itamfungulia fursa ya kupata tenda za kujenga,anatakiwa ajikite zaidi ktk ujuzi aliosomea ambao kuna makanjanja wengi wanapiga hela hivyo asilaze damu.
Fursa ya pili hapo kigoma ni ya kuuza mafuta ya mawese kwa watengeneza sabuni viwandani,sabuni ni big sekta kwa sasa hivyo aichunguze vizuri halafu si bidhaa kuoza changamoto ni kuingia sokoni ambapo kuna wajasiliamali wengi.
Fursa ya tatu hapo KGMA ni ya ufugaji samaki,watu wa kigoma hawajachangamkia kufuga samaki hali kuna maeneo mengi yanatuama maji (swamps) yeye ni kutafuta aneo la kukodi aanze kazi,mashudu,dagaa wabovu,,migebuka wabovu wamejaa tele.For sure siku nikirudi kigoma miaka yangu miwili tu inatosha kuitwa mfalme.
Fursa nyingine kama hio hela inatosha nunua mtambo wa kukamulia mawese nenda vijiji ambavyo mitambo ni adimu,maganda ya mise nayo ni fursa ya kutengenezea mkaa,Ukiingia ktk kazi ya mawese na mise kuna kazi muambatano mfano unaweza anzisha ufugaji wa kuku kwa kuwa utakuwa na mashudu mengi.
 
Ukimsoma Robert Kiwasoki anasema hakuna mda mzuri wa kuacha kazi vinginevyo kila siku utasubiri labda mwakani mpaka unazeeka.Waajiriwa wengi ni waoga kuacha kazi,.Mwanzo mgumu ila atashinda tu.
 
Asante sana mkuu kwa ushauri
 
Afuge samaki Gani? Pia jua Consumption power ya watu wa Kigoma iko Chini sana
 
Afuge samaki Gani? Pia jua Consumption power ya watu wa Kigoma iko Chini sana
Naomba data ya consumption ya watu wa kigoma.Kwa hio samaki wanaovuliwa kigoma huoza maana hakuna wa kuwanunua? Acha kupotosha,Hivi viazi wanavyolima mbeya vinaliwa na watu wa mbeya? Mahindi yanayolimwa songea yanaliwa na watu wa songea.Hoja yako ni dhaifu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…